Taifa_Kwanza
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 443
- 86
Kazi kweli kweli.
Shetani kazi yake ni kuchinja na kuharibu. Lakini ni mwerevu(soma kitabu cha Mwanzo utaona werevu wake). Hachinji na kuua wazi wazi. Akifanya hivyo si utamkimbia haraka? Anatumia maandiko. Alipomjaribu Yesu kwa kumwambia ajitupe chini alitumia maandiko. Kama babu anavyothibitisha "uponyaji" wake kwa kutumia maandiko(imani, maombi, ndoto,mungu).sidhani kama kuna sababu za kumhusisha babu na shetani kwani shetani kazi yake kubwa ni kuharibu sio kutengeneza.
Sijajua umri wako lakini nafikiri wewe utakuwa mtoto, kwa maana mambo uliyoandika hayana kichwa wala mkia. Hivi kwa akili yako unataka utuambie shetani alishawahi kuumba mti au mzizi au kitu chochote chini ya jua? wewe kama ni mlokole basi ni wale ambao ni walokole waliofurika ushamba wa kujua neno la mungu.Kuna visa vingi sana ambavyo ukisoma biblia utakumbana navyo ambavyo kama utatafsiri maandiko hayo kwa tafsiri zako ulizotafsiri kwa babu basi hata bwana yesu utamweka kwenye upande babu wa loliondo.
Kwa mfano kuna wakati yesu alifinyanga tope ili kumponya kipofu kwa hilo tu hebu niambie kulikuwa na sababu gani kwa yesu kufinyanga tope wakati watu wote tunajua uwezo alionao?
kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha aliwaambia watu wajaze mabalasi maji ndiyo ayaombee, kwanini asitamke neno mabalasi yakajaa maji bila kusumbua watu kuchota maji na kuwa divai?
kwenye kisa cha musa na farao, waganga walifanya mazingaombe na kutokea nyoka, musa aliamriwa na mungu atupe fimbo yake chini ambayo nayo iligeuka nyoka na kuwala nyoka wa washirikina wa farao, hebu niambie kwanini musa asitamke neno tu mpaka atumie vitu halisi (fimbo)
Yesu alipowakuta wakina Petro wamekosa samaki kwenye shughuli zao za uvuvi aliwaambia warudi wakavue na kushusha nyavu zao kilindini. kama wewe ni wakiroho sana tuambie kulikuwa na sababu gani ya kuwasumbua wavuvi hao ambao walikuwa wamechoka? si angetamka tu neno samaki wakatokea na kujaa chomboni?
sidhani kama kuna sababu za kumhusisha babu na shetani kwani shetani kazi yake kubwa ni kuharibu sio kutengeneza. Wewe ndiyo agenti wa shetani maana inaonyesha unadhani shetani hutumia mitishamba na mungu hutumia miujiza katika uponyaji, hebu tuambie ni wapi kwenye biblia imeandikwa dawa za mitishamba zinauhusiano na mambo ya kishirikina?
wakati wa Yesu hakukuwa na hospitali na dawa kama panadol kwa hiyo watu walikuwa wanategemea nguvu za maombi tu sio pamoja na mitishamba?
Usia wangu wa bure kwako ni kuwa usiwe na mawazo finyu katika imani, Mungu hana mipaka duniani na mbinguni.
Niandike kwa herufi kubwa ndio mtanielewa? Miujiza inayotokana na Mungu huambatana na Injili. Watu lazima wahubiriwe Injili. Sio kupewa kikombe tu cha dawa! Soma Matendo ya Mitume 2 utaona jinsi Petro alivyohubiri Injili watu wakachomwa mioyo yao wakatubu na kisha miujiza mingi ikafanyika na idadi ya watu waliookoka ikaongezeka kila siku. Hapo kwa babu baada ya kupewa kikombe wangapi wamechomwa mioyo yao na kutubu ufisadi wao, uzinzi wao na ujambazi wao? Shetani hawezi kuhubiri Injili maana hapendi watu waende mbinguni. Ataumbuka tu hawezi kushindana na Mungu kwa Jina la Yesu Kristo..
Ni kweli tupu uliyoinena mkuu.
Huyu ni mtoto mchanga anayehitaji maziwa. Sasa analilia mifupa wakati meno hayajaota bado.
Tena nyongeza kea faida ya mediaman bwana alipowashibisha maelfu kwa mikate na samaki, mtaji ulikuwa ni samaki halisi na mkate halisi. Ingeliwezekana kwake kutamka neno tu lakini hakufanya hivyo kwa kusudi maalumu na lililo takatifu.
.
Hakika umesema ukweli ndugu kwa wale wanaopotea. Wamwamini babu tu wapone. Lakini mimi namwamini Yesu Kristu ambaye huyo babu hathubutu hata kulitaja jina lake.
Niandike kwa herufi kubwa ndio mtanielewa? Miujiza inayotokana na Mungu huambatana na Injili. Watu lazima wahubiriwe Injili. Sio kupewa kikombe tu cha dawa! Soma Matendo ya Mitume 2 utaona jinsi Petro alivyohubiri Injili watu wakachomwa mioyo yao wakatubu na kisha miujiza mingi ikafanyika na idadi ya watu waliookoka ikaongezeka kila siku. Hapo kwa babu baada ya kupewa kikombe wangapi wamechomwa mioyo yao na kutubu ufisadi wao, uzinzi wao na ujambazi wao? Shetani hawezi kuhubiri Injili maana hapendi watu waende mbinguni. Ataumbuka tu hawezi kushindana na Mungu kwa Jina la Yesu Kristo.
Niandike kwa herufi kubwa ndio mtanielewa? Miujiza inayotokana na Mungu huambatana na Injili. Watu lazima wahubiriwe Injili. Sio kupewa kikombe tu cha dawa! Soma Matendo ya Mitume 2 utaona jinsi Petro alivyohubiri Injili watu wakachomwa mioyo yao wakatubu na kisha miujiza mingi ikafanyika na idadi ya watu waliookoka ikaongezeka kila siku. Hapo kwa babu baada ya kupewa kikombe wangapi wamechomwa mioyo yao na kutubu ufisadi wao, uzinzi wao na ujambazi wao? Shetani hawezi kuhubiri Injili maana hapendi watu waende mbinguni. Ataumbuka tu hawezi kushindana na Mungu kwa Jina la Yesu Kristo.
Sio kweli kwamba Babu wa Loliondo ametumwa na Mungu kutumia dawa hiyo kuwaponya watu. Huyo Babu ametumwa na "mungu wa dunia hii(shetani) ili kuwadanganya watu waache kumtumaini na kumwamini Mungu wa kweli ili hatimaye waangamie siku ile ya mwisho. Soma 2 Wakorintho 4:4 na kisha tafakari kwa makini hoja zifuatazo utathibitisha ukweli huo.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu. Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?
Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Jamani Watanzania Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo"
Siri imefichuka! Hoja hizo na maandiko hayo ya Biblia yanathibitisha wazi kwamba huyo Babu hajatumwa na Mungu. Ila ni shetani anamtumia kuwadanganya watu. Tusikubali kudanganywa. Hata waganga na wachawi wa leo na wao huwaambia wateja wao kwamba wanaponya au kufanya miujiza kwa uweza wa mungu. I dare to talk openly Huyo mungu wanayemtaja ni mungu wa dunia hii (shetani). Mwenye masikio na asikie.[/
Sababu zote ulizotoa zinaonyesha huelewi huduma anayoifanya Mchungaji Masapila na pili unavyotumia Maandiko Matakatifu unaonyesha ufahamu mdogo sana. Nakushauri kabla hujasema ama kuandika jambo utafakari
Kama ni mwenye dhamboi sijui, kama ni wa shetani au mungu sijui, ila nalikua kipofu na mimi sasa naona, the rest are details,
Shetani kazi yake ni kuchinja na kuharibu. Lakini ni mwerevu(soma kitabu cha Mwanzo utaona werevu wake). Hachinji na kuua wazi wazi. Akifanya hivyo si utamkimbia haraka? Anatumia maandiko. Alipomjaribu Yesu kwa kumwambia ajitupe chini alitumia maandiko. Kama babu anavyothibitisha "uponyaji" wake kwa kutumia maandiko(imani, maombi, ndoto,mungu).
Mitishamba kama dawa huna haja ya kuifanyia maombi ndio iponye. Huo ni ujanja wa shetani ili aonekane ametumwa na Mungu. Kumbe sivyo