Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na Shetani

Nakusifu umekaa kitako na kuandika ujinga wako humu nawe walau upate kundi litakalokufata HUNA UTAKAYEMPATA PENGINE SHETANI MWENZAKO USHINDWE. Hayo maandiko ungekuwa unayafata na kujali ungegundua toka mwanzo wa makanisa yenye kutumia nguvu za kiza yaliyopo Mwenge, Msasani, Mbezi na kungineko ambayo yanapotosha wengi wa watu kwa kuwatajirisha wao waendeshao hayo makanisa, hao hukuwaona umeona ushetani wa Babu wa Loliondo wewe amini kile ujuacho moyoni mwako na mungu wako na mwenzio naye muache amuamini huyo babu na mungu wake kisha wote mtachaguliwa na Muumba kwa kila mtu na stahili yake. Shetani kwanza unamjua wewe anamiguu mingapi au sura gani??? wacha ukakobe wako humu.
 
sidhani kama kuna sababu za kumhusisha babu na shetani kwani shetani kazi yake kubwa ni kuharibu sio kutengeneza.
Shetani kazi yake ni kuchinja na kuharibu. Lakini ni mwerevu(soma kitabu cha Mwanzo utaona werevu wake). Hachinji na kuua wazi wazi. Akifanya hivyo si utamkimbia haraka? Anatumia maandiko. Alipomjaribu Yesu kwa kumwambia ajitupe chini alitumia maandiko. Kama babu anavyothibitisha "uponyaji" wake kwa kutumia maandiko(imani, maombi, ndoto,mungu).

Mitishamba kama dawa huna haja ya kuifanyia maombi ndio iponye. Huo ni ujanja wa shetani ili aonekane ametumwa na Mungu. Kumbe sivyo
 
Kumbe humjui shetani? Ndio maana unadanganyika kwa urahisi! Soma Biblia kwa makini Mwanzo mpaka Ufunuo habari za shetani zimeelezwa vizuri.
 
Sijajua umri wako lakini nafikiri wewe utakuwa mtoto, kwa maana mambo uliyoandika hayana kichwa wala mkia. Hivi kwa akili yako unataka utuambie shetani alishawahi kuumba mti au mzizi au kitu chochote chini ya jua? wewe kama ni mlokole basi ni wale ambao ni walokole waliofurika ushamba wa kujua neno la mungu.Kuna visa vingi sana ambavyo ukisoma biblia utakumbana navyo ambavyo kama utatafsiri maandiko hayo kwa tafsiri zako ulizotafsiri kwa babu basi hata bwana yesu utamweka kwenye upande babu wa loliondo.

Kwa mfano kuna wakati yesu alifinyanga tope ili kumponya kipofu kwa hilo tu hebu niambie kulikuwa na sababu gani kwa yesu kufinyanga tope wakati watu wote tunajua uwezo alionao?

kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha aliwaambia watu wajaze mabalasi maji ndiyo ayaombee, kwanini asitamke neno mabalasi yakajaa maji bila kusumbua watu kuchota maji na kuwa divai?

kwenye kisa cha musa na farao, waganga walifanya mazingaombe na kutokea nyoka, musa aliamriwa na mungu atupe fimbo yake chini ambayo nayo iligeuka nyoka na kuwala nyoka wa washirikina wa farao, hebu niambie kwanini musa asitamke neno tu mpaka atumie vitu halisi (fimbo)

Yesu alipowakuta wakina Petro wamekosa samaki kwenye shughuli zao za uvuvi aliwaambia warudi wakavue na kushusha nyavu zao kilindini. kama wewe ni wakiroho sana tuambie kulikuwa na sababu gani ya kuwasumbua wavuvi hao ambao walikuwa wamechoka? si angetamka tu neno samaki wakatokea na kujaa chomboni?

sidhani kama kuna sababu za kumhusisha babu na shetani kwani shetani kazi yake kubwa ni kuharibu sio kutengeneza. Wewe ndiyo agenti wa shetani maana inaonyesha unadhani shetani hutumia mitishamba na mungu hutumia miujiza katika uponyaji, hebu tuambie ni wapi kwenye biblia imeandikwa dawa za mitishamba zinauhusiano na mambo ya kishirikina?

wakati wa Yesu hakukuwa na hospitali na dawa kama panadol kwa hiyo watu walikuwa wanategemea nguvu za maombi tu sio pamoja na mitishamba?

Usia wangu wa bure kwako ni kuwa usiwe na mawazo finyu katika imani, Mungu hana mipaka duniani na mbinguni.

.
Ni kweli tupu uliyoinena mkuu.
Huyu ni mtoto mchanga anayehitaji maziwa. Sasa analilia mifupa wakati meno hayajaota bado.
Tena nyongeza kea faida ya mediaman Bwana alipowashibisha maelfu kwa mikate na samaki, mtaji ulikuwa ni samaki halisi na mkate halisi. Ingeliwezekana kwake kutamka neno tu lakini hakufanya hivyo kwa kusudi maalumu na lililo takatifu.
.
 
.
Ni kweli tupu uliyoinena mkuu.
Huyu ni mtoto mchanga anayehitaji maziwa. Sasa analilia mifupa wakati meno hayajaota bado.
Tena nyongeza kea faida ya mediaman bwana alipowashibisha maelfu kwa mikate na samaki, mtaji ulikuwa ni samaki halisi na mkate halisi. Ingeliwezekana kwake kutamka neno tu lakini hakufanya hivyo kwa kusudi maalumu na lililo takatifu.
.
Niandike kwa herufi kubwa ndio mtanielewa? Miujiza inayotokana na Mungu huambatana na Injili. Watu lazima wahubiriwe Injili. Sio kupewa kikombe tu cha dawa! Soma Matendo ya Mitume 2 utaona jinsi Petro alivyohubiri Injili watu wakachomwa mioyo yao wakatubu na kisha miujiza mingi ikafanyika na idadi ya watu waliookoka ikaongezeka kila siku. Hapo kwa babu baada ya kupewa kikombe wangapi wamechomwa mioyo yao na kutubu ufisadi wao, uzinzi wao na ujambazi wao? Shetani hawezi kuhubiri Injili maana hapendi watu waende mbinguni. Ataumbuka tu hawezi kushindana na Mungu kwa Jina la Yesu Kristo.
 
Hakika umesema ukweli ndugu kwa wale wanaopotea. Wamwamini babu tu wapone. Lakini mimi namwamini Yesu Kristu ambaye huyo babu hathubutu hata kulitaja jina lake.


AMINA KUBWA NDUGU YANGU - MIMI NASUBIRI WATAKAPO ANZA KUMTUNGIA BABU NYIMBO ZA KUMTUKUZA .....................HAPO NDIO PATAKUWA PATAMU KWANI WAMESHAMBADILI BABU KUWA YESU .............NYAKATI HIZI NI ZA HATARI TUTAONA MENGI.

YOTE YAMEANDIKWA KATIKA BIBLIA - KITABU CHA 2TIMOTHEO: YOTE


mie na Uyatima wangu ............ pamoja na kushindwa kununua dawa ghali za hospital ................hata nikipata malaria sugu shauri ya mbu..............mmmm nimeamua KULIITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE HAI - kikombe kwangu mwiko - kwani kinaponya mwili lakini hakiponyi ROHO - mwili una mwisho ila Roho itaishi milele - so ukiijaza imani ya KIKOMBE badala ya imani ya YESU.... UNALO!!!!!!!! nsunipige mawe jamani - ni uamuzi wangu ........ chonde chonde -matusi kwangu mwiko!!!!
 
Niandike kwa herufi kubwa ndio mtanielewa? Miujiza inayotokana na Mungu huambatana na Injili. Watu lazima wahubiriwe Injili. Sio kupewa kikombe tu cha dawa! Soma Matendo ya Mitume 2 utaona jinsi Petro alivyohubiri Injili watu wakachomwa mioyo yao wakatubu na kisha miujiza mingi ikafanyika na idadi ya watu waliookoka ikaongezeka kila siku. Hapo kwa babu baada ya kupewa kikombe wangapi wamechomwa mioyo yao na kutubu ufisadi wao, uzinzi wao na ujambazi wao? Shetani hawezi kuhubiri Injili maana hapendi watu waende mbinguni. Ataumbuka tu hawezi kushindana na Mungu kwa Jina la Yesu Kristo.

mkuu shida uliyo nayo ni kuwa kila unachosikia unaamini na unataka kukisema kwa jamii ambayo haiwezi kukuelewa....Mimi binafsi sikubaliani kuwa yule babu aliambiwa/kuoteshwa na Mungu kwa hoja hii..
1 - Hakuna mwenye ushahidi kuwa sauti ya Mungu inafananaje
2 - Ndoto inaweza kuletwa hata na mamlaka au nguvu zingine za nuru au giza.
3 - Ukisoma kitabu cha Daniel au Ufunuo, utakutana na maneno...nikasikia sauti kuu kama sauti ya maji mengi, baragumu, etc...kisha nikaona mmoja aliye mfano wa mwanadamu (Daniel 10:1-) Ndipo huyo Gabriel akaniambia.....

Lakini ikiwa mtu anakwenda kupata kikombe kwa context tu ya kupata dawa ya kienyeji na si kulihusisha na imani ya Kikristo bali utaalamu alionao huyo babu juu ya mizizi, basi na aende siwezi kumzuia, kwani hata aspirin au panadol zinatokana na mizizi ila zimehifadhiwa ziweze kudumu muda mrefu.

Wapo watu wengi wanajua hata dawa-mizizi na majani yanayotibu malaria na wanatumia na huyo ni utaalamu tu ambao mababu zetu wamekuwa nao kwa miaka mingi, na si dhambi hata kidogo as long as ramli haihusiki.
 
Niandike kwa herufi kubwa ndio mtanielewa? Miujiza inayotokana na Mungu huambatana na Injili. Watu lazima wahubiriwe Injili. Sio kupewa kikombe tu cha dawa! Soma Matendo ya Mitume 2 utaona jinsi Petro alivyohubiri Injili watu wakachomwa mioyo yao wakatubu na kisha miujiza mingi ikafanyika na idadi ya watu waliookoka ikaongezeka kila siku. Hapo kwa babu baada ya kupewa kikombe wangapi wamechomwa mioyo yao na kutubu ufisadi wao, uzinzi wao na ujambazi wao? Shetani hawezi kuhubiri Injili maana hapendi watu waende mbinguni. Ataumbuka tu hawezi kushindana na Mungu kwa Jina la Yesu Kristo.



Hapo kwenye red, nimegundua unabisha without reference. Haujasikia habari ya wachawi ambao baada ya kunywa kikombe cha babu wakapagawa na kukiri wameuwa watu na kuwaweka misukule?. Unapobisha inabidi uwe umefanya research ya kina na sio kubisha bila kujua nini kinachoendelea. Wewe kama kweli una upako badala ya kuanza kuargue huku kwenye jamii forums kwanini usiende Loliondo kwa babu na kumkemea kwa jina la Yesu ashindwe kutoa hiyo huduma ? Babu hajawahi ingia kwenye mtandao na kujustify huduma yake kama wewe na hao watu wanaojazana huko hawaendi kwa matangazo bali wanaenda baada ya kupata ushuhuda wa wale waliokuwa wanaumwa na sasa wamepona, after all yote unayoyaandika hapa babu hawezi na hana muda wa kuyasoma, nyie kama mnaona huduma anayofanya ni ya kishetani kwanini hamumuombei akaacha ? Mnaishia kuargue tu kwenye media au imani zenu ni haba. Damnnnn
 
Mbona watu wanalalama hakuna hata mmoja alieweza kuhusisha na madhara ya huduma ya babu kiimani. Je baada ya kunywa kikombe watu watamuhasi Mungu kwa kutenda mabaya ama lah? watu hawata mtumikia tena mungu au vp?
 
mh! Me ctii neno hapo mana naona cjui niegemee wap mana kama ingekuwa tofaut makanisa na misikit viongoz wake wangeshazungumza na kukemea kama ilivyokuwa DECI
 
Ulivyoanza 'SIRI IMEFICHUKA' nkadhani labda umeliona jini kwa Babu, au umemuona babu kavaa hirizi... Kumbe ni theory!??..
 
Sio kweli kwamba Babu wa Loliondo ametumwa na Mungu kutumia dawa hiyo kuwaponya watu. Huyo Babu ametumwa na "mungu wa dunia hii(shetani) ili kuwadanganya watu waache kumtumaini na kumwamini Mungu wa kweli ili hatimaye waangamie siku ile ya mwisho. Soma 2 Wakorintho 4:4 na kisha tafakari kwa makini hoja zifuatazo utathibitisha ukweli huo.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu. Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Jamani Watanzania “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo"
Siri imefichuka! Hoja hizo na maandiko hayo ya Biblia yanathibitisha wazi kwamba huyo Babu hajatumwa na Mungu. Ila ni shetani anamtumia kuwadanganya watu. Tusikubali kudanganywa. Hata waganga na wachawi wa leo na wao huwaambia wateja wao kwamba wanaponya au kufanya miujiza kwa uweza wa mungu. I dare to talk openly Huyo mungu wanayemtaja ni mungu wa dunia hii (shetani). Mwenye masikio na asikie.[/

Sababu zote ulizotoa zinaonyesha huelewi huduma anayoifanya Mchungaji Masapila na pili unavyotumia Maandiko Matakatifu unaonyesha ufahamu mdogo sana. Nakushauri kabla hujasema ama kuandika jambo utafakari
 
Kama ni mwenye dhamboi sijui, kama ni wa shetani au mungu sijui, ila nalikua kipofu na mimi sasa naona, the rest are details,

Hongera! Na wote walioponywa kwa kikombe cha babu na waseme ... AMEN!
Rev 12:11 They overcame him by the blood of the Lamb and by the word of their testimony; (NIV)
 
Shetani kazi yake ni kuchinja na kuharibu. Lakini ni mwerevu(soma kitabu cha Mwanzo utaona werevu wake). Hachinji na kuua wazi wazi. Akifanya hivyo si utamkimbia haraka? Anatumia maandiko. Alipomjaribu Yesu kwa kumwambia ajitupe chini alitumia maandiko. Kama babu anavyothibitisha "uponyaji" wake kwa kutumia maandiko(imani, maombi, ndoto,mungu).

Mitishamba kama dawa huna haja ya kuifanyia maombi ndio iponye. Huo ni ujanja wa shetani ili aonekane ametumwa na Mungu. Kumbe sivyo

Ati? Am I smelling a heresy here? I doubt your theological understanding! God commands that we receive everything with prayer and thanksgiving. And you say hakuna haja ya kufaifanyia maombi ... Hapa si kama dawa inaponya au la; ila kila tukipokeacho twakipokea kwa shukurani na kwa kufanya hivyo hata sumu huhuishwa,
(1 Tim 4:4-5) For everything God created is good, and nothing is to be rejected if it is received with thanksgiving, 5 because it is consecrated by the word of God and prayer (NIV)
 
[/QUOTE]Sababu zote ulizotoa zinaonyesha huelewi huduma anayoifanya Mchungaji Masapila na pili unavyotumia Maandiko Matakatifu unaonyesha ufahamu mdogo sana. Nakushauri kabla hujasema ama kuandika jambo utafakari[/QUOTE]

Ndugu, kama ufahamu wako ni mkubwa sana kuliko wangu, uonyeshe wazi huo ufahamu wako kwa kutoa hoja zako hapa, uwasaidie wengine. Hujasikia idadi ya watu waliokufa wakiwa njiani kwenda kwa babu, wakiwa kwa babu, na waliokufa baada ya kutoka kwa babu? Unasubiri watu waendelee kufa ndio uwasaidie? It will be too late. Faida unayopata kwa kujiunga na JF ni nini sasa kama hutoi hoja wala kujibu hoja kwa ufahamu wako mkubwa? Mimi ntaendelea kusema. Sioni ajabu ukipinga. Yesu alipokuwa hapa duniani aliwaambia watu ukweli. Wakampinga, wengine wakataka kumpiga kwa mawe, hatimaye wakamuua. Lakini ukweli wake bado unaendelea kutangazwa hata leo.
 
Back
Top Bottom