Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na Shetani

Nimeumwa magonjwa mengi sana katika maisha yangu. Lakini kwakuwa ninamwamini Yesu nimekuwa nikiliitia Jina lake na kukemea hayo magonjwa, na kwa jina hilo kuu la Yesu nimepona magonjwa mengi. Ndio maana nawahurumia Watanzania wenzangu wanaopoteza pesa(nauli) na muda wa kwenda na kukaa kwa babu wakati kuna uponyaji bure unaopatikana katika Yesu. Kama ulienda kanisani ukaombewa na hujapona huenda imani yako ni haba au labda unataka uponyaji tu lakini Yesu mwenye kutoa huo uponyaji humtaki.
Ndugu yangu kwenye ugonjwa na matatizo watu hupoteza pesa nyingi.hyo nauli ya kwenda loliondo ni kidogo.Huko unaposema watu waende wamekuwa wakidaiwa michango mingi na mikubwa mno.Kuna watu waliodanganyika na kujikuta wakitoa mali zao na hata zile zilizokuwa zikimilikiwa na familia jambo lililopelekea mifarakano na hata ndoa kuvunjika.Mahosptal nako gharama ni kubwa sana,gharama ya kumwona specialist inafika mpaka elfu 30, magonjwa mengine yanahitaji kumeza dawa kila siku
Nadhani Mungu wetu ni Mungu wa upendo hapendi kuona wanadamu wanateseka ndio maana akamwonyesha huyo babu dawa,Waache waende loliondo wakapate tiba na wanaotaka huduma zaq kiroho wataenda makanisani.
 
Wapendwa,

MUNGU alituumba kwa mfano wake.
Tuondokane na ujinga unaotuletea wasiwasi na woga usiokuwa na msingi unaoingiza watu utumwani.
Tupeane MAARIFA ya KIMUNGU kwa HEKIMA bila kugombana au kuudhi wengine.
 
Mediamen anaelewa biblia kinyume,unajua hata dini ya shetani wana biblia yao?
-Hivi Musa alivyotumwa kuwaokoa waisreli janwani alikubali kirahisi? kule alikokwenda kuchunga kondoo alikwenda kutafuta nini huko.
- Hivi hiyo sadaka ianyopikelewa huko kanisani kwenu inafanya kazi gani.jibu unalo hivi mkiwaombea watu kwa kutumia neno wakipona na wakitoa sadaka yao ikawa kubwa mnairudisha?mbona babu karudisha mamilioni na anataka 500 tu kwa imani kuwa inamtosha na huduma yake ni endelevu vinginevyo atakuwa anajitafutia utajirisho.
-Angalia TV uone ushuhuda wa watu waliopona usituletee hadithi.
-Soma kitabu chote cha ufunuo wa Yohana ukielewe siyo kutukatia mstari unaoupenda wewe.
-Kwa waliokwenda kwa Babu ametoa ushuhuda kuwa Alfajiri watu wanakula neno la nguvu kutoka biblia ndiyo huduma inaendelea na ukumbuke babu ni mtumishi wa mungu tena msomi wa biblia miaka 5 siyo wale wa miezi 3 halafu wanajiita wachungaji.
Neda Loliondo ukapate la kutuambia siyo kusikia unatuletea falsafa zilizokufa huku JF.
-
 
Hivi kama babu hatibu wewe inakuwasha nini.......? Kwanza umeingia humu mwezi huu wa tatu kwa ajili ya kumkadia Babu huna jipya!!! watu wanapona kwa muujiza wa Mungu na si mungu kama unavyosema wewe!!!! Babu go on uponye watu wenye matatizo.

Mungu ameona kwamba watanzania wana matatizo maana madawa na aina ya vyakula vinavyoingizwa nchini ni kiwango cha chini au tayari vimechakachuliwa, (expired) watu wanapata kansa kwa ajili ya uzembe wa watu kujipenda wenyewe na kupenda utajiri kupita kiasi.
Wengine wanapokea Rushwa wanapitisha madawa ambayo wanajua kwamba ni feki lakini kwa vile kuna percent hawajali. Watu wanadiliki hata kuchakachua maziwa ya watoto (S26, Lactogen etc).... nimeshuhudia watoto wanakunywa maziwa ambayo ni feki wanaharisha... Jamani hayo matendo yanayofanyika Mungu ameyaona na amekuja kupoza uonevu........

Pia Mungu ameona kwamba kuna watu wanaanzisha dini kwa ajili ya kutumia matatizo ya watu kujitajirisha hivyo sioni kwa nini watu wanakerwa na jambo jema wanashindwa kukemea mambo mabaya kabisa............................
 
Huo ni mtizamo wake na hata mimi simpingi sana maana Babu pia namuona 50/50 tusubiri tuone matokeo ya uponyaji wake mwaka huu; kama anadanganya kwa jina lolote...Mungu au Shetani? tutajua karibuni. Mashaka yangu yalikuja niliposikia hataki kumtaja YESU katika uponyaji wake?????? Kama amestaafu akimtaja Yesu mbona sasa asimtaje, we christian are proud of JESUS what happens to him? ni mtizamo tu ukweli mwenyezi Mungu atauonyesha.... then we'll praise kikombe or curse it in future! Mimi yangu masikio
 
Hakuna lolote zaidi ya wivu.Tangu lini shetani akafanya kazi ya uponyaji ?.
 
Hakuna lolote zaidi ya wivu.Tangu lini shetani akafanya kazi ya uponyaji ?.

he he he heeeeeeeeeee,

mwenzetu uko wapi? mbona anafanya kila siku?

tumeaswa hivi: amka wewe usinziaye, ufufuke katika wafu na Bwana atakuangaza.

Glory to God
 
Kweli sikio la kufa halisikii dawa.Jamani babu hakufunuliwa na mungu. nina ushaidi wa watu watatu kufariki baada ya kutoka loliondo.Walikwenda kupata kupata kikombe waliporudi hali ilizidi kuwa mbaya,sukari ikazidi kupanda na presha juu hatimaye wamekufa.

wanayemsikiliza huyo nabii muongo shauri yao!

Suala la kufa kuna sababu nyingi sana mkuu, kama wewe moyo na roho yako vinakwambia babu ni washetani, usiende, ila kama lah! nenda. wewe kina kuuma nini? na kama ni hvyo kwani kuna dini ngapi duniani, hizo zote ziko sahihi according to wewe? kama hapana, bsi achana na babu. Wababu ni wale wanaomkubali babu. kaangalie movie moja inaitwa TEN COMMANDMENTS, kuna kizee kimoja kilikuwa na hoja za ajabu sana za kumpinga Musa, ili wana wa islael warudi misri baada ya kutolewa utumwani huko Misri, hoja zake zinafanana na zako. Kwa hyo sikushangai mkuu, watu kama wewe walikuwa tangu enzi za Mussa.
 
Karibu chai kwanza, lakini jee umenawa mikono yako? Ukinywa bila kunawa utaugua halafu uchanganyikiwa uanze kuandika upupu kama huu
 
Huo ni mtizamo wake na hata mimi simpingi sana maana Babu pia namuona 50/50 tusubiri tuone matokeo ya uponyaji wake mwaka huu; kama anadanganya kwa jina lolote...Mungu au Shetani? tutajua karibuni. Mashaka yangu yalikuja niliposikia hataki kumtaja YESU katika uponyaji wake?????? Kama amestaafu akimtaja Yesu mbona sasa asimtaje, we christian are proud of JESUS what happens to him? ni mtizamo tu ukweli mwenyezi Mungu atauonyesha.... then we'll praise kikombe or curse it in future! Mimi yangu masikio

Nashukuru na wewe unaona kama ninavyoona, cha msingi hapa, ni maombi tu, Anga la Loliondo lizungukwe na nguvu za Mungu. Halafu Uwepo wa Mungu utafanya kazi sawasawa. Wakati ni mzuri sana, kwenye mambo kama haya. Hapa Mungu naye anataka kuona, ni namna gani amejibakishia waombaji wachache kwenye anga la Tanzania. Tusilaumu, Tusitukane, Tusigombane. TUOMBE KWA IMANI. Hakuna cha kumzuia Bwana kuokoa, iwe kwa wingi au kwa uchache.
 
binadamu ndivyo tulivyo ,yaani babu anaponyesha wewe unasema nguvu za giza ,ila wale wanaombewa makanisani na kutoa mamilioni ya feza unona ndio wanamungu,,mambo ya imani ni magumu sana huwezi kuyahoji kwa hoja wala uchunguzi wa kisayansi,yanatakiwa kuachwa kama yalivyo ,, "u cant question one's faith its a dogma"
 
Sio kweli kwamba Babu wa Loliondo ametumwa na Mungu kutumia dawa hiyo kuwaponya watu. Huyo Babu ametumwa na "mungu wa dunia hii(shetani) ili kuwadanganya watu waache kumtumaini na kumwamini Mungu wa kweli ili hatimaye waangamie siku ile ya mwisho. Soma 2 Wakorintho 4:4 na kisha tafakari kwa makini hoja zifuatazo utathibitisha ukweli huo.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu. Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Jamani Watanzania "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo"
Siri imefichuka! Hoja hizo na maandiko hayo ya Biblia yanathibitisha wazi kwamba huyo Babu hajatumwa na Mungu. Ila ni shetani anamtumia kuwadanganya watu. Tusikubali kudanganywa. Hata waganga na wachawi wa leo na wao huwaambia wateja wao kwamba wanaponya au kufanya miujiza kwa uweza wa mungu. I dare to talk openly Huyo mungu wanayemtaja ni mungu wa dunia hii (shetani). Mwenye masikio na asikie.

Sijajua umri wako lakini nafikiri wewe utakuwa mtoto, kwa maana mambo uliyoandika hayana kichwa wala mkia. Hivi kwa akili yako unataka utuambie shetani alishawahi kuumba mti au mzizi au kitu chochote chini ya jua? wewe kama ni mlokole basi ni wale ambao ni walokole waliofurika ushamba wa kujua neno la mungu.Kuna visa vingi sana ambavyo ukisoma biblia utakumbana navyo ambavyo kama utatafsiri maandiko hayo kwa tafsiri zako ulizotafsiri kwa babu basi hata bwana yesu utamweka kwenye upande babu wa loliondo.

Kwa mfano kuna wakati yesu alifinyanga tope ili kumponya kipofu kwa hilo tu hebu niambie kulikuwa na sababu gani kwa yesu kufinyanga tope wakati watu wote tunajua uwezo alionao?

kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha aliwaambia watu wajaze mabalasi maji ndiyo ayaombee, kwanini asitamke neno mabalasi yakajaa maji bila kusumbua watu kuchota maji na kuwa divai?

kwenye kisa cha musa na farao, waganga walifanya mazingaombe na kutokea nyoka, musa aliamriwa na mungu atupe fimbo yake chini ambayo nayo iligeuka nyoka na kuwala nyoka wa washirikina wa farao, hebu niambie kwanini musa asitamke neno tu mpaka atumie vitu halisi (fimbo)

Yesu alipowakuta wakina Petro wamekosa samaki kwenye shughuli zao za uvuvi aliwaambia warudi wakavue na kushusha nyavu zao kilindini. kama wewe ni wakiroho sana tuambie kulikuwa na sababu gani ya kuwasumbua wavuvi hao ambao walikuwa wamechoka? si angetamka tu neno samaki wakatokea na kujaa chomboni?

sidhani kama kuna sababu za kumhusisha babu na shetani kwani shetani kazi yake kubwa ni kuharibu sio kutengeneza. Wewe ndiyo agenti wa shetani maana inaonyesha unadhani shetani hutumia mitishamba na mungu hutumia miujiza katika uponyaji, hebu tuambie ni wapi kwenye biblia imeandikwa dawa za mitishamba zinauhusiano na mambo ya kishirikina?

wakati wa Yesu hakukuwa na hospitali na dawa kama panadol kwa hiyo watu walikuwa wanategemea nguvu za maombi tu sio pamoja na mitishamba?

Usia wangu wa bure kwako ni kuwa usiwe na mawazo finyu katika imani, Mungu hana mipaka duniani na mbinguni.
 
Kuna watu wameumizwa sana na kazi ya Babu. Hata vipindi vyao vya kwenye vyombo vya habari watu wanaviangalia kama vya tamthilia na wakati mwinginne ku grrreee na kuhama. Babu "katumwa" kutibu wana wa Adamu bila ubaguzi. Akija na bango la Yesu wana Adamu wengine watibiwe na nani. Magonjwa huletwa na shetani na Mungu hutibu na kuwapa uhuru wana wa Adamu. Leo iweje shetani aanze kutibu wakati kazi yake ni kuleta magonjwa na kifo??. Hao wanaotumia Biblia kuwapora watu mamilioni ya hela bila kuwaponesha au kufanya usanii wa kukusanya "vilema na kujifanya wamewaponya" kwa fedha nyingi ndio wanaomtumikia shetani ili wana wa Adamu waendelee kuteseka. Watu kama kina "safari-bia " wanasema serikali imeshindwa ndo maana watu wote wanakimbilia kwa Babu. Kwani Yesu alipoponya watu Serikali ya kirumi ilikuwa imeshindwa kazi. Yesu mbona alisema ya Kaisari mwachie Kaisari na ya Mungu yawe ya Mungu. Kina ""safari-bia" wasiiteke hali hii kuufufua umaarufu. Mifano inayotolewa katika Biblia inaweza kuwa michache kwa sababu ya nafasi lakini Yesu yumkini alitibu watu wengi. Mfano mdogo ni kule kulisha halaiki ya watu kutumia mikate na vipande vya samaki visivyozidi 5. Wanaoendesha Serikali ni watu na wana Adamu nao. NENDA AU ACHA!!!
 
Naomba nikujibu hoja zako kama ifuatavyo:
- Huyo babu anatumiwa tu na shetani. Nguvu za giza zikiondoka ndani yake atakuwa mtu "normal" tena atashangaa kwanini alikuwa anapoteza muda wake kugawa vikombe. * Tunachofanya sasa ni kupambana na roho hiyo inayotenda kazi ndani ya babu. Na hiyo roho ya shetani itashindwa tu kwa Jina la Yesu. Time will tell.
- Agizo la kuponya liliishatolewa na Yesu mara moja(Mathayo 10:1) na halitarudiwa kutolewa tena kwa ndoto wala kwa maono. Na agizo hilo ni la kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Mungu hana kigeugeu(Malaki 3:6) Aliyesema ponyeni magonjwa yote hawezi leo kubadilisha kauli yake na kusema ponya magonjwa manne tu. HA-TU-DA-NGA-NYI-KI!!
- Agizo la kuponya linaenda sambamba na agizo la kuhubiri Injili(na kuanzisha makanisa - Marko 16:15-18). Anayesema ametumwa kuponya tu, Mungu amsamehe kwa kuwa hajui alisemalo wala alitendalo.
- Yesu aliwaambia waliopona ukoma waende wakajionyeshe kwa makuhani. Hao waliopona kwa babu nao waende wakajionyeshe kwa madaktari(wapimwe) na ukweli ujulikane maana Waongo ni wengi na wachakachuaji ni wengi.
- Wanaosema watu wanapona kwa babu kwa imani hawajui hata maandiko yanasema nini juu ya imani. Imani huja kwa kulisikia Neno la Kristo(Warumi 10:17). Kama babu anataka tuamini anachokisema, ni lazima ahubiri Neno la Kristo. Watumishi wa Mungu(Mitume: Paulo, Petro...walihubiri Injili na kuwaombea watu). walifanya yote. Yesu alihubiri Injili na kuponya. Alifanya yote. Waganga wa kienyeji ndio wanaofanya moja tu "kuponya" na uponyaji wao ni feki. Shetani ataumbuka tu. Roho Mtakatifu yupo kazini kutujulisha kweli yote nayo kweli itatuweka huru.

Kimsingi hapa tunaelimishana kwa hoja, inawezekana kweli tumepotea au vinginevyo

  1. Babu ni mchungaji mstaafu. ni muhubiri wa neno la Mungu kupitia kanisa la KKKT, Tunataka afungue kanisa lake binafsi kama ilivyo wakina Mwingira na Kakobe? then aponye watu bure lakini awe anakusanya sadaka ambazo hatujui ni kiasi gani and for sure huwa watu wanatoa zaidi ya 500 kwa siku.
  2. Watu waliopona kwa babu naamini ni wengi, ila ni vigumu kuthibitisha kwa kuwa hiyo ni personal case. Kungekuwa na forum au organisation ya wagonjwa wa ugonjwa fulani ingekuwa rahisi kuthibitisha hilo. Kwa hiyo hata kama mimi nitakuambia nimepona kisukari, huwezi kuamini kwa sababu kwanza hujui kama nilikuwa naumwa kiasi gani. Kinachowezekana ni kwa serikali au NGO fulani kuanzisha mpango wa kudhibitisha tiba kupitia kwa wagonjwa waliopona. Lakini kwa hali ilivyo sasa mimi naenda kupimia mbeya, wewe Arusha, mwingine anaenda kupimia zahanati fulani ipo kigoma au bukoba nani atakeye weza kukusanya hizo data kama si serikali au taasisi fulani? Au tunataka babu aanze kazi ya kukusanya hizo data?
  3. Katika imani, hatuamini babu ndio anaponya bali ni Mungu ndo anaponya kupitia kwa huyo mtumishi aliye mchagua. Tukumbuke mtume paulo alikuwa mpinga Kristu lakini Yesu akaamua kumtumia kutangaza neno lake. Hivyo kama Mungu kaamua kumtumia babu kuponya na tunajua babu hamkatazi mtu kuendelea na ukristu wake tabu iko wapi? Au watu wakishapona wanakuwa hawaji tena makanisani kwetu kuendelea na ibada? Kama ndivyo basi hilo si tatizo la babu bali ni la makanisa kutumia udhaifu wa watu kwenye magonjwa yao ili kuendelea nao
 
Mediamen anaelewa biblia kinyume,unajua hata dini ya shetani wana biblia yao?
-Hivi Musa alivyotumwa kuwaokoa waisreli janwani alikubali kirahisi? kule alikokwenda kuchunga kondoo alikwenda kutafuta nini huko.
- Hivi hiyo sadaka ianyopikelewa huko kanisani kwenu inafanya kazi gani.jibu unalo hivi mkiwaombea watu kwa kutumia neno wakipona na wakitoa sadaka yao ikawa kubwa mnairudisha?mbona babu karudisha mamilioni na anataka 500 tu kwa imani kuwa inamtosha na huduma yake ni endelevu vinginevyo atakuwa anajitafutia utajirisho.
-Angalia TV uone ushuhuda wa watu waliopona usituletee hadithi.
-Soma kitabu chote cha ufunuo wa Yohana ukielewe siyo kutukatia mstari unaoupenda wewe.
-Kwa waliokwenda kwa Babu ametoa ushuhuda kuwa Alfajiri watu wanakula neno la nguvu kutoka biblia ndiyo huduma inaendelea na ukumbuke babu ni mtumishi wa mungu tena msomi wa biblia miaka 5 siyo wale wa miezi 3 halafu wanajiita wachungaji.
Neda Loliondo ukapate la kutuambia siyo kusikia unatuletea falsafa zilizokufa huku JF.
-
"Wanakula Neno la nguvu kutoka kwa mchungaji mstaafu!" Mwapotea kwakuwa hamyajui maandiko. Unastaafu ndio unaanza kutoa Neno la nguvu?! Ni wapi katika Biblia palipoandikwa watumishi wa Mungu wa kweli walistaafu? Shetani ataumbuka tu safari hii. Hana ujanja. Roho Mtakatifu yupo kazini.
 
Suala la kufa kuna sababu nyingi sana mkuu, kama wewe moyo na roho yako vinakwambia babu ni washetani, usiende, ila kama lah! nenda. wewe kina kuuma nini? na kama ni hvyo kwani kuna dini ngapi duniani, hizo zote ziko sahihi according to wewe? kama hapana, bsi achana na babu. Wababu ni wale wanaomkubali babu. kaangalie movie moja inaitwa TEN COMMANDMENTS, kuna kizee kimoja kilikuwa na hoja za ajabu sana za kumpinga Musa, ili wana wa islael warudi misri baada ya kutolewa utumwani huko Misri, hoja zake zinafanana na zako. Kwa hyo sikushangai mkuu, watu kama wewe walikuwa tangu enzi za Mussa.
Wewee, fumbuka! Unaangalia movie ndio unaleta masimulizi yake humu? Hizo movie ni "maigizo". Soma historia ya video camera ndio utajua wakati wa Musa hapakuwepo cameramen. Taja mistari ya Biblia kuthibitisha hoja zako. Sio movie!
 
Back
Top Bottom