Watanzania wamejaa matatizo, hivyo yoyote wa kuwapa matumaini, watamfuata kama watu walivyomfuata Yesu, Babu wa Loliondo. Sasa Mwamposa na Makonda

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,028
144,382
Ukiacha matatizo ya kiafya(magonjwa, n.k), watanzania wana matatizo mengi huku wakiwa wamepoteza matumaini ya matatizo yao kutatuliwa na mfumo huu mbovu wa kiutawala tulionao. hivyo, yoyote wa kuwapa matumaini, watamfuata mradi tu awe na mamlaka na zaidi awe na kipaji cha kuigiza mbele ya hadhara kubwa ya watu huku akionyesha kuwapa matumaini.

Hii ndio hulka ya Binadamu kama ilivyokuwa wakati wa Yesu kwa watu kumfuata Yesu awatatulie matatizo yao ambayo walikuwa wameshayakatia tamaa.

Nimetolea mfano wa Yesu kukumbusha na jinsi gani Mwanadamu aliekata tamaa anaweza kumfuata Mwanadamu mwenzake na hata kuwa mfuasi mradi tu awe na imani juu ya huyo mtu au akijua mtu huyo ana madaraka na hivyo anaweza kuyatumia kumsaidia hasa mtu huyo anapotumia style ya kukusanya watu na kuahidi kutatua matatizo yao.

Ukiwa na madaraka, unahitaji kipaji cha kuigiza mbele ya makundi makubwa ya watu, huku kwenye maswala ya kiimani, unachohitaji na kufanya watu wakuamini kuwa wewe ni Nabii basi kazi unakuwa umeimaliza/

Hata kwa waganga wa kienyeji hali ni hio hio hasa kwa watu ambao changamoto walizonazo katika maisha, hazina suluhiso mfano maradhi yasiyotibika, n.k.

Babu wa Loliondo watu walimfuata kwa misingi hiyo hiyo na hata Mwamposa leo watu wanamfuata kwa misingi hiyo hiyo ya kupatiwa majawabu ya matatizo waliyonayo katika maisha ikiwemo pia kutimiza ndoto zao au matamanio yao.

Wanaomfuata Makonda ni wahanga waliokataa tamaa wa huu mfumo mbovu wa kiutawala na usiowajibika. Hivyo, kupitia Makonda, wanaamini Makonda anaweza kuwasaidia, ila nachoweza kuwaambia watu hawa ni kuwa, majibu yao watayapata baada ya muda wa maigizo kuisha.

Makonda atamaliza ziara yake, lakini sio kero za watanzania kwasababu anahangaika na matotizo na sio chanzo cha matatizo ya watanzania.

Pia, msisahau kuna uchaguzi wa serikali za mitaa hivi karibuni na uchaguzi mkuu mwakani.
 
Ni kweli kabisa. Je tatizo ni shida walizo nazo au ni ukosefu wa elimu na maarifa
Ni ujinga tu unaochagizwa na watu kukata tamaa. Makando, kama alivyokuwa Magufuli, anahangaika na individuals badala ya mifumo inayazalisha, kulinda na kulea individual wazembe na wasiowajibika huku wananchi wakiteseka.

Kuna wakati Makonda analalamikia wanasiasa(viongozi wa kuchaguliwa), lakini sijamsikia akipendekeza au kulilia mfumo utaowawezesha wananchi kuwajibisha viongozi wa kuchaguliwa halafu watu bado wana imani Makonda ataleta suluhisho au anafaa kuwa kiongozi mkubwa.

We are so stupid!!
 
Ukiacha matatizo ya kiafya(magonjwa, n.k), watanzania wana matatizo mengi huku wakiwa wamepoteza matumaini ya matatizo yao kutatuliwa na mfumo huu mbovu wa kiutawala tulionao. hivyo, yoyote wa kuwapa matumaini, watamfuata mradi tu awe na mamlaka na zaidi awe na kipaji cha kuigiza mbele ya hadhara kubwa ya watu huku akionyesha kuwapa matumaini.

Hii ndio hulka ya Binadamu kama ilivyokuwa wakati wa Yesu kwa watu kumfuata Yesu awatatulie matatizo yao ambayo walikuwa wameshayakatia tamaa.

Nimetolea mfano wa Yesu kukumbusha na jinsi gani Mwanadamu aliekata tamaa anaweza kumfuata Mwanadamu mwenzake na hata kuwa mfuasi mradi tu awe na imani juu ya huyo mtu au akijua mtu huyo ana madaraka na hivyo anaweza kuyatumia kumsaidia hasa mtu huyo anapotumia style ya kukusanya watu na kuahidi kutatua matatizo yao.

Ukiwa na madaraka, unahitaji kipaji cha kuigiza mbele ya makundi makubwa ya watu, huku kwenye maswala ya kiimani, unachohitaji na kufanya watu wakuamini kuwa wewe ni Nabii basi kazi unakuwa umeimaliza/

Hata kwa waganga wa kienyeji hali ni hio hio hasa kwa watu ambao changamoto walizonazo katika maisha, hazina suluhiso mfano maradhi yasiyotibika, n.k.

Babu wa Loliondo watu walimfuata kwa misingi hiyo hiyo na hata Mwamposa leo watu wanamfuata kwa misingi hiyo hiyo ya kupatiwa majawabu ya matatizo waliyonayo katika maisha ikiwemo pia kutimiza ndoto zao au matamanio yao.

Wanaomfuata Makonda ni wahanga waliokataa tamaa wa huu mfumo mbovu wa kiutawala na usiowajibika. Hivyo, kupitia Makonda, wanaamini Makonda anaweza kuwasaidia, ila nachoweza kuwaambia watu hawa ni kuwa, majibu yao watayapata baada ya muda wa maigizo kuisha.
📌📌
 
Ni ujinga tu unaochagizwa na watu kukata tamaa. Makando, kama alivyokuwa Magufuli, anahangaika na individuals badala ya mifumo inayazalisha, kulinda na kulea individual wazembe na wasiowajibika huku wananchi wakiteseka.
Mifumo ndio haipo vizuri..
 
Sio hao tu hata shetan akija leo hii akatangaza kutoa msaada/solution kwa matatizo ya watu by 100% hata angalau 80% nina uhakika 98% ya watu watamfuata na kumsujudu,

kama watu wanaamini ushirikina na waganga wa kishirikina ili kusolve mambo yao ilihali dini zimeshindwa kuwasaidia na zinawakataza kujihusisha na ushirikina, lakn watu hawatii wanafuata njia inayowaokoa na sio porojo na stories za kuwachosha na kuwapa matumaini hewa, hapo suala ni watu kupata solution ya changamoto zao bila kujali ni nani anawasaidia hayo mtajua wenyewe.

Uraiani kuna changamoto nyingi sana zinazowafanya watu watumie njia yoyote kutatua changamoto zao, anapotokea mtu wa kuwatatulia changamoto zao hiyo kwao ni BAHATI, haijalishi huyo mtu ni muovu kiasi gani hayo watu hayawahusu, wao wanakwenda na ule usemi wa kufuata maneno yako na sio matendo yako.

Tuache kuhukumu tunajitesa bure.
 
Nimekuelewa.

Ili kuielewa hii pointi yako, mtu lazima awe na fikra huru, atoke nje ya koti la kiitikadi alilovaa ili aweze kuona mambo kwa mapana yake.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mleta mada umeanza vizuri kuanzia title, lakini baadae umenishangaza kabisa pale ulipoweka mpaka mfano wa Yesu Kristu kuwaponya wagonjwa, halafu ajabu unaita yale yalikuwa maigizo.

Hujui hata kule kwa Mwamposa wapo wanaoponywa kweli kwa imani zao? hata kwa waganga wa kienyeji pia...

Ajabu hawa wanaoponywa kwenu mnawaita wajinga, na ili wawe na werevu, kwenu basi wachague njia ya kubaki na matatizo yao mpaka ile siku mifumo ya nchi itakapoanza kufanya kazi!.

Halafu hii idea ya kuita wengine wajinga mnaigiliziana karibia wote, mmoja anabeba kosa la mwingine kama kondoo, mpaka siku mtoke nje ya makoti ya kiitakadi mliyovaa ndio mtaelewa mambo.

Kwa sasa endeleeni kuita maigizo kile anachofanya Makonda, kama mnavyoamini hata kwa Yesu pia yalikuwa maigizo. Hiki mnachoonesha hapa ni kutoheshimu shida za watanzania, mmekaa kibinafsi zaidi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ukiacha matatizo ya kiafya(magonjwa, n.k), watanzania wana matatizo mengi huku wakiwa wamepoteza matumaini ya matatizo yao kutatuliwa na mfumo huu mbovu wa kiutawala tulionao. hivyo, yoyote wa kuwapa matumaini, watamfuata mradi tu awe na mamlaka na zaidi awe na kipaji cha kuigiza mbele ya hadhara kubwa ya watu huku akionyesha kuwapa matumaini.

Hii ndio hulka ya Binadamu kama ilivyokuwa wakati wa Yesu kwa watu kumfuata Yesu awatatulie matatizo yao ambayo walikuwa wameshayakatia tamaa.

Nimetolea mfano wa Yesu kukumbusha na jinsi gani Mwanadamu aliekata tamaa anaweza kumfuata Mwanadamu mwenzake na hata kuwa mfuasi mradi tu awe na imani juu ya huyo mtu au akijua mtu huyo ana madaraka na hivyo anaweza kuyatumia kumsaidia hasa mtu huyo anapotumia style ya kukusanya watu na kuahidi kutatua matatizo yao.

Ukiwa na madaraka, unahitaji kipaji cha kuigiza mbele ya makundi makubwa ya watu, huku kwenye maswala ya kiimani, unachohitaji na kufanya watu wakuamini kuwa wewe ni Nabii basi kazi unakuwa umeimaliza/

Hata kwa waganga wa kienyeji hali ni hio hio hasa kwa watu ambao changamoto walizonazo katika maisha, hazina suluhiso mfano maradhi yasiyotibika, n.k.

Babu wa Loliondo watu walimfuata kwa misingi hiyo hiyo na hata Mwamposa leo watu wanamfuata kwa misingi hiyo hiyo ya kupatiwa majawabu ya matatizo waliyonayo katika maisha ikiwemo pia kutimiza ndoto zao au matamanio yao.

Wanaomfuata Makonda ni wahanga waliokataa tamaa wa huu mfumo mbovu wa kiutawala na usiowajibika. Hivyo, kupitia Makonda, wanaamini Makonda anaweza kuwasaidia, ila nachoweza kuwaambia watu hawa ni kuwa, majibu yao watayapata baada ya muda wa maigizo kuisha.

Makonda atamaliza ziara yake, lakini sio kero za watanzania kwasababu anahangaika na matotizo na sio chanzo cha matatizo ya watanzania.

Pia, msisahau kuna uchaguzi wa serikali za mitaa hivi karibuni na uchaguzi mkuu mwakani.
Makonda atamaliza ziara yake, lakini sio kero za watanzania kwasababu anahangaika na matotizo na sio chanzo cha matatizo ya watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada umeanza vizuri kuanzia title, lakini baadae umenishangaza kabisa pale ulipoweka mpaka mfano wa Yesu Kristu kuwaponya wagonjwa, halafu ajabu unaita yale yalikuwa maigizo.

Hujui hata kule kwa Mwamposa wapo wanaoponywa kweli kwa imani zao? hata kwa waganga wa kienyeji pia...

Ajabu hawa wanaoponywa kwenu mnawaita wajinga, ili wawe na werevu kwenu basi wachague njia ya kubaki na matatizo yao mpaka ile siku mifumo ya nchi itakapoanza kufanya kazi!.

Halafu hii idea ya kuita wengine wajinga mnaigiliziana karibia wote, mmoja anabeba kosa la mwingine kama kondoo, mpaka siku mtoke nje ya makoti ya kiitakadi mliyovaa ndio mtaelewa mambo.

Kwa sasa endeleeni kuita maigizo kile anachofanya Makonda, kama mnavyoamini hata kwa Yesu pia yalikuwa maigizo. Hiki mnachoonesha hapa ni kutoheshimu shida za watanzania, mmekaa kibinafsi zaidi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Makonda anafanya maigizo 100%, ni mkakati usiotoa suluhisho lolote kwa matatizo lukuki yanayoikabili jamii.
 
Wale wanaopata msaada wa Makonda kwenye hizo ziara wa matatizo yao yanayowakabili ndio mnawaita wajinga.

Nyie "werevu" mnataka wale wajinga waendelee kukumbatia matatizo yao mpaka siku mifumo ya nchi itakapoanza kufanya kazi, sijui kama mmewahi kuwa na matatizo mkahangaika nayo.. au mnaimba tu kuigiliziana kile wengine wanachosema.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Uwe una tofautisha mambo Mwamposa,Babu wa Loliondo na Makonda ni tofauti Makonda anatatua matatizo ya Watanzania yanasababishwa na Mafisadi,Mazembe,Malaghai,yanajipambanua yamesoma,Matapeli,yako kwenye ofisi za Umma lkn hayana uzalendo na utu kwà Watanzania wanyonge na maskini msijaribu kupunguza maumivu kwà kutuletea hàbari za Mwamposa na Babu wa Loliondo wanayopitia hawa Wananchi ni Makubwa tulioko huku mashambani tunaona
 
Wale wanaopata msaada wa Makonda kwenye hizo ziara wa matatizo yao yanayowakabili ndio mnawaita wajinga.

Nyie "werevu" mnataka wale wajinga waendelee kukumbatia matatizo yao mpaka siku mifumo ya nchi itakapoanza kufanya kazi, sijui kama mmewahi kuwa na matatizo mkahangaika nayo.. au mnaimba tu kuigiliziana kile wengine wanachosema.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Nadhani hakuna mahali nimemuita mtu yeyote mjinga. Anachokifanya Makonda sio suluhisho la hayo matatizo, bali ni kutafuta umaarufu wa kisiasa tu. Makonda anajua kuna tatizo kubwa sana kwenye mifumo yetu ya utendaji serikalini, anajua kuwa hao wananchi wachache anaotaka kuonekana anawasaidia hakutakuwa na impact yeyote kama mifumo haitawekwa na kusimamiwa vizuri.
Makonda anajua kuwa baada ya ziara yake hiyo mambo yataendelea kama kawaida, na hao watendaji kwa sasa wanamchora tu na hayo maigizo yake ya kitoto kabisa. Anajua wananchi wana matatizo lukuki na ameamua kuwafanya watoto kwa manufaa yake. Kwa hili SSH amefeli na atafeli sana.
 
Back
Top Bottom