Sioi Solomon Sumari kugombea Arumeru

hizi kelele zote ni woga wa CDM, mtu yeyote ana haki ya kugombea ubunge, mbona nyie mlipeana ubunge kindugu?Na wengi kupeana kimapenzi.
 
Jamni msililijua na kama usiku wa giza.A.Mashariki hakuna ufalme na hatushindani kwa vigezo hivyo.Yeyote anaweza kushinda so long ana vigezo
 
Mtoto wa marehemu jeremiah solomon sumary amechukua fomu ya ugombea ubunge kwa tiketi ya ccm . Kuna uwezakano mkubwa akapitishwa kuwa mgombea wa ccm kupambana na upinzani .


Mkwe wake atamsaidia
 
Tunakaribia kuipita Kenya kwa kurithishana vyeo na madaraka. Mfumo huu unaozidi kuimarika utatutesa sana. Mazingira wanayotengenezewa watoto wa vigogo ambao pia ndio mafisadi kuanzia shule, vyuo, ajira na biashara mbalimbali usipotazamwa upya basi.
 
Kwa mwendo unavyoenda ccm watashinda hili jimbo labda cdm wafanye kazi kubwa na wamuweke mtu ambaye anakubalika haswa .
 
mtei amrithisha mkwe wake mbowe uenyekiti wa chama
hii ina kuexpose namna ulivo tabula rasa hoja iliyo mbele yetu ni Arumeru na uteuzi wa mgombea kupitia ccm ya Mtei na Mbowe yanatoka wapi?? kwanza Mtei aliacha uenyekiti kwa Mzee Bob Makani na sio kwa mbowe na kama Mbowe ni mkwe wake ana uwezo, hata huyo mtoto wa sumari bado ana haki kikatiba kuchaguliwa pointi anaweza?? au njia ya kupata uteuzi itakuwa halali na haitatoa upendeleo hapo ndio pa kujadili..
 
hizi hulka za Lowassa kuhakikisha kila anayemjua anakula serikalini ndiyo zinatuogopesha kuliko hata ufisadi wake...anapenda sana ukubwa /ufalme falme anataka akina Bashe au Millya wawe wabunge EAC huku anataka mtu wake kule anataka mtu wake, kila mahali na kibaya zaidi watu wake wengi hawana uwezo wala uzoefu
 
UTAWALA WA KIFALME!
Hata kama taratibu za kisheria zote zimefuatwa, na fomu zimetolewa, ni ****** sana kumchagua mtoto anayetokea familia hizi kuongoza tena!...Wameru watakuwa wamerogwa na nani hawa?...Hakuna Vijana wengine wasomi Meru, wanaoumizwa na utawala wa Kifalme?
Si yupo yule kijana Joshua Naari ambaye nimeona hapa thread moja ikisema wameisha jipanga kumsaport!!! Usihofu mkuu zote hizi ni propoganda za wenzetu CCM kwani huwajui?????Wanajaribu kuwapaka rangi watu wao!!!

 
Tanzania ina rasilimali watu wengi sana wenye uwezo wa kuongoza jimbo hilo. Na hao watoto wa vigogo ni sehemu ya rasilimali hiyo. Lakini hatuwezi kuchagua mtu asiye na sifa tunazozihitaji eti kwa kuwa tu "NI MTOTO WA KIGOGO" na hatuwezi kuacha kumchagua mtu mwenye sifa zoote tunazozihitaji eti kwa sababu "NI MTOTO WA KIGOGO".

Cha msingi ni kuwepo kwa uwanja tambarare wa mapambano kwa watu wote, na tume iheshimu maamuzi ya watu wa Arumeru. Mimi sina Tatizo na watoto wa vigogo wanaojikongoja wenyewe, tatizo ni wale wanaotegemea nafasi za kubebwabebwa
Kasheshe ni wakati wa kuhesabu kura, ndipo wanapotaka kutumia ubabe, kama unakumbuka mbinu za EL Arusha mjini!!!!! Wana Arumeru wanatakiwa kujipanga ili kura zisiibiwe kuwe na matokeo ya haki!!!!

 
Kila mtu ana haki ya kuchukua fomu.
Kura za maoni ndio zitaamua mshindi,sio kama nyie kamati kuu 'ikipima'
OTIS
Mara ngapi maamuzi ya kura za maoni yalibatilishwa?? Kiukweli hako ka chama kana wenyewe hakuna cha kura kuamua kama unavyotaka kutusadikisha hapa..
 
Nasari kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo yupo on line kwa mapambano tena na huu uongozi wa kuridhishana nafsi yangu inaikataa sana na cjui hw mafisadi wanafikiri bado tupo kwenye karne ya 10 Mi cjui.

Na nafikiri hili litakuwa fundisho kwa hawa mafisadi wachumia matumbo yao!
 
kudadaedeki, siasa zinautamu wake jamani, naona wtu hawatoki huko, sasa huyu si aendelee tu nakazi za professional aliyoisomea?
 
Kuna wakati najiuliza hivi kama huyu SIOI kama angeamua kugombea kwa kupitia CDM, mtizamo wa watu si ungebadilika sana? Tunachotaka sisi akipitishwa asimame yeye kama yeye na si kutumia kivuli cha baba yake kama ilivyokuwa kwa V. Nyerere
 
Huo ni mtazamo wangu tu, kwani nadhani katika mazingira ya sasa, CCM inajaribu kuepuka mchakato wa kura za maoni katika chaguzi ndogo kwani kura za maoni kwa kawaida zinaambatana na gharama na vurugu nyingi zisizo za lazima.

So ccm by not having preferential votes to get their candidate is trying to avoid unnecessary costs? CCM is the GRAND OLD PARTY it should know that democracy is never cheap!! Anaefanya vurugu ni nani ; si hao ccm wenyewe na wanashindwa kuthibitiana kwavile hawana nidhamu!
 
Kama Marehemu Jeremia Sumari alikuwa ni kipenzi cha wana Arumeru, then, mtoto wake ndie atasimamishwa na CCM na ndiye atakayechaguliwa!. Huu ni ukweli mchungu, ila ndio ukweli halisi!.

Hizi siasa za kurithishana hazikuanza leo. Kwani Abedi Karume anajua siasa gani?. Kisiasa Abedi Karume, si lolote sii chochote zaidi ya jina la Baba yake (wa kufikia?). Dr. Husein Mwinyi ana siasa gani?, ni jina la baba!. Vita Kawawa ana siasa gani?, ni jina la baba na jimbo la baba!. Adam Malima ana siasa gani?, ni jina la baba na jimbo la baba! and the list goes on!.

2015, Ndesamburo hatagombea tena Moshi mjini, wala Mrema hatagombea Vunjo. Hawa wote ni vipenzi vya watu wa majimbo yao, hivyo yoyote watakayemshika kumnyanyua mkono, ndiye atakaye chaguliwa!.

CCM italazimika kumpitisha Sioi sio kwasababu ndio inampenda sana, no!, itampitisha ili kujiokoa vinginevyo jimbo linakwenda Chadema!.
 
Back
Top Bottom