Shule aliyosoma Mkapa yafungwa kwasababu ya udini (waislam vs wakristu) ni kasheshe!

Status
Not open for further replies.
Jamani tunaelekea wapi waTanzania? Nakumbuka wakati nasoma Kibaha Secondary miaka ya 80 waislamu walikuwa wana sehemu yao maalum ya kuabudu na wapo waliokuwa wakipiga sala 5 bila ya matatizo yoyote. Pia kwa waliopita Tosamaganga watakumbuka kuwa kuna kanisa eneo la shule lakini sikupata kusikia waislamu wakidai nao wajengewe msikiti wao. Walikuwa wakifanya ibada zao kwenye vyumba vya madarasa bila ya matatizo yoyote.

Hao vijana wa Ndanda Secondary wameshindwa kutumia chumba kimoja cha darasa kama sehemu ya kuswalia? Mimi nadhani walitaka kugoma tu so the looked for a reason to do so. What a pity!!!
 
Hivi hawa watoto laiti wangejua jinsi gani tunavyopata shida ya kutafuta pesa kwa ajili yao halafu wanakwenda shule kuleta ujinga badala ya kusoma wanakera sana. Wanajua fika hiyo ilikuwa ni shule ya mission na ilijengwa na wakatoliki wanachotaka ni elimu ama msikiti????

Kama wanakwenda kusoma wakae wasome na kama wanafuata miskiti na makanisa basi warudishwe wakashindi miskitini na makanisani waaache wale wanaohitaji kusoma.

Wazazi tunajinyima sababu yao wapate elimu kwa manufaa yao wanaleta upuzi walimu fanyeni kazi yenu charaza wote bakora inaumma sana kwakweli kama kunaninaye mkwaza anisamehee ila sipedi migomo ya kijinga :embarassed2:

Mhhh jamani nimesoma Pugu High School ambapo ni Makao Makuu ya Roman Catholic Dayosisi ya Pwani, lakini tulikuwa na chumba cha kusalia, na mara baada ya idadi yawanafunzi wa kiislamu kuongezeka tukapewa eneo la kujenga Mosque.Kwa nini iliwezekana Pugu ishindikane Ndanda??? Kumbuka kwa kijana wa kiislamu kusoma kwake ni sehemu ya Ibada kama ilivyo kusali. Na iwapo kimoja kikikosekana basi unakuwa umemlazimisha afanye ibada yake nusunusu. Ushauri wangu kwa mkuu wa shule Ndanda, please hebu wape sehemu japo wafunge makuti waweze kumsujudia mola wao.
 
Unavyosomeka wewe unaweza kudai nyumbani kwako haki ya ubaba iwe kwa zamu, leo wewe, wiki ijayo zamu ya mwanao mkubwa, baada ya wiki jirani yako umezeeka kweli we mzee
I love JF... Na siku zamu itakaponifikia ndiyo utakuwa mwisho wa zamu...
 
Mhhh jamani nimesoma Pugu High School ambapo ni Makao Makuu ya Roman Catholic Dayosisi ya Pwani, lakini tulikuwa na chumba cha kusalia, na mara baada ya idadi yawanafunzi wa kiislamu kuongezeka tukapewa eneo la kujenga Mosque.Kwa nini iliwezekana Pugu ishindikane Ndanda??? Kumbuka kwa kijana wa kiislamu kusoma kwake ni sehemu ya Ibada kama ilivyo kusali. Na iwapo kimoja kikikosekana basi unakuwa umemlazimisha afanye ibada yake nusunusu. Ushauri wangu kwa mkuu wa shule Ndanda, please hebu wape sehemu japo wafunge makuti waweze kumsujudia mola wao.

Kwa hiyo kila Ofisi ya Serikali iliyo na Waislamu ijengewe msikiti? Kweli itakuwa ni sumu mbaya sana kuingiza mambo ya kidini kwenye Katiba mpya ijayo!
 
Hawa watoto nao wasisumbue watu kama hurudhiki na yaliyopo shuleni hapo si pata uhamisho ukaende kwenye shule itakayokidhi mahitaji yako. Fukuza wote wanaohusika na sakata zima wasituletee upumbavu wao. Hiyo ni shule jamani sio msikiti wala kanisa bana!
 
mmmmmhh,tunaelekea kubaya sana uongozi wa shule tena high school unapandikizwa chuki za kidini where are we going?
 
mimi sijaona kosa hao watoto kudai usawa! mara ngapi humu JF ikiwekwa list ya viongozi yakizini majina ya waislamu 3 mnaanza kuhoiji udini.!!

sasa hapo shuleni kama kaka mkuu na viranja wote wakristo! sijui kama kutakuwa na usawa wowote! vijana walikuwa na kila haki ya kugoma..
 
Kwa iyo na sisi wakristu tuandamane kwa kuwa RAISI NA MAKAMU WAKE WAISLAMU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Huo mfano wakiuelewa nadhani watajiona wapumbavu sana.
Ivi HP akiwa mwisalamu au mkristu ina impact yoyote kwenye accademic?
JK ndo anapaswa kutupiwa ilo zigo maana ndo analielewa zaidi
 
Wangetokea watu mia nane wenye ufikiri mbovu kama wako basi dini flani ingeandamana kumpinga JK na makamu wake hapa TZ.
 
Kwa iyo na sisi wakristu tuandamane kwa kuwa RAISI NA MAKAMU WAKE WAISLAMU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Huo mfano wakiuelewa nadhani watajiona wapumbavu sana.
Ivi HP akiwa mwisalamu au mkristu ina impact yoyote kwenye accademic?
JK ndo anapaswa kutupiwa ilo zigo maana ndo analielewa zaidi
Nadhani akili zao zinawaza advantages kwenye line ya msosi(top layer), maana kwa kula wale!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom