Waumini wa Msikiti wa Ijumaa Mwanza wamvaa Bim na nduguye Sheraly kuhusu shule ya Thaqafa na Msikiti wa Ijumaa

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
MAJIBU YA WAUMINI WA MSIKITI WA IJUMAA KWA UPOTOSHAJI WA BIM NA NDUGUYE SHERALY
KUHUSU SHULE THAQAFA NA MSIKITI WA IJUMAA

Assalam alaykumu.

Ndugu waislamu
Wa Mwanza na waTanzania

Waumini wa msikiti wa ijumaa imetulazimu kuunda kamati maalumu ya watu wachache ili kuwaelimisha waislamu dhidi ya propaganda zozote zinazohusu msikiti wetu na uislamu kwa ujumla.

Tumeamua kufanya hivi baada ya kuona kuna watu wasiokitakia mema uislamu baada ya kuona maslahi yao hayapatikani tena kupitia msikiti wa Ijumaa au shule ya thaqafa hapa mwanza.

Ndugu waislamu tunaomba tuwafahamishe kwamba huyo BIM na ndugu yake Sheraly ambao
Ni mtu na kaka yake hivi karibuni wametumia mitandao ya kijamii kutoa shutuma nyingi na kumshambulia Imamu wetu Sheikh Hamza Mansur pasina ulazima wa kufanya hivyo.

Aidha ndugu BIM ametoa shutuma nyingi za uongo na kashfa dhidi ya kiongozi wa shule Alhaji Maruzuku Magongo huku akijua wazi anawadanganya na kuwapotosha waislamu.

Ndugu BIM amemtaka Imamu wetu athibitishe kwamba shule ya Thaqafa ni shule ya waislamu.

Kamati yetu ya waumini wa msikiti wa Ijumaa Mwanza imeamua kumjibu yeye BIM Hussen kaka yake Sherrally Hussen
na mwingine yeyote atakayejitokeza kuzungumzia mambo ya msikiti wa Ijumaa na Shule ya Thaqaafa kwenye mitandao.

Licha ya kumjibu Ndugu BIM lakini kamati yetu imeamua kusahihisha upotoshaji mkubwa uliofanywa na Ndugu BIM kuwapotosha waislamu katika mazungumzo yake.

KABLA YA YOTE KAMATI INGEPENDA KUWAFAHSMISHA WAISLAMU KWA UFUPI.

Msikiti wa Ijumaa Mwanza sasa upo chini ya uendeshwaji na usimamizi wa kamati ya mpito inayoongozwa na Sheikh Aman Mahuba ..Kamati iliiundwa kwa kuchaguliwa na Waumin na wamo kwawakilishi kutoka pande zote za waumini,bodi ya zamani,serikali na Bakwata.

Kamati hii imeundwa kwa usimamizi wa RITA na vyombo vingine muhimu ikwemo Bakwata ili kuleta utulivu na kuendeleza shughuli zote za msikiti wa Ijumaa.

Kamati hii iliundwa imetokana na mgogoro wa muda mrefu baina ya waumini wa msikiti wa Ijumaa na familia ya Sheikh Abdallah Amini waliokuwa wanaamini msikiti wa Ijumaa na mali zake za Waqfu ni mali ya familia yao.

Baada ya kesi nyingi mahakamani na kwenye vyombo vingine mamlaka iliamua kuwepo kamati ya mpito mpaka hapo utakapofanyika uchaguzi wa Bodi mpya..

Sisi kama waumini sasa tumefarijika sana kwa kazi nzuri inayofanywa na kamati ya mpito imeleta utulivu msikitini ,
imebadili hali ya msikiti kwa kupiga rangi na kuweka mazuri mapya ..Pia kukusanya kodi kuwekwa kwenye acounti ya msikiti ,mambo haya hayakuwepo kabla ya kamati ya mpito.
Kabla Sheikh Abdallah Amin
Alikuwa anakusanya fedha zote mkononi..
SheikhAbdalla Amin
Hakuwahi kutoa mahesabu ya Fedha kwa miaka yote ishirini amekuwa Katibu..

Kama ingekuwa inawezekana basi waumini tuko tayari kuipitisha kamati hii ya msikiti iwe ndiyo bodi kamili ya msikiti wa Ijumaa.

Ndugu yetu BIM na Shelali waliwahi kupata kuwa wajumbe wa bodi ya msikiti wa Ijumaa huko nyuma lakini kwakuwa walikuwa Bize sana na shughuli zao walijitoa wao wenyewe kwenye bodi zote kuanzia msikiti wa Ijumaa mpaka bodi ya Thaqafa.

Wakati huo wakiamini kwamba msikiti wa Ijumaa ni mali ya familia ya Abdallah Amin na wao wapo kwa hisani ya familia hiyo.

Wakati huo kila mmoja alijigawia mali ya kunufaika nayo yeye binafsi bila hofu yoyote kwa waislamu wala kwa Mungu.
Sheikh Abdallah Amin aliwagawia watoto wake Frem za maduka na watoto wakamiliki kama mali zao..Akampa mke wake mlango katika nyumba ya Waqfu iliyopo mtaa wa uhuru na mke wake akaweka Hotel kwa miaka 10..hajawai kulipa kodi ya pango karibu million 45
Haya kina BIM hawayasemi..

Bahati mambo mawili yakatokea kwa pamoja na ikawa bahati mbaya kwao.
BIM na Sherell walipojitoa walikuwa ni matajiri hawakuwa hata na muda wa kumsalimia mtu..
Lakini baadaye mambo yalibadilika

Mosi Kulianza kuyumba kiuchumi kwa shughuli za Ndugu yetu BIM na ndugu yake Shelali katika wa biashara zao huko DSM.

Pili huku waumini wakaanzisha VIGUVUGU Na kuamka na kutaka bodi mpya ya kusimamia mali za msikiti wa Ijumaa na kuachana na dhana ya msikiti wa Ijumaa kuwa ni mali ya familia ya Sheikh Abdalla Amin..

Bahati mbaya kwa Ndugu yetu BIM na Shelali wakati huo wakawa wamefilisika kiuchumi kwa wakati huo hadi kufikiria kurudi msikiti wa Ijumaa na Thaqafa ili kula mali za Waqfu waweze kuendesha maisha yao kama zamani lakini bahati mbaya kwao hali na mambo yakawa yamebadilika.

Kuanzia hapo ndipo walipo ungana na sheikh Abdalla Amina
N ndipo ilipoanza migogoro na kufunguliwa kesi nyingi mahakamani kila uchao wakipigania kurudishwa katika hizi bodi
Kwani wakati huo na Sheikh Abdalla Amin na yeye alikuwa tayari ameondolea Bodi ya Thaqaafa..

Huu ndiyo msingi mkubwa na chanzo cha migogoro ya msikiti wa Ijumaa na shule ya Thaqafa.

MAJIBU YETU KWA BIM NA NDUGUYE SHELALI.

Shule ya THAQAFA ni shule ya waislamu pasinashaka yoyote.


Shule ya Thaqafa inasimamiwa na bodi ya wadhamini inayowakilisha waislamu wa Mwanza ,bodi hiyo inaundwa na waislamu wakiotuwakilisha waislamu tangu mwanzo hadi sasa yakiwa yamejengwa magorofa kutokana na usimamizi mzuri wa Alhaj Maruzuku..

Wajumbe wa bodi ni waislamu wacha Mungu ambao wameyatoa maisha yao yote miaka yote kuijenga Shule na kuifikisha shule hiyo pale ilipofikia.

Bodi ya Thaqafa inayowakilisha waislamu kusimamia shule ile kama zilivyobodi zingine za shule na taasisi za waislamu.

Bodi ya Thaqafa imethibitishwa na mamlaka zote na inafata miongozo yote inayotakiwa.

Kamati yetu waumini wa msikiti wa Ijumaa inapenda kumkumbusha BIM na ndugu yake Shelali wao waliisha shindwa kesi zote walicotaka kulazimisha wawemo kwenye bodi baada ya kufilisika tunawataka watambue kutokuwemo wao kwenye bodi hakuondoi Thaqafa kuwa ni shule ya waislamu.
Wakati wao wakiwemo katika hizo bodi hawakuwai kusema shule sio ya waislamu.leo wametolewa ndio kelele zote..

Ndugu waislamu tunapenda kuwakumbusha kwamba.

Ndugu hawa wawili kwa muda mrefu wamepigania pia kituo cha ILEMELA YATIMA ISLAMIC FOUNDATION kama ni mali ya Familia yao kwa madai kwamba kaka yao Marehemu Bashiri ndiye alitoa sadaka kubwa kuanzishwa pale basi wao ndiyo wanahaki wakimiliki.
Wameka katika bodi wao na watoto wao wawili Husein na khalid..

Katika muda wa kipindi cha dharura wakati Mzee Chilwan alikuwa hayupo
alichopewa kukisimamia kituo kile ndugu yetu Shelali wakati msimamizi ndugu yetu Marehemu Chiluwan akiwa mahabusu,basi Ndugu yetu Shelali akachukulia ndiyo tayari urithi kabidhiwa yeye.

Shelali alifanya uharibifu mkubwa sana na kukirudisha kituo nyuma zaidi mpaka lilikaribia kufa.

Wajumbe wa bodi walipomuondoa kwenye nafasi hiyo Shelali hakukubali aliamua kwenda mahakamani kukishitaki kituo cha yatima kimlipe mamilioni ya pesa.Anadai alipwe milion 20..
Hata hivyo mahakamani ameshindwa..

Hata hivyo Shelali hivi karibuni alionekana mbele ya waandishi wa habari akiishawishi mamlaka kuifungia shule ya Thaqafa ..

Shelali na BIM furaha yao ni kuona vituo vinakufa baada ya kuona maslahi yao hayawezi kupatikana kwenye kituo hicho.Hawa watu hawana Dini.. ni watu hatari kwa Uislam.. Ni maadui wa Uislam..Tutaje Faida ya Thaqaafa..

MAMBO UNAYOFANYA SHULE YA THAQAFA KUWANUFAISHA WAISLAMU.

1.Thaqafa ndiyo shule pekee inayoendesha madrasa kubwa ya watoto na kutoa Elimu hadi Muttawasit(sekondari ya kwa dini)
Thaqafa ina toa Vijana vijijini na kuwapa Dini
Pia imeweza kuajiri walimu wenye sifa na viwango bora na watoto kusoma kwa ubora kwa viwango safi vya elimu vinavyoweza kuwaendeleza elimu zajuu baada ya kutoka hapo na madarasa hii ipo kwa muda mrefu sana na imetoa wasomi wengi wa dini na shule kutokana na ubora wake.
Leo hii maimamu wa misikiti Mwanza mjini ni zao la Thaqaafa
Leo hii hadi masheikh wametokea Thaqaafa..
Sheikh wa Wilaya ya Sengerema ni zao la Thaqaafa

2.Thaqafa inaedesha mashindano ya Quran kwa gharama kubwa bila kuchangisha popote na washindi wanapewa zawadi nono.

3.Thaqafa ina somesha bure kila mwaka watoto zaidi ya 10 wanaoshinda katika mashindano ya Quran na wanaofaulu vizuri mitihani ya ELIMU YA DINI YA KIISLAMU DARASA LA SABA.

4.Thaqafa inawalipa posho walimu wengi wa madarasa huko vijijini na inasaidia kujenga na kuboresha madrasa zao
5 Thaqafa inapeleka misafara ya kwenda kufanya dawah vijijini na ina inawapa nguvu makundi mengi yanayokwenda vijijini.

6.Thaqafa inatia nguvu kubwa katika ujenzi wa vituo vya Afya vya Bakwata na hivi karibuni imetoa mifuko miamoja ya saruji na michango mingine ikiwemo fedha taslimu milion 3 ili kufanikisha ujenzi huo wa vituo vya afya vya kiislamu

7.Thaqafa kumekua ni kituo chashughuli za kiislamu inatoa ukumbi na vifaa vyake na chakula kwa shughuli zote za semina ,makongamano na vikao wanavyohitajia kufanya waislamu na hupewa bila malipo.Mwaka juzi Thaqaafa ilidhamini Ijtmai/Mkutano wa Tabligh iliyofanyika Mwanza

8.Thaqafa imekuwa ndiyo mpokeaji wa wageni wakubwa wa kiislamu wa kitaifa na kimataifa bila kujali itikadi wala taasisi Thaqafa imekuwa ilikubali uenyeji na kuhudumia ugeni huo.

9.Thaqafa imekubali kuiendesha hospitali ya msikiti wa Ijumaa na kuifanyia maboresho makubwa kwa gharama kubwa karibu Bilioon 2 baada ya kila muendeshaji wa hospitali hiyo kushindwa na kuitekeleza lakini sasa Hospital hiyo ya Aljumaa ndiyo kituo bora cha Waislaamu hapa Mwanza likiwa chini ya Thaqafa.

10.Thaqafa ina gari la kubebea wagonjwa Ambulance gari ambalo limekuwa misaada kwa waislamu na wanajamii wa kwanza pindi wanapohitajia huduma hiyo na wanaipata bila malipo.

BIM na Ndugu yake Shelali wawaambie waislamu shule gani ya kiislamu imeweza kufanya hayo au wao wameweza kufanya hayo wapi?

Kwa mambo yote hayo ya kuendeleza uislamu wanapinga shule sio ya waislamu kwa kuwa wao wamekwama kurudi kwenye bodi?

Tunawaomba waache kumchafua imamu wetu imam Sheikh Hamza majibu waliyoyataka kamati imewapatia hayo hapo juu.
Leo walivyo na Roho mbaya wametaka shule ya Thaqafa ifungwe..Bila kujali Elimu ya Dini Madrasa iliyopo hapo..

Sasa BIM ni zamu yake kuithibitishia ummah kwamba Thaqafa sio shule ya waislamu ila ni ni shule ya nani?aseme kwa mujibu wa usajiri na sio Majungu na porojo.Ache kudai kuwa shule ya Thaqaafa ni mali ya Bodi ya Msikti wa Ijumaa ..
Thaqaafa ina Bodi yake..mbona walipokuwepo kwenye Bodi ya Thaqaafa
Hawakusema hayo..

UFAFANUZI KUHUSU UPOTOSHAJI WA BIM.

Ndugu yetu BIM amemlaumu sana kiongozi wa Thaqafa Alhaji Marufuku Magongo kwamba amepanga katika Frem za msikiti wa Ijumaa na halipi kodi.

Kamati yetu tunapenda kuwafahamisha waislamu kwamba.

Alhaji Maruzuku Magongo sio mtu masikini wala sio mtu anaetegemea shule kuishi.Yeye na Viongozi wenzake wanabiashra zao na wamekuwa na mali hata kabla Thaqaafa kujengwa..

Bali Alhj Maruzuku nimtu pekee aliyetumia muda wake wote asubuhi hadi usiku kukaa shuleni Thaqafa na kusimamia kila kitu kwa miaka yote mpaka shule imefikia pale.

Aidha ndiye yeye Alhaji Maruzuku akishirikiana na Marehemu Mohamed Salehe ndio waliokuwa mstari wa mbele kuziboresha nyumba za Waqfu za msikiti wa Ijumaa kutoka nyumba za tope hadi magorofa na ndio waliojenga fremu za biashara zilizopo hapo msikitini
wakati huo akiwa viongozi wa bodi ya msikiti wa Ijumaa.

Licha ya kufanya hayo Alhaji maruzuku ni mfanya biashara .
Biashara zake zilizopo kwenye frem za msikiti wa Ijumaa
Tumefuatilia na tuna taarifa rasmi kuwa
Alhaj Maruzuku amelipa madeni yote ya kodi kwa kipindi chote cha nyuma na imebakia mwaka huu tu.

Hata deni la kodi la hospitali kwenye msikiti wa Ijumaa pia limelipwa lote imebakia mwaka huu tu.
Wanachosema kina BIM ni kutaja barua ya RITA ya miaka ya nyuma
BIM na nduguye Shelali wanawadanganya waislam kwa makusudi kwa lengo la kuchochea chuki na farka kwa waislamu ili matatizo yatokee wakidhani hiyo itawasaidia kurudi kwenye bodi waje kuendesha maisha yao.

BIM arudi kwa waumini akafute kauli zake za uongo chuki fitina na Majungu mambo ambayo ni kinyume na uislamu huku wao wakijinadi ni maanswar sunnah wa Mwanza.

Waumini wa msikiti wa Ijumaa Mwanza wanawaona BIM na nduguye Shelali ni watu hatari katika uislamu kwa fitina Majungu na uchonganishi hawafai hata kujinadi kuwa wao ni waislamu sembuse huo uanswar.
Kila mara wanatumia Nembo ya kujidai wanawapigania waislamu wakti wanapigania matumbo yao..
Mbona hawana hata kikao kimoja wakiwa na waumini wanao wapigania..

KAMA BIMU NI MKWELI NA MCHA KUNGU ASEYASEME HAYA MBELE YA UMMAH.

Ikiwa leo Alhaji Maruzuku amepanga kwenye Nyumba za Waqfu na kufanya biashara maduka,bekary ni na analipa kodi mamilioni ya fedha msikiti unapata pesa nyingi sana.
Mbona Hamsemi
Dhalimu Abdalla Amin aliyekaa katika nyumba ya msikiti yeye na mke wake na kuwapagisha watoto wake ..leo kwa hesabu za haraka kwa miaka 20 aliyokaa bure
Abdala Amin anadaiwa karibu millik 70.

BIM aseme wazi kabla ya kamati ya mpito fremu nyingi na nyumba za kuishi zikishikiliwa na familia ya Sheikh Abdullah Amini wakizitumia wao na kukusanya kodi wao llkwa miaka zaidi ya 20
BIM awaambie waislamu baada ya kodi kulipwa Fedha zilienda wapi?
Na kwanini kodi hizo hawazipiganii ili hali ni miaka mingi na mamilioni ya pesa kuliko kipindi hiki kifupi cha kupanga Alhaji Maruzuku.?

Waumini wa msikiti wa Ijumaa kupitia kamati hii tunapenda muyapokee majibu haya na ufafanuzi huu kwa maslahi mapana ya uislamu.

Aidha tunapenda kuwafahamisha kwamba MSIKITI WA IJUMAA UKO SALAMA NA MALI ZOTE ZIKO SALAMA SANA CHINI YA UONGOZI WA KAMATI YAMPITO MSIKITI UMETULIA NA KILA KITU KINAKWENDA VIZURI

Waislamu wapuuzeni wapotezeeni BIMna nduguye Sherraly
kwa propaganda zao dhidi ya Msikiti wa Ijumaa na Shule ya Thaqafa ukweli ndiyo huuu.

Wao hawana jambo hata moja hapa Mwanza la kuwaonesha waislamu kwamba wamefanya vizuri kuliko viongozi wanao wachafua leo.Hao wanao wanaowachafua ni binaadamu hawawezi kukosa makosa..
BIM wewe ulitoa nyumba iliyopo mtaa wa Makongoro karibu na shuke ya Taqwa ukawapa kituo cha Yatima Ilemela kama Waqfu ..
ulipofilisika umeidai nyumba yako na umeiuza ili upate Dunia..
Wewe BIM wakati ule alipokuja mwanza
sheikh Lukaka wa kutoka Ubalozi wa Burundi mwaka ule..
Waislamu wa Mwanza pale katika ukumbi wa shule ya Thaqaafa tulichanga
milion 20 na hizo fedha ukakabidhiwa wewe ili waislamu tuanzishe Radio ya waislamu.
Tuambie hizo hela BIMumezipeleka wapi..?

KUTOKANA NA KUKOSA KAZI ZA KUFANYA BAADA YA KUFILISIKA TUNAWASHAURI BIM NA SHELALI WAKAE NA KAMATI YAPITO WAOMBE FREMU NA MISAADA MINGINE ILI WAFANYE BIASHARA WASIOGOPE KUANZA UPYA LAKINI KAMWE WASITEGEMEE KUTOKA TENA KUPITIA MSIKITI AU SHULE YA THAQAFA.
Leo Sherraly unakwenda kutangazia dunia eti shula ya Thaqaafa inapata faida Bilion 2 kwa mwaka..
Humuogopi ALLAH
Shule yenye wanafunzi hawazidi hata 600 unawezaje kupata hiyo faida..leo
Wewe Sheralli unafanya juu chini urudi katika Bodi ya Msikti ili ufanye nini kipya..
Ulikuwa mwenyekiti wa Msikiti kwa miaka 20 hadi ukashindwa ukajiuuzuru..Leo huna zaidi ya Majungu na unasema aibu na siri za Taasisi za kislamu kwa wasio kuwa waisalamu ili tu upate Dunia..


Tumewasilisha ujumbe huu na utakuwa endelevu kwa kila mpotoshaji ili kuweka kumbukumbu vizuri na watu wasiuchafue uislamu na kuuchafua msikiti wa Ijumaa na imamu wetu.

Ndugu waislamu
Ndugu WaTanzania.

Tunawashukuru sana kwa kusoma ujumbe wetu

TUNAOMBA MUWASAMBAZIE WENGINE WASOME WAELEWE.
SAMBAZA KWA WOTE.

Ni sisi waumini wa msikiti wa Ijumaa.

Kupitia kamati maalumu tunayoitambua..

Asanteni sana.
 
Kuna familia hazifiki hata 10 ndizo zinafaidika na hiyo miradi na cha ajabu hata misaada inakuja kwa jina la taasisi cha ajabu wanafaidika wachache tu
 
Tutafuteni Hela jamani baada ya kupitia tamko hili kwa kina nimejiridhisha kinachotafutwa hapa ni maslahi au kujichotea fedha kutokana na miradi mbalimbali ya msikiti ushauri wangu tusichanganye dini na fedha au mambo ya Dunia
 
Back
Top Bottom