Billie
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 12,726
- 19,874
Mambo mengi yanapaswa yatutoe kwenye jiza cha kufikiri.
1. Dhana ya udini: Hapa nitadodosa haya: kabla ya kutoa lawama kwa yeyote tafakari namna uchaguzi ulivyokwenda na ushiriki wa misikiti na makanisa katika kuwapandikiza wagombea. Hili huhitaji 'degree' wala 'diploma' kulibaini bali ubinadamu wa kawaida tuliojaliwa na Muumba.
2. Ndanda: Kanisa katoliki lilinyang'anywa ile shule pamoja na majengo ya shule si shule tu: ukweli ni kuwa kanisa lililojengwa pale lilikuwa la jumuiya yote ya waroma si wanafunzi pekee. Waislamu, ambao pia ni wanafunzi wa pale, walipa kodi wanahaki ya kuabudu, ila busara inahitajika, je mazingira ni mwafaka kwa msikiti? Wasio waroma lakini ni Wakristo wanasali wapi? Ndanda ni mahali ambapo shughuli zote za kanisa, pamoja na malezi ya masista na mapandri yanafanyika! Ni mahali palipotapakaa uturi wa bibilia!!! Waislamu nawashauri haya: a) Tumieni msikiti ulio nje ya maeneo hayo b) Zingatieni Masomo ili nanyi mfungue himaya zenu c) Mwambieni kiongozi wenu aandike barua ya kuomba mrudi shuleni na kuendelea na masomo d) Kama umbali wa msikiti unaathari kubwa kwa ibada zenu, ombeni chumba cha kudumu hapo shuleni! Mmenyimwa? Nawatakia uamuzi wenye busara katika suala hili.
Chumba cha kudumu hapo shuleni wanacho mbona pale kuna dhana fulani ya waislamu kuwa watawala wa kila kitu hicho kinachowafanya wakurupuke na kuona wanadai madai ya msingi kumbe Pumba tupu.