Shibuda: "Hakuna chama kama CCM" akitoa Semina elekezi MaRC na MaDC Dodoma

Anasubiri nini kuondoka kwenye huo uchokoraa? Ana laana. Amesahau kuwa huo anaouita uchokoraa ndio uliomfadhili alipotimuliwa na CCM? Inaelekea siasa inamuendea kombo, ningemshauri ajaribu biashara nyingine. Haiwezekani kila wakati awe anauota uraisi kwa kiwango anachofanya wakati hajafanya vya kutosha katika ngazi ya ubunge. Angerejea CCM mapema huenda angekumbukwa katika nafasi za u-DC zilizopita. Lakini hajachelewa sana anaweza kupata nafasi nyingine. Kila la heri Shibuda!
 
watu wanaotumikia tumbo ndo mauti ya watz na huuyu ameonyesha dhahiri kabisa kwanza huyu hajawahi kuwa CHADEMA toka mwanzo ameingia tu bungeni akamtambua JK aliyeingia madarakani kwa uchakachuaji .................... kabla huo usalti haujasahulika akaomba posho ziongezwe kinyume kabisa na msimamo wa chama. ............... kumuondoa huyu gharama ngogo mno
 
MBUNGE wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ameibuka na kusema kuwa kama angekuwa na uwezo, angehakikisha kuwa chama chenye kauli za uchochezi kinashikishwa adabu na kwamba hadi sasa hajaona chama chenye nguvu mithili ya CCM.

Amekifananisha chama hicho tawala kuwa na nguvu sawa na mngurumo wa ndege ya kivita (Airforce). Alisema kuwa, mfumo wa sasa wa vyama vingi umezaa hasira kwa
KAMA SOURCE NI HABARI LEO BASI SIKO TAYARI KUJADILI UPUUZI HUO
 
Huyu ni mbumbumbu of the highest order. Mkubwa mzima anafanya vitu utafikiri ni mtoto wa darasa la pili akipewa pipi baada kuchapwa viboko anaona aliyemchapa kumbe ni mzuri wakati pengine alimchapa kwa kumwonea..Anahitaji akapimwe akili
 
NILIVYOKUWA NAMFIKIRIA MWANZO BAADA YA KUSIKIA VYOMBO VYA HABARI ; TOFAUTI KABISA NI MTU ANAYETAKA TANZANIA KWANZA (TUNAYOITAKA); Km anatoa semina na anitwa NGO kubwa km hii ; anabusara za kutosha ;

NGO ipi?
 
Shibuda anawafunda wote, si CCM si Upinzani.

Nna uhakika ukimsoma na au ukimsikiliza kwa makini, utaelewa kuwa huyu mtu ana falsafa ya hali ya juu na si wengi wanaoweza kumuelewa. Ni mtu mahiri, makini, na ni mwansiasa wa ukweli.

Kila mwanasiasa mwenye fikra njema inapaswa ajifunze kutoka kwa huyu Mzee.

With due respect, napingana nawe! Sijaona falsafa yoyote, hekima wala uelewa wa huyu mzee! Falsafa zinamsaida mtu kuangalia mazingira halisi ya mwanadamu na kujenga hoja zitakazompeleka katika tarajio lake! Sioni hata chembe ya hilo kwa Shibuda zaidi ya mipasho na taarabu kama mzee Yusufu! Falsafa gani ya kuwa mbunge wa CDM, unaitwa CCM, unaponda CDM, kweli?
 
Hao waliomteua huyu kibaraka wa magamba kutoa semina yaani ndo kusema walikosa mtu kabisa hadi wakamteua huyu kilaza!!Hata hao wajumbe wa hiyo semina naamini kabisa hawakuambulia hata pointi moja yakuondoka nayo zaidi ya pumba tu.
 
Shibuda ni sawa na mbwa atapikaye kisha kuyarudia matapishi yake.

Demokrasia ya CCM ya kutumia nguvu ya pochi ilimshinda, huku kafyata kajimkia kake akaenda CDM wakampa nafasi ya kugombea. Leo ni mbunge anarudi kuipongeza CCM iliyo mbana kende zake na kumwach uchi. Huko si kuyarudia matapishi yake mwenyewe??

Ni shida sana kuishi na watu wenye mawazo na msimamo wa mbwa, hujui saa na dakika watakayo yarudia matapishi yao au hata kula kinyesi.
 
Inawezekana waandishi wa habari ndio wanaokuza mambo; hata ukisoma kichwa cha bandiko hili na habari yenyewe haviendani wal usaliti wa Mh Shibuda hauonekani kwenye habari kuu. Hapa kuna chokochoko ili CDM wamtimue Shibuda na kuanza kujenga uhasama wa kabila analotoka Shibuda na CDM.

Nawaona waandishi wa habari kama ndio wapikaji wakuu na jina la Shibuda linatumika tuu.
 
kuna ukweli ambao huwa hautakiwi kusemwa. Hata ccm wanajua hili kuwa cdm hapo ilipofika ni moto chini na lolote laweza kutokea. Wanahofia madaraka yao na ndio maana wanafanya mbinu kila leo kudhoofisha upinzani, lakini hawajawahi kukiri kuwa cdm ina nguvu. Hili ni kosa sana kisiasa. Hivi leo asimame mwanaccm mahali rasmi kabisa aseme, 'lakini cdm wanaweza kuchukua nchi...' ccm watamvumilia?

Kuna mawili hapa. Aidha shibuda bado anadharau upinzani akiamini au kuaminishwa na vyanzo vyake kuwa ccm itaendelea kushika hatamu, so sema utakayo. Hata wakikutosa huko nafasi yako ccm ipo. Yawezekana huu ni upuuzi anaojazwa shibuda kila anapokutana na wanaccn wenzake. Katika siasa naamini hakuna ukweli ambao shibuda anataka tuuamini. Kwamba mtu azungumze ukweli japo ni mchungu. Kwa faida ya nani?

Suala la pili yawezekana ndio yale aliyosema mzee Makamba kuwa ukiona upinzani wanakusifia basi uwe makini. Yawezekana sifa anazotoa shibuda zikawapumbaza watawala na siku wakajikuta chali.

Lakini kwa kauli za shibuda anaposema kuwa hapendi kuona cdm wala ccm kinakufa ni kwamba anataka wagawane madaraka? Kitu anachotaka shibuda ni kuwa vyama vya siasa vishirikiane kama taasisi zisizo za maslahi fulani. Shibuda ameishi kwenye siasa kwa muda mrefu kujua kuwa siasa ni mchezo wa kumalizana, wa kuviziana. Kumalizana kiutawala na si vingine. Na kwa hoja zake ni wazi kuwa bado ana mahaba na mtaliki wake. Anataka kuleta habari za soka kwenye siasa kwamba kuhama club ni suala la maslahi tu na anaweza kufanya kama alivyofanya Thiery Henry. Soka no maslahi binafsi lakini siasa ni kwa maslahi ya Taifa.

Napenda falsafa za shibuda ila si katika na,na anavyotaka tuaminiane nae. Aache kuwaogopa ccm maana hayuko huko tena! Atakachofanya afanye kwa maslahi ya cdm na Taifa! Kwake ajue kuwa ccm ni historia kwa sasa. Asipotaka kujua haya ni kuwa ANADHARAU UPINZANI. Anakidharau cdm. Ananyea kambi. Anakata tawi alilokalia. Kifupi anaonekana JUHA!
 
Ni dhahiri Shibuda anakata tawi alilolikalia, mwangu wake hauko mbali maana tawi limeshaanza kunepa
 
shibuda rudi ulipotoka kumbe pazuri mbona uliomba hifadhi kwa machokoraa ama kweli waliozoea vyakunyonga hata vikichinjwa atahakikisha ananyonga kwaza ndio ale sasa shibuda subiri watakacho kufanya machokoraaa
 
kweli shibuda anafaa kuwa Rais Mchumia Tumbo, kwani ni kama magambaz, labda angoje mgombea binafsi maana urais haliutaka tangu enzi za Mkapa, du kama kutakuwepo mapopo kama huyu nchi itauzwa mara kumi.
 
Nna uhakika huielewe ARPM ni nini, ili kujuza tu, kwa faida yako na ya wengine wasiyoielewa, naomba nikupe darsa dogo, labda utamuelewa Shibuda:

The African Peer Review Mechanism is the brainchild of the African leaders. It is voluntarily acceded to by Member States of the African Union for self-assessment. The primary purpose of the APRM is to enable participating countries to learn and adopt policies, standards and practices of countries with success stories for achieving similar successes in their countries.

H.E Jakaya Mrisho Kikwete Launches the APRM - NGC.

The APRM National Governing Council was launched on 11th sept 2009 by the President of the United Republic o Tanzania.

Soma zaidi: APRM Tanzania
kwenye hizo initiatives za kula alawansi tu, just kidding yupo juu

BTW, hivi mkuu ulijishusha hadi kujiita ribosome??? to a man of you caliber ile ilikua chaka mno mkuu, hata kama ni intelijensia, pale ile ilikua very machakaras
 
Watu wa hovyo kama shibuda humezwa na historia na upepo unaovuma katika jamii kwea wakati husika.nionavyo mimi shibuda yupo katika upande mbovu wa kihistoria na jina lake litafutika haraka kama yalivyofutika majina ya akina cheyo na mrema na ofcoz lipumba.
 
Shibuda anawafunda wote, si CCM si Upinzani.

Nna uhakika ukimsoma na au ukimsikiliza kwa makini, utaelewa kuwa huyu mtu ana falsafa ya hali ya juu na si wengi wanaoweza kumuelewa. Ni mtu mahiri, makini, na ni mwansiasa wa ukweli.

Kila mwanasiasa mwenye fikra njema inapaswa ajifunze kutoka kwa huyu Mzee.

yaani kwa uelewa wako mdogo wa falsafa na propaganda......shibuda ndio role modal wa wanasiasa bora tz? better go'nd sleep! its your night, no more thinking.
 
Back
Top Bottom