Tanzania hakuna chama cha upinzani

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
347
462
Nimefuatilia kwa muda mwenendo wa siasa za hapa nchini na kugundua kuwa nchi haina chama cha upinzani hata kimoja bali ni hivi vyama vingine ni miradi tu kama miradi mingine ya utafutaji pesa.

Siku sheria itakapofuta ruzuku za vyama na kuelekeza pesa hizo kwenye miradi ya kweli ya maendeleo na huo ndiyo utakuwa mwisho wa vyama na tutabaki tu na chama mama lao CCM.

Naendelea kuishauri serikali ya CCM ifute ruzuku za vyama vya siasa ili kila chama kijiendeshe kwa pesa zao. Chama chenye agenda chanya kitapata sapoti kutoka kwa wanachama wake.
 
Back
Top Bottom