Shibuda: "Hakuna chama kama CCM" akitoa Semina elekezi MaRC na MaDC Dodoma

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,884
6,885
Kikwete-right-greets-Maswa-West-MP-John-Shibuda.jpg

MBUNGE wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ameibuka na kusema kuwa kama angekuwa na uwezo, angehakikisha kuwa chama chenye kauli za uchochezi kinashikishwa adabu na kwamba hadi sasa hajaona chama chenye nguvu mithili ya CCM. Amekifananisha chama hicho tawala kuwa na nguvu sawa na mngurumo wa ndege ya kivita (Airforce). Alisema kuwa, mfumo wa sasa wa vyama vingi umezaa hasira kwa sababu CCM inataka kutawala, ilihali wapinzani nao wanaitaka nchi ili waitawale.

Shibuda aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akitoa mada ya Demokrasia na Siasa wakati wa mafunzo elekezi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea hapa. Alikuwa akiwasilisha mada hiyo iliyoandaliwa na Mpango wa Kutathimini Utawala Bora Afrika (APRM). Alisema kuwa gazeti moja la kila wiki mapema wiki hii lilikuwa na habari iliyokuwa na maneno `CCM yakaribia kuaga Ikulu’, lakini akasema kamwe hajawahi kuona chama chenye mngurumo wa Airforce kuweza kuizidi CCM na kushika nchi. “Ningekuwa na uwezo mara ninaposikia kuna uchochezi sitamkamata mtu aliyetoa maneno ya uchochezi, bali nitakipiga faini chama chake kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinabadili lugha zake, kwani chama chenye uchochezi kikipigwa faini mara nyingi kitakuwa na nguvu tena?” alihoji Shibuda.

Alisema kuwa, fitna mara nyingi zimekuwa malighafi za kisiasa kutokana na maneno matamu, lakini APRM ni chujio na kuwa mfumo wa vyama vingi huzaa wawindaji. “Kiongozi anayekaa ofisini hawezi kujua kiu ya wananchi wake, ni lazima kujisahihisha na kujitathimini, kwani Serikali na siasa ni kama mapacha, lakini cha muhimu ni kujiuliza vipi tutalinda mitaji yetu? Kwani kuna vishawishi vya kuacha mema na kukumbatia upumbavu, lakini matunda matamu hutambulishwa na mbegu za kuzaa matunda matamu,” alisema.

Aliongeza kuwa, siasa za sasa zimejaa unafiki mfano wa malezi ya machokoraa (watoto wasio na makazi maalumu) ambayo hayakupata malezi ya baba na mama. “Mfumo wa vyama vingi unazaa hasira kwa sababu tunataka kuwakomoa wapinzani na CCM inasema inataka kuwamaliza wapinzani, lakini ukimaliza mazalia ya mbu malaria haitakuwepo,” alisema.

Alisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete ni mwanasiasa na bila siasa hakuna kilainishi cha kuongoza na kutawala . “Wakoloni walitumia machifu wa Kisukuma kutawala, wanaweza kukushangilia ukajua wanafurahia kumbe wanatafuta mwanya wa kukuadhibu,” alisema Shibuda. Alisema kuwa mwanzoni alikuwa CCM na sasa yuko upinzani, hivyo ana taswira ya nchi inakoelekea. Aliongeza: “Najiuliza, naacha urithi gani kwa wadogo zangu waliochaguliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?”.

Shibuda aliwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanatunza vizuri historia ya nchi akisisitiza historia inahifadhiwa, lakini kama mtoto ni chokoraa, hatakuwa na uwezo wa kutunza historia. Aliongeza kuwa, siasa ni daraja la maoni kwa ajili ya kuongoza umma na kila chama kimekuwa kikishindana kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinashinda uongozi.

Aidha, Shibuda alitumia fursa hiyo kukishukuru CCM kutokana na uelewa wake, huku akisema hataki chama hicho kife, kama ambavyo pia hataki Chadema ife. Mafunzo hayo elekezi yanayofanyika mjini Dodoma yanahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa 24, Makatibu Tawala wa Mikoa 25 na Wakuu wa Wilaya 133.

Mimi mrengo wa kati ngoja nipite waje wa mrengo wa kushoto watakavyo mshukia atajuta.Sitaki kuona damu
 
Shibuda anawafunda wote, si CCM si Upinzani.

Nna uhakika ukimsoma na au ukimsikiliza kwa makini, utaelewa kuwa huyu mtu ana falsafa ya hali ya juu na si wengi wanaoweza kumuelewa. Ni mtu mahiri, makini, na ni mwansiasa wa ukweli.

Kila mwanasiasa mwenye fikra njema inapaswa ajifunze kutoka kwa huyu Mzee.
 
Jambo moja muhimu la kujiuliza, kwa nini CCM na Serikali yak wamekazana kumwalika Shibuda kwenye makongamano na semina elekezi? Kwa nini hawakumwalika mtu mwingine kutoka Chama Cha upinzini kutoa mada hizo isipokuwa Shibuda? Kuna kila dalili nyuma ya pazia kinachoendelea, na busara ya viongozi wa Chadema kutuliza vichwa na kitakachotokea Shibuda atawakumbuka akina Masumbuko Lamwai, Kaburu, Shitambala na wengineo.

CCM ni mabingwa wa kumwaga cho chote pale wanapokuhitaji, wakishafanikisha walichokusudia unatelekezwa.
 
ndo kauli mbiu mnayokuja nayo siku hizi ili muendele kumtumia mamluki wenu cdm.
 
Huo mpango wao tulisha ushtukia zamani,kwa sasa hauna nguvu tena acha waendelee kubwabwaja tu,na kujipa matumaini wakati wanasubiri kaburi lao 2015.
 
Shibuda anawafunda wote, si CCM si Upinzani.

Nna uhakika ukimsoma na au ukimsikiliza kwa makini, utaelewa kuwa huyu mtu ana falsafa ya hali ya juu na si wengi wanaoweza kumuelewa. Ni mtu mahiri, makini, na ni mwansiasa wa ukweli.

Kila mwanasiasa mwenye fikra njema inapaswa ajifunze kutoka kwa huyu Mzee.

Unataka kutwambia CCM hawakuilewa "falsafa ya hali ya juu" ya Shibuda ndiyo maana wakamtema 2010?
No wonder JK na NEC yake sasa wanajifunza kwa Shibuda BRAVO Shibuda!
 
kwa nini shibuda anawatukana watoto wa mitaani?kuwaita chokoraa maana yake nini?
 
Shibuda anawafunda wote, si CCM si Upinzani.

Nna uhakika ukimsoma na au ukimsikiliza kwa makini, utaelewa kuwa huyu mtu ana falsafa ya hali ya juu na si wengi wanaoweza kumuelewa. Ni mtu mahiri, makini, na ni mwansiasa wa ukweli.

Kila mwanasiasa mwenye fikra njema inapaswa ajifunze kutoka kwa huyu Mzee.

Apimwe akili, unasema nyumba hii chafu nawe hutoki ina maana una matatizo. Jana wananchi wamesema aondolewe,mkiti kasema kadogo sana hako hakana ubavu taratibu zinafuatwa ili kumwadabisha. Mchukue anawafaa cha pombe, hakuna aliye juu ya chama kaondoka Kaburu sembuse huyo cha urafi.
 
Politics is a dirty game! No formula to guide it whenever you feel to conquer then it applies to the situation.
Definetely he exaggerated to CCM this will not be perceived clear to CHADEMA
Think on terming Airforce One to the gambaz... do you think Gwandaz will like this?
Any way I am trying to stay far from politics kwa kweli!
 
Kikwete-right-greets-Maswa-West-MP-John-Shibuda.jpg

MBUNGE wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ameibuka na kusema kuwa kama angekuwa na uwezo, angehakikisha kuwa chama chenye kauli za uchochezi kinashikishwa adabu na kwamba hadi sasa hajaona chama chenye nguvu mithili ya CCM. Amekifananisha chama hicho tawala kuwa na nguvu sawa na mngurumo wa ndege ya kivita (Airforce). Alisema kuwa, mfumo wa sasa wa vyama vingi umezaa hasira kwa sababu CCM inataka kutawala, ilihali wapinzani nao wanaitaka nchi ili waitawale.

Shibuda aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akitoa mada ya Demokrasia na Siasa wakati wa mafunzo elekezi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea hapa. Alikuwa akiwasilisha mada hiyo iliyoandaliwa na Mpango wa Kutathimini Utawala Bora Afrika (APRM). Alisema kuwa gazeti moja la kila wiki mapema wiki hii lilikuwa na habari iliyokuwa na maneno `CCM yakaribia kuaga Ikulu', lakini akasema kamwe hajawahi kuona chama chenye mngurumo wa Airforce kuweza kuizidi CCM na kushika nchi. "Ningekuwa na uwezo mara ninaposikia kuna uchochezi sitamkamata mtu aliyetoa maneno ya uchochezi, bali nitakipiga faini chama chake kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinabadili lugha zake, kwani chama chenye uchochezi kikipigwa faini mara nyingi kitakuwa na nguvu tena?" alihoji Shibuda.

Alisema kuwa, fitna mara nyingi zimekuwa malighafi za kisiasa kutokana na maneno matamu, lakini APRM ni chujio na kuwa mfumo wa vyama vingi huzaa wawindaji. "Kiongozi anayekaa ofisini hawezi kujua kiu ya wananchi wake, ni lazima kujisahihisha na kujitathimini, kwani Serikali na siasa ni kama mapacha, lakini cha muhimu ni kujiuliza vipi tutalinda mitaji yetu? Kwani kuna vishawishi vya kuacha mema na kukumbatia upumbavu, lakini matunda matamu hutambulishwa na mbegu za kuzaa matunda matamu," alisema.

Aliongeza kuwa, siasa za sasa zimejaa unafiki mfano wa malezi ya machokoraa (watoto wasio na makazi maalumu) ambayo hayakupata malezi ya baba na mama. "Mfumo wa vyama vingi unazaa hasira kwa sababu tunataka kuwakomoa wapinzani na CCM inasema inataka kuwamaliza wapinzani, lakini ukimaliza mazalia ya mbu malaria haitakuwepo," alisema.

Alisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete ni mwanasiasa na bila siasa hakuna kilainishi cha kuongoza na kutawala . "Wakoloni walitumia machifu wa Kisukuma kutawala, wanaweza kukushangilia ukajua wanafurahia kumbe wanatafuta mwanya wa kukuadhibu," alisema Shibuda. Alisema kuwa mwanzoni alikuwa CCM na sasa yuko upinzani, hivyo ana taswira ya nchi inakoelekea. Aliongeza: "Najiuliza, naacha urithi gani kwa wadogo zangu waliochaguliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?".

Shibuda aliwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanatunza vizuri historia ya nchi akisisitiza historia inahifadhiwa, lakini kama mtoto ni chokoraa, hatakuwa na uwezo wa kutunza historia. Aliongeza kuwa, siasa ni daraja la maoni kwa ajili ya kuongoza umma na kila chama kimekuwa kikishindana kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinashinda uongozi.

Aidha, Shibuda alitumia fursa hiyo kukishukuru CCM kutokana na uelewa wake, huku akisema hataki chama hicho kife, kama ambavyo pia hataki Chadema ife. Mafunzo hayo elekezi yanayofanyika mjini Dodoma yanahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa 24, Makatibu Tawala wa Mikoa 25 na Wakuu wa Wilaya 133.

Wapi W, B, M, JS, K, na wale wote wanaomsapoti Shibuda ili watuambie tena kuhusu hili la Shibuda.
 
Mbowe anena kuhusu Shibuda: "Sikuja hapa kumng'oa mtu…Tumng'oe?" Alihoji Mbowe na kuongeza: "Ngoja nitoe kauli ya chama. Chama chetu hakitayumbishwa na mtu yeyote msaliti. Tutatumia vikao vya chama. Tuzungumze mambo yenye maslahi ya taifa, siyo mtu mmoja mwepesi. Kama mtu hajui moto auchezee."
 
NILIVYOKUWA NAMFIKIRIA MWANZO BAADA YA KUSIKIA VYOMBO VYA HABARI ; TOFAUTI KABISA NI MTU ANAYETAKA TANZANIA KWANZA (TUNAYOITAKA); Km anatoa semina na anitwa NGO kubwa km hii ; anabusara za kutosha ;
 
Unataka kutwambia CCM hawakuilewa "falsafa ya hali ya juu" ya Shibuda ndiyo maana wakamtema 2010?
No wonder JK na NEC yake sasa wanajifunza kwa Shibuda BRAVO Shibuda!

Hata Slaa alitemwa au umesahau.
 
Mbowe anena kuhusu Shibuda: "Sikuja hapa kumng'oa mtu…Tumng'oe?" Alihoji Mbowe na kuongeza: "Ngoja nitoe kauli ya chama. Chama chetu hakitayumbishwa na mtu yeyote msaliti. Tutatumia vikao vya chama. Tuzungumze mambo yenye maslahi ya taifa, siyo mtu mmoja mwepesi. Kama mtu hajui moto auchezee."

Kwa msimamo huu ni dalili tosha ya kuonyesha ukomavu katima masuala ya siasa na uongozi. Utumiaji majukwaa katika kutolea maamuzi si busara na ni hatari sana. Hali kadhalika suala la mtu mmoja si la kujenga hoja ya kuumiza vichwa katika zana nzima ya mikutano ya movement for change.

Suala la Shibuda dogo sana na ipo siku atajutia kuburuzwa na wanaomtumia. Yuko wapi Masumbuko Lamwai? Kaburu? Shitambala? nawengineo? Historia ni mwalimu.
 
Jambo moja muhimu la kujiuliza, kwa nini CCM na Serikali yak wamekazana kumwalika Shibuda kwenye makongamano na semina elekezi? Kwa nini hawakumwalika mtu mwingine kutoka Chama Cha upinzini kutoa mada hizo isipokuwa Shibuda? Kuna kila dalili nyuma ya pazia kinachoendelea, na busara ya viongozi wa Chadema kutuliza vichwa na kitakachotokea Shibuda atawakumbuka akina Masumbuko Lamwai, Kaburu, Shitambala na wengineo.

CCM ni mabingwa wa kumwaga cho chote pale wanapokuhitaji, wakishafanikisha walichokusudia unatelekezwa.

kama toilet paper!
 
Back
Top Bottom