Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Nimemsikiliza askari aliyekuwa akihojiwa na CloudsTV anasema sheria ya mavazi ya jeshi unasema;-
"Ni marufuku raia kuvaa sare za jeshi ama mavazi yanayofanana na sare za jeshi". Ili iweje?

Yaani ktk zama hizi za sayansi na teknolojia bado jeshi letu linataka kujitofautisha na raia kwa mavazi? Mwanajeshi ajitofautishe kwa umahiri wa kung'amua na kuzima nia na jaribio la adui kutaka kuivamia nchi yetu. Baasi! Siyo hizi blah blah za kuwalingishia raia gwanda za jeshi.

Kule nchi za watu mpk walevi na mateja wanavaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya nchi zao. Mbona hatujasikia wakipata shida ya kiusalama?

Tuachane na ushamba huu. Nakumbuka hata bendera ya taifa kabla ya Kikwete kuwa rais ilikuwa ni marufuku kukutwa hata na leso inayofanana na bendera yetu ya taifa. Mhe. Kikwete akaondoa ushamba huu.

Ni wakati wa kuondoa ushamba wa kuzuia raia mavazi yanayofanana na sare za kijeshi sasa.

IMG-20230905-WA0000.jpg
 
Lakini kwanini wavae. Hebu fikiria mtu kavaa full uniform kama mjeda au polisi huoni Kwa nchi kama yetu anaweza tumia huo mwanya kutapeli/kunyanyasa watu?
Nguo za jeshi zina nembo bosi. Mabaka ya kwenye nguo hayajengi uhalali wa sare za jeshi bali nembo ya jeshi.

Kuzuia utapeli ni kisingizio tu. Mbona kila siku watu wanatapeliwa fedha kwa kutumia simu? TCRA wapo na jeshi lipo lkn hawana wanachofanya? Wanauona utapeli kwenye mavazi tu?
 
Lakini kwanini wavae. Hebu fikiria mtu kavaa full uniform kama mjeda au polisi huoni Kwa nchi kama yetu anaweza tumia huo mwanya kutapeli/kunyanyasa watu?
Acha upumbavu huu, combat za jwtz ni tofauti kabisa na camouflage clothes, uoga wako na kutojua sheria ndio unafanya nchi hii iwe kama police state, mwanajeshi hana uwezo wa kupiga raia au to arrest,kazi ya arresting ni police pekee, jwtz watimize wajibu wao wa kulinda our borders ambazo sasa ni porous borders, msomali anakatiza nchi yetu kutoka North hadi South bila ya kuonekana
 
Nguo za jeshi zina nembo bosi. Mabaka ya kwenye nguo hayajengi uhalali wa sare za jeshi bali nembo ya jeshi.

Kuzuia utapeli ni kisingizio tu. Mbona kila siku watu wanatapeliwa fedha kwa kutumia simu? TCRA wapo na jeshi lipo lkn hawana wanachofanya? Wanauona utapeli kwenye mavazi tu?
Hivi raia zinajua mambo ya nembo kweli...just think mtaani Kila mtu anafanana na jeshi. Kwangu Mimi haijakaa poa.
 
Acha upumbavu huu, combat za jwtz ni tofauti kabisa na camouflage clothes, uoga wako na kutojua sheria ndio unafanya nchi hii iwe kama police state, mwanajeshi hana uwezo wa kupiga raia au to arrest,kazi ya arresting ni police pekee, jwtz watimize wajibu wao wa kulinda our borders ambazo sasa ni porous borders, msomali anakatiza nchi yetu kutoka North hadi South bila ya kuonekana
Sijasema wapige raia ila naona sio sawa raia kuvaa sare zinazofanana na majeshi.
 
Sioni mantiki ya raia kukomalia kuvaa kama wanajeshi!
Hakuna anayekomalia. Tunachosema hakuna uhalali Wala sababu ya jeshi kuacha majukumu yake ya msingi na kuanza kugombana na raia eti kisa wamevaa mavazi yanayofanana na sare zao. Ni ujuha.

Mavazi ya jeshi yana nembo. Raia akivaa sare za jeshi (vazi lenye nembo ya jeshi ) hapo akikamatwa Sina nongwa. Lkn akivaa vazi halina nembo ya jeshi, ikn linafanana rangi na kila kitu cha jeshi, hilo siyo mali ya jeshi. Ni ujinga.
 
Nimemsikiliza askari aliyekuwa akihojiwa na CloudsTV anasema sheria ya mavazi ya jeshi unasema;-
"Ni marufuku raia kuvaa sare za jeshi ama mavazi yanayofanana na sare za jeshi". Ili iweje...
Kila nchi inaongozwa kwa utaratibu huwezi kuamka tu huko Umeshiba maharage unafikira kuvaa Combart za jeshi Watu wametoa machozi,jasho na damu kuzipata hizo.

Licha ya hivyo Tukumbuke kuwa kila mtu akianza kujiamria kutumia Mavazi ya Jeshi au taasisi yoyote kwa kuamua tu sidhani kama itakuwa sahihi.

Na hakuna nchi ambayo mtu anaamua tu kuvaa combart its Either ni msanii ama mwanamziki ambao kwa sheria hiyo hiyo ya Penal code 178 imeruhusu mtu yyte kutumia ila kwa kibali maalum cha kuzitumia kwa shughuli za kisanii

IMG-20230831-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom