Jeshi la Wananchi lipewe hadhi yake. Wanasiasa wanaliharibu kwa kuliingiza kwenye mivutano ya kisiasa

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Ni wakati mwongine tunashuhudia kauli za yule RC anayependa kumwaga damu akilielekeza Jeshi kufanya usafi jiji la Dar ambapo kwa mujibu wa kanuni na sheria Jeshi haliwezi kupokea amri kutoka kwa wanasiasa zaidi ya Bunge na Amiri Jeshi Mkuu.

Mkuu huyo wa mkoa ambaye hajaridhika na matokeo ya maagizo yake kwa polisi kutunia nguvu kuwasaka wanawake wanaojiuza na hatimaye polisi wakiwa wanatekeleza maagizo yake wakaua raia kwa risasi za moto.

Kana kwamba haitoshi, mhitimu huyo wa Sheria Tumaini University anatamka kuwa hakuagiza polisi kuua wakati anajua kabisa theoreum ya Accessory to crime.

Mamlaka yake ya uteuzi imeendelea kuamini kuwa kila.analolifanya mkuu huyo wa mkoa lina turufu kwa nchi. Sasa imekaa kimya hata pale RC huyo anapoamua kuingilia mamlaka ya utruzi kwa kutoa amri na maagizo kwa JWTZ na nina uhakika watatii agizo hilo.

Tulitegemea Jeshi letu litumike kama kitivo cha vumbuzi na majaribio mbalimbali ya kisayansi na tiba. Tuna jeshi ambalo kipaumbele chake ni pamoja na kupiga piga raia mitaani, kuwapora nguo wananchi na hata kuhatarisha maisha ya wananchi badala ya kuwalinda.

Lakini hatushangai sana, tunashuhudia wastaafu wengi wa jeshi wakipewa nafasi za kisiasa mara tu wanapostaafu na wengine wakiteuliwa makamisaa wa siasa mikoani na wilayani wakiwa bado jeshini.

Tuliheshimishe jeshi letu kwa kutolihusisha na maanguko ya kisiasa ya wapuuzi walioshindwa kudeliver na badala yake kazi kubwa wanayoifanya kwa nguvu na utashi wote ni kusalia madarakani wao na vizazi vyao.

Tamko la Chalamila kuwa jeshi watafanya usafi tarehe 24 January, limekuja baada ya CHADEMA kuandaa maandamano ya amani kupinga miswada mibovu iliyowasilishwa Bungeni na pia kupitia tamko hilo ni sawa na kutoa amri jeshi kuingilia harakati za kisiasa zisizowahusu.
 
Back
Top Bottom