Shehe: Walichokifanya polisi ni sahihi

Je kweli DK Slaa aliwambia wananchi wakavamie kituo cha polisi?, tujulisheni ukweli mliokuwepo huko AR.
 
cha mhimu hapa ni kama aliwambia je, chanzo ni nini? kusolve conflict yoyote na iishe ni lazima ushauri au utatuzi wa mgogoro ule uangaliwe tokea kwenye chanzo. ndiyo maana watu huwa wanakutwa na kesi za kuua bila kukusudia.
 
JESHI la Polisi nchini halistahili kulaumiwa kwa mauaji ya Arusha, kwani halikuwa na njia ya mkato ya kujihami zaidi ya kufanya lilivyofanya.

Hiyo ni kauli ya Imam wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa jijini hapa, Shehe Mohamed Hambal, aliyekuwa akihutubia msikitini hapo katika swala ya Ijumaa jana.

Alisema hivyo wakati akitoa msimamo wa Waislamu wa Arusha juu ya tukio hilo lililosababisha vifo vya watu watatu, Watanzania wawili na raia mmoja wa Kenya.

Shehe alisema katika mkutano wa hadhara wa Chadema ulioongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, kwa nyakati tofauti walitoa kauli za uchochezi kwa wafuasi wao zilizoashiria uvunjifu wa amani.

Alisema kwa kauli yake, Dk. Slaa aliwataka wafuasi wake kuandamana hadi kituo kikuu cha Polisi walikokuwa wameshikiliwa viongozi wao wa kitaifa, baada ya kufanya maandamano yasiyo na kibali, huku akitoa saa moja waachiwe, hali ambayo Shehe alisema ilikuwa na lengo la kuvunja amani.

“Mbali na kauli hiyo, pia Dk. Slaa alitoa kauli mbaya zaidi ya kuwa kila kijana aliyeko katika mkutano ule, apite njia yake wakutane Polisi huku akiwahadharisha wanawake wenye watoto,
kutokwenda huko kwa kuwa kungetokea mapigano,” alisema.

Shehe Hambal alisema kutokana na kauli hizo ni wazi kuwa viongozi hao walikuwa wamedhamiria na walifahamu nini kitatokea, baada ya wao kuamuru vijana na wafuasi hao kuvamia kituo cha Polisi wakiwa na mawe na silaha zingine.

“Hali hiyo ilisababisha polisi nao wajihami kwa mabomu, risasi za mpira na walipoona wanataka kuzidiwa nguvu, walilazimika kutumia risasi za moto ili kuwatawanya wafuasi hao,” alisema Shekhe.

Kuhusu kauli ya Ndesamburo kwa Rais Jakaya Kikwete kuwa kamwe nchi haitatawalika, Hambal alisema ni ya kichochezi na kumdhalilisha, kwani ni rais aliyepo kikatiba na ana mamlaka kubwa.

“Jamani Polisi ni Dola na ni Serikali ile, na pale kuna silaha mbalimbali za hatari sasa ingekuwaje kama wafuasi wale wangefanikiwa kukiteka kituo, si wangeua hadi watu wasio na hatia?” alihoji Shehe Hambal.

HabariLeo | Shehe: Walichokifanya polisi sahihi

ya mwembe chai polisi walikuwaje sahihi pia!?
 
Na kuna Mapdri na Mapadiri, Padir!, kwa nini usimshngae padiri aliyeamrisha fujo?

tayari kale ka mdudu "udini" kameingia janvini, hoja nyingi ni udini tu?. Hatufiki mbali, jf inapoteza mwelekeo. Ningewasihi waliojaa udini waanze mbele watuachie janvi letu.
 
Back
Top Bottom