Shehe: Walichokifanya polisi ni sahihi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la Polisi nchini halistahili kulaumiwa kwa mauaji ya Arusha, kwani halikuwa na njia ya mkato ya kujihami zaidi ya kufanya lilivyofanya.

Hiyo ni kauli ya Imam wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa jijini hapa, Shehe Mohamed Hambal, aliyekuwa akihutubia msikitini hapo katika swala ya Ijumaa jana.

Alisema hivyo wakati akitoa msimamo wa Waislamu wa Arusha juu ya tukio hilo lililosababisha vifo vya watu watatu, Watanzania wawili na raia mmoja wa Kenya.

Shehe alisema katika mkutano wa hadhara wa Chadema ulioongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, kwa nyakati tofauti walitoa kauli za uchochezi kwa wafuasi wao zilizoashiria uvunjifu wa amani.

Alisema kwa kauli yake, Dk. Slaa aliwataka wafuasi wake kuandamana hadi kituo kikuu cha Polisi walikokuwa wameshikiliwa viongozi wao wa kitaifa, baada ya kufanya maandamano yasiyo na kibali, huku akitoa saa moja waachiwe, hali ambayo Shehe alisema ilikuwa na lengo la kuvunja amani.

“Mbali na kauli hiyo, pia Dk. Slaa alitoa kauli mbaya zaidi ya kuwa kila kijana aliyeko katika mkutano ule, apite njia yake wakutane Polisi huku akiwahadharisha wanawake wenye watoto,
kutokwenda huko kwa kuwa kungetokea mapigano,” alisema.

Shehe Hambal alisema kutokana na kauli hizo ni wazi kuwa viongozi hao walikuwa wamedhamiria na walifahamu nini kitatokea, baada ya wao kuamuru vijana na wafuasi hao kuvamia kituo cha Polisi wakiwa na mawe na silaha zingine.

“Hali hiyo ilisababisha polisi nao wajihami kwa mabomu, risasi za mpira na walipoona wanataka kuzidiwa nguvu, walilazimika kutumia risasi za moto ili kuwatawanya wafuasi hao,” alisema Shekhe.

Kuhusu kauli ya Ndesamburo kwa Rais Jakaya Kikwete kuwa kamwe nchi haitatawalika, Hambal alisema ni ya kichochezi na kumdhalilisha, kwani ni rais aliyepo kikatiba na ana mamlaka kubwa.

“Jamani Polisi ni Dola na ni Serikali ile, na pale kuna silaha mbalimbali za hatari sasa ingekuwaje kama wafuasi wale wangefanikiwa kukiteka kituo, si wangeua hadi watu wasio na hatia?” alihoji Shehe Hambal.

HabariLeo | Shehe: Walichokifanya polisi sahihi
 
Bila shaka huyu shekh hajaenda shule. Kama ni sawa anachosema na huyo Mkenya aliyeuawa? Hawa ndo wanaopewa 20,000 wanalopoka

"Wana macho lakini hawaoni"
 
kuna masheikh na mashehe.
Mambo hayo ni ya kitaalam yanahitaji kuyajua kwa kaangalia chanzo.
Hata mimi namshangaa huyo shehe!
Haya ...
 
Bila shaka huyu shekh hajaenda shule. Kama ni sawa anachosema na huyo Mkenya aliyeuawa? Hawa ndo wanaopewa 20,000 wanalopoka

"Wana macho lakini hawaoni"

Huyo Mkenya kilimpeleka nini kwenye fujo?
 
kuna masheikh na mashehe.
Mambo hayo ni ya kitaalam yanahitaji kuyajua kwa kaangalia chanzo.
Hata mimi namshangaa huyo shehe!
Haya ...

Na kuna Mapdri na Mapadiri, Padir!, kwa nini usimshngae padiri aliyeamrisha fujo?
 
angeuwawa mwanawe au mmoja wa wakeze ndio angejua ni sahihi au la! Ss hv anaongea tu kama anaharisha!
 
JK: "Mauaji ya Arusha ni bahati mbaya"
Shehe: "Mauaji ya Arusha ni sawa"
Membe: "Mauaji ya Arusha ni ukiukwaji wa maadili"
Nahodha: "Mauaji ya Arusha ni ya kisiasa"

Ukiona mauaji yanaitwa BAHATI MBAYA au SAWA ujue ni kawaida kwao
 
Kama aliesema ni shehe basi hayana uzito yachukulieni poa tu, subirini tamko na Masheikh wa Dsalaam muone tofauti ya "Shehe" na "Sheikh"
Masheikh hawatatetea watu wa zanzibar pekee kama wengine wanaoumia wa Tanzania bara kuuwawa na kuchukulia "powa" wa Visiwani kumiminiwa risasi.
 
Kazi kweli kweli.
Watu wanawekewa maneno midomoni mwao wayatamke kama yao.
Na maneno yao watayaweka mdomoni mwa nani ili asemee?
 
Shehe huyu ameongea ukweli ambao chadema wanaujua lakini hawataki jamii ifahamu ya kwamba slaa na ndesamburo walihamasisha wafuasi wao kuvamia kituo cha polisi kama lilivyoripoti gazeti la Tanzania daima, nanukuu:

Mbowe na wabunge hao ndio walikuwa wa kwanza kukamatwa jana mchana wakati wakiongoza maandamano hayo huku Dk Slaa akiwa amekamatwa jioni ya saa mbili kasorobo usiku pamoja na mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo.

Kabla ya Dk Slaa na Ndesamburo kukamatwa walihutubia maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja vya NMC eneo la Unga Limited lakini baadae walitangaza kuuvunja mkutano huo na kuamuru umati wote uelekee kwenye kituo kikuu cha polisi walikokuwa wameshikiliwa Mbowe na viongozi wengine ili wakafuatilie kwa pamoja hatima ya viongozi wao.

Source: Tanzania Daima, ukurasa wa 2, alhamisi tarehe 6 Januari. 2011


My take: Busara hapa Slaa angewatutliza wafuasi wake na kuwaeleza warudi majumbani kwa amani na wao viongozi waende polisi kufuatilia hatima ya viongozi wenzao badala ya kuhamasisha umati wote kuelakea kituoni, nachelea kuhoji busara na uadlifu wa Slaa.
 
HUYU NI SHEHE UBWABWA
alikuwa anasubiri jumaaa kwenda kula ubwabwa na alichokiongea hakijui.

Shehe ubwabwa huyooooooooooooooooooo kazi kuka ubwabwa. Yahke yakhe ubwabwa leo
 
HUYU NI SHEHE UBWABWA
alikuwa anasubiri jumaaa kwenda kula ubwabwa na alichokiongea hakijui.

Shehe ubwabwa huyooooooooooooooooooo kazi kuka ubwabwa. Yahke yakhe ubwabwa leo

tusubirini tu tamko la mashekhe kiujumla leo nadhani watalitoa!sio la mmojammoja maana watu wanaweza kuwa wengi ila kila mmoja ana lake so viongozi wao wana kikao leo!
 
SHEHE KASEMA LILILO SAHIHI......chadema walijitakia kilichotokea kwa viongozi kuamuru wafuasi waelekee kituo cha polisi.....THEY GOT WHAT THEY WANTED.....ANYTHING MORE...?
 
Back
Top Bottom