Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Hii sio taarifa ya tukio bali ni tathmini ya utendaji wa jeshi letu la Polisi katika kukiuka haki za wananchi wa Tanzania, binadamu walioapa kuwalinda.
Hivi karibuni huko Kibaha kumetokea tukio la mtu kuuwawa kwa risasi, na mwili wake "kuokotwa" na wananchi. Ndugu wa mtu alieuwawa wanasema mtu huyo aliuwawa na Polisi wakiwashambilia kwa risasi wauza mkaa. Polisi, japo wanakiri kulikuwa na "mapambano" kati yao na wauza mkaa, wanajaribu kuonyesha sio wao waliomuua mtu huyo - naona wakimaanisha kwamba katika mpambano ule wauza mkaa wote walikwepa risasi zao!
Nitaweka hapa sehemu ya habari kuhusu muuza mkaa anaedaiwa kuwawa na Polisi huko Kibaha, halafu watu mtafakari kuhusu hizi kauli zinazotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo
Sasa Lutumo anasema waliwasimamisha wakiwa na boda boda zao, wakakaidi, na tunajua unaposema bodaboda alisimamishwa akakaidi ina maana alikimbia na bodaboda yake. Sasa suala la kupambana na askari linakujaje?
Sasa cha ajabu, mwili wa muuza mkaa unapatikana akiwa amepigwa risasi, polisi wanasema "umeokotwa na wananchi" kama vile wao hawahusiki na kuuwawa kwa mtu huyo, ambae ni mmuuza mkaa, na huku wakikiri waliwarushia risasi wauza mkaa. Hivi kweli, tumefikia mahali polisi anamfyatulia raia risasi, kosa likiwa kuuza mkaa isivyo halali?
Kama Polisi waliona ni halali kuwaua wauza mkaa kwa risasi, basi kwa nini angalau wasichukue mwili wa mtu waliemuua na kumpeleka hospitali kwa kuhifadhiwa? Kitendo cha kwenda kumlaza mahali na wao kuondoka ni wazi walijua wamefanya makosa, halafu wanakuja kutoa hadithi zisizo na pua wala mdomo kwa wananchi.
Tuseme ukweli, baadhi ya Polisi wetu ni wauaji, katili na waongo!