Wataalam wa ulinzi na usalama tutafsirieni kauli hii ya IGP. Je, ameelekeza polisi ama kuwarai?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Video imejaa na kusheheni taarifa muhimu ambazo raia tunapaswa kufahamu kuhusu utendaji wa polisi, itazame hadi mwisho....



NImekosa mlinganisho wa vifungu vya sheria kwa kauli ya IGP. Neno reasonable force inatafsiriwaje kisheria?

Je, polisi anapomkamata mtuhumiwa ambaye hana silaha na akamletea ubishi anaruhusiwa kumuua?

Mafunzo ya ukamataji salama yana nafasi gani kwenye majukumu ya polisi?

Je, Katiba ilikosea kwa kuamrisha kuwa mtuhumiwa hapaswi kuhukumiwa nje ya utaratibu wa kimahakama?

Sheria gani inaruhusu polisi kuua wanapomkamata mtuhumiwa?

Je, panyaroad imekuwa declared threat kwa taifa au ni kikundi cha ugaidi?

Kwa nini IGP hafanyi rejea ya vifungu vya sheria anapozungumzia suala la kutoa uhai wa mtuhumiwa?

Kauli ya IGP inatafsiriwaje kwenye utawala wa sheria?
 
Back
Top Bottom