JKU na POLISI: Lipi lina hadhi kubwa zaidi Zanzibar?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Yote ni majeshi, lakini Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ni linatumika Zanzibar pekee na Polisi linafanya kazi pande zote za Muungano.

Kwa uelewa wangu, JKU ni kama ilivyo JWTZ.

Japo JWTZ na POLISI yote ni majeshi, lakini kwa mtazamo wa watu wengi, hasa Watanyika(sijui Sheria inasemaje katika hilo), JWTZ linaizidi Polisi kwa hadhi.

Kwa muktadha huo basi, JKU kule Zanzibar inaweza kuwa na hadhi iliyo nayo JWTZ upande wa Tanganyika?

Nauliza hivyo kutokana na tukio lililowahi kutokea kule Zanzibar, la askari wa JKU kuvamia kituo cha Polisi cha Mwembe Madema ambacho ni Kituo Kikubwa cha Polisi cha Unguja Mjini, na kushikilia mateka askari Polisi aliyemkamata mwenzao kwa kosa la kukiuka Sheria ya usalama barabarani.

Ujasiri wa kukivamia kituo Kikuu cha Polisi waliutoa wapi? Hapo ndipo kulipo na ofisi kuu ya Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi. Kwa hiyo ni sawa kusema walivamia makao makuu ya Jeshi la Polisi Mjini Magharibi.

Walikuwa na silaha nzito kuzidi za Jeshi la Polisi?

Kati ya Jeshi la Polisi na JKU, lipi lina hadhi kubwa zaidi Zanzibar?
 
Attachments

  • KILICHOWAKUTA_ASKARI_JESHI_JKU__WALOMKAMATA_POLISI_KISHA_KUMPELEKA_KAMBINI(144p).mp4
    4.1 MB

JKU=JKT
 
Ndani ya swali lako kuna jibu lako,ila kwa kukazia zaid polis wakishindwa jku inaamua.
 
2015 uchaguzi baada ya kuwa na matishio ya uvunjifu wa amani,yalikwenda majeshi ya muungano visiwani.
 
Yote ni majeshi, lakini Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ni linatumika Zanzibar pekee na Polisi linafanya kazi pande zote za Muungano.

Kwa uelewa wangu, JKU ni kama ilivyo JWTZ.

Japo JWTZ na POLISI yote ni majeshi, lakini kwa mtazamo wa watu wengi, hasa Watanyika(sijui Sheria inasemaje katika hilo), JWTZ linaizidi Polisi kwa hadhi.

Kwa muktadha huo basi, JKU kule Zanzibar inaweza kuwa na hadhi iliyo nayo JWTZ upande wa Tanganyika?

Nauliza hivyo kutokana na tukio lililowahi kutokea kule Zanzibar, la askari wa JKU kuvamia kituo cha Polisi cha Mwembe Madema ambacho ni Kituo Kikubwa cha Polisi cha Unguja Mjini, na kushikilia mateka askari Polisi aliyemkamata mwenzao kwa kosa la kukiuka Sheria ya usalama barabarani.

Ujasiri wa kukivamia kituo Kikuu cha Polisi waliutoa wapi? Hapo ndipo kulipo na ofisi kuu ya Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi. Kwa hiyo ni sawa kusema walivamia makao makuu ya Jeshi la Polisi Mjini Magharibi.

Walikuwa na silaha nzito kuzidi za Jeshi la Polisi?

Kati ya Jeshi la Polisi na JKU, lipi lina hadhi kubwa zaidi Zanzibar?
Civic education kuhusu majeshi yetu, polisi na migambo inahitajika!. Tanzania tuna Majeshi ya Ulinzi, JWTZ, chini ya CDF, chini ya JWTZ kuna Jeshi la Kujenga Taifa, JKT.

Tuna Jeshi la Polisi PT Tanzania, chini ya IGP, chini yake kuna Jeshi la Zimamoto na ukosoaji, chini ya Commissioner, kunaJeshi la Uhamiaji, chini ya Commissioner, kuna Jeshi la Magereza chini ya Commissioner na Tume ya madawa ya kulevya chini ya Commissioner.

Tuna jeshi la Usalama chini ya DGIS, wale 'jamaa zetu'.

Majeshi mengine yote ni majeshi usu or polisi usu, yaani auxiliary army or police, hawa wote ni migambo, wakiwemo askari wanyapori, KMKM, JKU, Vikosi vya SMZ, ziko taasisi kibao zina majeshi yake wakiwemo Ultimate, Group 4 security, walinzi wa mgodi, walinzi wa meli baharini, etc. Wote hawa ni migambo!. Ni lini Vyeo vya Kijeshi (Collar Insignia) vimebadilishwa hapa nchini?

P
 
Civic education kuhusu majeshi yetu, polisi na migambo inahitajika!. Tanzania tuna Majeshi ya Ulinzi, JWTZ, chini ya CDF, chini ya JWTZ kuna Jeshi la Kujenga Taifa, JKT.

Tuna Jeshi la Polisi PT Tanzania, chini ya IGP, chini yake kuna Jeshi la Zimamoto na ukosoaji, chini ya Commissioner, kunaJeshi la Uhamiaji, chini ya Commissioner, kuna Jeshi la Magereza chini ya Commissioner na Tume ya madawa ya kulevya chini ya Commissioner.

Tuna jeshi la Usalama chini ya DGIS, wale 'jamaa zetu'.

Majeshi mengine yote ni majeshi usu or polisi usu, yaani auxiliary army or police, hawa wote ni migambo, wakiwemo askari wanyapori, KMKM, JKU, Vikosi vya SMZ, ziko taasisi kibao zina majeshi yake wakiwemo Ultimate, Group 4 security, walinzi wa mgodi, walinzi wa meli baharini, etc. Wote hawa ni migambo!.

P
JKU imeundwa na sheria ipi na sifa za mkuu wake ni zipi au ipo chini ya jeshi gani?
 
Mkuu kwa mujibu wa Katiba Ya zanzibar hayo uliyoyataja KMKM na JKU na Jeshi la mafunzo (magereza) ni Idara maalumu na sio mgambo..
 
Mkuu JKU,KMKM NA Jeshi la Mafunzo..
Vyote vimeundwa chini ya Katiba ya zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 121 mpaka 123 kama Idara maalumu..
Na kumbuka huko hakuna magereza..
Kuna Jeshi la Mafunzo ambalo nalo liko chini ya Idara hii maalumu..
CC: Wakili msomi Pascal Mayalla
Screenshot_20240203_091319_Adobe Acrobat.jpg
 
Mkuu kwa mujibu wa Katiba Ya zanzibar hayo uliyoyataja KMKM na JKU na Jeshi la mafunzo (magereza) ni Idara maalumu na sio mgambo..
Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT ina rais mmoja na Amiri Jeshi Mkuu mmoja tuu ambaye kwa sasa ni Amirati. Hayo majeshi ya Zanzibar, yote ni migambo tuu, ndio maana kule kuna polisi na jeshi letu.

Ila Tanzania ina sehemu mbili, Bara na Zanzibar, katiba ya Zanzibar inaitambulisha Zanzibar kama nchi na kuitambulisha hiyo migambo kama jeshi na rais wa Zanzibar ndie Amiri jeshi wa migambo hao, hayo ni mambo yao ya ndani, ki nchi hatuwatambui!.
P
 
Mkuu JKU,KMKM NA Jeshi la Mafunzo..
Vyote vimeundwa chini ya Katiba ya zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 121 mpaka 123 kama Idara maalumu..
Na kumbuka huko hakuna magereza..
Kuna Jeshi la Mafunzo ambalo nalo liko chini ya Idara hii maalumu..
CC: Wakili msomi Pascal Mayalla
View attachment 2892651
Hayo ni mambo ya ndani ya Zanzibar, katiba ya JMT, haiyatambui, Ulinzi ni jambo la muungano, hao ni wagambo tuu!.
Hata huo ukamanda wa rais wa Zanzibar kwa wagambo hao, sio Amiri Jeshi Mkuu ni kamanda wa wagambo!.
P
 
Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT ina rais mmoja na Amiri Jeshi Mkuu mmoja tuu ambaye kwa sasa ni Amirati. Hayo majeshi ya Zanzibar, yote ni migambo tuu, ndio maana kule kuna polisi na jeshi letu.

Ila Tanzania ina sehemu mbili, Bara na Zanzibar, katiba ya Zanzibar inaitambulisha Zanzibar kama nchi na kuitambulisha hiyo migambo kama jeshi na rais wa Zanzibar ndie Amiri jeshi wa migambo hao, hayo ni mambo yao ya ndani, ki nchi hatuwatambui!.
P
Mkuu Pascal..
Kwa Mujibu wa Katiba ya zanzibar, Katiba yao ni kubwa kuliko sheria yeyote ile...
Rais wao hawajibiki wala kuulizwa na Mtu yoyote yule kwenye uongozi wala hawajibiki kwa kiongozi yoyote..

Kwa mujibu wa katiba ya zanzibar Zanzibar ni nchi Iliyo kamilika..
Ina Spika wa Bunge..
Ina Jaji Mkuu..
Ina Rais Wa serikali..
Ina waziri Mkuu..
Ina mahakama kuu..
Ina mwansheria Mkuu..
......
Unasema Kama nchi hamuyatambui hayo kwa sababu wao kama nchi wanayatambua na Katiba ya Tanzania kule haitumiki..

Na kuhusu Majeshi ya Bara kuwa Kule mbona kule hakuna Magereza?
 
Hayo ni mambo ya ndani ya Zanzibar, katiba ya JMT, haiyatambui, Ulinzi ni jambo la muungano, hao ni wagambo tuu!.
Hata huo ukamanda wa rais wa Zanzibar kwa wagambo hao, sio Amiri Jeshi Mkuu ni kamanda wa wagambo!.
P
Unazungumziaje siku ya Mapinduzi Rais wa zanzibar kutambulishwa kama kaimu Amiri Jeshi mkuu...
Huoni kuna Ukakasi kisheria ukiwa kama wewe ni mwanasheria..
Kabla hatujaingia kwenye mjadala wa kisheria?
 
Back
Top Bottom