Kinachoendelea Loliondo: Shame on them! - Mwinyi, Mkapa, and Kikwete!

Haya mwingine huyooo, Nyerere ametokea wapi ktk mada hii! yaani tafran tupu...

Uwataje MaRais wa awamu tatu baada ya Nyerere usimtaje Nyerere, inakuwa aidha humtendei haki Nyerere au huwatendei haki hao wengine. Hapo ndipo Nyerere alipotokea katika mada hii. Ukweli unauma na ndio maana inakupata hiyo tafrani.
 
Umeshaenda kwa daktari?Unaumwa "something" nishakwambia!Ebu pita kwa daktari si mzima wewe!Kweli Nyerere kiboko!Yaani hata baada ya miaka 10 ya kuondoka bado "jamaa" wanamuota tu!!!ama kweli!!
 
Inaelekea huu ni mradi wa kudumu mpaka wahakikishe hatuna mbuga hata moja ya wanyama.
 
Shida tuliyonayo leo hakuna mpinzani wa kweli na Mzalendo kama Augustino Lyatonga Mrema alivyochachamaa mwaka 1993 kwenye hiyo kashfa ya Loliondo,Chadema hivi leo ukimtuliza Mboe basi umemaliza kila kitu,yule Tundu ni makelele tu kapewa chake nae kashiba,Lema anakula bure uko alipo na ada za watoto zinalipwa bure,huku Arusha anadaiwa sana na hana uwezo wa kushinda hata udiwani, salama yake ni kubaki huko aliko akiamka anaweka bando anaitukana na Serikali, mchana ukifika anaenda kuchukua mapaja ya kuku KFC anakula.
 
kumbe upo na Lema? unasema mchana anakuja kushika mapaja yako.... daaah wewe dada umejitoa mhanga sana. hongera
 
nyererer alishiriki kuwachagua mwinyi na mkapa.he must share the blame.....
Kwahiyo kama Nyerere alishiriki kuwachagua ndio akawa anawafundisha kila walilofanya kwenye utawala wao?

Akili ya sampuli gani hii!.
 
Shida tuliyonayo leo hakuna mpinzani wa kweli na Mzalendo kama Augustino Lyatonga Mrema alivyochachamaa mwaka 1993 kwenye hiyo kashfa ya Loliondo,Chadema hivi leo ukimtuliza Mboe basi umemaliza kila kitu,yule Tundu ni makelele tu kapewa chake nae kashiba,Lema anakula bure uko alipo na ada za watoto zinalipwa bure,huku Arusha anadaiwa sana na hana uwezo wa kushinda hata udiwani, salama yake ni kubaki huko aliko akiamka anaweka bando anaitukana na Serikali, mchana ukifika anaenda kuchukua mapaja ya kuku KFC anakula.
Wewe ni mbumbumbu.
Wakati wapinzani wanafanyiwa ufirauni na madhira kibao kipindi cha mwendazake, si ulifurahia wewe!!???
Leo ndio unaona umuhimu wao!!!???
Waambie hao wa chama chako ndio wakutetee.
 
Baada ya kuligusa suala la Meremeta nilidokeza kuwa ripoti tunayoifanyia kazi sasa ni ile ya kuelezea historia ya ufisadi wa makuwadi wa wizi wa kimataifa ulioanzia Loliondo na kugusa Ikulu yetu (chini ya Mwinyi) hadi suala Meremeta ambalo nalo liligusa utawala wa Mkapa, na suala la Dowans linalogusa utawala wa Rais Kikwete.

Lakini kabla hatujafika huko kote hatuna budi kusikitishwa na taifa letu kurudi nyuma tena karibu miaka 17 sasa kwenye kashfa ya Loliondo. Kama nilivyodokeza kwenye suala la Loliondo::connections watu wale wale waliokuja kama wawekezeji wamerudi tena na watarudi tena na kutufanya sisi tuwe watumwa katika nchi yetu.

Kampuni ya OBC ya UAE mdau wake mkubwa ni Brigadier wa jeshi la UAE na mtu wa karibu wa familia ya mtawala wa huko. Kwenye Dowans kampuni hewa ya Dowans (ambayo JK hakufuatilia kama vile hakufuatilia Richmond) nayo inamilikiwa na Generali wa jeshi hilo hilo la UAE na ambaye naye ana ukaribu na watu wa familia hiyo.

Kama vile tulio na wazimu katika vichwa vyetu tukawa tayari kupiga magoti mbele ya watu hawa hawa na kuwanyanyasa watu wetu ili tuwafurahishe makuwadi wa ufisadi wa kimataifa. Wamasai wa Loliondo leo hii wanaitwa wakimbizi katika nchi yao na malalamiko yao hayapewi kipaumbele wala kutiliwa maanani!

Na ni watu hawa hawa wa familia ile ile waliojaribu kuchukua eneo la Yaeda Chini na kusababisha njaa kwa watu wetu na watawala wetu wakawatetea; watu wa familia ile ile ya kina Zayed. Angalau kwenye kesi ya Bonde la Yaeda Chini tuliweza kupiga kelele na kuwatimua lakini Loliondo na Dowans hawako tayari kutuachilia.

Hawa watu wanatuahidi vitu gani hadi tuwe wanyonge na dhaifu mbele zao utadhani mbwa mbele ya chatu? Hawa majenerali wenye nyotanyota wanawaahidi nini watawala wetu na wanalainika mbele zao kama waliolishwa limbwata za kitanga?

Hadi inafika mahali waliochaguliwa na wananchi wanawatetea makuwadi wa ufisadi wa kimataifa ambao rekodi yao iko wazi ya jinsi gani wametumia vibali tulivyowapa vibaya, jinsi gani wameua wanyama wetu kiholela na kutorosha wanyama hai kwenda makwao kwa fahari ya watawala wa huko.

Kama vile watawala hawa hawa walivyoruhusu madini yetu kule Buhemba kuchotwa na mamluki wa kivita wa Afrika ya Kusini na kuendelea kutuimbia wimbo wa umaskini wetu huku tukijichekelesha mbele yao.

Nani alitulaani? Tuache kupiga kelele ili wauze hadi nepi za watoto wetu, na vitanda vya vikongwe vyetu vipigwe mnada? Tuache kuandika na kuhoji yanayotokea nchini mwetu kwa vile wao ni watawala? Tuache kuliamsha taifa kutoka katika usingizi wake kwa sababu tukifanya hivyo tunawaudhi wanaotembea na ving'ora na kutetemewa wakitembea?

Mnatupa uchaguzi rahisi; mnatupa uchaguzi ambao hatuwezi kuacha kuuchukua; ni uchaguzi usiohitaji shahada za Harvard wala utaalamu wa fizikia ya anga za mbali. Hatuwezi kufumba macho yetu na vinywa vyetu ili mtutawale mpendavyo.

Jifunze kuhusu original Loliondo Scandal ambayo inahisiwa kuhusishwa na kifo cha mwandishi mahiri wa uchunguzi Stan Katabalo hapa Bonyeza Hapa

View attachment 1021624

Napenda kujua msimamo wa wabunge wafuatao kuhusu Loliondo:

Dr. Harrison Mwakyembe
Lucas Selelii
mama Anna Kilango
Mzee Yusuph Makamba
John Chiligati
Samwel Sitta (Spika)

NB: Nilituma salamu kwa Apson na Mboma wiki chache zilizopita; nikatoa wito kwa RO juu ya kuwadi wenu. Mtu wenu mliyemtuma (DB) nimempa ujumbe wangu wa ana kwa ana wiki moja sasa (bahati mbaya kwenu, taarifa za ujio wake zilimtangulia); natumaini ameufikisha pasipo kuongeza chumvi. Endeleeni tu, kwani historia yenu imeonesha mmesimama upande wa kushindwa mara zote.
2009
 
Aiseeh

Wahusika wa madili haya ni wale wale, je ni nini dawa yake ya kudumu?
 
Wamasai wa Loliondo lazima waletwe kwenye karne ya 21 kama watanzania wengine. Mambo ya kuwafanya kama kivutio cha watalii kama nyumbu hayana ubinaadamu.

Mbuga ya Loliondo ni hifadhi ambayo inaleta fedha za kigeni, kwa hiyo lazima watu waondolewe kama maeneo ya makabila menginr yalivyo chukuliwa kuwezesha miradi ya maendeleo kwa manufaa ya watanzania wote.
 
Back
Top Bottom