Serikali yanunua V8 25mpya kutoka Toyota!

Jamani tuache kufuru ina maana haya ni ya wale waheshimiwa wa kuandaa mchakato wa katiba mpya au ya sensa? Walalahoi tunaangamia vifaa na madawa hospitalini hakuna, walimu ndio hivyo tena. Kama mambo ndio hayo inamaanisha hata chama kingine kitafanya hivyo hivyo kwa kufuata ule msemo wa aliyenacho ataongezewa!
 
Haya ni kwaajili ya kilimo kwanza, msilalamike jamani watagawawiwa mabwana shamba wa mikoa then tutaagiza mengine kwaajili ya kilimo kwanza wilayani.Matrekta, mbolea, training za wakulima sio mhimu kwasasa. Subirini
 
Haya ni kwaajili ya kilimo kwanza, msilalamike jamani watagawawiwa mabwana shamba wa mikoa then tutaagiza mengine kwaajili ya kilimo kwanza wilayani.Matrekta, mbolea, training za wakulima sio mhimu kwasasa. Subirini

MFuko wa mbolea zaidi ya laki moja,Mabwana shamba wanapewa pikipiki na kazi yao kubwa ni kuangalia machinjio ya ngombe basi na wakitoka hapo wanapiga muhuli wanavuta pesa na wanaondoka na steak kilo 5 wanaenda kuuza maisha yanasonga,hii ndio tz bwana!
 
Serikali ya Japan yenyewe haitumii haya magari!!!!!

Haki ya NANII
attachment.php
 
MFuko wa mbolea zaidi ya laki moja,Mabwana shamba wanapewa pikipiki na kazi yao kubwa ni kuangalia machinjio ya ngombe basi na wakitoka hapo wanapiga muhuli wanavuta pesa na wanaondoka na steak kilo 5 wanaenda kuuza maisha yanasonga,hii ndio tz bwana!

Kilimo kwanza ni hadithi ya siku hizi, ni kisingizio, hata viongozi wakitaka kutoka nje ya ndoa zao wanaaga kuwa wanaenda kufanya ufuatiliaji wa kilmo kwanza. Kilimo kwanza haina uhusiano wowote na maendeleo ya kilimo hapa nchini. sana sana wajanja wachache wa mjini wakiwemo wajeda.
 
Samahani jamani lakini naomba kuuliza. Mleta mada kaja na maneno tu kuwa serikali imenunua magari na kuweka thamanbi yake. Kisha akabandika na picha ya magari. Hivi hapa kuna uthibitisho wowote kwua serikali imenunua magari haya yanayoonekana kwenye picha?
 
The last time I checked Kikwete alisema ni mwisho wa kununua haya magari.
Just like he claimed to significantly reduce his tour trips abroad!
To my suprise, he still maintains a record if not to break his own.

Hata Waziri Mkuu ndani ya bajeti yake Bungeni alisema kuwa wanabana matumizi kwa kuto nunua magari haya.

Huenda wamepewa Bure na gharama za uendeshaji wanalipiwa na wafadhiri.

Yangu macho, na wewe ukitaka kula vizuri gombea uongozi wa juu serikalini utakula pasipo kuulizwa. Na mtu akikuuliza utamwambia "JAMBO HILO lipo MAHAKAMANI"



MIZAMBWA
INANIUAM SANA!!!!
 
INASIKITISHA SANA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nashindwa kuelewa ktk hili, kama ni kweli hayo ni magari ya serikali---kwa nini yamenunuliwa na ni mradi wa nani? kwa maslahi ya nani? ili kumkomoa nani? ili iweje?

NANI NI MKUU WA NCHI HAPA TANZANIA?
PM amesema V8 no..
MKUU WA NCHI amesema mashangingi no.. au kuna watu wengine wanaongoza serikali ambao wananchi hatuwajui? maana haiwezekani RAIS aseme no, halafu ajitokeze mwingine kumpinga, wenye kujua tujulisheni tujue nani anaongoza nchi

Kuna kucha asubuhi mashangingi yamepanga foleni, ukiuliza ya nani? jibu ni ya serikali.
Nani kanunua wakati PM na MKUU WA NCHI wamesema no kununua V8,
hili linasababisha hata viongozi kutukanwa bure kwa kutosimamia ukweli waliouweka wenyewe hadharani, kama walituongopea waseme tu

naomba ajitokeze msemaji wa serikali akanushe hii habari kuepusha aibu kwa viongozi wetu
 
Inawezekana wakati wa kutoa agizo la kutonunua aina hii ya magari yalikuwa yamekwishaagizwa
 
Back
Top Bottom