Serikali ondoeni haraka tozo hizi za matengenezo ya nyumba wakati huu wa mvua

Hiyo sheria imetungwa na Bunge au ni vi-sheria vya municipal? Sasa Mbona kuna kazi, nchi yetu hii dunia ya tatu, tuna umizana hivyo? Wangapi watajenga au ndio wameamua tusijenge wote tuwe wapangaji?

Yani Marekebisho ya nyumba yangu niilipe serikali kwa lipi? Cementi nikinunua nalipa kodi sasa kwanini nilipie kibali au wanajenga wao?
 
Malalamiko ni pale mvua imebomoa sehemu ya nyumba na mimi ninapoamua kurekebisha ili mvua isiendelee kubomoa ninakamatwa!
 
Hiki ni chanzo cha mapato cha mtendaji wa mtaa wetu. Tena anavuzia mwenyewe bila mwenyeji wake kitongoji
 
Hismastersvoice using'ang'ane kusema mvua imekuharibia ndio wakusamehe, unachotakiwa kuhoji ni uhalali wa tozo za hivyo vibari na kukemea mambo ya tozo kwa kila kitu katika nchi yetu. Haya matozo yanafanya miji yetu iendelee kuwa kama mapango ya walanguzi, miji nyumba zimepauka rangi au nyumba fupi, hali ya uchumi kwasasa sio nzuri kabisa wachache wanaweza mudu gharama za ujenzi au ukarabati kwa mara moja sasa hawa/ambao hatuwezi ni lazima tujichange na tufanye kwa awamu, sasa kwa kila awamu tutakuwa tunalipia hizo tozo?.

Tunaponunua vifaa vya ujenzi wanachukua kodi, kwenye biashara wanachukua kodi na ushuru wa huduma tena pesa nyingi 0.3% ya turnover lakini hizo tozo zote hakuna cha maana wanachofanya kwamba wanajenga barabara zetu mitaani hapana, wanaboresha hali ya upatikanaji wa umeme hapana, kwamba wanawezesha wananchi kiuchumi hapana, kwamba wana boresha huduma za afya, maji na elimu hapana matokeo yake wanazidi kukukopa sana nje ya nchi na deni la taifa linazidi kupaa, wananunua ma V8 new model kila mwaka, wana neemeshana wao kwa wao na bado wanataka waendele kuchukua tozo kila mahali.

Ni wakati sasa na muhimu sana kuwakemea hawa viongozi kwasababu hawana tofauti na wanyang'anyi.

Tozo zinaangamiza hii nchi wala hazijengi kwasababu wakusanya tozo hawajui kuzitumia. Kuna rule ya 20/80% ni muhimu serikali iitumie.
 
Wewe unaniambia nilipe service Levy ya 5,400,000 kweli kwa lipi ambalo mnalifanya? Leseni ya biashara nalipa, tena service levy ambapo hakuna chochote cha maana mnafanya kupitia hiyo. Pesa ya takataka mnakuja chukua kwangu mwenyewe, pesa za mwenge mnapita mtaani mnaomba michango, umeme kodi kibao na sio wa uhakika, tunapoteza pesa nyingi, hali ya maisha sio nzuri, uchumi kila siku unazidi kudorora. Serikali inashindwa kusimamia baadhi ya mambo au sijui wanashirikiana kweli tunauziwa dola 1 shilingi 3000 za kitanzania na baadhi ya makampuni. This is not fear. Wananchi watakuja wachoke hii nchi kinuke. Sio vizuri tuheshimiane aisee.
 
Hismastersvoice using'ang'ane kusema mvua imekuharibia ndio wakusamehe, unachotakiwa kuhoji ni uhalali wa tozo za hivyo vibari na kukemea mambo ya tozo kwa kila kitu katika nchi yetu. Haya matozo yanafanya miji yetu iendelee kuwa kama mapango ya walanguzi, miji nyumba zimepauka rangi au nyumba fupi, hali ya uchumi kwasasa sio nzuri kabisa wachache wanaweza mudu gharama za ujenzi au ukarabati kwa mara moja sasa hawa/ambao hatuwezi ni lazima tujichange na tufanye kwa awamu, sasa kwa kila awamu tutakuwa tunalipia hizo tozo?.

Tunaponunua vifaa vya ujenzi wanachukua kodi, kwenye biashara wanachukua kodi na ushuru wa huduma tena pesa nyingi 0.3% ya turnover lakini hizo tozo zote hakuna cha maana wanachofanya kwamba wanajenga barabara zetu mitaani hapana, wanaboresha hali ya upatikanaji wa umeme hapana, kwamba wanawezesha wananchi kiuchumi hapana, kwamba wana boresha huduma za afya, maji na elimu hapana matokeo yake wanazidi kukukopa sana nje ya nchi na deni la taifa linazidi kupaa, wananunua ma V8 new model kila mwaka, wana neemeshana wao kwa wao na bado wanataka waendele kuchukua tozo kila mahali.

Ni wakati sasa na muhimu sana kuwakemea hawa viongozi kwasababu hawana tofauti na wanyang'anyi.

Tozo zinaangamiza hii nchi wala hazijengi kwasababu wakusanya tozo hawajui kuzitumia. Kuna rule ya 20/80% ni muhimu serikali iitumie.
Tozo lazima ziwepo kwa sababu sisi wananchi tunawakumbatia wanaofuja kodi zetu, leo hii serikali inaajiri wapigadebe akina Mrisho Mpoto na mzee wa v8!
 
Yamenikuta najuta kuwa na kibanda, wiki iliyopita mvua ilinyesha usiku na kubomoa choo cha nyumba yangu cha mtindo wa pasipoti sasa hivi, asubuhi kulipokucha nikaenda kununua simenti na matofali na kuamua kukijenga upya, hamadi serikali ya mtaa kumbe nao wanajua watatupata, wakanidaka.

Baada ya kunifikisha ofisini kwa nikidhani naenda kupewa msaada nikaambiwa ninajenga bila kibali!

Nikajiuliza hiyo mvua imebomoa bila amri ya mahakama mimi naamniwa adhabu yangu nilipe shilingi laki mbili! Sijui nitazitoa wapi huku nikiwaza kwanini wao wasinipe msaada huo lakini jamaa hawna utani nilipe hizo hela.

Hili limenikuta lakini je, ni watanzania wote waliobomokewa na nyumba zao watalipa pesa za kibali cha ujenzi au bahati yangu mimi kuiingizia mapato serikali wakati huu wa mvua?

Nimesimamisha ujenzi na sina choo inabidi nitumie cha jirani wakati wa mchana na usiku kuna lile kopo letu la jadi maarufu kwa jina la sululu.
Usisahu hili wakati unaenda kuikataa CCM uchaguzi ujao
 
Watu hawana huruma na watu, inawekana wazo la alieanzisha kuwe na kibali cha ujenzi, alikua na maana mzuri, hasa kwa ujenzi mpya, ili kudhibiti migogoro ya Ardhi.
Lakini watu sasa wamegeuza biashara hivyo mtu akiwa na pesa ndefu, anaweza kupewa kibari na kwenda kujenga eneo la mtu mwingine.
Hivi mtu anarekebisha makazi yake halali, kibali cha nini, kinasaidia nini, kujenga choo, au kubadili sinki la choo ndani ya nyumba yangu, eti mpaka kwa kibali cha serikali, na mara nyingne marekebisho hufanya kwa kulazimika. Serikali hii sheria iangalie upya watanzani wamskini sana tusibanwe kila kona ni hatari sana hii.
 
Mama alikwisha sema "chagueni upande ule lakini CCM ndiyo itaunda serikali".
Usiyumbishwe na maneno ndo hao hao wakati mzee yupo kwenye life support machine wao walituambia anachapa kazi na anatusalimu...
 
Mtaani kwetu mtendaji amewema maspy kila kona. Ukionekana na kakoleo tu au umemwaga mchanga wajomba wanatia timu.
Kujenga fensi, flemu, kupaka rangi au kufanya boresho lolote achilia mbali ujenzi kabisa sharti ulipie kibali, Tena kama ni marekebisho lifespan ya kibali ni mwezi tu baada ya hapo kama ujenzi unaendelea basi utakat na kulipia kipya.

Hatare sana.
Huyo Mtendaji hawafai
 
Usiyumbishwe na maneno ndo hao hao wakati mzee yupo kwenye life support machine wao walituambia anachapa kazi na anatusalimu...
Mbona salamu zake mlizipokea kwa nyimbo za mapambio, Patapanda italalia parapanda...
 
Back
Top Bottom