Serikali kukopa Stanbic ni sahihi?

Tumedanganya danganya mpaka sasa tumeishia kujidanganya wenyewe. Hii nchi haina mjomba wala shangazi wa kuiletea maendeleo. Kila kukicha ni kuzunguka duniani kwa kutumia hela nyingi eti kuomba misaada ya donors. Sasa mbona tumerudi kwenye basics zinazotumiwa na yoyote anayetaka kujiletea maendeleo?
Tutumie vichwa vyetu vizuri jamani!!!
 
Pia mishahara ya wabunge na marupurupu yao ianze kukakwa kodi kama ilivyo kwa Wafanyakazi wengine nchini.
 
Mimi bado naona kutakuwa na tatizo la ukiritimba kumpa waziri mkuu madaraka ya maamuzi yote hayo. And in future akitokea waziri mkuu say too lax, au extra strict and stringent tunaweza tusiachieve what we think we ca n achieve. Wakati mzuri wa kudeal na mambo yoter haya ni wakati wa budget of which every expenditure has to be justified. Pia kuwe na a strict follow up na uwajibikaji, Something that I do not see hata kwenye hiyo ofisi ya PM.

The other important thing is to introduce a government shared database for expenditures. Say any thing above 1 million $ must be approved or seen by the president, above $300,000 but not 1m by PM, and above $100 mn but less $300,00mn by respective ministers. Just as it is in Corporates. It will be simple kujua on the same day govt imespend how much and on what! I know most of us think it is impossible in Tanzania. Just think of wizara, ziko ngapi? But in reality inawezekana tena we can start this coming financial year! Hela ya kuinvest in the said database inaweza kuonekana nyingi lakini in the end savings will be much more. Kama project yeyote kutakuwa na some hurdles in the beginning lakini with continous improvement tunaweza kufika tu!!
 
Pia mishahara ya wabunge na marupurupu yao ianze kukakwa kodi kama ilivyo kwa Wafanyakazi wengine nchini.

Kwi kwi kwi!
BAK unatafuta ugomvi na wabunge weye! Watakutoa macho.
Anyway, just kidding.
Nadhani hio ni njia mwafaka ya kupunguza vitambi vya wabunge, posho na mishahara yao ikatwe kodi kubwa tu!
 
Mkulo, mkopo huu unaleta wasiwasi


Wednesday, 26 May 2010 04:36
Majira

SERIKALI imesema itakopa dola za Marekani mil.250 (sawa na sh. bil.350) kutoka benki ya Stanbic ili kuziba mapengo kwenye bajeti ijayo ya mwaka wa fedha wa 2010/11.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo wakati akizungumza na waandishi wa habari .

Bw. Mkulo, alisema hatua hiyo imetokana na uamuzi wa baadhi ya wafadhili kupunguza michango yao kwenye Mfuko wa Bajeti (GBS) kwa jumla ya kiasi cha dola za Marekani 220

Akabainisha kwamba serikali ipo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo kati yake na benki hiyo (Stanbic), ambayo imekubali kutoa mkopo huo utakaolipwa kwa kipindi cha miaka mitano na wakati huo huo, aliwatoa wasiwasi wananchi kwamba hatua hiyo kamwe haitaongeza mzigo kwa walipa kodi.

Pamoja na nia nzuri ya kuziba mapengo hayo, tunachelea kuunga mkono moja kwa moja hatua ya serikali kukopa fedha kwenye mabenki ya biashara kwa ajili ya matumizi yake.
Duniani hakuna serikali inayokopa kutoka kwenye mabenki ya kibiashara (commercial banks) kwa ajili ya matumizi yake. Hii inatokana na ukweli kwamba riba za benki hizo ziko juu na masharti ya marejesho yake, ni kwa muda mfupi.

Mashirika ya fedha ya kimataifa kama Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Maendeleo ya Afrika na mengine ya namna hiyo yenye riba nafuu, ndiyo yanayopaswa kuzikopesha serikali kama Tanzania na kamwe benki za kibiashara, haziwezi kukopesha nchi kwa ajili ya kuendesha shughuli zake kwenye bajeti ya serikali.
Mikopo inayotolewa na benki hizo inaweza kutumika tu kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa maana ya kuongeza wigo wa kukusanya kodi.

Ni ukweli ulio bayana kwamba benki nyingi za kibiashara nchini riba zake ni kubwa kwa wastani wa asilimia 18 wakati vyombo kama IMF, WB, ADB riba zake ziko chini na vinatoa muda wa kutosha kurejesha fedha hizo na masharti nafuu ya kulipa.

Wasiwasi wetu ni kwamba pamoja na kauli ya Waziri Mkulo kuwa mkopo huu hauwezi kuwabebesha mzigo walipa kodi, bado tunaona jambo hilo haliepukiki.Ili kuzuia hilo, serikali itafute vyanzo vingine vya kuziba mapengo ya bajeti badala ya kukimbilia kukopa kwenye mabenki ya kibiashara.
 
Hii habari nafikiri wameitoa JF anyway huo ndio wasiwasi wetu mkubwa tusije kuambiwa nchi imeshauzwa kwa mabenki halafu tukaanza stori
 
Kama nchi tunakopa benki kwa ajili ya kucover budget yetu?? where is cash budget system??

hii kwa haraka haraka inaonyeshaa uchovu wa serikali katika kusimamia mapato na matumizi yakee..

mkopo huu wa stanbic una athari kubwaa kwa walipa kodi na utaathirii uchumi kwa maana ya kuchochocheaa mfumukoo wa bei!!!

wapi heshima ya tanzaniaa katika kupunguzaa madeni yake kutoka taasisi za kimataifa mpaka tukafutiwa sehemu ya madeni hayo (ref HIPC)!!!
 
Ni Mkulo huyo huyo anaedai uchumi wetu unakuwa sasa kitu gani kinaleta haya. Hivi kweli unaweza kuw na uchumi imara ukashindwa kujilisha bila kutegemea wafadhili. Tunahitaji mabadiliko ya serikali na sio hii inayotupa hadithi za alinacha.
 
hii sasa ni dhahiri kwamba CCM imefika ukomo wa kufikiri katika kufika suluhu ya matatizo ya nchi=kuinua/kuimarisha uchumi.

Nakerwa sana na fikra za viongozi wa CCM kutuona watanzania 'hamnazo' a.k.a mbumbumbu!!! kwamba mkopo huu hautakuwa na athari kwa mtanzania na nchi kwa jumla wake....hiyo bank ni ya mjomba wetu? the best solution ilikuwa ni kusahau hiyo deficit na ku-identify maeneo yote yanayopoteza pesa na yatakayoingiza pesa na kukomaa nayo ila nasikitika yote mawili CCM hawayawezi hata wakipewa miaka 100. wao ni kutafuta TShs. 1000 na kutumia TShs. 3000!!

Tuwaondoe hawa watu kisha tupeni CHADEMA muone madini, uvuvi, utalii tu vinavyoweza kufanya wonders forget about kodi za PAYE na kukimbizana na mama ntilie huku kina Somaiya na Manji na Barick wanabembelezwa kulipwa kodi.
 
Tra inakusanya bil 400 kwa mwezi bado vyanzo vingine, halafu yeye akakope bil 200 kwa haraka namna hiyo badala ya kufikiria adjustment ya budget.kwani ni mambo mangapi ya huduma za wananchi directly tunaambiwa budget haitoshi?atuambie hizo bil 2 atatumiaje?wizi mtupu
 
Msajili wa HAZINA JANA KASEMA MASHIRIKA MZIGO KWA SERIKALI TRL NA ATC YAVUNYWE YAUNDWE UPWA KWA UFANISI KAMA TIC -BIMA, KAWAMBWA HATAKI ETI ANATAFUTA WACHINA WAWEKEZE MATOKEO YAKE WAFANYAKAZI WANAKULA MISHAHARA ETC YA BILA KUFANYA KAZI.HAPO TUNA VIONGOZI?ATC-ATCL-AT....----,TRC-TRL-TR....
 
Serikali hii ina rekodi mbaya sana katika kulipa madeni yake. Madeni yake ya matumizi ya umeme, maji na huduma nyingine hukaa miaka chungu nzima bila kulipwa na kufikia mabilioni ya shilingi.

Kwa hiyo kutokana na rekodi yao mbovu hili deni halitalipwa na kama riba itakuwa 18% baada ya miaka mitano deni hilo litaongezeka toka $250 millioni na kufikia $571.93 millioni ili tu kuendeleza matumizi mabovu ambayo hayaleti maendeleo yoyote katika Tanzania yetu.
 
Huyu Mkulo bora ata ya mawaziri waliopita, nakumbuka kama si kosei aliyekuwa waziri wa fedha kabla, alisimamisha serekali kufanya biashara na mabenki ili kushusha garama za mikopo kwa wananchi.

Benki wakifanya biashara na serikali, huduma kwa jamii inalega. Afterall, wanapata faida kubwa na riba kutoka kwenye serikali. Rates za mikopo benki TZ ni wizi mtupu!.

Waandishi wa habari, ninajua mnapoitwa na huyu Mkullo kila mtu anaondoka na fungu. Sasa hii isiwe ndio sababu ya kutohabarisha wananchi ya kweli...Mkullo ni kilaza, kucheka cheka kama ndugu yake. Akiletewa matumizi ya safari kutoka ikulu, haulizi maswali au kujaribu kubana matumizi, yeye nikutoa tu. Aseme ukweli safari za JK na maafisa wake zimetugharimu taifa letu.

Si lazima uwe donor kuona ufujaji wa tax payers money


NDIO MAMBO YA BONGO MNAMPENDA YULE MNAYEKULA NAYE
 
kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya majibu ya mkulo.

1) hivi kama ni kweli ilifahamika toka awali kwamba wafadhili watapunguza msaada wao mwaka huu, kwanini imemchukua zaidi ya wiki moja mkulo kutoa msimamo huo.....na kwanini his initial reaction iliyokuwa reported kwenye media alionekana kustuka? Hili linaleta walakini juu ya majibu ya bw mkulo (unless kama alikuwa hajui hizo latest info.....ndio amekuwa briefed....na if that is the case then ameonyesha kukosa umakini...itakuwaje mtu mwenye dhamana ya masuala ya pesa asiwe informed kwenye jambo nyeti kama hilo?

2) hio altenative measure waliyochukua ya kukopa kwenye commercial bank....terms zake ni zipi? Serikali italipa riba kiasi gani? Kwa kawaida, serikali haikopi from commericial banks.....kwasababu riba zake zipo juu na pia ni mara chache commercial banks kutoa long term soft loans - kama matumizi yake ni kwa ajili ya kugharamia recurrent expenditure...

3) hivi hakuna altenative ways za serikali ku raise hizo fedha? Je ile option ya kuuza treasury bonds haifai kutumika kwa hapa? Kwa kuwa mkulo anasema uchumi ni imara na sasa nchi inaheshimika na imetoka kwenye kundi la nchi masikini sana....kwanini wasi issue bonds zikanunuliwa kwenye soko.....nikiri wazi mie sio mchumi hivyo pengine sielewi vizuri mfumo huu...

4) kwanini maelezo ya mkulo yanatofautiana na maelezo ya donors...? Who is not telling the truth? Donors wanasema wamesitisha kwasababu serikali haijaweza kutekeleza makubaliano kadhaa.....mkulo anasema walishakubaliana na donors kwamba mwaka huu watapunguza pesa za msaada kwakuwa waliikopesha serikali wakati wa economic crisis mwaka jana? Statment hiii ya mkulo ni mpya....donors waulizwe kama ni kweli haya ndio yalikuwa ni makubaliano....

5) nilitegemea katika statment yake mkulo angeweza kuelezea kwamba serikali ina mkakati wa ku cut costs ili kukabiliana na upungufu huo wa fedha, na pia kukabiliana na hali mbaya ya uchumi kwa ujumla inayoikumba dunia na haswa nchi za ulaya ambazo ndio wafadhili wakuu wa tanzania.

nadhani waandishi wetu wa habari wanahitaji kuuliza maswali haya ya msingi kwa mkulo na donors ili ukweli halisi ufahamike

bonds wanauza sana kwa nssf ndio maana unaona miradi mingi ya serikali inafanywa na nssf.
Halafu serikali yetu credibility yake sio nzuri kwa hiyo haiwezi kuuza bonds kubwa kwa watu wa nje

misamaha ya kodi ni mingi mno na ukwepaji wa kodi unaofanywa na wachangiaji wa ccm uko wazi kabisa. Kama ukihakikisha wachangiaji wa ccm wote wanalipa kodi vizuri basi hiyo hela inapatikana
 
Nimeamua kusema, ndiyo imeniuma na nimesikitika sana ati Serikali ya Awamu ya nne ya Rais Kikwete baada ya kunyimwa misaada na Wahisani imeamua kukopa Benki ya Biashara tena ya watu binafsi na Makaburu wa zamani wa Afrika Kusini iitwayo STANBIC!

Waziri wa Fedha alikaririwa na vyombo vya habari akidai eti Serikali itakopa DOla za Marekani milioni 200 kutoka Benki ya STANBIC ili kuziba pengo lililosababishwa na Wafadhili kugoma kutoa pesa hizo ili kuziba pengo la Bajeti ya Serikali mwaka 2010/2011 akijigamba ati Tanzania kwa sasa inakopesheka na inaweza kukopa popote- WB, IMF na TAasisi nyingine za Kimataifa. Cha kushangaza ni hatua ya Serikali kuomba mkopo Benki ya Biashara ya STANBIC badala ya Taafisi za fedha za Kimataifa (WB, IMF etc)!

Badala ya kukimbilia kukopa STANBIC benki binafsi ya biashara tena kwa riba kubwa, kwa nini isingechukua hatua mbadala zifuatazo?

1. Kubana Matumizi ya Serikali kupitia kupunguza au kuacha kabisa safari zisizo tija za Rais, Mawaziri kwenda nje ya nchi na hata safari za ndani?

2. Kuachana na Semina na vikao ambavyo vimekithiri kwenye Wizara na Idara za Serikali ambazo kwa makusudi hufanywa kwa madhumuni ya kupata posho.

3. Kuondoa kabisa bajeti za chai na viburudisho kwenye Wizara za Serikali ambazo mwaka huu pekee ni zaidi ya shilingi bilioni kumi!

4. Kubana mianya ya wizi na matumizi mabaya ya pesa za umma ambao kwa mwaka huu umeigharimu Serikali zaidi ya shilingi bilioni 200!

5. Kupandisha kiwango cha kodi ya VAT hadi asilimia 20 iliyokuwa mwaka uliopita kabla ya kupunguza na kuifanya iwe asilimia 18.

Serikali ingewashirikisha Wachumi na Taasisi mbali mbali zenye kuheshimika kama ERB (UDSM), REPOA, na ESRF ili kujadili namna ya kuziba nakisi hiyo badala ya kwenda kukopa Benki ya STANBIC. Ni afadhali mara mia moja kama Serikali ingeenda IFM, WB, IFC au hata Benki za hapa nchini kama vile CRDB ili kuweza kupunguza nakisi hiyo kuliko kwenda Benki ya STANBIC ambayo riba yake ni ya kibiashara zaidi kulinganisha na IMF,au WB.
 
hatuna viongozi........watanzania tumelala,hatujui impact ya mikopo kwenye mabenki ya kibiashara......hv serikali yetu kama iliweza kukopa nssf na kufund ujenzi wa udom why not kutokutafuta mikopo huko?na kama ccm ambayo ndio chama tawala wanaraise 40 billion kwa kampein why not wasiongezee kwa budget??fine labda kiwango ni kikubwa why not wb...........mmh kunakitu hapa.....interest rate haipungui 22%hadi vijukuu vyetu vitakuja kulipa haya madeni.....tunauzwa jamani hivi hivi......kwanini tusiungane kuquestion hivi vitu??fedha hizi wanazokopa ni kwaajili ya kwao ...vikao vyao na kamati zao........chunguza uone security wameweka nn.......usije ukashangaa ukakuta na mbuga za wanyama ama eneo fulani lenye madini ya urenium......mmh kazi ipo!!!
 
Serikali makini haiwezi kukopa kwenye benki za kibiashara kwani yenyewe haifanyi biashara. Huu ni upuuzi wa Mkullo, nahisi kuna ajenda ya siri!

Anachotakiwa kufanya ni kuuza goverment securities ambazo huwa ni long term na zina riba ndogo kwa kuwa serikali ni kitu kinachoaminika 100%
 
Kama kawaida watu wengi hapa wanalalamika tu wachache sana wanajaribu kutoa suluhisho na nina uhakika hakuna anayejaribu ku-implement. Wanajamvi mi nadhani imefikia wakati tuamue kitu kimoja aidha tufanye vitendo vya kukomesha huu ujinga ujinga unaondelea hapa Tz au tukae kimya. Tunaandika tu kila siku inasaidia kitu gani........
 
Back
Top Bottom