Serikali kukopa Stanbic ni sahihi?

Niliwahi kuayazungumza haya before the aftermath ya hii ni kwamba nchi itauzwa tutakuwa tena wananchi hatuna sauti na rasilimali zetu kwani zitakuwa chini ya mabenki ambayo yanamilikiwa na watu binafsi. Sasa sijui tutaita ni ukoloni au nchi ndio inauzwa sijui but hii ndio CCM
 
bila mabadiliko hamna kitu.mkulo anataka akope azuge miaka mitano bila kulipa kimbembe atuachie baada ya muda wake kuisha.maelezo yalikuwa ni faida ziara za rais nje.mbona naona hizo wanazokopa ni ndogo kuliko alizotumia kwenye ziara.na hao wahisani hawana huruma?hela yetu tumemaliza kwa safari za kwenda kwao leo wanaona tumeishiwa wanatutolea nje.na sisi siku nyingine hatuji tena.tunachanganya na zetu.
 
Tukiwaambia ukweli they call us names, utasikia wavivu wa kufikiri! Mkullo alipoulizwa kuhusu impact ya serikali kukoba pesa zote hizo ( Tshs 220bn) kutoka benki ya biashara kwa walipa kodi, eti anajibu hii haitawaathiri walipa kodi! sasa ukajiuliza serikali hii haifanyi biashara, sasa italipaje deni hili kama sio kutoka kodi zetu?
 
Dah wakati mwingine inashangaza kuona JF ni sehemu ya kulalamika na kulialia juu ya kila uamuzi wa serikali. Ni serikali ipi duniani haikopi?

Serikali ina njia kadhaa ya kupata fedha, borrowing is among them. Wanaosema kwamba serikali haifanyi bihashara ni dhahiri kwamba elimu yao haijai kiganjani; serikali inauza na kununua securities takriba kila juwa linapochomoza. Kabla hatujaendeleza "tamaduni" ya kulalamika na kukemea ni bora tukarejea darasani kidogo na kuangalia mahusiano ya shughuli za serikali, benki, na uchumi wa nchi. Vinginevyo wanaotusoma hapa JF (including the Mkulos) wanatuona kana kwamba akili zetu ni mchanyato wa ubongo na togwa.
 
Nadhani ndugu yangu una uhuru wa kusema kama sie tulivyo na uhuru wa kusema. But unapotuhukumu kuwa sie tuna mtindio wa akili kwakweli unakuwa umetukosea haki kwani tunatumia haki yetu ya kikatiba kuzungumza lile tunaloliona. Sasa ngoja nikupe darasa kwanini sie tunalalamika maana umetwambia hatuendi darasani.

Serikali inapokopa kwa kukutumia T-bills, au government bonds ni kwamba zile ni securities ambazo inazitumia kuraise liquidity (mkusanyiko wa fedha). Lakini tofauti yake na mkopo ni kwamba serikali inatangaza gawio au interest inayotaka kulipa kwa kuazima hizo pesa hivyo basi unakuta maranyingi interest hiyo haiwi kubwa kulinganisha na mkopo wa kawaida. Vile vile Serikali inakuwa na discretion ya lini italipa hizo pesa mfano kuna 90 days bills, 180 days, 360 days, 1 year bond, 2 year, 5 year etc. Lakini unapokuwa umekopa katika mabenki mfano overdraft facility kila siku wanakuwa wana charges zinazoambatana na mkopo huo. Vilevile ile overdraft inachajiwa interest in accordance to the prevailing market rates.

Sasa kwa Tanzania interest katika loanable funds ni 18-23% kama haijabadiilika kuzidi. Wakati interest kwenye Tbills ni lower zaidi ya hiyo kwa akili ya mtu wa kawaida unadhani inamake sense kwenda kuchukua mkopo wenye riba ya juu ukaacha mkopo wenye riba ya chini unless uwe umekunywa pombe. Na kwanini wasiissue securities kuraise more capital? Unakuta kwamba serikali imekwama with liquidity shortage na sasa inatafuta a quick alternative ya kuraise cash.

Sasa katika bank njia rahisi ya kupata cash ni kuchukua overdraft facility ambayo ni mara moja kuipata kama wewe mteja mkubwa. Hatari iliyopo ni charges zinazoambatana na facility hiyo na interest inayochagiwa. Vilevile kama serikali ikishindwa kulipa inamaana serikali itakuwa imeweka collateral (rehani) rasilimali fulani ambazo sijui bunge lina taarifa nazo au la? Sasa kimkopo kama serikali yetu iko makini sio tatizo but kama serikali yetu haina misingi mizuri ya usimamiaji wa kodi matumizi ya mabovu ya pesa ni hatari kwasababu hizi pesa zinatakiwa kulipwa on time na ukichelewa deni linaongezeka.

Sasa usifikiri watu tunapayuka kama wendawazimu bali tuna akili zetu na vilevile tumeshaona vyanzo vyote unavyovitazama wewe tukaona kwamba hili linaweza kusababisha a sovereign debt crisis kama iliyopo Greece na Spain. Na vilevile hatulalamiki ila tunaleta changamoto kwasababu nchi ikishatawaliwa na mabenki ndio hatuna sauti wananchi zaidi ya kukubali mabadiliko hivyo kabla hatujafika huko tusema tusije tukaambiwa mlikuwa wapi wakati tunafanya maamuzi.

Kuna maswali matatu naomba niwaulize Mkulo na wenzie:

a. Wameshindwa nini kuraise funds kwenye capital market (soko la mitaji) kwa kuuza hisa za serikali mfano bonds?

b. Wameshindwa nini kwenda kukopa katika development banks kama World Bank, IMF, ADB, EADB kuna ishu gani inaendelea?

c. Wameshindwa nini kupunguza fiscal policy budget instead budget ya serikali inakua kila siku? Hawajui kuwa mtu ukiwa huna kitu unapunguza matumizi yako kuweza kusave kiasi kidogo cha pesa?
 
Dhahabu bado hiko juu usd 1241.00/ounce na TZ ni nchi ya Tatu kwa uzalishaji Africa....

....inayoingia treasury haifiki hata 1%,forget about gold maana haina msaada wowote kwa Tanzania,sana sana kinachoingia serikalini ni payroll tax ya wafanyakazi wa migodini (wazawa maana wazungu hawalipi),if you look deep kwenye hii mikataba utajua hata machinga na mama ntilie walioishia darasa la pili wana akili kuliko hawa viongozi waliotuingiza humu...aibu tupu!
 
mnategemea nini kutoka kwa mtu kama Mkullo? hana akili kabisa yule,na kwa speed ya shillings inavyoanguka na ukiongeza inflation inayosababishwa na akili fupi za kina mkullo na wenzake wa BOT sijui kama kuna mtu anaweza nunua securities kwa bei ya madafu,TB za BOT ni hasara tupu...na hata hao stanbic itakuwa ni rushwa tupu,ukiangalia kwenye ratings agency zote(moody,finch etc) Tanzania haikopesheki kabisa ni D category....wakate matumizi tuu na waongeze efficient TRA hizo 200bn watazipata kwa week mbili tuu.
 
Sawaaa, lakini hata kama ukiambiwa ukope kwani na wewe ndio huna akili ya kupambanua?

Kwanini tusitumie rasilimali zetu kibao kwa ajili ya bajeti na matumizi yetu? Sijui tunaenda wapi na ni nani atatuongoza
Tunaongozwa na CCM na CCM ingekua na uwezo wa kupambanua mambo Tanzania ingeshaendelea siku nyingi.
 
Pamoja na matatizo mengine, hili pia nimeliona. Ikimweka Mkulo aongee na hawa donors, kwa kweli huyu mtu anapwaya. Hawa wafadhili wanapokutana na mtu anayeweza kujieleza, kuwavutia na mwenye msimamo mambo huwa yanakwenda. Lakini wanapokutana na huyu Mkulo wanatuona kama watu wasio na mwelekeo..Viongozi wetu nao wanatupoza. Kama Mkulo unapitia hapa, naomba mara nyingine deligate someone who can do the job!
 
Tatizoo serikali (Tanzania) ni matumizii mabovuu na usimamizii hovyoo wa mapatooo yetuu.. Mkulo kama kiongozii wa sera za kifedha na usimamizi wake nchinii ameonyeshaa uwezoo mdogoo kulikoo inavyowezaa kupimikaa katika nafasii aliyonayooo.. Lawama hizii ni za muungwana (jk) kwani huwa anafanya maamuzi mabovu ya kuteua aina ya waziri wa fedha kama mkullo na meghji...

Haiwezekani taifa lililopiga hatua kubwa katika ukusanyaji wa kodi (1995-2005) leo hii kuwa na halii mbovuu namna hii kifedha!! kuna zaidi ya tatizoo na yote haya ni kutokana na matumizii mabaya ya muungwana na idara zake, ukosefu wa vision katika uchumi, na kukosaa mbinuu za kutambuaa kiuchumii taifa hili lisongee vipii...

nasikitika maamuzii yao ni majerahaa kwa wananchii.
 
Mtalalamika sana but nothing will change mpaka mtakapoacha kulalama na ku-take things into your own hands.
 
Nadhani ndugu yangu una uhuru wa kusema kama sie tulivyo na uhuru wa kusema. But unapotuhukumu kuwa sie tuna mtindio wa akili kwakweli unakuwa umetukosea haki kwani tunatumia haki yetu ya kikatiba kuzungumza lile tunaloliona. Sasa ngoja nikupe darasa kwanini sie tunalalamika maana umetwambia hatuendi darasani.

Serikali inapokopa kwa kukutumia T-bills, au government bonds ni kwamba zile ni securities ambazo inazitumia kuraise liquidity (mkusanyiko wa fedha). Lakini tofauti yake na mkopo ni kwamba serikali inatangaza gawio au interest inayotaka kulipa kwa kuazima hizo pesa hivyo basi unakuta maranyingi interest hiyo haiwi kubwa kulinganisha na mkopo wa kawaida. Vile vile Serikali inakuwa na discretion ya lini italipa hizo pesa mfano kuna 90 days bills, 180 days, 360 days, 1 year bond, 2 year, 5 year etc. Lakini unapokuwa umekopa katika mabenki mfano overdraft facility kila siku wanakuwa wana charges zinazoambatana na mkopo huo. Vilevile ile overdraft inachajiwa interest in accordance to the prevailing market rates.

Sasa kwa Tanzania interest katika loanable funds ni 18-23% kama haijabadiilika kuzidi. Wakati interest kwenye Tbills ni lower zaidi ya hiyo kwa akili ya mtu wa kawaida unadhani inamake sense kwenda kuchukua mkopo wenye riba ya juu ukaacha mkopo wenye riba ya chini unless uwe umekunywa pombe. Na kwanini wasiissue securities kuraise more capital? Unakuta kwamba serikali imekwama with liquidity shortage na sasa inatafuta a quick alternative ya kuraise cash.

Sasa katika bank njia rahisi ya kupata cash ni kuchukua overdraft facility ambayo ni mara moja kuipata kama wewe mteja mkubwa. Hatari iliyopo ni charges zinazoambatana na facility hiyo na interest inayochagiwa. Vilevile kama serikali ikishindwa kulipa inamaana serikali itakuwa imeweka collateral (rehani) rasilimali fulani ambazo sijui bunge lina taarifa nazo au la? Sasa kimkopo kama serikali yetu iko makini sio tatizo but kama serikali yetu haina misingi mizuri ya usimamiaji wa kodi matumizi ya mabovu ya pesa ni hatari kwasababu hizi pesa zinatakiwa kulipwa on time na ukichelewa deni linaongezeka.

Sasa usifikiri watu tunapayuka kama wendawazimu bali tuna akili zetu na vilevile tumeshaona vyanzo vyote unavyovitazama wewe tukaona kwamba hili linaweza kusababisha a sovereign debt crisis kama iliyopo Greece na Spain. Na vilevile hatulalamiki ila tunaleta changamoto kwasababu nchi ikishatawaliwa na mabenki ndio hatuna sauti wananchi zaidi ya kukubali mabadiliko hivyo kabla hatujafika huko tusema tusije tukaambiwa mlikuwa wapi wakati tunafanya maamuzi.

Kuna maswali matatu naomba niwaulize Mkulo na wenzie:

a. Wameshindwa nini kuraise funds kwenye capital market (soko la mitaji) kwa kuuza hisa za serikali mfano bonds?

b. Wameshindwa nini kwenda kukopa katika development banks kama World Bank, IMF, ADB, EADB kuna ishu gani inaendelea?

c. Wameshindwa nini kupunguza fiscal policy budget instead budget ya serikali inakua kila siku? Hawajui kuwa mtu ukiwa huna kitu unapunguza matumizi yako kuweza kusave kiasi kidogo cha pesa?

Interesting analysis Mdondoaji.

Serikali, kama msimamizi na mchochezi wa shughuli za uchumi wa nchi, inapokopa kutoka kwenye benki za ndani uchumi wetu una athirika vipi? Serikali ikiuza bonds vs kukopa benki uchumi wetu unaathirika vipi?

Hatuwezi kulinganisha maesabu ya mfanya biashara wa kawaida na yale ya serikali katika kukuza uchumi na kuchochea maendeleo. Biashara ambazo hazina tija kwa mfanya bihashara wa kawaida zaweza kuwa na tija kwa uchumi na mendeleo ya nchi. Kwa mantiki hii mawazo yako kwamba serikali ikwepe riba ya juu hayana maana kwa serikali endapo inakopa ndani ya nchi yake. Serikali ni baba wa uchumi kamwe haogopi kutozwa riba ya juu kutoka kwa mtoto wake.

Kusema ati serikali ikakope kutoka World Bank, IMF, ADB, EADB nikutuzamisha zaidi kwenye umasikini, mana huko tumekuwa tukikopa tangu tupate uhuru na bado umaskini tunao...riba za huko tutaendelea kuzilipa hadi vizazi 15 vijavyo. Mdondoaji utakuwa mchumi wa kwanza ku suggest tukakope nje hali tunaweza kukopa ndani na hivyo kuongeza harakati za shughuli za uchumi.

Sasa naona unachanganya mambo hapa. Kupunguza fiscal policy kunatatua vipi tatizo la mkopo in the short-run? Serikali inahitaji fedha leo, impact ya kupunguza matumizi ya serikali inakuja in medium au in long-run! Yani nikija kwako kukopa badala ya kunipa mkopo utaniambia nipunguze matumizi? Kwanini nimekuja kukukopa in the first place?
 
Kwanza kabisa kabla sijakujibu maswali lazima utafautishe baina ya World Bank, IMF na Commercial Banks. Hizi bank ni Development banking institution both IMF na World Bank na sio Commercial Banking institutions. Pengine hufahamu tofauti ya hizi institution ndio maana unapata ugumu wa kunifahamu kwanini nadvocate Tanzania ni bora wakakope huko kuliko kukopa katika commercial banks za Tanzania.

Pili Interest wanazochaji katika mikopo ya hawa jamaa ni zero interest but wanataka kuwapo na results na ulipaji wa muda mliokubaliana. Tena mikopo mengine unapewa na grace period (muda wa kutokulipa) between 5 years to 10 years depending on the agreement itself. Sasa tukiangalia haya mazingira na ukitazama Commercial banks ni mazingira mawili tofauti. Kwanza malengo ya benki hizi mbili tofauti whereby commercial banks aimed at maximization of profits, Development banks wanataka maendeleo. Hii inamaana hawa watakuwa na terms tofauti nikuulize unadhani ni wa kina nani watakuwa na favourable terms???

Kuhusu malimbikizo ya madeni nadhani wakuwauliza ni CCM zile pesa walizokopa IMF, World Bank zimeenda wapi??? Tukipewa jibu ndio tutapata kwanini kuna malimbikizo ya madeni. Likewise, malimbikizo ya deni wakati mna zero interest ni vichekesho ambavyo tusiseme kwa wenzetu maana watatucheka na kutuona hatuna maana. Sasa ndio maana serikali wanaenda kukopa kwenye commercial banking as desperate measure na sio best alternative kwasababu wanajua kuna masharti magumu.

Tuje kwenye athari za kukopa nadhani nimeainisha before athari za kukopa katika commercial banks nazo ni kwanza interest tunayochajiwa ni kubwa, pili kama ni overdraft ni kwamba watakuwa wanachaji per day, tatu if both loan au overdraft tuna rasilimali lazima imewekwa kama collateral rasilimali hio ni mali ya watanzania ambao mie na wewe ni haki yetu na sio vibosile wachache. Pia unapokopa pesa benki tuwe na malengo ambayo yanauwezo wa kurejesha fedha hizo na usimamizi mzuri wa pesa (which Tanzania hatuna) Sasa tukishindwa kulipa deni hatuna grace period (kama IMF, WB), hatuna concession mwisho wa siku deni linakuwa serikali inashindwa kulipa. If I am being honest that is the way tunakoenda kwani commercial banks hawasamehi madeni kama WB, IMF bali wao watachukua rasilimali na kutafuta mtu anaweza kununua na ndio nchi imeuzwa hivyo!!!!

Tuje katika wazo la kupunguza bajeti ya serikali. Kuna theory moja ya Corporate finance inaitwa Pecking Order Theory (founded by Myers and Majluf, 1984) inasema kwamba kila kampuni ina order way of financing na mara nyingi kampuni nyingi zinaprefer kufinance kwa kutumia internal financing. Sasa tukija kwa nchi nadhani itakuwa busara au njia bora kwanza tukapunguza matumizi yetu yasiyokuwa na maana kama kunununua mavX kila kukicha na ile hela ikaenda kwenye reserve ya nchi (Treasury department). Kama tukiweza kuzuia ununuzi wa mavx tutakuwa tumesave mabilioni mangapi? Hayo mabilioni kwanini yasiende kwenye sekta zenye umuhimu.

Wamarekani kutokana na kuona deni lao kubwa wametumia the same approach ya kusave na kupunguza matumizi ya serikali (Keynesian economics). Although Keynes anasema excessive saving is harmful but at aleast is useful way of stabilizing the economy. Sasa ukiangalia Serikali yetu kwanza ina deni kubwa nje ya nchi, hatupati msaada wa wahisani unadhani pesa watazitolea wapi wewe? Au unadhani wahisani hawayaoni yanayofanyika Tanzania no wonder budget yetu kila kukicha inaongezeka dependency on foreign aid. tulifika up 20% tukarudi tena mpaka 60% of foreign aid. Sasa sijui tuko 40% of foreign aid mpaka lini jamani???

Nakaribisha maswali yako mengine.

Nilikuwapo!!!!
 
Ah nilisahau kujibu tofautisha between government bonds, tbills na commercial loans. Government bonds ni promissory note ya kulipa pesa huitaji kuweka collateral kukopa. Similar to Tbills. Mkopo mzee lazima pawepo na collateral hata kama wewe ni Bill Gates. Sasa mengine utajaza mwenyewe kuhusu athari zake kwa nchi yetu.
 
huyu jamaa anayeitwa mgonjwa wa ukimwi, anaweza kuwa mmoja wapo wa hao wanauchumi wetu waliopropose mkopo,...hapa anaonekana ndo kilaza wa kwanza sasa...
 
Dah wakati mwingine inashangaza kuona JF ni sehemu ya kulalamika na kulialia juu ya kila uamuzi wa serikali. Ni serikali ipi duniani haikopi?

Serikali ina njia kadhaa ya kupata fedha, borrowing is among them. Wanaosema kwamba serikali haifanyi bihashara ni dhahiri kwamba elimu yao haijai kiganjani; serikali inauza na kununua securities takriba kila juwa linapochomoza. Kabla hatujaendeleza "tamaduni" ya kulalamika na kukemea ni bora tukarejea darasani kidogo na kuangalia mahusiano ya shughuli za serikali, benki, na uchumi wa nchi. Vinginevyo wanaotusoma hapa JF (including the Mkulos) wanatuona kana kwamba akili zetu ni mchanyato wa ubongo na togwa.

nafikiri wewe baada ya kuona hata world bank wanatoa tamko lao sasa, ndo itabidi urudi shule upyaaaa, kwasababu kwa shule uliyonayo hapo, tutaliangamiza taifa kama utaendelea kulifanyia kazi taifa letu kwa uelewa huo..
 
Tanzania ina umasikini wa viongozi wenye AKILI na ELIMU zenye manufaa kwa jamii.
Wafadhili wastishe ufadhili wote wa kifedha ila watoe ufadhili wa AKILI BORA kwa viongozi wanaotawala!
90% ya maamuzi muhimu kwa jamii yanayofanywa na viongozi wa siku hizi ni ???????????????????????
MWAKA HUU NI MWAKA WA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA VIONGOZI WABOVU!!!!!
 
Pamoja na matatizo mengine, hili pia nimeliona. Ikimweka Mkulo aongee na hawa donors, kwa kweli huyu mtu anapwaya. Hawa wafadhili wanapokutana na mtu anayeweza kujieleza, kuwavutia na mwenye msimamo mambo huwa yanakwenda. Lakini wanapokutana na huyu Mkulo wanatuona kama watu wasio na mwelekeo..Viongozi wetu nao wanatupoza. Kama Mkulo unapitia hapa, naomba mara nyingine deligate someone who can do the job!

Mzee atoe ujiko kwa mtu??? na hiyo misafari amwache nani... lazima awepo yeye tu , hata kama anaboa na kuchemka!!!:angry:
 
Back
Top Bottom