Serikali kama imeshindwa Kuweka mishahara ya watumishi katika usawa ni vizuri ipunguze idadi ya watumishi

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,157
Mara nyingi viongozi wakigusiwa jambo hili hutoa wito kwa mashirika mengine ya umma kuongeza ubunifu na uzalishaji ili nao walipane vizuri.

Kuna mashirika ya umma

Kuna taasisi za umma

Kuna wakala wa serikali.

Kuna Mamlaka za udhibiti na usimamizi.

Kuna bodi mbalimbali

Kuna tume mbalimbali

Kuna ofisi mbalimbali

Kuna idara mbalimbali
N.k

Hivi vyote hapo juu vina majukumu tofauti.

Kuna wanaofanya kibiashara, kuna ambao wanatoa huduma kwa kutegemea ruzuku pekee.

Kuna ambao hawaingizi hata Senti.

Sasa msajili wa HAZINA anapowaomba wengine wazalishe zaidi ili nao waneemeke ina maana hajui miundo ya idara zote za serikali?

Kila mmoja anaweza kuwa productive akikaa sehemu inayozalisha. Je, watumishi wote waombe kuhamia kwenye uzalishaji mkubwa?

Kuna mtumishi katoka taasisi moja ya umma kwenda taasisi nyingine, mshahara wake kule umeongezeka mara 3.

Mifano iko mingi.
Nasema hivi kama serikali haiwezi kuwapandisha watumishi wote wakalipwa sawia kwasababu ya kuogopa gharama za kuendeshea serikali itakuwa kubwa ni vyema ipunguze watumishi wake ili wabaki watakaolipwa vizuri, hao ndio wabanwe kwa Sheria zote za utumishi wa umma.

Hivi kweli zama hizi za kumlipa mtumishi sh. Laki 4 ambayo ina Makato mengi ndani yake?

Tena nasikia basic salary ni chini ya laki 4.
Laki 5 ukitia psssf, NHIF na makato mengine kinabaki nini?
Kama kuna watumishi nature ya kazi yao ni ngumu na inahitaji muda zaidi ya watumishi wa idara zingine basi walipwe posho kwa mujibu wa Sheria.
 
Bado hujavitaja zile ajira lukuki za kuteuana na kutenguana kila siku, huku kigezo kikuu cha kuteuana kikiwa ni undugu, urafiki, ukada, nk.

Hii nchi kimsingi ina upungufu mkubwa tu wa watumishi wa kada muhimu kama zile za udaktari, ualimu, uuguzi, ugani, nk. Ila cha kushangaza kila mwezi fedha nyingi eti zinatumika kwenye kulipa mishahara!
 
Mara nyingi viongozi wakigusiwa jambo hili hutoa wito kwa mashirika mengine ya umma kuongeza ubunifu na uzalishaji ili nao walipane vizuri.
Kuna mashirika ya umma
Kuna taasisi za umma
Kuna wakala wa serikali
Kuna Mamlaka za udhibiti na usimamizi.
Kuna bodi mbalimbali
Kuna tume mbalimbali
Kuna ofisi mbalimbali
Kuna idara mbalimbali
N.k
Hivi vyote hapo juu vina majukumu tofauti.
Kuna wanaofanya kibiashara , kuna ambao wanatoa huduma kwa kutegemea ruzuku pekee.
Kuna ambao hawaingizi hata Senti.
Sasa msajili wa HAZINA anapowaomba wengine wazalishe zaidi ili nao waneemeke ina maana hajui miundo ya idara zote za serikali?.
Kila mmoja anaweza kuwa productive akikaa sehemu inayozalisha. Je, watumishi wote waombe kuhamia kwenye uzalishaji mkubwa?
Kuna mtumishi katoka taasisi moja ya umma kwenda taasisi nyingine, mshahara wake kule umeongezeka mara 3.
Mifano iko mingi.
Nasema hivi kama serikali haiwezi kuwapandisha watumishi wote wakalipwa sawia kwasababu ya kuogopa gharama za kuendeshea serikali itakuwa kubwa ni vyema ipunguze watumishi wake ili wabaki watakaolipwa vizuri, hao ndio wabanwe kwa Sheria zote za utumishi wa umma.
Hivi kweli zama hizi za kumlipa mtumishi sh. Laki 4 ambayo ina Makato mengi ndani yake?
Tena nasikia basic salary ni chini ya laki 4.
Laki 5 ukitia psssf, NHIF na makato mengine kinabaki nini?
Kama kuna watumishi nature ya kazi yao ni ngumu na inahitaji muda zaidi ya watumishi wa idara zingine basi walipwe posho kwa mujibu wa Sheria.
Hapo ni sawa na kumpigia kengele mbuzi.haitawezekana kwa mfumo wa nchi hii mishahara ikawa equalized au kukawa na slight differences.Hii nchi ni nchi ya kinyonyaji na wanaangaliwa sana wanasiasa sababu wao ndio watunga sheria.Ili kuondokana na hali hii ni bora tukafocus kwenye katiba ambayo ikiwekwa vzr itabalance hayo mambo.
 
Hilo suala ni nyeti kuna kipindi magufuli alikua analifanyia kazi sijui alifikia wapi nakumbuka na tume ikaundwa. Ila nina amini Samia atawaangalia watumishi wa umma maana aliyoyafanya mpaka sasa ni makubwa tuendelee kuwa na imani nae.
 
Mara nyingi viongozi wakigusiwa jambo hili hutoa wito kwa mashirika mengine ya umma kuongeza ubunifu na uzalishaji ili nao walipane vizuri.

Kuna mashirika ya umma

Kuna taasisi za umma

Kuna wakala wa serikali.

Kuna Mamlaka za udhibiti na usimamizi.

Kuna bodi mbalimbali

Kuna tume mbalimbali

Kuna ofisi mbalimbali

Kuna idara mbalimbali
N.k

Hivi vyote hapo juu vina majukumu tofauti.

Kuna wanaofanya kibiashara, kuna ambao wanatoa huduma kwa kutegemea ruzuku pekee.

Kuna ambao hawaingizi hata Senti.

Sasa msajili wa HAZINA anapowaomba wengine wazalishe zaidi ili nao waneemeke ina maana hajui miundo ya idara zote za serikali?

Kila mmoja anaweza kuwa productive akikaa sehemu inayozalisha. Je, watumishi wote waombe kuhamia kwenye uzalishaji mkubwa?

Kuna mtumishi katoka taasisi moja ya umma kwenda taasisi nyingine, mshahara wake kule umeongezeka mara 3.

Mifano iko mingi.
Nasema hivi kama serikali haiwezi kuwapandisha watumishi wote wakalipwa sawia kwasababu ya kuogopa gharama za kuendeshea serikali itakuwa kubwa ni vyema ipunguze watumishi wake ili wabaki watakaolipwa vizuri, hao ndio wabanwe kwa Sheria zote za utumishi wa umma.

Hivi kweli zama hizi za kumlipa mtumishi sh. Laki 4 ambayo ina Makato mengi ndani yake?

Tena nasikia basic salary ni chini ya laki 4.
Laki 5 ukitia psssf, NHIF na makato mengine kinabaki nini?
Kama kuna watumishi nature ya kazi yao ni ngumu na inahitaji muda zaidi ya watumishi wa idara zingine basi walipwe posho kwa mujibu wa Sheria.
Haitawezekana asilani.
Muasisi wa hili jambo ni marehemu Mkapa enzi za privatisation akitaka productivity iongezeke
 
Vp ufanisi wa kazi umeongezeka au mnataka kuongezewa mishahara tuu.?

Kuwa na kazi serikalini ni kudumaza watu kiakili mana kuna uhakika wa kazi bila hata kuwa productive.

Anyway, serikali naombeni mniajiri mm mtoto wa mkulima huku Mbalali - Mbeya 😔
 
Wewe ni tahira.
Kwahiyo mkataba wa kazi unasema mtumishi atalipwa maslahi nzuri pindi atakapoongeza ufanisi katika kazi?
Naamini wewe tahira hata maana ya neno ufanisi katika kazi hujui maana yake.
Ni mwajiri ndiye anayepaswa kumwezesha mtumishi kwa semina, warsha, maslahi bora na kumwendeleza kielimu mtumishi ili kuleta ufanisi.
Kama nitajiendeleza kielimu Mimi mwenyewe hiyo ni kwa future yangu na malengo yangu, mwajiri hapaswi kutegemea elimu ninayojiendeleza kwa pesa yangu ya mfukoni. Nasoma ili nipande wadhifa nile mema ya nchi.
 
Back
Top Bottom