HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 717
- 971
Ahsante sana Zyansiku kwa kunifagilia na kunipa pongezi.
Wengine wanadhani mimi na wewe tuna ubia, naomba tu kusema hapa kwamba sikufahamu wala sijawahi kuwasiliana na wewe wala kujadili lolote lile kuhusu azma yangu ya kuwania Ubunge Nzega! Naomba tu pia niwataarifu ndugu zangu wanaJF kwamba mimi sina ubia na mtu yeyote yule katika harakati zangu za kuwania Ubunge, sijaombwa na wazee, sijatumwa na mtu yeyote yule - ila ni nafsi na dhamira yangu pekee iliyonituma kuutafuta Ubunge wa Nzega!
Jimbo la Nzega lina mtego tu kwamba yeyote atakayejitokeza kugombea basi atadhaniwa kuwa ametumwa na mtu, hususan akiwa na ushawishi na anakubalika zaidi ya Selelii! Hili lilijitokeza hata pale nilipoamua kutangaza nia yangu kwa umma kupitia vyombo vya habari, pale Habari maelezo! Hili linakuja kutokana na Selelii kujipambanua kama ni mbunge shupavu anayepambana na ufisadi! Wengi wanakuja kufikiri kwamba jimbo la Nzega lina maslahi ya watu fulani wanaoitwa mafisadi...na kwamba yeyote anayempinga Selelii basi anaungwa mkono na au ametumwa na hawa watu.....and this is a big misnomer! Kugombea Uongozi ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania, na hatuwezi kuliacha jimbo chini ya Selelii kwa kuhofia kusemwa tumetumwa! Tayari kuna watu zaidi ya watano wamekwishatangaza nia ya kuwania Jimbo la Nzega. Hivi wote hawa ni vibaraka wa mafisadi?
Regards,
Dr. Hamisi Kigwangalla.