Selelii agoma kurudi Bungeni!?

Status
Not open for further replies.

Zyansiku

Member
Jul 27, 2009
49
10
Wana JF,

Ni muda mrefu kidogo sijawa na mawsiliano na mtandao huu hii ni kutokana na shughuli nzito ya kuvuna mpunga inayonikabili hapa tongi (Nzega) nimeamua kuandika hili ili basi tuendelee kupata wasaa mzuri wa kutafakari mengi ambayo tumekuwa tukiyajadili kuhusiana na siasa.

Ikiwa ni wiki moja sasa imekatika toka bunge letu tukufu lianze vikao vyake mjini Dodoma katika hali ya kushangaza bado namuona Mh Selelii akiendelea kuhangaika katika jimbo la Nzega na hasa vijijini akiomba msaada wa watu kumuunga mkono ili aweze kurudi mjengoni huku akiwaomba radhi baadhi ya watu ambao anadhani wamemuhama katika kumpigia debe tena mwaka huu.

Mh yupo bize kweli kweli jimboni japo hali yake inazidi kuwa mbaya kila kukicha na katika hali ya kushangaza amekuwa akitoa lugha mbaya za matusi kwa baadhi ya viongozi wa CCM hasa anapogungundua kuwa hawamuungi mkono.

Naomba wote walio karibu na Mh Selelii mshaurini arudi mjengoni tunamuhitaji sana lakini pia nitoe pongezi kwa Dr Kigwangala mbunge mtarajiwa wa Nzega maana amembana kweli kweli Selelii
 
Zyansiku
14th May 2010 07:43 PM
Katibu mkuu wa CCM Taifa Mh Yusufu Rajab makamba wiki hii atafanya mkutano mkubwa wilayani Igunga ambapo … atamuapisha Rostam Aziz kuwa kamanda wa vijana wilaya ya Igunga kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, shughuli za kumuapisha R.A ilikuwa zifanyike miezi karibu miwili iliyopita lakini ziliahirishwa kutokana na R.A kuwa nje ya nchi kikazi.
Zyansiku
10th August 2009 09:18 PM
Jamani simuelewi SS na sitamuelewa kabisa! simuelewi kwa sababu amekuwa akilalamika sana kuwa kundi la mafisadi linamwaga misaada majimboni ili kuwaangusha wale wanaopambana na ufisadi,
Zyansiku
31st July 2009 03:18 PM
umenikumbusha ndugu yangu, SS aliomba wabunge wawe na ngozi ngumu yeye kuguswa tu kidogo kwenye mtandao karuuka! mkaaali! No nae twamuomba awe tu awe na ngozi ngumu Urambo watamuuliza kwa miaka karibu 30 aliyokuwa kwenye System ameifanyia nini urambo zaidi ya Bara bara ya mashimo tu toka Tabora hadi Urambo
Zyansiku
30th July 2009 04:27 PM
katika kile nilichokiona kuwa ni dalili za kukata tamaa kwa SS leo asubuhi Mh huyo alitoa kauli zenye utata huku akijua kabisa anavunja taratibu za katiba ya CCM hasa pale alipo sisitiza kuwa lazima yeye atakuwa ni mbunge wa Urambo katika uchaguzi mkuu ujao lakini lazima pia atakuwa Spika wa bunge lijalo
Zyansiku
30th July 2009 04:10 PM
bado mazoea yatatusumbua sana! sikuamini macho yangu pale nilipomuona na kumsikia SS bungeni, akitamba ,aking'aka kuwa lazima atakuwa tena mbunge wa urambo, na lazima atakuwa tena Spika katika bunge lijalo hivi hayo ni maneno ya kuongea mtu mzima kama yeye tena mwenye dhamana kubwa katika chombo cha maamuzi yaani bunge? Sita its your time to quit! we are fed up
Zyansiku
31st March 2010 11:28 PM
Mbunge wa jimbo la Nzega na mmoja kati ya wale walioitwa wapambanaji wa ufisadi Lucas Lumambo Selelii kesho saa nane mchana atahutubia wakazi wa mji wa Nzega kuonyeshwa kufurahishwa kwake na kitendo cha ujasili cha aliyekuwa mpambanaji mwenzie wa ufisadi na mbunge wa kishapu mpendazoe cha kujitoa CCm na kuhamia CCj akisema kitendo hicho hakipaswi kupita bila kupongezwa.

Mwenye macho haiambiwi ona, mkuu una post 41 zote zinamponda au mkejeli Samwel Sitta na Lucas Seleli. Mwenye macho anaona na kuujua ukweli, fisadis at work!.
 
Wana JF,

Ni muda mrefu kidogo sijawa na mawsiliano na mtandao huu hii ni kutokana na shughuli nzito ya kuvuna mpunga inayonikabili hapa tongi (Nzega) nimeamua kuandika hili ili basi tuendelee kupata wasaa mzuri wa kutafakari mengi ambayo tumekuwa tukiyajadili kuhusiana na siasa.

Ikiwa ni wiki moja sasa imekatika toka bunge letu tukufu lianze vikao vyake mjini Dodoma katika hali ya kushangaza bado namuona Mh Selelii akiendelea kuhangaika katika jimbo la Nzega na hasa vijijini akiomba msaada wa watu kumuunga mkono ili aweze kurudi mjengoni huku akiwaomba radhi baadhi ya watu ambao anadhani wamemuhama katika kumpigia debe tena mwaka huu.

Mh yupo bize kweli kweli jimboni japo hali yake inazidi kuwa mbaya kila kukicha na katika hali ya kushangaza amekuwa akitoa lugha mbaya za matusi kwa baadhi ya viongozi wa CCM hasa anapogungundua kuwa hawamuungi mkono.

Naomba wote walio karibu na Mh Selelii mshaurini arudi mjengoni tunamuhitaji sana lakini pia nitoe pongezi kwa Dr Kigwangala mbunge mtarajiwa wa Nzega maana amembana kweli kweli Selelii

Mijitu mingine sijui ikoje, inakuhusu nini? wewe nenda kawaambie waliokutuma kiama chao kipo karibu
 
Zyansiku wewe ndio huyu Dr Kigwangala! Unafaa kuogopwa kama ukimwi! Selelii ni mpiganaji wetu. Ameendika historia Tz. Wewe pamoja na hao waliokutuma hatukutaki!
 
Huyu mtu vipi? Mbona humsemi Rostam unayeonekana kumpigia debe -- kwa kukosa vikao vingi tu vya Bunge, na pia huwa hachangii katika mijadala wala kuuliza maswali?
 
Unajua wakati nasoma heading ya posts nilipoiuona hii nilishtuka sana nikawaza inamaana selelii ametangaza kutogombea? haraka nikaingia kuona kulikoni loooh bora ningeendelea na posts zingine kuliko kukutana na huyu kibaraka wa mafisadi

wewe unajua kazi ya kuvuna mpunga lakini ilivyo ngumu? usingepata hata muda wa kuona selelii anazungumza nini na watu hao ....wewe hauko shambani upo nyuma ya selelii unamfuatilia
Halafu waliokutuma watakudai hela yao huwezi kuandika post ki bias kiasi hili ukadhani wasomi wa JF hawatakung'amua....yani unamponda selelii halafu unasema siju Dr nani mbunge wetu mtarajiwa!!!! rudi shule ukasome zaidi itakusaidia zaidi kujua namna ya kuzunguka mbuyu
Mix with yours
 
Zyansiku wewe ndio huyu Dr Kigwangala! Unafaa kuogopwa kama ukimwi! Selelii ni mpiganaji wetu. Ameendika historia Tz. Wewe pamoja na hao waliokutuma hatukutaki!
Mmmmmmmhhhhhh umeamua kumpa ya uchi uchi isiyo na nguo huyu fisadi?
Hutamuona tena hapa. Kesha kimbia kivuli chake.
 
Mwenye macho haiambiwi ona, mkuu una post 41 zote zinamponda au mkejeli Samwel Sitta na Lucas Seleli. Mwenye macho anaona na kuujua ukweli, fisadis at work!.

Mkuu thanks for doing the needful, this person deserves to be in our ignore list!!!
 
Right on Guys....Tuna watu makini sana hapa....now we know who are the hyenas in sheep's skin..
 
uyo anaweza kuwa ni Rostam azizi, manji, kundi la el etc....si unaona argument zake zilivyo cheap!
 
Ahsante sana Zyansiku kwa kunifagilia na kunipa pongezi.
Wengine wanadhani mimi na wewe tuna ubia, naomba tu kusema hapa kwamba sikufahamu wala sijawahi kuwasiliana na wewe wala kujadili lolote lile kuhusu azma yangu ya kuwania Ubunge Nzega! Naomba tu pia niwataarifu ndugu zangu wanaJF kwamba mimi sina ubia na mtu yeyote yule katika harakati zangu za kuwania Ubunge, sijaombwa na wazee, sijatumwa na mtu yeyote yule - ila ni nafsi na dhamira yangu pekee iliyonituma kuutafuta Ubunge wa Nzega!

Jimbo la Nzega lina mtego tu kwamba yeyote atakayejitokeza kugombea basi atadhaniwa kuwa ametumwa na mtu, hususan akiwa na ushawishi na anakubalika zaidi ya Selelii! Hili lilijitokeza hata pale nilipoamua kutangaza nia yangu kwa umma kupitia vyombo vya habari, pale Habari maelezo! Hili linakuja kutokana na Selelii kujipambanua kama ni mbunge shupavu anayepambana na ufisadi! Wengi wanakuja kufikiri kwamba jimbo la Nzega lina maslahi ya watu fulani wanaoitwa mafisadi...na kwamba yeyote anayempinga Selelii basi anaungwa mkono na au ametumwa na hawa watu.....and this is a big misnomer! Kugombea Uongozi ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania, na hatuwezi kuliacha jimbo chini ya Selelii kwa kuhofia kusemwa tumetumwa! Tayari kuna watu zaidi ya watano wamekwishatangaza nia ya kuwania Jimbo la Nzega. Hivi wote hawa ni vibaraka wa mafisadi?

Regards,
Dr. Hamisi Kigwangalla.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom