Sekretarieti ya Ajira/serikali itupe ufafanuzi kuhusu hili la ukosefu wa ajira katika taasisi za serikali

kiu ya haki

Senior Member
Jul 17, 2015
103
55
Neno ukosefu wa ajira ni hali ya mtu yeyote ambaye anaweza kufanya kazi, lakini hana kazi. Ukosefu wa ajira ni mojawapo ya matatizo ya duniani hivi sasa.

Ukosefu wa ajira unaonyeshwa kama asilimia ya jumla ya nguvu kazi inayopatikana ambayo haina ajira, lakini inatafuta kazi kikamilifu na ipo tayari kufanya kazi kama ikipewa nafasi. Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kimekuwa kikubwa sana.

Ukosefu wa ajira tanzania umekuwa wa misimu kiasi cha kukadiriwa kulingana na utawala wa maraisi.

Alipoingia hayati Dr. Magufuli kauli mbiu ilikuwa ni kujiajiri na viongozi kupigia upatu kujiajiri hali ya kuwa wao wenyewe wameajiriwa na hata ukiwambia waachie nafasi ili wakajiajiri kama kujiajiri ni dili hawako tayari.

SAFARI YA RAISI SAMIA NA AJIRA TANZANIA

Awamu ya raisi mama Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani alijipambanua kufungua milango ya ajira na kuwasaidia vijana waliohitimu kupata ajira.

Kiukweli huenda jambo hili mh.raisi anania njema lakini kiukweli tangu 2015 hadi leo 2022 serikali haijaajiri katika kiwango kinachoweza kukidhi hata nusu ya vijana ambao wako mitaani bila ajira kwa muda mrefu.

Kuna mwingine atasema kama huwezi kujiajiri basi elimu yako haiwezi kukusaidia ila mimi nadhani mtu huyo hajawahi kupitia changamoto kiasi cha kushindwa kupata hata mtaji wa kuanza kujiajili mathalani kama ni biashara.

Mwingine atasema fungua tuition ili upate fedha za kujiajiri, hapa lazima uelewe kuna watu wamesomea fani ambazo hazihusiani na kufundisha na kuna watu hawana talent za kufundisha pia.

Leo tar 7/4/2022 kupitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira imeeleza mengi kumsifia raisi katika swala la kuupiga mwingi kuhusiana na ajira.

Kwa uchunguzi wangu mfupi taasisi za serikali zina uhaba mkubwa wa wafanyakazi katika vitengo mbalimbali tovuti ya sekretarieti ya ajira imetaja “ Vibali vilivyopokelewa ni pamoja na kibali cha kuajiri Watanzania elf mbili na mia moja (2100) kwa ajili ya Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kibali cha ajira za wahandisi mia mbili sitini na nane (268) kwa ajili ya TAMISEMI na nafasi mia tano na nane (508) kwa ajili ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambao wote wamepangwa kazini.”

Mifano ya kuupiga mwingi kwa mh.Raisi kwa mwaka mmoja imejikita TRA,TRC hii ni kwa sababu kwa mwaka huo mmoja TRA na TRC ndio taasisi pekee zilizopata vibali vya kuajiri peke yake jee taasisi nyinginezo hazina haja na wafanyakazi au bajeti ya kuajiri haipo kwa taasisi hizo?

Mfano mimi binafsi nina muda wa miaka kadhaa sijaona tangazo la kazi kwa taasisi kama TASAC, TBS, TAA nk ukichunguza taasisi hizi zina mfumo wa kutumia internship kwa vijana kwa muda wa mwaka mmoja mmoja kisha wanawaacha kutokana na kuisha kwa mikataba yao kisha kuchukua vijana wengine.

Hali hii nadhani inawafanya wajione hawana haja ya kuajiri kwa sababu wanavijana ambao wanawatumia.

Juzi nilikuwa nazungumza na kijana wa internship TBS anasema wao katika ofisi za bandarini ni wengi sana kuliko hata waajiriwa na katika taasisi zenye uhaba wa wafanyakazi ni TBS lakini haelewi kwanini hawataki kuajiri na badala yake wanatumia vijana wa internship ,Je!! tatizo ni uongozi wa taasisi kuomba vibali au serikali kutoa vibali?

Maswali ya msingi kwa sekretarieti ya ajira.

1. Lini Mh. Rais atatoa ajira za kukidhi angalau nusu ya wahanga wa ajira tangu mwaka 2015 hadi leo mwaka 2022?maana mara nyingi zinakuwa ni ajira za siasa !!!ajira za uhakiaka lini?

2. Bajeti ya mgawanyo wa nafasi za kazi kwa walimu,madaktari ukoje ukilinganisha na kada nyinginezo? Maana naamini kila taaluma ina wigo wake wa umuhimu.

3. Kwanini serikali inaruhusu baadhi ya taasisi kuajiri vijana wa internship kila mwaka na kuwatumia kufanya majukumu yao jambo ambalo linapelekea kutotilia umuhimu wa kuajiri wafanyakazi wa kudumu kwa mujibu wa sekretrieti za ajira? (ajira iwepo na internship ziwepo ili kujenga uzoefu wa kazi kwa vijana wanaohitimu)

4. Je, kwa mwaka mmoja ni TRA, TRC na TAMISEMI TU ndo yakutolea mifano ya raisi kuupiga mwingi !!!taasisi nyinginezo hazina haja ya kuajiri?

Kama na wewe unaswali la ziada ongeza ili tupewe majibu ya mambo haya kutoka kwa wahusika.

Naomba kuwasilisha.
 
Hizo ajira 2,100 za TRA mbona kama sio sahihi? Mwaka jana wala mwaka huu TRA hawajaajiri watu 2,100 labda kama waliajiri kimya kimya bila kutangaza.
 
wanasema washapangiwa na vituo .
Sasa hapa kuna uhujumu uchumi. Watuonyeshe ni lini walitangaza nafasi za kazi 2,100 TRA? Dah! Masikini nchi yangu. Kwa hiyo watu wanapeana tu kazi wakati kuna watoto wa wanyonge wanasota mtaani bila kazi.
 
Neno ukosefu wa ajira ni hali ya mtu yeyote ambaye anaweza kufanya kazi, lakini hana kazi. Ukosefu wa ajira ni mojawapo ya matatizo ya duniani hivi sasa.

Ukosefu wa ajira unaonyeshwa kama asilimia ya jumla ya nguvu kazi inayopatikana ambayo haina ajira, lakini inatafuta kazi kikamilifu na ipo tayari kufanya kazi kama ikipewa nafasi. Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kimekuwa kikubwa sana.

Ukosefu wa ajira tanzania umekuwa wa misimu kiasi cha kukadiriwa kulingana na utawala wa maraisi.

Alipoingia hayati Dr.Magufuli kauli mbiu ilikuwa ni kujiajiri na viongozi kupigia upatu kujiajiri hali ya kuwa wao wenyewe wameajiriwa na hata ukiwambia waachie nafasi ili wakajiajiri kama kujiajiri ni dili hawako tayari.

SAFARI YA RAISI SAMIA NA AJIRA TANZANIA

Awamu ya raisi mama Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani alijipambanua kufungua milango ya ajira na kuwasaidia vijana waliohitimu kupata ajira.

Kiukweli huenda jambo hili mh.raisi anania njema lakini kiukweli tangu 2015 hadi leo 2022 serikali haijaajiri katika kiwango kinachoweza kukidhi hata nusu ya vijana ambao wako mitaani bila ajira kwa muda mrefu.

Kuna mwingine atasema kama huwezi kujiajiri basi elimu yako haiwezi kukusaidia ila mimi nadhani mtu huyo hajawahi kupitia changamoto kiasi cha kushindwa kupata hata mtaji wa kuanza kujiajili mathalani kama ni biashara.

Mwingine atasema fungua tuition ili upate fedha za kujiajiri ,hapa lazima uelewe kuna watu wamesomea fani ambazo hazihusiani na kufundisha na kuna watu hawana talent za kufundisha pia.

Leo tar 7/4/2022 kupitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira imeeleza mengi kumsifia raisi katika swala la kuupiga mwingi kuhusiana na ajira.

Kwa uchunguzi wangu mfupi taasisi za serikali zina uhaba mkubwa wa wafanyakazi katika vitengo mbalimbali tovuti ya sekretarieti ya ajira imetaja “ Vibali vilivyopokelewa ni pamoja na kibali cha kuajiri Watanzania elf mbili na mia moja (2100) kwa ajili ya Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kibali cha ajira za wahandisi mia mbili sitini na nane (268) kwa ajili ya TAMISEMI na nafasi mia tano na nane (508) kwa ajili ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambao wote wamepangwa kazini.”

Mifano ya kuupiga mwingi kwa mh.Raisi kwa mwaka mmoja imejikita TRA,TRC hii ni kwa sababu kwa mwaka huo mmoja TRA na TRC ndio taasisi pekee zilizopata vibali vya kuajiri peke yake jee taasisi nyinginezo hazina haja na wafanyakazi au bajeti ya kuajiri haipo kwa taasisi hizo?

Mfano mimi binafsi nina muda wa miaka kadhaa sijaona tangazo la kazi kwa taasisi kama TASAC, TBS ,TAA nk ukichunguza taasisi hizi zina mfumo wa kutumia internship kwa vijana kwa muda wa mwaka mmoja mmoja kisha wanawaacha kutokana na kuisha kwa mikataba yao kisha kuchukua vijana wengine .Hali hii nadhani inawafanya wajione hawana haja ya kuajiri kwa sababu wanavijana ambao wanawatumia.

Juzi nilikuwa nazungumza na kijana wa internship TBS anasema wao katika ofisi za bandarini ni wengi sana kuliko hata waajiriwa na katika taasisi zenye uhaba wa wafanyakazi ni TBS lakini haelewi kwanini hawataki kuajiri na badala yake wanatumia vijana wa internship ,Je!! tatizo ni uongozi wa taasisi kuomba vibali au serikali kutoa vibali?

Maswali ya msingi kwa sekretarieti ya ajira .

1.Lini mh.Raisi atatoa ajira za kukidhi angalau nusu ya wahanga wa ajira tangu mwaka 2015 hadi leo mwaka 2022 ?maana mara nyingi zinakuwa ni ajira za siasa !!!ajira za uhakiaka lini?

2.bajeti ya mgawanyo wa nafasi za kazi kwa walimu,madaktari ukoje ukilinganisha na kada nyinginezo? Maana naamini kila taaluma ina wigo wake wa umuhimu.

3.kwanini serikali inaruhusu baadhi ya taasisi kuajiri vijana wa internship kila mwaka na kuwatumia kufanya majukumu yao jambo ambalo linapelekea kutotilia umuhimu wa kuajiri wafanyakazi wa kudumu kwa mujibu wa sekretrieti za ajira.?(ajira iwepo na internship ziwepo ili kujenga uzoefu wa kazi kwa vijana wanaohitimu)

4.je kwa mwaka mmoja ni TRA,TRC na TAMISEMI TU ndo yakutolea mifano ya raisi kuupiga mwingi !!!taasisi nyinginezo hazina haja ya kuajiri?

Kama na wewe unaswali la ziada ongeza ili tupewe majibu ya mambo haya kutoka kwa wahusika.

Naomba kuwasilisha.
Mimi tuu nimeomba tuu nafasi ya kuhamia kutoka Halmshauri ili nikafanye kazi TBS kama quality assurance officer Ila naona hawanijibu barua yangu mpaka Leo tokea mwaka Jana. Kama wameshindwa kuajiri hata kuhamia tuu
 
Utumishi ni wahuni tu kama wahuni wengine.. wanajipendekeza kwa mama ili waendelee kushiba hapo,, toeni Ajira nyie acheni janjajanja.. ety mama katoa Ajira Sasa zikowapi mbona vijna wanalialia tu huku
 
Hizo ajira 2,100 za TRA mbona kama sio sahihi? Mwaka jana wala mwaka huu TRA hawajaajiri watu 2,100 labda kama waliajiri kimya kimya bila kutangaza.
Kiswahili kigumu . Wamesema vibali vilivyopokelewa ni 2100 kwa TRA ,265 wahandishi Tamisemi ambazo nafasi hizo zinatarajiwa kutangazwa muda si mrefu ila itategemea na uhitaji wa database yao na nafasi 508 TRC ambao wamepangiwa vituo vya kazi.
 
Mojawapo ya Sababu za Kukosa Ajira ni kusoma Co

Tunakosa Ajira kwa Sababu tumesoma Course zile ambazo job Market hazihitaji. Inaitwa Structural Unemployment. Kwa mfano umesoma Chemical Engineering hakuna muajiri anayehitaji mwenye hivyo Dani miaka 10. Ila umesoma IT Kampuni nyingi zinawahitaji na mengineyo.

Mwalimu was Lugha hakuna Shule inawahitaji. Kwa hivyo Unemployment itatokea.
 
Mimi tuu nimeomba tuu nafasi ya kuhamia kutoka Halmshauri ili nikafanye kazi TBS kama quality assurance officer Ila naona hawanijibu barua yangu mpaka Leo tokea mwaka Jana. Kama wameshindwa kuajiri hata kuhamia tuu
Wewe nae si unakazi utulie unapofanyia hiyo kazi waachie wengine nao watafute huko unapotaka kwenda
 
Back
Top Bottom