Sasa umeamini kwamba Lowassa ni visionary?

You do not have to be a scientist to realize that joblessness among youth is a time bomb. Lowassa is simply a political opportunist.
 
Acha kulinganisha vitu viwili tofauti.Ina maana ukosefu wa ajira ni kwa vijana wa kiislam tu.
 
tatizo nhi hii ss hv , baada ya Nyerere, hakuna mtu/kiongozi anayeweza kukemea maovu na watu wakamsikiliza/wakamtii. Kila mtu anaongea/anafanya tu jinsi anavyojisikia. Eti uhuru wa mawazo/matendo haiwezekani kukawa na uhuru bila kikomo. Hata kwenye familia lazima kuwe utaratibu ambao kila mtu ndani ya familia lazima aufuate vinginevyo ni vurugu.

Ni kweli, lakini hizi si zama za kikomunisti, wala utawala wa kiimla. Kwenye demokrasia ya kweli, kwa sheria walizojitungia WANANCHI WENYEWE, Katiba ndiyo inachukua nafasi ya mtu huyo. Lakini ikiwa katiba inapindishwa, au haijatungwa na wananchi wenyewe, kama kiini macho cha TUME YA KATIBA tunachofanyiwa sasa hatutaenda mbele.
 
Acha kulinganisha vitu viwili tofauti.Ina maana ukosefu wa ajira ni kwa vijana wa kiislam tu.
Nimejibu hapo juu hili swali, vijana wa Kiislamu wameathirika zaidi. Pia tusiegemee sana kwenye udini, kumbuka hapa tunazungumzia tatizo la ajira nchini.
 
Kwame, EL angekuwa visionary angetumia mali anayotapanya kuongeza ajira zaidi kwa vijana wa mkoa wake. Thats vision!

Mtu aliyefikia kuwa na cheo cha PM na bado anahangaika na siasa, huyo hana vision kwa kuwa uzoefu wake pekee bila mali vinatosha kuajiri maelfu ya Watanzania.
 
Huu ni u.pupu, Lowassa alifanya nini alipokua PM kuondoa hilo bomu? je ni kweli si dhahiri kua ukiwa vijana wengi wasio na kazi wanaweza kutumiaka vibaya? hii nayo inahitaji rocket scientist EL kuliona? kweli watumia akili ni wachache!
 
Kwame, EL angekuwa visionary angetumia mali anayotapanya kuongeza ajira zaidi kwa vijana wa mkoa wake. Thats vision!

Mtu aliyefikia kuwa na cheo cha PM na bado anahangaika na siasa, huyo hana vision kwa kuwa uzoefu wake pekee bila mali vinatosha kuajiri maelfu ya Watanzania.

JohnShaaban.

Hii inaitwa EXPIRIENCE. Ni moja ya vigezo vinavyotakiwa ili uweze kupata madaraka ya juu zaidi. Ni kwa sababu hizihizi G.H Bush na Al Gore waligombea Urais licha ya kuwa waliishawahi kua ma VP.
 
Huu ni *****, Lowassa alifanya nini alipokua PM kuondoa hilo bomu? je ni kweli si dhahiri kua ukiwa vijana wengi wasio na kazi wanaweza kutumiaka vibaya? hii nayo inahitaji rocket scientist EL kuliona? kweli watumia akili ni wachache!

Alikua ni PM tu, hakua na ultimate powers to run this country.
 
Lowassa naye ni BOMU linalosubiria kupasuka. Of course, likipasuka CCM ndicho kitaumia zaidi. IKULU kuna nini?
 
tatizo sio vijana kukosa ajira bali ni upotofu wa fikra kushindwa kutambua kitu kizuri na kibaya
 
haya yanayotokea hayana uhusiano na ukosefu wa ajira. Ni upungufu tu wa ufahamu na maarifa kadhaa. Ni sawa na kutaka kutuaminisha kuwa hili ni Taifa la kiislam kwani wanaosumbua huko ni wao pekee. Hakuna wakristo wasio na ajira? Wamevunja cha mtu? Tatizo ni mbegu ya chuki na utengano inayopandikizwa kisiasa kwa mgongo wa imani
WEWE UMESEMA VIZURI SANA. Ila swala la ajira nalo linasaidiaga watu kutokuwa watumwa wa maneno ya mtu kama Ponda.
 
watu kama ninyi ndo akili mgando badala ya kuchangia hoja unatokwa mapovu...kisa EL. Achana na jina la mtu tathmini maudhui ya ujumbe.
mimi nafikiri ya kwako ndio ime freeze ina hitaji kumwagiwa chumvi iyeyuke kama kule london wanapo mwaga chumvi kipndi cha winter yaani hapa tulipo na matatizo yote walioleta hao ccm huyaoni
 
Nawakumbusha tu, EL aliyasema hayo ya vijana ni bomu, wakati analishauri kanisa katoliki kujenga vyuo vya ufundi [VETA} kwa ajiri ya vijana ili waweze kujiajiri kuliko hivi sasa ambako vijana wengi huishia mtaani na kufanya shughuli zisizo na utaalamu wowote, kauli yake hii ilipingwa na wale ambao wanataka kumpinga kwa kila kitu kwa kuwa tu wanahofu naye kisiasa. MH BEN MKAPA akihutubia kwenye kigoda cha mwl Nyerere alishauri serikali na wadau wengine kufungua vyuo vya ufundi [VETA} kuliko kushabikia vyuo vikuu vinavyoibuka kila kukicha na vile vile kwa maendeleo ya taifa alishauri serikali ijenge viwanda vipya, jambo ambalo EL aliishauri serikali iweke dhamana gas iliyogunduliwa ili ikope fedha na kujenga viwanda ili vijana wapa
 
Tatizo la ajira ni kwa wote. Lakini kwa sababu ya various factors, waislam wamekua affected disproportionaly. Kuna baadhi ya madai yao ni valid. Hayatatuliki kwa kutupiana lawama na kupigana virungu [ kwa pande zote mbili] bali kwa kukaa chini na kuyaongelea.

madai validi ya waislam ni yapi ambapo wakristu hawana? Au wakristo hawana tena wanachohitaji?
 
mimi nafikiri ya kwako ndio ime freeze ina hitaji kumwagiwa chumvi iyeyuke kama kule london wanapo mwaga chumvi kipndi cha winter yaani hapa tulipo na matatizo yote walioleta hao ccm huyaoni

Kila tatizo ccm kunamatatizo mengine yapo wazi...haya basi PONDA nae CCM. Ishue ya sasa haihitaji uccm wala umarangu....wa CDM hilisuala ni janga la taifa na sio siasa...funguka macho.
 
mtoa mada unapindisha ukweli, ukweli ni KUWA TATIZO NI KIKWETE, full stop. bado vijana hawajawa tishio kihivyo katika nchi yetu, narudia, tatizo ni kikwete.
 
Kwani matatizo ya ajira kwa vijana hayakuwepo akiwa waziri mkuu ! Wacha kuendekeza njaa. Nani atadanganywa kitoto hivyo. Apumzike tu awaachie wengine. Kwani JK na EL wanatofauti gani?
 
Back
Top Bottom