Adui wa Taifa ni nani? Je, ni wapendwa wetu waliokufa au ni Ujinga, Maradhi na Umasikini?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
Utamaduni wa Mtanzania umebomoka nani asimame mahali pale palipobomoka na kupajenga tena,nimeona maridhiano kwa watu fulani lakini maridhiano hayajafika kwenye dhihaka,kashfa na shutuma kwa wapendwa wetu waliokufa,tuliozaliwa mwaka 1980 tulikuta utamaduni mzuri wa Watanzania,tulishirikiana kwenye mazishi ya wapendwa wetu,hatukuwahi kuona dhihaka kwa wapendwa wetu waliokufa zaidi ya watani msibani ambao walitumika kuondoa majonzi na kumpa faraja mfiwa,miaka arobaini mbele tunaona dhihaka kwenye vifo vya viongozi wa nchi,mtu anasimama hadharani anasema kama ulimpenda sana basi nenda kazikwe nae Chato,haikuwa busara na wala si hekima,

Leo nimeingia mtandaoni nimekutana na habari ya msiba wa Kiongozi mstaafu,Waziri wa zamani,Mtumishi wa Umma na kachero wa Usalama wa Taifa,lakini nimeona dhihaka kubwa iliyokomaa na msemo mkubwa ni ule wa "wazuri hawafi" na "bahari imetulia"ndugu zangu viongozi kuweni hekima katika maneno na sentensi zenu, Watanzania wanang'amua kuwa hii sentensi ni kijembe kwa Marehemu fulani,sasa kulikuwa na haja gani ya vijembe kwa marehemu waliotangulia mbele ya haki,nani asimame mahali pale palipobomoka kukemea hili?.Nakumbushia tu kauli za hadharani zilizoligawa Taifa,Tundu Lisu aliwahi kumsema mungu ameliponya taifa amemuondoa Bwana yule,Godbless Lema:mungu amenijibu/ametujibu kilio chetu sasa Mwendazake ameuwawa kwa upanga wa Bwana,January; Mwendazake alikuwa ni fundi aliyeshona shati vibaya sisi sasa tunarekebisha,

Nape;Mungu ameamua ugomvi bahari imetulia sasa,Zitto kabwe;anayempenda Mwendazake akazikwe naye Chato,kulikuwa na ulazima gani wa wao kutoa kauli hizo baada ya kifo cha Hayati Magufuli? Je tumemsahau adui wetu wa Taifa na sasa tunapambana kutukana wapendwa wetu wanaokufa,kumbuka wewe utakufa je utapenda watu wakutukane,tuchunge kauli zetu,tuchunge ndimi zetu, tuchunge midomo yetu,kauli hizi zikawe juu ya Ujinga,maradhi na umasikini,siasa ya Ujamaa ilitufundisha kutowahurumia mafisadi,mabepari,mabwenyenye na wezi wa Mali ya Umma,Wezi wa rasilimali za taifa hili wanapaswa kuwajibishwa mbele ya hadharani ili iwe fundisho kwa vizazi vilivyopo na vijavyo,mwizi wa mali ya Umma kwa sheria za Ujamaa anapaswa kunyongwa hadharani,tusimwache aanze kutufundisha kuwatukana wapendwa wetu marehemu waliotangulia mbele ya haki.

Tulifanya makosa makubwa sana kuruhusu dhihaka, matusi na kashfa kuwa juu ya uwezo pengine kwa kuwa pamoja na watoa kashfa na dhihaka kwa wapendwa wetu marehemu waliotangulia mbele ya haki matokeo yake ndio haya! tabia imekomaa,sasa watu hawana uoga wala aibu kumtukana marehemu,watu hao hawajali ya kwamba marehemu alikuwa na wapendwa wake, ndugu jamaa na marafiki,huu si utamaduni mzuri uko tuendako,watu watakuja kupigana siku moja na kuleta madhara kwa Taifa letu kwa ujinga wa tabia mbaya ambayo haikukemewa zaidi ya kifurahiwa na wenye dhamana ya kukemea,tunahitaji maridhiano kwenye hili kabla tabia hii haujaleta janga kwa yaifa,nadhani ili liwe somo kwa siasa zetu za kashfa na dhihaka kwa marehemu,hivi tunadhani watu hawakujeruhiwa katika awamu zote tano,je waliwasema vibaya Hayati na marehemu viongozi wetu waliotangulia mbele ya haki,tulivumilia kwa maana kisasi na hukumu ni vya Mungu aliyetuumba sisi wetu na kutuweka hapa duniani kama wapita njia tu.

Napenda kuwa muwazi kabisa na kuwataka vijana wa kitanzania kuachana na siasa za chuki ndani ya Chama chetu! cha CCM,huu ni mtego kwa CCM,wapinzani watasema wana laana ya kutuibia kura zetu,kama walivyosema ya kwamba Mh Lowassa aliibiwa kura zake katika uchaguzi wa mwaka 2015,ambazo zingemfanya awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,sasa tuachane na habari za kashfa na dhihaka kwa viongozi ambao walikufa wakipambana Chama cha CCM kiwe bora bila ufisadi,kiwe chama cha kijamaa kama misingi yake ilivyo,kiwe chama cha kutetea wananchi wanyonge,kiwe chama cha kulinda maliasili za Watanzania lakini katika mapambano hayo wakatangulia mbele ya haki,hatupaswi kuwafanyia dhihaka watu hao waliokipambania chama cha Mapinduzi,CCM kwa jasho na damu,tukiendeleza siasa za kashfa na dhihaka kwa viongozi wanaokufa basi mpasuko ambao tunautengeneza leo unahatarisha sana safari ya Amani,Umoja na utulivu wa Watanzania,Wote kwa Mungu tutarejea!Tuwaombee waliotangulia bila kudhihaki wala kuwanenea mabaya!

Common sense is not common to every body,nichukue nafasi hii kuwatakia Usiku mwema viongozi wetu waliotangulia mbele ya haki,Kwaheri Mzee wangu Bernard Kamilus Membe,Kachero bora wa enzi zote katika Ulinzi na Diplomasia ya Taifa!, Pumzika kwa amani Hayati Rais John Pombe Magufuli,Daima utabaki shujaa wa Taifa la Tanzania kwa vizazi hata vizazi kwa uthubutu wako na kutembea kwenye nyayo za Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere,Daima tutakukumbuka Rais wa kwanza wa Tanzania,Mwalimu Julius Nyerere,Daima tutakukumbuka Waziri Mkuu,Edward Moringe Sokoine,Daima tutakukumbuka Waziri Mkuu,Mzee Rashid Kawawa,Daima tutakukumbuka Rais wa tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa,tunawashukuru na tunawathamini sana kwa mchango wenu adimu katika kulijenga Taifa la Tanzania,Usiku mwema, tutaonana tena Paradiso,Mungu ndiye mwenye kusamehe na kuhukumu,Bwana alitoa na bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Ujinga, maradi na umaskini
Ukiwa na hivi vitatu, unakuwa mpumbavu, bwege na mvivu!
Kumbuka:
IMG_1762.jpg

Umasikini ni laana kubwa sana walahi
 
Ongeza na CCM hapo chini
Naogopa kupigwa mvua ya mawe, mkuu. But, Juliasi alishatuambia kwamba maadui wa taifa ni hao watatu tu. Sina hakika kama wewe una maono kuliko Mwalimu; kwa sababu yeye mwenyewe, kauli yake ni sawa na katiba, au hata zaidi. :)
 
Adui wa Tanzania ni ujinga pekee.

 
Unahangaika kuuliza maswali kwenye kichwa cha mada yako?

Mimi sijasoma hayo uliyojaza huko kwa maandishi mengi, huku jibu likiwa wazi:
CCM pekee ndiye adu mkuu wa Tanzania kwa miaka hii ya karibuni.

Siku waTanzania wakifanikiwa kupata mbinu za kukiondoa chama hiki, ni hapo hapo nchi itaanza hatua mpya, kumalizana na hivyo viadui vingine vidogo dogo kama hivyo ulivyovitaj kama : maradhi; ujinga, n.k.,

Adui namba moja kwa sasa kwa Tanzania ni CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom