Sasa umeamini kwamba Lowassa ni visionary?

if not cdm 2015 basi awe lowassa manake ndani ya ccm mimi naamini hamna kifaa kama lowassa.
sifa kubwa ya lowassa ni elements za kibabe alizonazo
lowassa sio mtu wa kuchezea, au wa kumletea usanii uchwara

lowassa ni mbabe na hii nchii inahitaji ubabe wa lowassa .

kashfa za richmond ni uzushi na chuki za sitta samwel za kunyimwa uwaziri mkuu.lowassa aligeuzwa mbuzi wa kafara .

hatuitaji rais wa aina ya membe au asha migiro.

tunataka wabebe wanaoogopwa, wanaofukaza watendaji kazi on spot

viva lowassa , lowassa 4 ccm 2015

cdm ikiteleza nafuu tudondokee kwa lowassa na sio akina membe

On this issue..tunafikiria sawasawa 100%, kila mstari hapa ni kama nimeandika mimi, na wengine wanaopenda maendeleo ya nchi hii. ningekua na uwezo ningegonga likes 100.
 
Kwame Nkrumah:

Maana ya Visionary ni: A person with unusual powers of foresight; Je unaweza kumjadili Lowassa katika muktadha husika kwa kutumia maana ya dhana hii?

What is so unusual kuhusu alichozungumza Lowassa? Nadhani hata Lowassa mwenyewe sana sana atakubali kuchukua credit kwa kulizungumzia akiwa kiongozi wa CCM, lakini atakwepa kwa kila njia kuitwa A Visionary kwa suala ambalo hata yeye anajua fika kwamba ameligundua kupitia tafiti na ripoti mbalimbali;

Suala hili limekuwa likizungumzwa kwa miaka mingi sana, kwa mfano rejea tafiti za REPOA, ESRF, na pia kutoka taasisi nyingine nyingi za nje ya nchi zinazojishughulisha na masuala ya Sera za Kutokomeza Umaskini Afrika; Suala hili limejadiliwa kwa kina sana pamoja na athari zake kwa miaka mingi, kabla hata Kikwete hajawa Rais wa Tanzania;

Kwame Nkrumah, kama tunampenda Lowassa kwa uongozi wake,jambo ambalo ni sahihi kabisa, tujaribu kumuunga mkono kwa hoja nzito, sio hizi nyepesi nyepesi; Lowassa anastahili sifa kubwa kwa kuwa Kiongozi wa CCM kulisemea hilo wakati wengine wakiwa wamelala, lakini tusinogewe na kuanza utamaduni wa kumjengea sifa zinazombatiza mambo mengine ambayo hata yeye anajua bado hastahili; Itafikia wakati tutasema Lowassa ni Visionary, lakini wakati huo sio sasa;

Mchambuzi.
Nafikiri utakubali pia kwamba Lowasa ni MTHUBUTU, na UTHUBUTU wa Lowasa kusema aliyoyasema akiwa CCM , kwa ngazi yake aliyonayo ni effectively kumkosoa Kikwete. That alone has never been done and should be enough to convince you that what i said is true. Uthubutu huu siyo utamaduni wa CCM wala serikalini kwa sasa wala huko nyuma. Lowasa ameona mbele na kuthubutu kusema aliyoyasema, ambayo na wewe unayakubali.
Pia sidhani kama mtu aliyemaliza Chuo yupo mtaani miaka mitatu hana ajira ya maana ukimueleza issues za ukosefu wa ajira atakuambia hii ni issue nyepesinyepesi kama ulivyosema. Pia nikubali kwamba tunapishana padogo kwa maana wewe unaiangalia mada hii at a macro level, na mimi at a micro level, unaiangalia more from an academic point of view mimi naiongelea kama si mtaaluma, lakini hii haindoi hoja ya mada yangu, na bado ninaisimamia.
 
EL ni opportunist yaaani hataki kufa bila kuwa raisi lazima tujiulize kuna nini ikulu?

kwani yuko peke yake? tena mi naona EL anataka ikulu coz theres so much he wants to do for this country..waulize akina zitto,membe,sitta, na ccm yote kwa ujumla kwanini wanang'ang'ania ikulu
 
Kwame Nkrumah
Lakini kwa sababu ya various factors, waislam wamekua affected disproportionaly

Mkuu, waislamu wanapolalamika kwamba wamepuuzwa kielimu hoja wanayojenga ni ipi? Hivi uandikishaji Drs la ! shule za msingi, shule za sekondari nk unawabagua waislamu? Tuwe wakweli. Mbona uandikishaji ni wa lazima kwa watoto wote? Na sekkondari ni wa lazima kwa watoto wote wanaofaulu? Na kwa nini hawamalizi shule hadi Chuo Kikuu? Uandikishaji Vyuo Vikuu chini ya TCU mbona kigezo ni credits zako tu na unapelekwa Chuo chochote ulichoomba?. Kwa nini hawashindani bila kujihisi kuonewa? Waliwahi kulalamika kwamba magerezani kuna waislamu wengi kuliko wakristu. Hoja hii walishindwa kwa kuulizwa swali: "Hivi wana maana kwamba polisi wanaposhika wahalifu, wawaulize majina yao kwanza kabla ya kuwatia pingu? Na kama wakigundua ni waislamu, basi wawaachie waendelee na uhalifu kwa kuchelea kwamba tayari magereza ina waislamu wengi?" Hoja gani ya waislamu kuonewa wakati sheria za nchi zilishaondoa ubaguzi wa kidini na ubaguzi mwingine wowote mara tu baada ya uhuru? Nyerere alitaifisha shule zote za msingi kuondoa kero hii ingawa sasa hivi anaonekana kwamba aliidumaza nchi na alikuwa anawabagua waislamu?. Kama Nyerere alikuwa mbaguzi angemuachia Mwinyi nchi na hali akijua ni muislamu? Ndiyo maana Ikulu kuna waislamu. Wameenda shule wale wote. Waislamu wajue kwamba kazi serikalini lazima uwe 'competent'! Au wanataka utaratibu wa kumiliki cheo (kama Idi Amin) na ukitakiwa kuhutubia UN, wewe unakaa pale pembeni na "speech" inasomwa na mwakilishi? Kisa haki sawa? Kwani yule anayesoma "speech" hana haki ya kuwa "presidaa"? Mimi hoja ya waislamu kulalamika kuonewa haiingii akilini hata siku moja kwa sababu Tanzania inatoa fursa sawa za kielimu bila ubaguzi wowote katika ngazi zozote kuanzia miaka 50 iliyopita. Inasomesha hata wageni. Akina Joseph Kabila walisoma Sangu, Mbeya. Sasa waislamu wakipuuzia elimu tuilaumu serkali? "Absenteeism" na uvivu kwa watoto wa kiislamu shuleni ni kubwa mno, kwa nini maimamu wasiwahimize watoto wa kiislamu wakazane kusoma? Wasiwahimize wazazi ya kiislamu wawapeleke watoto shule? Waislamu kulalamika kwamba wanaonewa ni uwongo ulio wazi wazi hata mtu asiyeona atashangaa. Kwa sababu "top brass" ya viongozi serikalini ni waislamu na hata Wizara ya Elimu ni wao, au walibatizwa? Kelele za ubaguzi kwa waislamu zinatoka wapi? Tafadhali wakazane shule kwa watoto wao, watawasaidia na walimu wetu kudhibiti utoro! Watanzania tumechoshwa kelele zisizokuwa na hoja!
 
Wote mnaom support hiyo EL nawasiwasi sana nanyi na uwezo wenu wa kufikiri na huenda ni sehemu ya wanufaika wa mtandao wa mafisadi ndani ya nchi yetu unaojitahidi kutukandmiza watanzania tuendelee kuwa maskini.

Kwa nini hatujadili watu makini ndani ya ccm tunajadili watu walioshindwa kama EL?

Tujadili magufuli, mwakyembe, kagasheki kwa sasa tuache waizi na wenye tamaa ambao hawana rekodi iliyotukuka ya utumishi wa umma zaidi ya hasara na ubinafsi.

EL kwa uchache tu: hasara serikalini ni pamoja na
1. Magorofa ya masaki na fidia kwa mmli
2. Richmond na aggreco.
3. Kufukuza watumishi wa serikali wilayani kupitia majukwaa bila sheria za utumishi.
4. Kukusanya fedha za michango ya maafa na kuingia nazo mitini
5. Uchakachuaji wa mradi wa maji kahama
6. City water na dawasco kumchangia kila mwezi milion 100
7. Barabara ya msata bagamoyo uchakachuaji wa awali na kukisha mradi.
8. Kpanda. Kwa garama ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka 300m kwenda 1.3b kwa 1km
9. Kufanyaaa biaashara ya madawa ya kulevya kwa kuwashirolsha wadau wake akina RA.
10. Kuongeza wazawa wa arusha ndani ya utumishi wa umma kwamba wanaonewa.

Haya yote ni mapungufu ya EL yanayoonyesha nafasi ya uraisi haimtoshi hata kidogo.

Mwacheni apumzike.
 
Kila wakati marais wa mwelekeo fulani wakiingia ikulu hali inakuwa kama hivyo... kuna haja ya kufanya tathmini fulani na kuwa makini huko mbeleni....
 
Back
Top Bottom