Sasa umeamini kwamba Lowassa ni visionary?

Kwa hiyo mtu akisema kwamba kuna tatizo la ajira Tanzania, na kwamba serikali iliyopo madarakani haifanyi jitihada zozote za maana kutatua tatizo hilo ni pumba?

naamini hata ulichokipost hujui maana yake, kiujumla umekurupuka!
 
Kama Lowassa ni visionary hao visinary leaders kama Nyerere watakuwa nani? Hata kama mnalipwa hayo mabaki ya ufisadi basi jaribuni kutumia akili zenu. Sifa inayomfaa ni fisadi na fisi finish.
 
Anyways, EL aliliona hili mapema na alilisema mapema. Angekua kwenye power haya yasingetokea. Serikali ya sasa imefanya juhudi za kichekesho za kuinua kiwango cha ajira nchini, mfano ni Kilimo Kwanza.
 
Tatizo la ajira ni kwa wote. Lakini kwa sababu ya various factors, waislam wamekua affected disproportionaly. Kuna baadhi ya madai yao ni valid. Hayatatuliki kwa kutupiana lawama na kupigana virungu [ kwa pande zote mbili] bali kwa kukaa chini na kuyaongelea.
Matatizo yapi yapo validi?
 
Ni mnafiki na muongo wa kawaida. Mbona hakuyafanya alipokuwa madarakani kama ni visionary kama unavyotaka tuamini kana kwamba hatuna ubongo. Go tell it to the birds Lowassa ni fisi na fisadi asiyetufaa tena. Afaa akae Segerea kama si Ukonga.
 
"Ameongea kwenye majukwaa, mashuleni hata vikao vya ndani ya CCM."

Jukwa gani ulishamwona EL kasimama kuhutubia? Labda sema aliongea huko monduli na kanisani tutakuelewa!
 
Matatizo yapi yapo validi?
Wapo nyuma kielimu, kwa sababu mbalimbali za kihistoria, zinatakiwa juhudi za makusudi kuinua elimu katika shule za kiislamu kuhakikisha kuna qualified teachers, labs , computers na mambo kama hayo. Kuwapa chuo cha TANESCO was a start.
 
"Ameongea kwenye majukwaa, mashuleni hata vikao vya ndani ya CCM."

Jukwa gani ulishamwona EL kasimama kuhutubia? Labda sema aliongea huko monduli na kanisani tutakuelewa!

Is that important to you? kwamba alisemea wapi?
 
Lakini ajue kuwa huo ufisadi anao upioneer unakwamisha juhudi zozote za kupatikana ajira, hata yeye analifahamu hilo kuna uhusiano wa karibu sana kati ya ukosefu wa ajira na ufisadi.

Lets put it this way "Nyerere [ au Dr. Slaa, au Mrema, au JK, au Lipumba, au Zitto] amesema ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiri kupasuka"
Je kauli hii ina ukweli kama tukibadilisha jina la msemaji????
 
yeye amesaidia vipi licha ya kuwa na nafasi kubwa nchi hii zaidi ya kutukamua watanzania na ufisadi wake wa kupindukia..hivi tatizo la ajira una hitaji prof kulitambua hilo..
 
Anyways, EL aliliona
hili mapema na alilisema mapema. Angekua kwenye power haya yasingetokea.
Serikali ya sasa imefanya juhudi za kichekesho za kuinua kiwango cha
ajira nchini, mfano ni Kilimo Kwanza.

lowasa si wa kwanza kuona hilo. ni mzindakaya!
 
yeye amesaidia vipi licha ya kuwa na nafasi kubwa nchi hii zaidi ya kutukamua watanzania na ufisadi wake wa kupindukia..hivi tatizo la ajira una hitaji prof kulitambua hilo..

Tatizo hapa ni kwamba utawala wa awamu ya nne hauna mikakati yoyote ya kuondoa tatizo hili ambalo halihitaji uwe prof. kulijua. hence kua bomu linalosubiri kupasuka kama alivosema EL.
 
tatizo nhi hii ss hv , baada ya Nyerere, hakuna mtu/kiongozi anayeweza kukemea maovu na watu wakamsikiliza/wakamtii. Kila mtu anaongea/anafanya tu jinsi anavyojisikia. Eti uhuru wa mawazo/matendo haiwezekani kukawa na uhuru bila kikomo. Hata kwenye familia lazima kuwe utaratibu ambao kila mtu ndani ya familia lazima aufuate vinginevyo ni vurugu.
 
Back
Top Bottom