Sasa umeamini kwamba Lowassa ni visionary?

Kwame Nkrumah

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
886
376
EL amekua akipiga kelele mpaka sauti kumkauka kwamba vijana wasio na ajira ni bomu linalosubiri kulipuka.

Ameongea kwenye majukwaa, mashuleni hata vikao vya ndani ya CCM. Vurugu zote zinazoendelea leo ni kutokana na umasikini na kukosekana kwa fursa [ opportunities] kwa vijana wengi nchini. Ajira hamna, vikwazo visivyo na maana katika ujasiriamali, manyanyaso na kujuana kumepelekea suala dogo kuyumbisha nchi. Amani tunayoichukulia for granted inaanza kuyeyuka nchini mwetu.

Licha ya kwamba kuna udhaifu wa serikali yetu wa kutochukua hatua mapema kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kutokufuatutilia madai halali yanayolalamikiwa na waislamu, sera za CCM za divide and rule, ni wazi kwamba sakata hili limechocheka kwa kiasi kikubwa na vijana wanaokaa vijiweni kwa kukosa ajira.

Lowassa angekuwepo haya yasingetokea.

Siyo mshabiki mkubwa wa Mjenga, hasa baada ya sakata la Mwangosi, lakini leo hebu soma hii masterpiece yake leo
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/340157-ya-mbagala-na-bedui-aliyekojoa-msikitini.html
 
wewe umetumwa na nani kuja kumsafisha mtu? Au chimpumu na mnazi zinakuchanganya? Kuwa smart na unacho post.
 
el amekua akipiga kelele mpaka sauti kumkauka kwamba vijana wasio na ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Ameongea kwenye majukwaa, mashuleni hata vikao vya ndani ya ccm. Vurugu zote zinazoendelea leo ni kutokana na umasikini na kukosekana kwa fursa [ opportunities] kwa vijana wengi nchini. Ajira hamna, vikwazo visivyo na maana katika ujasiriamali, manyanyaso na kujuana kumepelekea suala dogo kuyumbisha nchi. Amani tunayoichukulia for granted inaanza kuyeyuka nchini mwetu.
Licha ya kwamba kuna udhaifu wa serikali yetu wa kutochukua hatua mapema kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kutokufuatutilia madai halali yanayolalamikiwa na waislamu, sera za ccm za divide and rule, ni wazi kwamba sakata hili limechocheka kwa kiasi kikubwa na vijana wanaokaa vijiweni kwa kukosa ajira.
Lowassa angekuwepo haya yasingetokea.

Siyo mshabiki mkubwa wa mjenga, hasa baada ya sakata la mwangosi, lakini leo hebu soma hii masterpiece yake leo
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/340157-ya-mbagala-na-bedui-aliyekojoa-msikitini.html
acha upuuzi wewe?
 
wewe umetumwa na nani kuja kumsafisha mtu? Au chimpumu na mnazi zinakuchanganya? Kuwa smart na unacho post.
 
haya yanayotokea hayana uhusiano na ukosefu wa ajira. Ni upungufu tu wa ufahamu na maarifa kadhaa. Ni sawa na kutaka kutuaminisha kuwa hili ni Taifa la kiislam kwani wanaosumbua huko ni wao pekee. Hakuna wakristo wasio na ajira? Wamevunja cha mtu? Tatizo ni mbegu ya chuki na utengano inayopandikizwa kisiasa kwa mgongo wa imani
 
Ukweli husemwa:

Kama maneno hayo ya Lowassa yanakufanya umuone kama ni 'visionary' basi Watanzania bado tuko bado mbali kuyafikia mabadiliko kamili.

Mbona hata kipofu wa fikra alilijua hilo. Lowassa alichokuwa akifanya ni kutumia jukwaa la kisiasa ambalo ni pana kwake kutokana na nafasi yake katika jamii kusema jambo ambalo hata kipofu wa fikra alilijua.

Tatizo letu Watanzania, tumejengeka tabia ambayo pale tunapomkubali mwanasiasa basi hata akisema pumba tunaona ni mchele kwa sababu hatujongelei yale anayoyasema kwa walakini ili kuwa na kipimo mbadala.

Hebu tusimpe sifa ambayo hasitahili.
 
Ni kweli,pamoja na yote tunayofikiri ametenda Lowasa;bado anastahili kupewa haki yake kama mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ! Watanganyika,hakuna mema aliyotenda Lowasa ?Tukumbuke,sifa mojawapo ya kiongozi ni kuwa na macho ya kuona yatayojiri kama Baba wa taifa letu,Mwalimu Nyerere.Kiongozi asiye na maono,ni kipofu;na akiwaongoza vipofu,basi wote watatumbukia shimoni !
 
Soma mada vizuri, haijatajwa ukosefu wa ajira pekee, ni sababu anuai. Lakini ukosefu wa ajira ni eneo kuu.
 
Ni kweli,pamoja na yote tunayofikiri ametenda Lowasa;bado anastahili kupewa haki yake kama mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ! Watanganyika,hakuna mema aliyotenda Lowasa ?Tukumbuke,sifa mojawapo ya kiongozi ni kuwa na macho ya kuona yatayojiri kama Baba wa taifa letu,Mwalimu Nyerere.Kiongozi asiye na maono,ni kipofu;na akiwaongoza vipofu,basi wote watatumbukia shimoni !

Mwenye sifa hii huitwa visionary. EL anayo.
 
Ukweli husemwa:

Kama maneno hayo ya Lowassa yanakufanya umuone kama ni 'visionary' basi Watanzania bado tuko bado mbali kuyafikia mabadiliko kamili.

Mbona hata kipofu wa fikra alilijua hilo. Lowassa alichokuwa akifanya ni kutumia jukwaa la kisiasa ambalo ni pana kwake kutokana na nafasi yake katika jamii kusema jambo ambalo hata kipofu wa fikra alilijua.

Tatizo letu Watanzania, tumejengeka tabia ambayo pale tunapomkubali mwanasiasa basi hata akisema pumba tunaona ni mchele kwa sababu hatujongelei yale anayoyasema kwa walakini ili kuwa na kipimo mbadala.

Hebu tusimpe sifa ambayo hasitahili.

Kwa hiyo mtu akisema kwamba kuna tatizo la ajira Tanzania, na kwamba serikali iliyopo madarakani haifanyi jitihada zozote za maana kutatua tatizo hilo ni pumba?
 
Uzi huu unaweza kuwa ba ukweli lakini chokochoko za dini zimeanza muda mrefu na aliyezipalilia na kuziivisha vizuri ni JK na magamba yake wakati wa kampeni baada ya kuishiwa sera na kuzidiwa na cdm. Suala la ajira kwa vijana ni secondary na chuki za kidini ni primary.
 
haya yanayotokea hayana uhusiano na ukosefu wa ajira. Ni upungufu tu wa ufahamu na maarifa kadhaa. Ni sawa na kutaka kutuaminisha kuwa hili ni Taifa la kiislam kwani wanaosumbua huko ni wao pekee. Hakuna wakristo wasio na ajira? Wamevunja cha mtu? Tatizo ni mbegu ya chuki na utengano inayopandikizwa kisiasa kwa mgongo wa imani

Tatizo la ajira ni kwa wote. Lakini kwa sababu ya various factors, waislam wamekua affected disproportionaly. Kuna baadhi ya madai yao ni valid. Hayatatuliki kwa kutupiana lawama na kupigana virungu [ kwa pande zote mbili] bali kwa kukaa chini na kuyaongelea.
 
Uzi huu unaweza kuwa ba ukweli lakini chokochoko za dini zimeanza muda mrefu na aliyezipalilia na kuziivisha vizuri ni JK na magamba yake wakati wa kampeni baada ya kuishiwa sera na kuzidiwa na cdm. Suala la ajira kwa vijana ni secondary na chuki za kidini ni primary.

Kwangu mimi naona suala la ajira ni PRIMARY, kwa sababu vijana tungekua na ajira na elimu ya kutosha CCM wangetudanganya vipi ?
 
Lakini ajue kuwa huo ufisadi anao upioneer unakwamisha juhudi zozote za kupatikana ajira, hata yeye analifahamu hilo kuna uhusiano wa karibu sana kati ya ukosefu wa ajira na ufisadi.
 
Back
Top Bottom