Christiano Ronaldo
JF-Expert Member
- Feb 14, 2012
- 258
- 41
Huyu Nabii T. B. Joshua juzi kabla ya mechi ya Zambia na Ivory Coast, aliposema yeye ameshauona mpira kabla na kwamba Ivory Coast wangekosa penalti dakika ya 25 kipindi cha pili, na Zambia wangechukua kombe, ndipo nimemvulia kabisa kofia!Mimi nimeshajiandaa kisaikolojia kwa ujio wa Rais mpya, sioni cockroch yeyote ndani ya CCM wa kuweza kumzuia mwanaume huyu wa Shoka, na kwa jinsi nijuavyo JK ni lazima ajisalimishe mapema kwa Lowasa ili visenti vyake vya uzeeni aweze kuvitumbuwa kwa amani.
Lowasa ni stering wa Kihindi, huwa anaanza kwa kupigwa na kuteswa lakini mwisho wa Sinema mtabaki vinywa wazi. na kwa wale wanaoamini kwenye maombi yule Nabii ambaye yupo duniani TB Joshuwa yeye tayari ameshamhakikishia Lowasa asubili kuapishwa tu.