Sasa Lowassa hakamatiki: Waraka kwa Jakaya Kikwete!

Mimi nimeshajiandaa kisaikolojia kwa ujio wa Rais mpya, sioni cockroch yeyote ndani ya CCM wa kuweza kumzuia mwanaume huyu wa Shoka, na kwa jinsi nijuavyo JK ni lazima ajisalimishe mapema kwa Lowasa ili visenti vyake vya uzeeni aweze kuvitumbuwa kwa amani.

Lowasa ni stering wa Kihindi, huwa anaanza kwa kupigwa na kuteswa lakini mwisho wa Sinema mtabaki vinywa wazi. na kwa wale wanaoamini kwenye maombi yule Nabii ambaye yupo duniani TB Joshuwa yeye tayari ameshamhakikishia Lowasa asubili kuapishwa tu.
Huyu Nabii T. B. Joshua juzi kabla ya mechi ya Zambia na Ivory Coast, aliposema yeye ameshauona mpira kabla na kwamba Ivory Coast wangekosa penalti dakika ya 25 kipindi cha pili, na Zambia wangechukua kombe, ndipo nimemvulia kabisa kofia!
 
Huyu Nabii T. B. Joshua juzi kabla ya mechi ya Zambia na Ivory Coast, aliposema yeye ameshauona mpira kabla na kwamba Ivory Coast wangekosa penalti dakika ya 25 kipindi cha pili, na Zambia wangechukua kombe, ndipo nimemvulia kabisa kofia!
Baelezeee!!,......
 
Huyu Nabii T. B. Joshua juzi kabla ya mechi ya Zambia na Ivory Coast, aliposema yeye ameshauona mpira kabla na kwamba Ivory Coast wangekosa penalti dakika ya 25 kipindi cha pili, na Zambia wangechukua kombe, ndipo nimemvulia kabisa kofia!
No way!Hivi ni kweli?Na bado si alisema kuna rais wa Afrika atakufa?

Kazi kweli kweli.
 
No way!Hivi ni kweli?Na bado si alisema kuna rais wa Afrika atakufa?

Kazi kweli kweli.
Nadhani kama sio Abdolauye Wade basi atakuwa ni Mugabe, hawa ni wazee wa hovyo kabisa ambao wanajitafutia vifo vya ghafla uzeeni.
 
Pesa ya Lowassa na marafiki zake ni safi na halali?

na Nkwazi Mhango
Dira ya Mtanzaniauna
Hakuna shaka kuwa Edward Lowassa waziri mkuu aliyetimka madarakani kutokana na kuingiza kampuni feki ya Richmond iliyoishia kuleta maafa kwa taifa, ni mtu ambaye amegeuka kuwa mkarimu hata kupita kiasi.


Hivi karibuni akiwa Kigoma akichangia shule ya Sekondari ya FPCT Bigabiro, Kigoma, alitoa mchango wa shilingi 60, 500,000 cash ukiwa ni mchango wake na marafiki zake ambao hawatajwi kwa majina. Huu si mchango mnono wa kwanza wa Lowassa hasa baada ya kuondoka madarakani. Wengi wanajiuliza: Kama ana uchungu na taifa hili kiasi cha kulitakia maendeleo na mengine mema, mbona alitumia nafasi yake kujinufaisha kwa kuingiza kampuni feki iliyoliingiza taifa kwenye zahama? Mwaka 2006 alichanga jumla ya shilingi shilingi 60, 000,000 kati ya sh 88,340,000 kwa ajili ya shule ya sekondari ya michezo ya Kigamboni. Hapa bado hatujaorodhesha michango mingine ya kuanzia shilingi 10,000,000 kwenda juu ambazo Lowassa ameishachangia kwa vituo vya yatima, kuzindua album, makanisa na mingine mingi.

Je hii pesa inayochangwa imepatikana kihalali au ni matunda ya tuhuma zake za Richmond na nyingine za zamani za marehemu baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyedai mwaka 1995 kuwa Lowassa amejilimbikizia utajiri mwingi ambao hautokani na kipato halali-asioweza kuutolea maelezo ulivyopatikana. Na kweli, tangu mwalimu alirushe kimondo hicho, si Lowassa wala familia yake walikuwa tayari kuelezea walivyochuma huo utajiri!

Baada ya Lowassa kulazimishwa kuutema uwaziri mkuu, alijikuta akikabiliwa na pigo jingine takatifu. Pigo hili ni pale chama chake Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipomtuhumu kuwa gamba au mtuhumiwa mkuu wa ufisadi kiasi cha kumtaka aachie hata nyadhifa chache alizokuwa amebakia nazo. Lowassa hakukubali kutupwa nje ya uringo wa siasa hasa ikichukuliwa kuwa anatajwa tajwa kutaka eti kumrithi rais Jakaya Kikwete hapo 2015 jambo ambalo wanaojua alivyochafuka sana wanaona ni kama tusi na kejeli kwa taasisi ya urais na wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Ili kufanikisha azma yake hii, Lowassa, bila kujali kuwa watu wana akili za kuhoji na kuchambua, amekuwa akimwaga pesa kwa njia ya michango ili kujiweka karibu na wapiga kura akiwaaminisha kuwa anaweza kuwafaa wakati nafasi ya kufanya hivyo aliishaipoteza kwa kuitumia vibaya na kuliacha taifa kwenye zahama ya kiza na kulanguliwa umeme.

Je haya mamilioni anayotoa Lowassa yanatokana na malipo ya marupurupu ya ustaafu anayopewa kinyume cha sheria? Maana, Lowassa hakuwahi kustaafu zaidi ya kulazimishwa kuachia ngazi. Wengi wanashangaa ni kwanini Lowassa anaendelea kutanua bila kufikishwa mahakamani. Pia wengi wanashangaa jinsi CCM inavyomgwaya kiasi cha kumtishiatishia bila kumchukulia hatua. Kuko wapi kutekeleza dhana ya kujivua gamba ambako kumekuwa kukiahirishwa baada ya Lowassa kutishia kumwaga mtama? Je Lowassa kwa kukikamata mateka chama chake na serikali yake anaweza vile vile kuwakamata mateka watanzania akaishia kuwa rais wao hata kama ataingia kwenye vitabu vya historia kuwa anaweza kuwa rais mwenye kuchafuka kuliko waliowahi kumtangulia? Je watanzania ni wa hovyo kiasi hiki? Je wanapopokea mamilioni yake wanategemea kumpa kura wakati ukifika au kuyatumia kama ushahidi kutaka aeleze aliko na alivyoyapata huku pia wakimlazimisha atoe maelezo kuhusu shutuma zake?

Wengi pia wangetaka kuwajua hao marafiki wa Lowassa wenye uchungu na taifa letu kiasi cha kumwaga mamilioni kama wameyapata kihalali au ni watu wa kuaminika au kutisha shaka. Lazima kujiridhisha isijekuwa wananchi na michango ya maendeleo vinatumika kusafishia pesa chafu itokayo kwa magenge ya watu wachafu. Hata hivyo, kwa wanaokumbuka adha alizowasababishia Lowassa kwa kubariki na kuingiza kampuni ya Richmond na hatimaye Dowans, hata awape nini hawawezi kumsamehe. Kwa wanaokumbuka ni mabilioni mangapi ya shilingi yaliteketezwa na mradi huu ambao waziri wa zamani wa Nishati na Madini Ibrahim Msabaha aliwahi kusema ni waziri mkuu yaani Lowassa na mhindi wake yaani Rostam Aziz, hawezi kupumbazwa na misaada ya mamilioni wakati wao walichuma mabilioni ukiachia mbali kuendelea kuchuma ya ustaafu wakati Lowassa hakustaafu.

Kama michango yote ambayo Lowassa ameishaitoa ingefanyiwa mahesabu, ni pesa nyingi kuliko hata mishahara yake yote ya utumishi wake serikalini. Kwa mfano mifano miwili hapo juu ya michango ya Lowassa ya shilingi 120,000,000 ni zaidi ya mshahara wa mbunge wa mwaka mzima. Hapa hajala wala kulisha familia yake kuvaa na kufanya mambo mengine. Kama Lowassa akifanyiwa ukaguzi wa kimahasibu tangu aanze kazi na marupurupu yake yote vikalinganishwa na misaada aliyowahi kutoa na mali anazomiliki itagundulika kuwa maneno ya baba wa taifa yalikuwa ya kweli. Na hivyo, yasipuuzwe wala kusahauliwa hasa wakati huu ambapo nchi inahitaji uongozi adilifu na mpya.
Tumalizie kwa kumtaka Lowassa awataje hao marafiki zake na jinsi walivyopata hayo mamilioni. Lazima tujue kama wanafanya biashara au kazi halali, wakilipa kodi na kama ni watumishi wa umma akiwamo naye na Lowassa, je wametaja mali zao kama wanavyotakiwa na sheria? Kujua ukweli kuhusu jinsi wanavyopata pesa hii wanayotoa kwa jina jema la kusaidia jamii ni jambo jema. Lazima kila kitu kieleweke ili kuepuka jamii kugeuzwa kama fisi kulishwa nyama yake nayo ikaifakamia kwa uchoyo. Ni wakati muafaka kuangalia nani anatoa kuliko kuangalia nini kimetolewa. Hapa tuepuke cha baniani mbaya kiatu chake dawa.
 
Mkuu kama wewe ni muhudhuriaji mzuri hapa jamvini huwezi kutokuelewa msimamo wangu, lakini leo nimeamuwa NO porojo, tumechoka na hizi ngonjera za Lowasa Fisadi, tunahitaji evidence hapa. Full stop.
Ndio maana nimeup load picha hii hili wale wapiga vuvuzela watueleze hiyo ni bahasha ya nini? je huyo anaepokea ni Askofu!!??

1.JPG
Inawezekana kabisa mimi wewe yule na yule mwingine humu ndani ya jf tunahitaji kwa udi na uvumba evidence ili kujua kama lowassa ni fisadi ama la lakini bahati mbaya sana wenye ccm yao wakiongozwa na mwenyekitiwao hawahitaji evidence yeyote zaidi ya kura chache walizozipata kutokana na kwenda kwenye majimbo ya mafisadi na kuwashika mikono,ghazabu za wananchi juu ya ccm kuwakumbatia mafisadi walizozionyesha kwenye sanduku la kura ni ushahidi tosha wa kichama lakini nyie ambao hamko ndani ya chama mnaweza kuendelea kudai ushahidi wa kimahakama lakini kwa ccm lowassa hatufai,ila vyama viko vingi anaweza kwenda kungine mkamfuata haina shida.SISI UPANDE WETU KAZI IMEISHA KWENYE KIKAO CHA NEC KILICHOPITA KILE AMBACHO KINGUNGE NA PETER WALILIA SANA
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mi nafikiri mada hii ilifaa kwenye kura za maoni ndani ya chama. Rais wa wananchi 2015 ni DK SLAA iyo mbona mjadala ulishaisha au wanagombea uraisi wa kongo sielewi hii mada
 
Mi nafikiri mada hii ilifaa kwenye kura za maoni ndani ya chama. Rais wa wananchi 2015 ni DK SLAA iyo mbona mjadala ulishaisha au wanagombea uraisi wa kongo sielewi hii mada
 
hapa ndo kuna kila kitu




JK: Mimi sijui Bwana, sijui. Mimi ningependa kuamini kwamba nilifanya jitihada kubwa kushinda, na wasije wakafika mahali wakarahisisha mitihani niliyoipitia. Nilifanya jitihada kubwa sana. Sisi ni katika wale tunaoamini kwamba mwisho wa uchaguzi mmoja, ni mwanzo wa uchaguzi mwingine. Sisi tulianza mwaka 1995, tukaweka mkakati wa mwaka 2005.Nilifanya kazi kubwa kujenga mtandao. Nilifika mahali, kila mahali ukinitajia Ngara yuko nani, nakwambia yuko fulani. Nikawa nawajua watu kwa majina. Nimefanya kazi kubwa sana. Ndiyo, nakiri kwamba uzoefu wangu nao katika chama ulinirahisishia. Kwamba hawa watu ninawafahamu, nimeshaishi nao, ndiyo msingi ambao mimi ninadhani umesaidia.
Lakini wanaodhani nilishinda kwa hotuba ya Rais wanatafuta kurahisisha tu ili ionekane kwamba kama isingekuwa hotuba ile watu wasingenichagua. Hata kidogo! Mimi nilianza zamani. Ninaamini tu kwamba nilifanya jitihada mimi mwenyewe ya kuwaomba wana-CCM waniunge mkono, na ninashukuru walinikubali baada ya kuwaeleza nia yangu ni nini.


Alijiandaa kwa zaidi ya miaka kumi kuingia Ikulu lakini hakujua ni kitu gani hasa anaenda kufanya atakapokuwa Ikulu.
 
Najiuliza maswali ya kijinga......
1) U-rais ni nini hasa?
2) Je kwa nini Lowassa (au kambi yake) wanaona kuwa ni lazima yeye na yeye pekee ndiye (lazima) awe rais wa Tz 2015?
3) Kwa nini hawazioni nyufa lukuki ktk hoja zao nyepesi na mantiki zao tata juu ya mtu wao huyo?
4) Je Lowassa ana ushawishi gani kiuwezo na maadili hata kujaribu kufikiria nafasi ya Urais?
5) Ikiwa yeye anataka Urais kwa mbinde namna hiyo na wananchi hawamtaki......atatumia nini kutimiza azma yake hiyo?

In short what can he offer which ccm and Kikwete could not offer?

EL anajua fika kuwa yeyote atakayekuwa rais wa JMT either atoke CCM au upinzani ni lazima atafuatilia utajiri wake umepatikana vipi, na kama hakutakuwa na majibu ya kuridhisha he is likely to go to jail au kufilisiwa.

Option iliyobaki ni lazima yeye ndio awe rais kwa sababu ndio salama yake. Na kuthibitisha kuwa anautaka urais ili kujiponya na maovu yake mwenyewe na si vinginevyo, anatumia nguvu nyingi sana lakini hazungumzi kabisa kuhusu ufisadi ambao ndio adui nambari one wa maendeleo ya watanzania.

Lowasa hana vocabulary ya ufisadi kwenye kamusi yake, sijui atapambana vipi na wizi wa mali ya uma ikiwa hata kuongelea tu hataki. Wanaomtetea wanasema ni mchapa kazi. Hawafahamu kuwa ni mifumo (strong institutions) ndizo zinazotenda kazi kwenye nchi yeyote yenye nia ya maendeleo.

Watanzania wengi na hata wasomi wanamuona waziri au rais ni mchapa kazi wakimuona kwenye TV anafokea watu, anaenda kila mahali TZ na kutoa hotuba, bila kujua kuwa unapotengeneza institutions ambazo ni independent na strong rais au waziri anabaki kufanya kazi at a higher level, unaweza usimsikie sana ila kila kitu kinaenda sawa.

So Tanzania hatuhitaji mtu, tunahitaji strong institutions ambazo nna uhakika mtu kama Lowassa will be totally against it, hawezi kuweka institutions ambazo zitainvestigate ufisadi wake yeye au kuzuia madili yake ya wizi ( because he is a champion in this front).

I suggest we forget kwamba CCM candidate anaweza kufanya transformation kwenye taifa letu, Lowassa being one of them.
 
Nukuu ya maneno haya unajua maana ya upana na tafsiri yake?
Poleni kwa kazi ya kuahalalisha maovu kwa ulaghai wa maneno ya Mwl.

Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua kuwa hana makosa. Na msingi wa woga ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna wala tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi wote tunayo tamaa hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza ukamfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana.

 
..JK: Jibu ni ndiyo. Ni kweli tu kwa sababu, kwanza kwa maana tu ya uzoefu wangu katika utumishi wa umma, katika serikali. Lakini miaka 10 hii ambayo nimekuwa katika Wizara ya Mambo ya Nje, imenipa fursa kubwa na pana zaidi ya kuifahamu dunia na pia kufahamu hasa jinsi nchi zinavyoendeshwa.Nimepata uzoefu mkubwa wa kujifunza nchi zinazoendeshwa vizuri, na kwa nini wamefanikiwa. Nchi zinazoendeshwa vibaya, ni kwa nini wameshindwa...

Interesting
 
Vijana kazini na mamoderm/blackberry zao kumsafisha lowasa e,kazikwelikweli picha linaendelea.........
 
kwa nini umwite mwanaume wa shoka? ana nini kipya cha kuongoza taifa hili linalozama na hatimaye lirudi katika msawazo? Niaminivyo mimi ni wachache( kama wapo) katika "Chama Cha Magamba" taifa linaweza jipatie kiongozi shupavu wa kuliokoa taifa hili.
Tunahitahi "God fearing person to take us out of this corruptive cycle of leadership" na Magamba hayana mtu wa aina hiyo atakayeona raslimali za nchi hii ni za wanachi wa nchi hii!
Mungu utuondolee balaa hili la kuongozwa na EL, Tupatie mtu anayekuabudu na kuamini katika amri zako ili atuongoze kutupeleka upapendako wewe na si yeye.
Mimi nimeshajiandaa kisaikolojia kwa ujio wa Rais mpya, sioni cockroch yeyote ndani ya CCM wa kuweza kumzuia mwanaume huyu wa Shoka, na kwa jinsi nijuavyo JK ni lazima ajisalimishe mapema kwa Lowasa ili visenti vyake vya uzeeni aweze kuvitumbuwa kwa amani.

Lowasa ni stering wa Kihindi, huwa anaanza kwa kupigwa na kuteswa lakini mwisho wa Sinema mtabaki vinywa wazi. na kwa wale wanaoamini kwenye maombi yule Nabii ambaye yupo duniani TB Joshuwa yeye tayari ameshamhakikishia Lowasa asubili kuapishwa tu.
 
Kama kuna changamoto tutakayokumbana nayo kama Taifa mwaka 2015 ni kumpata Kiongozi muadilifu ambaye ataivusha Tanzania toka hapa ilipo.Kuna kutokuaminiana kwingi baina wa wananchi.Kama wananchi sisi kwa sisi hatuaminiani je itakuwa kwa kiongozi wa nchi kuaminiwa.

Lazima tuwe na mfumo imara wa kutupatia kiongozi shupavu atakayerejesha umoja wa nchi pamoja na heshima ya mwananchi katika nchi yao.Hili likienda sambamba na kuimarisha uchumi wa nchi na uchumi wamwananchi mmoja mmoja.

Tukubali kuwa makosa yalifanyika 2005 na gharama yake inalipwa mpaka sasa.Endapo makosa yatafanyika tena 2015 gharama yake itakwenda mpaka 2050 je tuko tayari kuilipa hiyo gharama.Kizazi hiki cha sasa kina kazi kubwa sana ya kufanya ili kuweka mustakabali wa Taifa sawa.Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom