SAKATA LA UMEME ZANZIBAR: Lawama kwa Serikali, Tanesco ama ZECO?

I thin that mr president is right, if they want their ASP, they will be given

Kwani wewe Mheshimiwa unaijua hiyo ASP au unaisikia katika story tu. na kuwa Sheikh Abeid Amani Karume ndiye alikuwa Rais wake. Na ilikuwa imetokana na Muungano wa African Association na SHIRAZI Association. Ogopa sana watu wakijadai kupewa SHIRAZI Association.
 
Umeme sisi tutachoma mafuta (Mungu si Athumani yapo tele huko) Huo wa maji kaeni nao wenyewe Mabwawa yakikauka shauri lenu. Lakini kura tutapiga ya maoni Muungano basi, na fidia mtatulipa. Hata ikiwa kulipiana "The Hague"

wewewewewe taratibu asikusikie Hatibu
 
Kwani mtakuwa wa kwanza? Mbona USSR, Chekoslovakia, Yugoslavia hatuna tena?

Hivi mnadhani mkipata nyinyi mafuta bara yatakosekana? The Hague atafutwa mwenye haki na usijekuta mnaambiwa nyinyi mtulipe maana vitabu vyote vitakuwa wazi na nyinyi mapato ya karafuu yaliisha zamani! Msipende kututishia kuwa mtavunja Muungano. Fanyeni kweli muone kama tutalia! Tuone wale wote walio Sharif Shamba na msasani kama watarudi kwenu. Msitubabaishe.

Hapa pametokea uzembe kama alivyohisi Pundit na waliosababisha wachukuliwe hatua. Si hii biashara ya kila siku kuwa hampendwi!
Vipi yakhe, vitabu vyote ameondoka navyo Marehemu Balali. Hizo,kumbukumbu ziko wapi? Lakini nyinyi mtaonekana mlivyotunyima mambo, kama hiyo miundombinu mkajitengenezea ya kwenu tu- (huo ni uchoyo). Nakubaliana nawe suala la uzembe lina nafasi kubwa katika hiyo kadhia ya umeme, na wafanye uchunguzi wa kina Kuna wengi wasioitakia mema Zenj yetu. Hatulii sana kutopendwa. Ndiyo ndugu mdogo Kaka- huelewi wewe.
 
Mambo yazidi kunoga ,sasa kama nilivyosema mwanzoni Bado Kikwete ana mpira ,wahafidhina walijaribu kupiga kona ya kusema wanatarajia mhandisi kutoka Norway ,sasa kona imebadilishwa umekuwa mpira wa kurushwa na safari hii anatarajiwa fundi kutoka France maneno ya dibaji ni yale yale kuwa fundi anatarajiwa kufika ndani ya siku mbili moja ikiwa imeshapita.
Na kila wahafidhina wanapopata na kuekewa microphone na watu wa habari na utangazaji utawasikia wakisema majenerata yamewasili na yanatarajiwa kuanza kazi ila wanasubiri mafuta ya dizeli ambayo yanatarajiwa kufika wakati wowote.
Kuna habari kuwa ikiwa itatimia mwezi serikali haijafanya chochote wananchi wataandamana kutaka serikali ya Karume ijiuzulu.Wanasema sasa huku ni kucheza na maisha ya watu wakati wao wakitafuna fedha za umma.
Hapa kwa taarifa yenu vyama vya upinzani havihusiki wala chama tawala kwani wote wanaonja joto ya kukosekana umeme ni wananchi na serikali iliyopo madarakani.

Mapaparazi mitaani hapo chini ,nafikiri unaclik inakuwa picha kubwa.
 
[media]http://bp0.blogger.com/_HO8ijU76ZcQ/SD7ETIw4zQI/AAAAAAAASdA/ERF_PkBv0Is/s400/charcoal_iron_by_Peter_Bennett_IMG_4235e.jpg[/media] [media]http://bp3.blogger.com/_HO8ijU76ZcQ/SD6tg4w4zJI/AAAAAAAAScI/OYDDVED7Y20/s400/generator_in_Stone_Town_by_Peter_Bennett_IMG_4192e.jpg[/media]

[media]http://bp1.blogger.com/_HO8ijU76ZcQ/SD6tgYw4zII/AAAAAAAAScA/xkgo1wURfQo/s400/fetching_water_by_Peter_Bennett_IMG_4221e.jpg[/media] Babaake


[media]http://bp0.blogger.com/_HO8ijU76ZcQ/SD6thIw4zKI/AAAAAAAAScQ/EXa_Mcw-W-4/s400/parafin_lamps_in_market_by_Peter_Bennett_IMG_4205e.jpg[/media] Tanesco super market

[media]http://bp1.blogger.com/_HO8ijU76ZcQ/SD6thYw4zLI/AAAAAAAAScY/zK8kA_IASIE/s400/parafin_stove_by_Peter_Bennett_IMG_4189e.jpg[/media] Jiko mbadala
 
Last edited by a moderator:
mwiba kweli umepinda
inapendeza sana pale serikali inapowalazimisha watu wafunguke macho lakini wananchi wanaendelea kulala
 
Shamhuna ndiye rais au? kama ndio hivyo naona ataweza kufanikisha hilo zoezi.
 
Rais Karume amesema nini kufuatia hii kasheshe?

Mheshimiwa Karume kasema watu watazoea mbona wenzao wa Pemba hawana umeme.
Ila wananchi wanasema kuwa kuna jamaa wale wanaovaa magwanda ,nimefahamu amekusudia polisi anasema wananuka ile mbaya , na pia watu siku hizi hawapiti chini ya zile nyumba za magolofa ,kuna viparcel vya vifuko vya rambo huwa vinarushwa kutoka kusiko julikana bila mpango usiombee kikakupiga cha kichwa ,unaweza ukaisahau bahari iko upande gani .
Hata mimi naona ikiwa hili jambo litatimia miezi mitatu na sio mmoja ni bora serikali ijiuzulu yaani ni kitu kiko wazi kabisa ,kuonyesha kuwa serikali imeshindwa kabisa ,halafu kila mmoja atafute njia aelekee.
Nyakati za usiku beach za Unguja hugeuka kuwa nude beach ,watu kibao wanakoga na kufanya haja zote ,hakuna kuona haya au yale ,ndio hivyo wameanza kuzoea.
 
Vipi yakhe, vitabu vyote ameondoka navyo Marehemu Balali. Hizo,kumbukumbu ziko wapi? Lakini nyinyi mtaonekana mlivyotunyima mambo, kama hiyo miundombinu mkajitengenezea ya kwenu tu- (huo ni uchoyo). Nakubaliana nawe suala la uzembe lina nafasi kubwa katika hiyo kadhia ya umeme, na wafanye uchunguzi wa kina Kuna wengi wasioitakia mema Zenj yetu. Hatulii sana kutopendwa. Ndiyo ndugu mdogo Kaka- huelewi wewe.

Bandari yenu ilikuwa chini ya Muungano. Mkalalamika, mkapewa. Hadi leo gati limewashinda kutengeneza! Tukisema na viwanja vyenu vya ndege viwe chini ya TAA nako mtapiga kelele. Barabara zinatengenezwa na kodi ya barabara, kwenu sidhani kama mnayo! sasa, mkuu, mlitaka tumkate kodi chogo ili tuwatengenezee nyinyi barabara. Wasioitakia mema zenj ni wazenj wenyewe. Hampendani wenyewe kwa wenyewe. Mkiacha visiasa vyenu vya vijembe na kuungana katika kuona zenj ni yenu wote ndipo patakuwa na matumaini. Kwa hali ilivyo hivi sasa hata mkijitenga hamtakuwa na amani.

Tatizo la umeme ni la kiutendaji. Wahusika bara waseme kama kwao ni kwema na wale wa zenj hivyo hivyo. Penye tatizo wapaweke wazi ili wananchi waelewe. Sioni sababu ya usiri.
 
Mheshimiwa Karume kasema watu watazoea mbona wenzao wa Pemba hawana umeme.
Ila wananchi wanasema kuwa kuna jamaa wale wanaovaa magwanda ,nimefahamu amekusudia polisi anasema wananuka ile mbaya , na pia watu siku hizi hawapiti chini ya zile nyumba za magolofa ,kuna viparcel vya vifuko vya rambo huwa vinarushwa kutoka kusiko julikana bila mpango usiombee kikakupiga cha kichwa ,unaweza ukaisahau bahari iko upande gani .
Hata mimi naona ikiwa hili jambo litatimia miezi mitatu na sio mmoja ni bora serikali ijiuzulu yaani ni kitu kiko wazi kabisa ,kuonyesha kuwa serikali imeshindwa kabisa ,halafu kila mmoja atafute njia aelekee.
Nyakati za usiku beach za Unguja hugeuka kuwa nude beach ,watu kibao wanakoga na kufanya haja zote ,hakuna kuona haya au yale ,ndio hivyo wameanza kuzoea.

Subutuuuu!!! hivi unategemea kabisa kutoka moyoni kuwa atajiuzulu mtu pale??? Mie nasema pigeni kura ya maoni kuhusu kuandamana au la. Maana kila kitu zenji ni kura ya maoni siku hizi. lakini fahamuni kuwa maumivu ya kichwa huanza tartibu.....
 
serikali iliochaguliwa na wananchi kwa ridhaa inaenda mbio kuhakikisha wanatatua tatizo hili.


ni kweli tatizo linaathiri maisha ya wananchi, serikali yenyewe na uchumi wa nchi yetu hili linajulikana na si kweli kama SMZ tunafurahia hili.


ni suala ambalo hakuna aliekuwa akitarajia kutokea na hatukuwa na mudaa na nguvu za kujiandaa nalo kabla.

juhudi zinafanywa na wakati huo tunawaelimisha wananchi wanachi wetu ukubwa wa tatizo lenyewe na juhudi zinazoendelea.

ama wachache ambao wamelichukulia kisiasa hatuna uwezo zaidi wa kuwaambia ila ni kuwaaacha wabwabwaje, ndio siasa wakipata nafasi moja wanaitumia

ila mazao kutoka pemba yaja na meli za CCM wakija unguja hupanda CUF imepoteza Ngome yake
 
meli zinazoenda pemba ni meli zinazomilikiwa na wana CCM na wao walisema hawapandi ndivyo livyokusudia \

kwani hujasikia walipokuwa wakitoa hadidu zao kwa wanachama wao. huu si wakati wa kulala wananchi wameamka.

macuf huharibu hali ya mambo wakati wao wakiishi maisha mazuri watoto wao wakisoma nje ya zanzibar na nje ya tanzania wakari makabwela wenye kuimbishwa nyimbo wasizozijua wakiumia. wananchi wamechoka, yeye asipeleke bidhaa zake unguja lkn hawampi njia ya pili kupata riziki ya kiuendesha maisha yao. kama kususia wangeanza viongozi wao kukataa mishahara wanayopewa na SMZ kwenye baraza la wakilishi na maalim seif angekataa mafao yake hadi hicho wanachokidai kitendeke.

unafiki mtupu kuwaumiza na kuwaonea makabwela tu
 
Indeed, with the black out zanzibar is a living hell.
I cant imagine how much people are suffering there, a mere charging of a phone is done at 2,000/- ? isitoshe even kabla the black out maisha in znz is too expensive, ukianza with food and housing and even transport ... with chakula usiseme, when one is going to znz unatamani ubebe kila aina ya chakula from bara but you are penalized kwenye meli; they charge you heavily as if you are carrying gold or what, i dont knw. ukija mahospitalini ndiyo usiseme, if you can when one is sick, take the first boat out to bara immediately.

Food stuffs .... please visit the market .. nyama alone is 6000 - 7000 per kilo mpo jamani ??? ndizi hizi kisukari zinapimwa kwenye minzani when here you just pick in bunches at a cheap price ... i guess thats why wanadevelop roho mbaya maana mtu kama hupati kula sawasawa unakuwa na mapungufu hata ya akili .....sorry

These people i think have the right to complain and if ccm doesnt find the right candidate bora they give cuf a chance .... otherwise shauri yao.
 
Sisi yetu macho, ninalazimika kuamini kuwa kuna mkono wa mtu yaani kifaa muhimu nchi inakaa bila spare, kweli viongozi na proffessional hatuna hao ZEC kwanini walikaa bila spare wakati wanajua kuwa kinaweza kuaribika na kuleta balaa kwa nchi kwama hivyo?
 
Sakata la umeme Z`bar: Wapinzani wacharuka

2008-06-01 17:42:11
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Viongozi wa upinzani Zanzibar wamecharuka na kuitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutafuta njia mbadala ya kumaliza sakata la umeme badala ya kusubiri Wazungu kutoka Ulaya.

Wakuu wa NCCR Mageuzi, CUF, TADEA na CHADEMA walisema hayo na kuongeza kuwa hali ya uchumi Zanzibar kwa sasa inasikitisha.

Wakati vigogo hao wakitoa maelezo hayo Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), limepata hasara ya Sh.milioni 360 kutokana na kila siku kupoteza zaidi ya Sh milioni 30 mapato ya biashara ya umeme.

Walisema tangu kukosekana kwa umeme wiki mbili gharama za maisha zimepanda na kuzidi kuongeza umaskini.

``Serikali itafute chanzo mbadala, wakati ikiendelea kusubiri watalaamu kutoka Ulaya kunusuru uchumi,`` alisema Katibu Mkuu wa TDEA Bw Juma Ally Khatib.

Aliitaka ZECO inununue majenereta na SMZ ifuate nyayo za Serikali ya Muungano, ambapo baada ya kukosekana umeme kutokana na ukame ililazimika kuagiza majenereta ili kufua umeme.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Kitaifa wa NCCR Mageuzi, Bw Ally Omari, aliwataka viongozi kuwajibika kutokana na tatizo la umeme Zanzibar.

Alieleza kuwa njia ya umeme wa baharini inayopeleka umeme Zanzibar umri wake wa kutumika ni miaka 30 lakini hadi sasa ina miaka 28 lakini hakuna chanzo mbadala.

``Ikizingatiwa misingi ya utawala bora, tunaona uzembe wa wazi na hakuna njia zaidi ya viongozi kujiuzulu kutokana na hasara iliyopata na wananchi kuteseka`` alisema Bw Ally Omari.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Hamadi Mussa Yusuph, alisema inashangaza kuona kuwa miaka 44 ya Uhuru wa Zanzibar hakuna wataalam wa kutatua tatizo la umeme.

Alisema Zanzibar ya sasa ni lazima iwe na wataalam wenye ubingwa katika masuala ya nishati.

Alieleza kuwa kuagiza wataalam kutoka nje ni kuibebesha gharama SMZ na kupitia walipa kodi.

Hata huivyo, alisema ni jambo la kushangaza Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano lakini serikali imekaa kimya licha ya wananchi kuwa gizani.

Zanzibar haina umeme kutokana na kulipuka kwa waya wa baharini unaopokea umeme kutoka gridi ya taifa Kidatu.

Sekta ya utalii ni moja ya maeneo yaliyoathirika kutokana na hoteli nyingi kushindwa kupokea na kuhudumia watalii kwa vile hakuna maji wala umeme.

CUF kwa upande wake imesema tatizo la umeme Zanzibar ni matokeo ya uzembe wa SMZ kuendelea kutegemea umeme wa Bara bila kutafuta chanzo mbadala.

Waziri Kivuli wa Wizara wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Bw. Hamad Masoud, alisema SMZ ingechukua hatua mapema ya kuwa na umeme wa dharura, Zanzibar isingekosa umeme.

Aliishutumu serikali kwa kushindwa kuwashirikisha mafundi wa TANESCO katika matengenezo ya kifaa kilichoharibika.

SOURCE: Nipashe
 
Hilo sakata ni kubwa kuliko linavyoelezwa ,inasemekana serikali ya wahafidhina ilikuwa tayari kuwabebesha lawama CUF na kuanza kuwakamata viongozi eti wamefanya hujuma lakini ikaonekana hujuma hiyo hainunuliki na huenda ikazidisha hulka za watu wa visiwani .
Na kila siku zikiongezeka kuna habari ambazo zinasemekana ni za uongo .kuagiza mafundi kutoka nchi za Ulaya wakidai watawasili baada ya siku mbili sasa imeshakatiza wiki nzima hakuna fundi alietokeza pua ,kama haitoshi inasemekana na kasha la mkarafuu nalo tupu fedha ya kulipa mafundi inaelekea kuwa ni tatizo linaloanza kuchukua sura ,hilo shirika la umeme lilikuwa linafanya biashara wameshau kama katika biashara kuna faida na hasara ,zaidi sielewi kwanini wanaita hii ni biashara wakati shirika hilo ni la serikali kwa hivyo hii ni huduma nambari one ambayo ilitakiwa kupewa kipau mbele kuiita biashara ni dharau ya hali ya juu maana anytime unawezakuamua kufunga biashara yako ikiwa hakuna faida na kwa mujibu wa habari hiyo hapo juu hawa jamaa sasa hawapati faida ni hasara tu ,Je ndugu msomaji ikiwa ni hasara inayopindukia mamilioni hivi upo uwezekano wa kumleta fundi hapo , naona biashara imefungwa au itafungwa na itakuwa hakuna wakulaumiwa.
Baada ya kukosekana mafundi kwa siku moja au mbili ambazo wangewasili wakati kifaa kitawasili baada ya mwezi ,sasa watu wanasubiri wiki zilizobakia kuona hicho kifaa kinachoagizwa wakati hakujasemwa kama kimeshalipiwa. Hapa ndio unapata matumizi ya neno Kasheshe.
 
Back
Top Bottom