Mwanza walia na mgawo wa umeme

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
WAKAZI wa Jiji la Mwanza, wamepaza sauti zao, hususan wafanyabiashara wa hoteli na sehemu za kutoa huduma za afya, kwa kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kutoa ratiba ya mgawo wa umeme inayoeleweka.

Pia wamesema biashara zinahitaji kutumia gharama kubwa katika uendeshaji, kutokana na kulazimika kutumia jenereta linalotumia mafuta ya dizeli ambayo inauzwa kwa Sh. 3,236 kwa lita.

Nipashe imefanya uchunguzi kwa siku tano kuanzia mwishoni mwa wiki, imebaini nishati ya umeme inakatika kila siku na ukiwapo unadumu chini ya saa sita hadi nane kwa siku, na kufanya baadhi ya wafanyabiashara zinazotumia umeme kufunga kwa muda.

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, jijini Mwanza, mmiliki wa duka la samaki, Florence Masanja, alisema hifadhi samaki ni kwa saa 24 katika friji, ingawa sasa inamlazimu kununua mzigo kidogo ambao hautakaa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom