Revealed: Watoto wa 'vigogo' waliotimuliwa TANROADS, Majina haya hapa...!

Kinyume na kauli ya Waziri wa ujenzi Dr. Magufuli pamoja na Mtendaji mkuu wa Tanroads Eng. Mfugale, imebainika kuwa waliofukuzwa kazi Tanroads si watoto wa vigogo.

Baadhi ya majina ya waliofukuzwa kazi ofisi ya Tanroads mkoa wa Pwani niliyopenyezewa ni haya hapa:
1. Bashiry Saidi: Elimu yake FTC (DIT)
2. Leonard Luther: Elimu yake FTC (Arusha Technical College)
3. Pendo Kibunje: Elimu yake Diploma (NIT)
4. Lusubilo: Elimu yake Diploma (NIT)
5. Ndibaza: Elimu yake haikupatikana mara moja.

Waziri Magufuli alidai kwamba wengi wa hao watoto wa vigogo hawana sifa za kielimu. Lakini kinyume chake wamewafukuza kazi watoto wa masikini.

Hii nchi ni ya propaganda nyingi sana
 
Ndugu wajumbe najaribu kutoa maana ya neno"Kigogo" kama lilivyotumika kisiasa, Kigogo ni mtu yeyote mwenye nguvu kipesa,mwenye/amewahi kuwa na mamlaka 'kwa kuwa na nafasi kubwa'katika taasisi za chama au serikalini.
 
Kwani walikuwa na nafasi zipi?
Make FTC ni elimu pia inayojitosheleza kwa nafasi fulani.

Pia najiuliza hivi hawa watoto wa vigogo waende wapi? mbona wanapigwa vita kila sehemu hata wale waliosoma vizuri akishakuwa mtoto wa kigogo basi kachomekwa. Je wao si haki yao kupata kazi nzuri hapa TZ?

Sikubaliani na wale wanaopewa nafasi sizizolingana na uwezo wao ila tukubali wako watoto wa vigogo wamesoma vizuri tu na wana uwezo mkubwa na wanastahili kupata kazi nzuri.

tatizo lao hawafanyi interview wao wanakuja na vikaratasi tu,hila wakipita njia kama za wengne hamna tatizo.
 
Watu wa mizani wafukuzwe kwa sababu nyingine lakin hili la kuwa ni watoto wa vigogo ni publicity stunt tu.mimi nawafahamu kama jamaa wa 2 hiv wapo mizani na wanatoka familia za kawaida tu.
Kwanza kigogo gan atampeleka mwanae mizan?labda kama hataki shule!taasis zenye watoto wa vigogo wanazijua wanataka kutuzuga.
 
Kinyume na kauli ya Waziri wa ujenzi Dr. Magufuli pamoja na Mtendaji mkuu wa Tanroads Eng. Mfugale, imebainika kuwa waliofukuzwa kazi Tanroads si watoto wa vigogo.

Baadhi ya majina ya waliofukuzwa kazi ofisi ya Tanroads mkoa wa Pwani niliyopenyezewa ni haya hapa:
1. Bashiry Saidi: Elimu yake FTC (DIT)
2. Leonard Luther: Elimu yake FTC (Arusha Technical College)
3. Pendo Kibunje: Elimu yake Diploma (NIT)
4. Lusubilo: Elimu yake Diploma (NIT)
5. Ndibaza: Elimu yake haikupatikana mara moja.

Waziri Magufuli alidai kwamba wengi wa hao watoto wa vigogo hawana sifa za kielimu. Lakini kinyume chake wamewafukuza kazi watoto wa masikini.

Mbona kigezo cha kuwafukuza haieleweki? Je, ni kwa sababu kuwa mtoto wa kigogo, hawana sifa za kuajiriwa au sababu za kinidhamu?

Kama ajira haijafuata utaratibu angefukuzwa huyo aliyewaajiri badala ya kuwafukuza watu ambao hawana makosa (innocent).
 
magufuli naye boya kumbeee??
ngoja tumsubiri mwakyembe na ripoti ya bandari sasa
 
Wamefukuzwa kwa sababu gani?

ELIMU HABA MKUU
MAGUFURI KAFANYA PhD sasa hawajamaa huenda anawaona elimu ndogo kulingana na nyadhifa walizo pewa kupitia vimemo...wakati kuna vijana magufuri alikua anakula nao desa pale UDSM wapo-kitaa na anawaamini.. So kusafisha njia kaanza na hawawachache.
MAWAZO YANGU TU JAMANI
 
kigogo ni nan? ukienda BOT ukiangalia majina unaweza ukadhani hakuna watoto wa vigogo, lakini wapo kibaooo watu wanacheza na majina tu
 
kama ni hivyo basi itakuwa ni mwendelezo wa Ufisadi-kuwafukuza watato wa masikini waajiriwe wa vigogo na hapo hapo jamaa anapata ujiko kwa kutangaza kufukuza watoto wa vigogo Ningeshangaa magufuli amepata wapi uwezo wa kufukuza watoto Wa vigogo wenzake!

Kaka usiwe mgeni wa Tanzania hii, hao wametolewa kafara tu, mnyonge siku zote hana haki, watoto wa vigogo ndo kwanza wanatumbua bata TANROADS ile kauli ya Magofuli ni daganya toto tu, da! inauma sana, lini Yesu atarudi? angalau wanyonge tutambuliwe.
 
kama ni hivyo basi itakuwa ni mwendelezo wa Ufisadi-kuwafukuza watato wa masikini waajiriwe wa vigogo na hapo hapo jamaa anapata ujiko kwa kutangaza kufukuza watoto wa vigogo Ningeshangaa magufuli amepata wapi uwezo wa kufukuza watoto Wa vigogo wenzake!

Kaka hao wametolewa kafara tu, watoto wa vigogo ndo kwanza wanakula bata TANROADS.
 
una ubongo finyu sana ndio maana huelewi IMPLIED CONDITIONS TO ONE NAME MTU KIGOGO.

Yawezekana upo njee ya Tanzania kwa muda mrefu ila kama upo bongo basi wewe ni sub-stratum yaan ungesoma shule zetu za kata hata kwa miaka 20 usingeweza kuikwepa div zero

Kaka Jamaa kauliza swali, we Mjibu kulingana na swali lake na sio kutumia lugha mbaya huo sio uungwana.Asante kwakuelewa.
 
Sasa Mods mmeihamisha hii thread kwenda jukwaa la nafasi za kazi kivipi wakuu? kwa mtazamo wangu hili si suala la nafasi za kazi bali kauli ya mwanasiasa nguli juu ya kuwashughulikia watoto wa vigogo, nilidhani ni muhimu ikabaki jukwaa la siasa.
 
Back
Top Bottom