Kwa mambo haya acha vijana wa sasa wadharau Mila za Wazazi na Wazee wao

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,892
KWA MAMBO HAYA ACHA VIJANA WA SASA WADHARAU MILA ZA WAZAZI NA WAZEE WAO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Vijana wa sasa wanaonekana kama hawana maadili lakini ukilinganisha na wazazi au Mababu zao utakuja kugundua vijana wa sasa wana maadili kuliko wazazi na wazee wao.

Taikon katika chunguzi zangu na kukusanya hesabu ya mambo nimebaini kuwa wazazi na wazee wetu ndio walikuwa na tatizo kubwa na ambalo waliling'ang'ania wakidhani ndio heshima na maadili wakati ikichunguza vizuri kwa kiasi kikubwa ulikuwa ni upumbavu.

Mila na matendo ambayo wazazi na wazee wetu walikuwa nayo na wengine mpaka sasa wanaamini katika mila hizo ambazo vinafanya vijana wa sasa wawadharau wazazi na wazee wao;

1. Ndoa za Mitala.
Kuoa wake wengi ni sifa ya Watu wabinafsi, wasio na upendo, wanaojijali nafsi zao wenyewé.
Ukiona mtu yeyote kwa nafasi yoyote na cheo chochote iwe ni Nabii, mtume, mfalme, Rais, kiongozi yeyote au mwanaume yeyote ameoa mke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Elewa mtu huyo anajieleza kama mtu Katili, mbinafsi, asiye na upendo, asiyejali nafsi za Watu wengine.

Ukitaka ujue mila hiyo niya kudharaulika na inafanywa na Watu wakatili basi namna bora ni kuipima katika mizania ya Haki na upendo. Swali ni je, Mwanaume aliyeoa Wake wengi atakubali mkewe naye amletee Mwanaume mwingine? Jibu litakalotoka hapo ndilo litaamua kuwa huyo mwanaume ni mkatili, mbinafsi na asiye na upendo na hiyo itamaanisha akili zake hazifanyi kazi vizuri.

2. Mtazamo kuwa Mzazi Hakosei.
Kitendo cha kuwa na fikra kuwa mzazi au wazee hawakosei pekeeke ni fikra ya ubinafsi, ukatili na kuzuia mawazo mapya, ubunifu.
Jamii yenye mtazamo kuwa mzazi Hakosei ikichunguza kwa umakini haiwezi kupiga hatua yoyote ya kimaendeleo.
Mtazamo wa mzazi Hakosei unamilikiwa na Madikteta wenye upeo mdogo wa kufikiri.
Mtazamo huo pia unazalisha kiburi cha wazazi na viongozi au watawala. Hiyo inafanya jamii kuwa ya kinafiki nafiki.

Mtazamo huo umesababisha dhana nyingine ya mzazi kutokuomba msamaha. Kwa sababu ataombaje msamaha ikiwa Hakosei. Kiburi cha hali ya juu Kabisa. Jamii yenye kiburi na yenye tabia za kishetani.

3. Kutoa Mahari.
Mahari ni moja ya mila za ajabu na hovyo kabisa zilizowahi kutokea katika dunia hii.
Hakuna mantiki yoyote ya maana katika utoaji wa mahari. Ubinafsina na udhalilishaji ndio maana halisi ya kumnunua Mwanamke kwa jina la Mahari.
Kwamba ili upewe hati na uhalali wa kumiliki Mwanamke unayempenda basi itakupasa utoe pesa(umnunue). Ni mfumo dume mbaya sana wenye lengo la kumdhalilisha na kumkalia kooni Mwanamke.

Watibeli hiyo kitu haitafanyika. Binti zangu kamwe msije kuchukuliwa mahari iwe nipo au nisiwepo. Vijana wangu, kamwe msijekutoa Mahari, niwepo au nisiwepo.

3. Mtoto kutengwa au kubaguliwa akiwa na kasoro kulingana na imani na mila potofu.
Picha linaanza mtoto akizaliwa wakike ati hawafurahi ingawaje watazuga na kufurahi kwa nje.
Nyakati nakua nilishawahi kuona mwanaume anaamua kumuacha mkewe kisa kamzalia watoto wakike watupu. Fikiria huo ni upuuzi wa kiwango gani. Fikiria wewe ndio huyo mtoto wa kike umezaliwa alafu baba yako ati alitaka uwe wakiume. Yaani kuna majitu yanamitazamo na kasumba za hovyo sana.

Fikiria ati mtoto akizaliwa na ulemavu kama wa ngozi kwa zamani angeuawa. Fikiria mapacha waliozaliwa wangeuawa. Embu fikiria hayo mambo. Kwa nini vijana wa sasa wasiwadharau wazazi na wazee wao kwa mila za kijinga kama hizo.

Watoto na vijana wangu, tumieni akili zenu vizuri, pimeni mambo katika upendo na Haki na ukweli. Hata kama mimi Baba yenu nimesema jambo lolote lipimeni kwanza. Msiwe wajinga.

4. Dhana potofu ya Mfalme au utawala wowote ni Mamlaka ya mungu.
Jamii yetu imerithi mila ya hovyo katika siasa. Kwamba ati kiongozi au mtawala yeyote amepewa nguvu ya kiungu. Na anatakiwa kuheshimiwa.
Hakuna kiongozi yeyote anayepewa mamlaka ya kiungu isipokuwa anayetenda Haki na mwenye Upendo.
Taikon nimeshaelezea hilo kila wakati. Nimesema hata baba yako au mama yako utamheshimu kwa habari za haki na upendo na sio zaidi ya hapo.

Mtawala sijui mfalme, sijui Rais, sijui Mkurugenzi na majina yoyote yale yanayorejelea mwenye mamlaka. Mheshimu kwa matendo yake ya kutenda Haki na sio kwa cheo chake.

Watibeli hatuheshimu Watu kwa vyeo, umri au nafasi walizonazo au utajiri walionao. Tunaheshimu na kudharau Watu kwa matendo yao.
Yaani hata ungekuwa nani kama matendo yako ni yakimavimavi na yananuka sisi hatuangalii cheo, umri, nafasi yako tutakudharau tuu.

Watu wengi wanajiuliza mbona zamani Ukiwa mwalimu au daktari au Mbunge au Waziri au Rais ulikuwa unaheshimika lakini siku hizi vijana hawaheshimu. Jibu nimeshawapa hapo ni kuwa vijana wa siku hizi hawawezi kukuheshimu kwa jina lako, umri wako, elimu yako, cheo chako kama unafanya matendo ya kipuuzi.

Nature ilivyo na mwanadamu yoyote ameumbwa kuheshimu Wema na uzuri. Ukiwa mwema utaheshimika pasipo unafiki. Utaheshimika kwa Wema na Waovu.

5. Kasumba mbaya zilizopo kwenye Ndoa.
Ndoa nyingi za sasa zinayumba Kutokana na mila na desturi za hovyo zilizorithiwa kutoka kwa wazee wetu. Sasa vijana wa sasa wanashindwa kuamua waishi katika nuru na ukweli au waishi kizamani kwenye giza katika ulimwengu wa sasa.

Mfumo wa zamani ulikuwa ni kandamizi, katili na wenye ubinafsi uliomuumiza Mwanamke na mwanaume kwa pamoja.
Mwanamke aliteswa kihisia na kifikra na muda huohuo mwanaume aliteswa kimwili.
Ukiambiwa ndoa ndoano walimaanisha hayo mateso.
Lakini Mwanamke aliteswa zaidi kwa sababu kuteswa kihisia kunauma zaidi ya kuteswa Kimwili.

Mwanaume ni kichwa cha familia lakini lazima ashirikiane na kiwiliwili ili mambo ya familia yafanyike kwa usahihi.

Kutumia mabavu kuliko akili ni moja ya mambo ambayo yamerithishwa. Kuongoza familia haihitaji kutumia mabavu ikiwa kweli mnaishi kama mume na mke.
Mapenzi na upendo ndio yanayoongoza familia, kisha Akili ndio itayalinda mapenzi na familia yenu.

Kutumia mabavu na kulazimisha mambo kumezifanya ndoa na familia nyingi kuanguka kwa sababu mabavu mengi hayahusishi Akili, upendo na Haki.

Mwanamke anataka kuhudumiwa tuu. Hii sio sahihi.
Mwanamke sio mtoto mdogo. Binti nyote ni Watu wazima, fanyeni kazi pamoja kwa upendo, jengeni familia yenu. Yale yote unayotaka kufanyiwa mfanyie mwenza wako.

Kama unataka kuhudumiwa, mhudumie mumeo/mkeo.
Kama unataka kupendwa basi fanya hivyo kwa mwenza wako.
Kama unataka kuheshimiwa fanya hivyo kwa mwenzako.

Ikiwa itatokea mnatofautiana katika mawazo katika jambo fulani basi hapo angalieni wazo la nani linatekelezeka kirahisi na kwa gharama nafuu na litawezekana kwa muda mfupi bila kuathiri mipango yenu ya baadaye mliojiwekea.

Msiwe na kiburi kama wazazi na wazee wenu. Kila mmoja kutaka kujiona bora kuliko mwenzake ni dalili ya Watu wenye upeo mdogo.
Mwanaume kujiona wewe ndiye bora na unayepaswa kusikilizwa katika nyumba pasipo kusikiliza mkeo na watoto ni dalili kubwa hutoshi kuwa Baba au mume wa hiyo nyumba.
Mwanamke kujiona wewe ndiye bora na malkia mwema unayetakiwa kujaliwa na kusikilizwa kuliko wengine ndani ya familia ni dalili kuwa huna sifa ya kuwa mke au mama wa hiyo familia.
Kila mmoja amtangulize mwenzake. Huo ndio Utibeli.

Taikon Master sijaandika kuwananga na kuwalaani wazee wetu isipokuwa nimeandika kuwaonya na kuwatahadharisha vijana na kizazi cha sasa kujiepusha na makosa ya wazazi na wazee wao.

Mimi sina la ziada. Acha nipumzike sasa.

Nawatakia Sabato njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Sijasoma yote ila namba Moja na namba mbili umeandika UPUMBAVU.
Kuna mambo huyajui asili na msingi wake na wewe ulitakiwa kukaa kimya kuliko kutangaza upumbavu uliopo kichwani mwako.
Nikishasoma yote nitacomment tena ila nilivyosoma namba 1 sikuimaliza nikaangalia namba 2 kidogo Kisha namba tatu nikaona kuwa mleta mada ni mmoja wa wendawazimu wa Karne ya 21.
 
Ukirudi uje na hoja zinaelezea vizur madhaifu ya hoja za mtoa mada, usipofanya hivyo mkuu mojakwamoja Ili jiwe litakuwa limekupapasa kikamilifu
 
Upo sahihi Sana
Lazima mtu apewe heshima kutokana na Matendo yake wema sio PESA Wala Mali Mimi naona watibeli wapo sahihi kwa hilo .
 
Mimi ninacho jua zama hupita na nyakati hubadillika.Washaanza kupinga tena bila ya maelezo ya kueleweka na wataapinga ila huo ndo ukweli.Kunabaadhi ya mambo huwahayaeleweki kabisa na yata achwa tu.

Kwanza Sasa hivi wakubwa/wazee wengi wao hawaitunzi heshima yao (Tabia/mambo yao ya hovyo yanaonekana hadharani) na ndo maana heshima inapungua.

Yani mtu unajiuliza hivi kumbe nao Huwa wanafanya hivi kumbe nilivyokuwa na wachukulia ilikuwa ndivyo sivyo
 
Sijasoma yote ila namba Moja na namba mbili umeandika UPUMBAVU.
Kuna mambo huyajui asili na msingi wake na wewe ulitakiwa kukaa kimya kuliko kutangaza upumbavu uliopo kichwani mwako.
Nikishasoma yote nitacomment tena ila nilivyosoma namba 1 sikuimaliza nikaangalia namba 2 kidogo Kisha namba tatu nikaona kuwa mleta mada ni mmoja wa wendawazimu wa Karne ya 21.

Ukishakuwa Mpumbavu huwezi elewa vitu vya namna hii
 
Mimi ninacho jua zama hupita na nyakati hubadillika.Washaanza kupinga tena bila ya maelezo ya kueleweka na wataapinga ila huo ndo ukweli.Kunabaadhi ya mambo huwahayaeleweki kabisa na yata achwa tu.

Kwanza Sasa hivi wakubwa/wazee wengi wao hawaitunzi heshima yao (Tabia/mambo yao ya hovyo yanaonekana hadharani) na ndo maana heshima inapungua.

Yani mtu unajiuliza hivi kumbe nao Huwa wanafanya hivi kumbe nilivyokuwa na wachukulia ilikuwa ndivyo sivyo

Na ipo hivyo.
Ukweli haupitwi na wakati
Haki haipitwi na wakati.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom