Regia alikuwa anaendeshaje gari? Wakati mguu wake wa kulia ndio wenye ulemavu?

gari hii hapa

attachment.php

Hilo sio gari, bali ni Picha.
R.I.P member mwenzangu wa JF
 
Kama hamna majibu ya swali ni bora kukaa kimya. Japo wote tuna machungu lakini hamuoni kuwa ni muhimu pia kujua chanzo cha ajali?
 
mkuu, swali la huyu bwana ni la kijinga na la maudhi at this perticular time. Anisamehe kama nimemkwaza, kwa bahati mbaya wengine wetu kifo chake kimetugusa kiasi ambacho discusion ya namna hii inaweza ikapelekea kichapo kama angekuwa karibu.
Hasira hasara. Watu wengi tumeguswa na kifo cha Komando wetu. Busara ni kumjibu tu kama unajibu
 
Swali lake lina logic. Tatizo waafrika hampendi kujiuliza au kutafiti vitu.
Je ni yeye kweli alikuwa anaendesha?
Tungejiuliza na kupeleleza ikiwa hata Chacha Wangwe pia alikuwa peke yake pengine tungezuia matukio mengine mengi bizarre. Tuache kuabudu vifo kiasi cha kugwaya hata ku question mazingira yake
 
Jamani we, search Mtu anaitwa Lena Maria, ( sorry about the spelling).Anaelezea kuhusu watu ambao wako physically handicapped lakini wanafanya vitu vingi sana kuliko watu wengi ambao ni physically able.

Someni Lena Maria Klingvall. Na Yule mwanariadha wa south Africa ambaye ni mwenye matatizo ya miguu na anataka kushiriki michezo na watu ambao wana miguu.

Thread hii inakera sana ili inabidi tujifunze kuwa watu handicapped wana uwezo wa kufanya vitu vingi sana kuliko hata watu wa kawaida.

Tuamke!!!!!!!!
 
Tukijua tutafanya nini?
Ni ajali and can befall anyone. Hata pro drivers wanapata ajali.

Kwa sasa lets mourn our sister!
 
Nimesikitishwa na taarifa za msiba wa muheshimiwa Regia Mtema, inasemekana alikuwa anaendesha gari yeye mwenyewe sasa mimi najiuliza hivi gari hiyo ilikuwa ni ya buttons za kubonyeza kwa mkono maana mguu wake wa kulia ndio wenye ulemavu sasa brake accelerator angewezaje kuzikanyaga au ilikuwa LHD? ni risk sana kuendesha gari kwa mtu ambaye ni physically challenged in udadisi tu

Mkuu pitia hiyo link inaweza kukupa majibu ya swali lako.

HabariLeo | Mbunge Chadema afa ajalini Ruvu
 
Nimesikitishwa na taarifa za msiba wa muheshimiwa Regia Mtema, inasemekana alikuwa anaendesha gari yeye mwenyewe sasa mimi najiuliza hivi gari hiyo ilikuwa ni ya buttons za kubonyeza kwa mkono maana mguu wake wa kulia ndio wenye ulemavu sasa brake accelerator angewezaje kuzikanyaga au ilikuwa LHD? ni risk sana kuendesha gari kwa mtu ambaye ni physically challenged in udadisi tu

Mkuu ni mazoea tu. Sidhani kama ni mara yake ya kwanza kuendesha mwenyewe.

Kwani ajali zote zinazotokea madereva wake walemavu? Tuchukulie kama ajali nyingine na tumuombee apumzike salama.
 
Alikua haendeshi bali alikua anaendeshwa na dereva wake...........haya acheni kubishana sana.Dereva wake na ndugu wengine waliokuwemo wamepona.
 
Haya maelezo lingejibiwa swal la msingi,lkn 2shakuwa na majibu cha msingi wa2 kujifunza kutokana na makosa,haiwezekan una presha alafu ufanye kaz kiwanda cha nondo
 
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Saleh Mbaga alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ilitokana na hatua ya Mbunge huyo kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla likatokea roli la mafuta na
alipotaka kurejea upande wake gari hilo lilimshinda na kubiringita mara saba.

Alisema hata hivyo ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya Mbunge huyo kuwa na ulemavu wa mguu na hivyo kuwa na mguu mmoja tu wa kushoto ambao alisema inadhaniwa ulimpa tabu katika kufanya uamuzi baada ya kutokea kwa lori hilo la mafuta mbele
yake.

"Kama mnavyojua pedeli za gari zipo upande wa kulia lakini yeye alikuwa anatumia mguu wa kushoto kwa hiyo inawezekana kutokana na mshituko wa kutokea gari mbele, alibabaika katika kuutumia mguu huo wa kushoto kufanya uamuzi na hivyo kusababisha gari kumshinda na kupinduka," alisema Mbaga.

Chanzo HabariLeo | Mbunge Chadema afa ajalini Ruvu

Nadhani sasa kuna haja ya mamlaka husika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanaendesha magari sahihi kwa hali zao
 
jaribu kutumia lugha nzuri, unapotumia neno "ki"lema au "vi"lema au mdhalilisha mtu. "Ki" inatumika kwa vitu. Mfano kisu,kijiko,kikombe nk. Hali kadhalika visu,vijiko,viti nk, tumia neno mlemavu. Asiyesikia(kiziwi) asiyeona(kipofu) nk. Acha kufananisha watu na vitu. Huko ni kudhalilisha.

mbona kiziwi nayo inaanza na ki?
 
nilijiuliza hilo tangu jana tatizo kuna watu wanajifanya wana uchungu kutupita wote,.mtaani unaweza kuwaita wachawi,kama kosa lilikuwa la marehemu tujue,r.i.p regia
 
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Saleh Mbaga alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ilitokana na hatua ya Mbunge huyo kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla likatokea roli la mafuta na
alipotaka kurejea upande wake gari hilo lilimshinda na kubiringita mara saba.

Alisema hata hivyo ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya Mbunge huyo kuwa na ulemavu wa mguu na hivyo kuwa na mguu mmoja tu wa kushoto ambao alisema inadhaniwa ulimpa tabu katika kufanya uamuzi baada ya kutokea kwa lori hilo la mafuta mbele
yake.

“Kama mnavyojua pedeli za gari zipo upande wa kulia lakini yeye alikuwa anatumia mguu wa kushoto kwa hiyo inawezekana kutokana na mshituko wa kutokea gari mbele, alibabaika katika kuutumia mguu huo wa kushoto kufanya uamuzi na hivyo kusababisha gari kumshinda na kupinduka,” alisema Mbaga.

Chanzo HabariLeo | Mbunge Chadema afa ajalini Ruvu

Nadhani sasa kuna haja ya mamlaka husika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanaendesha magari sahihi kwa hali zao

huyu polisi kichwa maji kabisa, amejuaje kwamba mguu ndii uliochangia? Amefanya any simmulations na kuona kuna possibility ya 'kuchangia'? Hizi statement za kitaalamu zinazotolewa kama story za kijiweni ni hatari sana.

Kama angekuwa na miguu yote na ajali ikatokea ingekuwa imechagiwa na nini?

Je, huyu polisi anajua capability na sensitivity ya mguu wa kushoto wa marehemu Regia? Anajua mguu wake ulikuwa na uwezo gani?

This is ridiculous!!!
 
Kazi ipo!
 
nilijiuliza hilo tangu jana tatizo kuna watu wanajifanya wana uchungu kutupita wote,.mtaani unaweza kuwaita wachawi,kama kosa lilikuwa la marehemu tujue,r.i.p regia
Wote tuna uchungu,inashangaza watu wanatukana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom