Regia alikuwa anaendeshaje gari? Wakati mguu wake wa kulia ndio wenye ulemavu?

Kwa status yake ya ubunge hakustaili kuendesha gari tena kwenye safari ndefu. Alishindwaje kutoa ajira kwa dereva?
 
Ajali nyingi za barabarani zinasababishwa na uzembe wa madereva. Ajali inapotokea kama kulikuwa na mazingira ya uzembe, hata kama kuna vifo vimetokea suala la mjadala halina kizuizi. Nakumbuka tulijadili sana ilipotokea ajali ilyochukua maisha ya hayati Sokoine kabla hata hajazikwa. Kwa mazingira ya ajali hii, yeyote anayesema kuna mkono wa mtu au serikali ni punguani wa akili. Nasikitika sana sijui ni kipi kilichompa msukumo marehemu aendeshe mwenyewe gari hilo. Hata kama lilikuwa katika mfumo wa Auto, aina hii ya magari mguu wa kulia ndiyo hutumika, mfumo huu dereva anashauriwa kutumia mguu moja wa kulia tu. Huu ni mguu ambao ndiyo uliokuwa na ulemavu kwa mheshimiwa Regia. Kitu ambacho kisinge wezekana. Vinginevyo walionusurika katika ajali hiyo watuambie kuwa marehemu alikuwa akitumia mguu wa kushoto. Hiyo inawezekana kwa dereva mwenye uzoefu. Jambo lingine, eneo la ajali kwa jinsi ninavyolifahamu ni hatari kuovateki kama unatumia gari dogo kutokana na barabara kuwa imebonyea sehemu ya kukanyaga matairi, kwa maana hiyo ukienda kulia. Halafu ghafla ukatakiwa kurudi kushoto, ni lazima upambane na ngema ya kati kati ya barabara. Ngema ambayo husababisha gari kuyumba. Kwa upande mwingine dereva wa mheshimiwa naye anapaswa kupokea lawama japo kiduchu. Yeye alikuwa na uhakika gani na uwezo wa bosi wake katika fani ya udereva? Ama kama alisha shuhudia bosi wake akiendesha kwa safari ndefu, atuambie. Yote kwa yote, ajali imesha tokea. Hakuna wa kumshika shati kwa sasa. Tumuombee marehemu tu, apumzike kwa amani.
 
Hivi kuna mwenye picha ya Marehemu Regia atuwekee kuna wengine kusema kweli tulikuwa hatumjui. Please serious.
 
Kwa sababu sasa tupo katika kipindi kigumu watu wote ,maswali mengine inabidi yaulizwe baadae hata marehemu hatujamzika tushaanza kuhoji
 
we ****** unauliza swali gani filauni mkubwa wewe,ajari inamtokea yoyote yule hata wewe inaweza kukutokea hata kesho,acha upuuzi kabisa watu tupo kwenye maombolezi wewe unaleta ujinga!

ningekuwa na uwezo ningemwomba mungu amrudishe regina akuchukue wwewe
 
Kayagila,nimeona na kin Pasco na wengine waliokusapoti juu ya kuuliza swali,lakini najua mnachikitafuta,ila jaribuni kuwa binadamu,na kama jambo halikukugusa nadhani busara ya kuwaacha wale liliowagusa wakaomboleza bila bughudha au bila kuongezewa uchungu ingrlifaa sana,maana huko ni kuchokonoa ili ujue,nadhani muda huu ni watu kupeana maneno ya kufarijiana,maneno ya upendo,sehemu pekee ambako matendo kama yako yanafanyika kipindi hiki cha majonzi ni kule hospitali kama watakuwa wanauchunguza mwili wake au polisi kama watakuwa wanachunguza chanzo cha ajali.
Hapa tupe muda wa kuomboleza na kufarijiana kwanza kama ilivyo kawaida ya watanzania,kama mila na desturi zetu zilivyo.
Haiingii akili leo unaanza kuuliza maswali hayo,nilidhani kwa busara za kawaida tu na kwa mtu mwenye ubinadamu ungelikuja na hoja ya kutaka mazishi lini,wapi,je kama ni mbali kuna usafiri kwa jamaa na marafiki?je kama member wa JF rambirambi itakuwaje?au je nitafikaje nyumbani kwenye msiba?lakini cha ajabu wewe na wenzio wachache tunaowajua upande wenu mnaanza kuchokonoa vijimambo hata dada yetu hatujamzika,kwngu mimi hii ni mbaya sana,sipendi !
 
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Saleh Mbaga alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ilitokana na hatua ya Mbunge huyo kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla likatokea roli la mafuta na
alipotaka kurejea upande wake gari hilo lilimshinda na kubiringita mara saba.

Alisema hata hivyo ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya Mbunge huyo kuwa na ulemavu wa mguu na hivyo kuwa na mguu mmoja tu wa kushoto ambao alisema inadhaniwa ulimpa tabu katika kufanya uamuzi baada ya kutokea kwa lori hilo la mafuta mbele
yake.

“Kama mnavyojua pedeli za gari zipo upande wa kulia lakini yeye alikuwa anatumia mguu wa kushoto kwa hiyo inawezekana kutokana na mshituko wa kutokea gari mbele, alibabaika katika kuutumia mguu huo wa kushoto kufanya uamuzi na hivyo kusababisha gari kumshinda na kupinduka,” alisema Mbaga.

Chanzo HabariLeo | Mbunge Chadema afa ajalini Ruvu

Nadhani sasa kuna haja ya mamlaka husika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanaendesha magari sahihi kwa hali zao

hapo mwisho si hoja sana. Watu wasio na ulemavu wanapata ajali kila siku
 
Yapo magari ambayo yametengenezwa maalum kwa ajili ya watu ambao wana ulemavu. dada Regia kama mlivyotujuza alikuwa na ulemavu wa mguu mmoja wa kulia. Kwa ulemavu huoo anaweza asihitaji gari maalumu maana kila kitu ni mafunzo na mazoea. wapo watu ambao hawana miguu yote na wanaendesha magari maalumu kwa ajili yao. Mengine yana vitufe vya kubofya na linamfanya dereva alimiliki kwa mikono yake. Kwa hio swali la msingi Je gari alilokuwa akiliendesha lilikuwa maalumu kwa ajili ya ulemavu wake?
Wahusika wa usalama barabarani wanahitaji kutuelekeza namna ya kuwafanya walema mbalimbali wenye uwezo au wanaotaka kuendesha magari , magari yao yawe na viwango/options zipi. Hii pia ni mahsusi kwa leseni zao.
Teknolojia imesonga mbele kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kwani hata wasio na uwezo wa kumudu miguu na mikono yao wanatumia tu macho yao kuelekeza computer kufanya wanayotaka!!!!
Dada Regia Ulale pema peponi. Kazi uliyotumwana na Muumba wako umeikamilisha. Tuliyobaki tuendeleze ndoto zako njema.

nadhani lingekuwa gari maalumu kwa walemavu asingelihitajh dereva mwingine. Kumbuka alikuwa na dereva wake. Ila jana alikuwa akiendesha yeye mwenyewe.
 
Wabongo bwana COMPLICATIONS kibaooo,sawali la kawaida hata mi najiuliza sasa cha ajabu nn?kwani kuna siri kama muheshimiwa Regia alikuwa mlemavu?kwani kuna tatizo gani kuuliza sasa huvi mbona misibani watu wanauliza marehemu kafaje?acheni kuleta siasa kila sehemu...wote mliokwazika ni CRAAP !wewe Brigita na wenzio!aliyeuliza thumbs Up!
 
mkuu, swali la huyu bwana ni la kijinga na la maudhi at this perticular time. Anisamehe kama nimemkwaza, kwa bahati mbaya wengine wetu kifo chake kimetugusa kiasi ambacho discusion ya namna hii inaweza ikapelekea kichapo kama angekuwa karibu.
Nimeuliza swali la msingi sasa natukanwa mimi ni mjinga haya....nabaki na ujinga wangu lakini I promise....road accidents will continue to take its deadly toll if the authorities continue with business as usual
 
Nimeuliza swali la msingi sasa natukanwa mimi ni mjinga haya....nabaki na ujinga wangu lakini I promise....road accidents will continue to take its deadly toll if the authorities continue with business as usual

Anayekuona mjinga, mjinga ni yeye. Usihangaike naye. Binadamu tumeumbwa tofauti. Kuna wengine mataahira, hata akiambiwa kitu cha maana anapinga.
 
Mimi nashauri sekali iwaajiri madereva wa wabunge ili mishahara yao ilipwe moja kwa moja kwani wabunge wengine wengine wanabana fedha hizo na kujilazimisha kuendesha wenyewe pengine bila uzoefu wa kutosha au hali zao kimaumbile kuwa na mapungufu yanayohitajika kuweza kendesha gari.
 
hiyo sio justification nzuri,kuna watu kibao hawajui hata kuendesha magari na wana leseni wamekata kabisa ili wakija kununua magari wasihangaike!!!hii ndio tz labda kama we mwenzetu uliondoka siku nyingi sana tz.Sema tu timing ya kuhoji inaweza kuwa haikua nzuri sana lakini swali la jamaa linahitaji majibu yanayojitosheleza zaidi kutoka kwa great thinkers kuliko hilo lako,may be limetokana na jazba ya kufiwa.Tusameheane sote wakati tulio nao unaeleweka.

Mnaniita mjinga sishirikishi ubongo kufikiri ..nabaki na ujinga wangu mtatanabahi ajali za kizembe zitakapozidi kuwatafuna
 
Mkuu

marehemu mh wangwe alikuwa anaendesha yeye ??
Yule mbunge aliesonga mbele na mkewwe wa cuf nao umeambiwa waliendesha wao ??umejiuliza kwa ni ni na pamoja walikuwa na miguu yote ok
namaanisha mungu akikupenda aijalishi uko wapi unaendesha wewe dereva...tuache tuhuzunike then uje ijumaa tafadhali tukusaidie jibu lako
 

Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom