Poleni wote kwa msiba. Unajua nimejiuliza swali kama hili mimi binafsi na sikupata jibu. Watanzania tuna unafiki mwingi sana na double standards. Tukifika msibani wataulizana swali hili watu na minong'ono kibao, kafaje, aliendeshaje nk nk kibao.
Alipokufa kaka yangu Mr Ebbo maneno yalisemwa sana, mara ngoma mara nini. Hapa tunajua kafa kwa ajali lakini ndiyo watu wanauliza amekufa kwa ajali kivipi? Watu wana haki ya kujua. Nchi zilizoendelea swali kama hili si siri. Tena kama amekosea inasemwa kabisa na mamlaka kwamba alikosea.
Swali lijibiwe tu msikasirike. Wote tuna majonzi. Tusiitane mbwa wala paka. Hata kama litajibiwa mwezi ujao lijibiwe tu.
Poleni wote kwa msiba mzito wa dada Regia!