Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu!

Status
Not open for further replies.
Na ile barua ya kwenda kwa Lowasa ya kushauri kuwa hoja za Dr Slaa zisijadiliwe bungeni ni nani alipitisha?

Wewe mdada huyu jamaa ana mamlaka gani ya kuzuia barua kama hizo ndani ya bunge?. RO siyo spika wa bunge na wala hana mamlaka kama hayo ndani ya bunge.

Ni spika ndiye mwenye mamlaka kama hayo.
 
CCM wanafukuana wenyewe na sisi popcorn zetu tayari kabisa for the second movie..... skandali za mswahili aka chinga aka mtalii aka ... ndio mwanzo zimeanza kuanikwa!

Yeye ajiandae tu ila majina hayatatajwa kama kawaida ya JF!

Anafanya mambo ya nje ndilo swali langu?
 
Wewe mdada huyu jamaa ana mamlaka gani ya kuzuia barua kama hizo ndani ya bunge?. RO siyo spika wa bunge na wala hana mamlaka kama hayo ndani ya bunge.

Ni spika ndiye mwenye mamlaka kama hayo.

Umeelewa swali? Kuna barua ya usalama wa taifa ilitumwa kwa Lowasa kumuagiza azuie hoja ya Dr Slaa bungeni. Nani aliiandika (just in case you know)?
 
Mkuu Kulikoni/Tafiti(SY),

Heshima mbele kaka, nimekusoma vizuri sana, na kama kawaida yako kuna wanokushangilia nimewaona, nitakurudia karibuni mkuu, ila karibu tena bro!
 
Mkuu vipi tena? naona unakuwa kama ndugu zetu wa St Peters pale...Speaking of St Peters kuna mtu anakumbuka incident yao moja waliyoenda kituo cha polisi kijitonyama na kuwatoa wenzao uku wakipiga mkwara wa nguvu...hizo nguvu wanazitoa wapi?

Bado nasubiria (ma)jibu, kazi za hawa agents wa TISS kwenye balozi zetu, mashirika ya umma na taasisi nyingine za serikali ni zipi?

Icadon, kwa kuangalia sheria ya TISS sidhani kama wanastahili hata kuwepo huko Ubalozini... hofu yangu kutokana na mjadala huu tuna parallel National Security Agency ambayo haiko chini ya TISS
 
Umeelewa swali? Kuna barua ya usalama wa taifa ilitumwa kwa Lowasa kumuagiza azuie hoja ya Dr Slaa bungeni. Nani aliiandika (just in case you know)?

Nimelielewa swali vizuri kabisa na bila shaka nimekujibu. Watu wa usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kuzuia mijadala katika bunge. Hiyo barua unaweza kuimwaga hapa JF ili tuone ukweli huo?.
 
Sidhani kama kuna ubaya kama mtu akija gundua kuwa aliyekuwa akimfahamu ni mchapakazi anayekubalika............na kwamba sasa ameonyesha udhaifu katika uchapaji kazi wake na hivyo mtu kutoa maoni yake.........kuna ubaya gani..........life is never static wazee.......

......mfano mi binafsi ninavyomfahamu Magufuli na kukubali uchapaji kazi wake..........haimaanishi kuwa eti akivurunda siku moja.........nitaacha kusema ukweli na kumtaka awajibike..........ukweli utabaki pale pale kuwa amevurunda (waswahili siku hizi wanasema amelikoroga)

Hivyo basi sioni hoja ya kumshupalia ES eti kwakuwa alisema "RO anakubalika" au whatever he may say.........it does not make any sense

Tunachotakiwa kuangalia hapa sio mtu bali ni kuwa........does it make sense kusema RO ajiuzulu?........is anybody making a sound argument?

sababu zetu zoote zitakuwa na maana sana kama tutajua hawa watu wanafanyaje kazi zao na mipaka yao iko wapi.............Je wale walioshauri RICHMOND isipewe mradi walijiuzuru?........je Mwakyembe na timu yake tukiangalia ushauri wao walioutoa usipotimizwa na huyo Pinda sijui nao tuwaambie watoke CCM!!.................haya ndio mambo tunatakiwa TUJADILI kwani bado yanajadilika

Nimeshatofautiana sana na washikaji zangu hapa JF wengi tu.....lakini haina maana kuwa huko nyuma hatukuwa pamoja.

Kazi za RO ni siri.......hata ushauri wake ni siri......hata kama JK alikataa ushauri wake haina maana basi RO ajiuzulu.......kwani ushauri wake unaweza kukubalika au kukataliwa......na RO anaelewa hilo..............kinachogomba hapa ni kuwa mbinu ya kutimiza wajibu wa TISS haishii kwenye ushauri pekee.......na ndipo hapo Mzee Mwanakijiji na FMES wanapoingia na kusema RO alikuwa wapi kuzuia haya yote yasitokee?? au alizidiwa kete (which is normal)............pamoja na maswali hayo ya msingi......sijui kama majibu yake yatapatikana
 
Re.Kishoka,

Nimesema hivyo baada ya kuisoma vizuri sheria ya Usalama wa Taifa. Ninachoweza kusema ni kuwa, kuna watu wana chuki na Othman au hawajui vizuri majukumu ya Usalama wa Taifa, na wamekuwa WAVIVU kuisoma au wamesisoma lakini HAWAJAIELEWA.

Hivyo unasema tunaodai RO ajiuzulu tuna chuki naye? Mimi RO simfahamu, ndio kwanza nimemsikia hapa JF mwaka jana. Lakini nikifanya upembuzi wa utendaji kazi wake na majukumu makubwa aliyopewa, ninaona udhaifu mkubwa wa kiutendaji na kiongozi kutoka kwake na TISS kwa ujumla.

Hata kama utasema kuwa sheria ya kuundwa TISS haikubaini masuala ya Uhujumu wa Uchumi, je ikiwa Uhujumu huu ungefanywa na wageni pekee bila kuhusisha mtanzania hata mmoja, ungedai bado si jukumu la TISS kulinda maslahi na usalama wa Taifa?

Je alipokula kiapo kwa kutumia katiba na kutamka kuwa ataitumikia Serikali na kuitii na kuilinda Katiba ya Jamhuri, je kile Kipengele cha 27 kina maana gani basi?

Tunaelewa sana Sheria ya kuundwa TISS zote za 1970 na hata marekebisho ya 1996.

Kinachoelekea unakifanya sawa na wale waliomtetea Lowassa, Karamagi na Msabaha ni kutumia mianya inayotokana na kuonekana kana kwamba kuna utata wa Sheria.

Kama hilo ndivyo kuwa kuna mapungufu katika Sheria na Katiba, basi jiunge nasi tunapodai kuundwa Katiba mpya kuishinikiza Serikali na CCM wakubali maana wao wanadai kuwa Katiba na Sheira kadhaa zinakidhi mahitaji na hakuna sababu ya kufutwa.
 
Nimesoma posting nyingi hapa lakini naona bado haieleweki hii taasisi ya usalama Tanzania inafanzaje kazi zake.

Napenda kuuliza kama kuna anaefahamu kama "Machinery" nzima ya ulinzi na usalama ikoje katika nchi yetu.

Kama mnafahamu ni nchi yoyote iliotulia kama Tanzania inapaswa kuunda mambo kama ya ulinzi na usalama katika standards zinazokubalika. Kazi ya usalama (intelligence services) kivyake na ulinzi(security services) kivyake.

Tukiishafahamu kwamba nani ni nani na taasisi ipi ni ipi na inafanzaje kazi zake na bajeti yake ikoje kwa mwaka, ndio tutafahamu kwamba nani wabanwe au abanwe na tuhuma kama za kuzembea kusimamisha "proceedings of crime".

Kwa mfano suala la Radar,IPTL, Richmond na midubwana mingine, ingeweza kuchunguzwa kupitia TAKUKURU ambao wangekuwa chini ya TISS ambao wangekuwa wapeleke "dossier" yote kwa kamati za Bunge za ulinzi na usalama na ile ya mahesabu ya serikali.

Lakini "technically" kama mkono wa raisi unapita hapo kabla ya "dossier" hio kwenda huko, basi hapa pana tatizo.

Nafikiri sasa imefika wakati mheshimiwa raisi akashirikisha watu mbalimbali wenye upeo kuunda vyombo kama hivi kumsaidia kazi zake.

Kwa mtazamo wangu RO na taasisi yake inaonekana wapo chini ya Mheshimiwa Membe na kama wanashiriki vitendo vya kihuni huko mitaani basi wanakuwa na matatizo binafsi.

Mheshimiwa raisi aunde upya chombo kipya imara na chenye sura mpya cha kulinda nchi yetu.
 
Icadon, kwa kuangalia sheria ya TISS sidhani kama wanastahili hata kuwepo huko Ubalozini... hofu yangu kutokana na mjadala huu tuna parallel National Security Agency ambayo haiko chini ya TISS

Duh!!! Tuna agency nyingine wihin TISS?
 
Ewe bibi unadanganya watu wazima? ukidai umekutana na mtu mara kibao na kisha baadae kudai humjui ni tofauti kabisa na kufananisha na issue za divosi, hapo ni kubadilika misimamo, mimi nikisema nakufahamu na tumeshaonana mara kibao na baadae kwenye issue nyigine nikasema sikufahamu kabisa HUO UNAITWA UONGO...

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mtu mwenye akili, ambae anajua kuwa una akili akakupa hoja ya kipumbavu kisha ukaikubali, amekudharau...[this is paraphrasing not actual quote]...bibie acha kuinsult intelligence za watu wazima humu!!

FMES ametundanganya afute kauli yake au aseme tuamini lipi anamfahamu RO ''kwa kukutana nae mara kibao'' au ''RO mwenyewe wala simfahamu'' which is true?!!

watu wazima mkishikwa pabaya mnahaha!! tehe tehe

Jamani,

Hata mtume Petro alimkana Yesu mara tatu kabla ya jogoo kuwika....:(:confused:
 
Mabalozi wengi tu wazee ukishaona mshua ana "Ofisi ya Rais" katika resume ujue mambo, ndiyo walivyokuwa wanaitwa.

Kazi zao supposedly ni mambo ya espionage :) .Gathering of intelligence in international relations and such vague bs.

In other words, drinking expensive Jack Daniels and turning in some James Bond like bills in the name of the Republic.

You mean Daraja? Naye ashikiwe bango kuhusu Richmond or whoever who was Station Chief DC!
 
Mzee ES,

Habari za masiku mkuu?

ingawa na uongo pia uko mwingi. Baadhi ya uongo ni kwa kutokujua lakini inakera pale inapokuwa ni uongo wa makusudi kabisa..
probably to serve certain interests/agenda.. and sadly, wana JF wengi wanauheshimu as ukweli, as long as uongo huo unaendana na trend ya kuponda na kulaumu viongozi, hata wasiostahili kupondwa!
Ukiwa Muongo .. especially wa aina yako Mzee ES.. inabidi uwe na good memory, otherwise utaumbuka. Maana mitandao hii ina keep records.. hakipotei kitu! Leo unadai wewe binafsi hata humfahamu RO... na unataka ajiuzulu kwa kushindwa kazi??!!!

Mkuu Kulikoni,

Heshima mbele bro, karibu tena:-

1. The fact kwamba katika hii topic nzima umerudi na kuanza kunishambulia mimi peke yangu, na ukamuacha hata mtoa mada, na wachagiaji wengine wote, maana yake ni moja tu nayo ni kwamba unayaogopa na kuyaheshimu mawe yangu.

2. Mkurugenzi wa sasa wa usalama, nimemuona mara nyingi sana na hata kusalimiana naye sana, lakini sina urafiki naye wala simfahamu kibinafsi, wala kikazi, lakini ninawafahamu wananchi wengi anaofanya nao kazi, na anaowafanyia kazi, alipochaguliwa tu kulikuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wananchi wa hiyo idara kuhusu suala zima la kuchaguliwa kwake, na mimi nilikuwa pia ninawawakilisha hao wananchi, kulingana na machache niliyokuwa nikiyafahamu kuhusiana na kazi yake akiwa ofisa wa kawaida kule UK, kwamba hakuwa tayari kushika hiyo nafasi,

Lakini ninaomba nirudie tena kuwa personal, simfahamu kabisa zaidi ya kumuona ona na kusalimiana naye kwenye masehemu sehemu, lakini ninajua for a fact kwamba Tanzania tuna mkurugenzi wa usalama na ninajua wajibu wake ni nini ndio maana kwenye hii topic kama umesioma vizuri sana, utagundua kuwa sijatumia jina lake, bali nimekuwa nikitumia mkurugenzi wa usalama tu, maana yangu ni kwamba hata kama asingekuwa yeye, mwenye hilo jina I could care less, ninachojali ni makosa au mapungufu ya mkurugenzi wa usalama kwa kushindwa kujumulisha rais mapema kuhusiana na ufisadi wa baadhi ya viongozi wetu, na hata rais kuishia kuwapa madaraka, sasa matokeo yake ni aibu nzito, sio kwa rais tu bali kwa taifa zima na hasa CCM kwa ujumla.

Na kitendo cha waziri Chenge, kujiuzulu inadhirisha wazi uzito wa hoja yangu kuwa rais angejua mapema, asingemchagua kuwa waziri, lakini kwa sababu hakupewa ripoti mapema na mkurugenzi wa usalama ambaye kisheria ndiye mwenye mamlamka hayo, sasa kwangu it does not matter kwamba mkurugenzi ni nani, lakini ninaungana na mtoa hii hoja kuwa ni lazima ajiuzulu kwa hilo, je hoja yako on kichwa cha hii topic ni ipi? zaidi ya kunishambulia mimi binafsi badala ya hoja?

....inaendelea.....
 
1.
ES baada ya kumponda sanaaa RO (while ukiwa humjui), baadae ulikuja kudai umekutana nae mara nyingi na ukakiri kumkubali na kumfagilia RO kuwa he is doing a great job na kuwa sasa hivi anakubalika, na kuwa mmeshakutana mara nyingi.

2
. Refer post zako za nyuma:
Quote: Field Marshall ES
.... tena finally nilikutana na RO, hivi karibuni amepata message na yeye piahe is doing just fine na ameanza kukubalika huko ndani, unajua sina tatizo hata siku moja kukubali ukweli, RO sasa hivi he is doing a great job, na tayari ameanza kukubalika.

1. "Finally, nimekutana naye" hivi maana yake inaweza kuwa nilikuwa ninamfahamu?

2. "Sasa ameanza kukubalika huko ndani", maana yake inaweza kuwa mimi kumfagilia? Je kuna mahali popote kwenye post zangu ambapo nilisema anfanya kazi nzuri kwa taifa? Nimesema ameanza kukubalika huko ndani, maana yake ni moja tu kuwa tatizo langu kwake lilikuwa kutokukubalika huko ndani, lakini I never mentioned taifa mkuu, ambalo sasa ndilo hasa tatizo langu la msingi, regrdless of nani ni mkurugenzi wa usalama.

3. "Amepata message", kwako ina maana gani mkuu kwamba sasa ninamfagilia? Yes nilipokuwa ninamponda mara ya kwanza nilikuwa nimepata dataz zake nyingi, na pia nilikuwa nimemuona kwa mbali na nilisema wazi kwenye kikao cha wa-Tanzania na Mkapa, otherwise, si kweli kwamba hapa JF tunawajua viongozi wote tunaowaongelea, lakini one thing ni kwamba tunafuatilia utendaji wao wa kazi kwa taifa, mimi simjui Chenge, lakini nimedai ajiuzulu na amejiuzulu, kutokana na habari zake za ufisadi, that is all I need to know sio lazima nimjue kiongozi kwa karibu kama unavyotaka kusema,

yes alipochaguliwa mkurugenzi nilikuwa simjui, na kwenye hizi post ambazo zingine umezitoa kwenye pm, nimesema wazi kwamba "Finally nimekutana naye", hivi kweli hayo maneno yanaonyesha nilikuwa ninamjua? Mimi huwa sina tabia ya kutoa ishu za kwenye pm hapa, maana ninaheshimu sana maana ya private, na wewe unajua vizuri sana kuwa nikizitoa pm zako hapa, hutarudi tena hapa, lakini sio tabia yangu hiyo mkuu hata useme nini, lakini I will never do that,

Sasa hebu nionyeshe uongo wangu ulipo mkuu, maana so far siouoni?

...inaendelea....
 
On January 5th 2007, President Kikwete signed the Tanzania Anti-Money Laundering Act of 2006 into the law.

Article no. 8 of the law lists individuals who are to be members of FIU Financial Intelligence Unit.

In addition to this AML-FIU act, the 1984 Economic Sabotage is still in place.

On both acts, TISS is to be involved in snooping any suspicious activity that threatens National Security.

So if we give a pass on BAE, what about Richmond in which the TISS DG claimed to have no knowledge of the whole deal?

Nini wajibu wa TISS?

Ikiwa Rais alimpigiasimu mkuu wa TISS kuhoji kuhusu Richmond na mkuu wa TISS wakati huo akasema yeye hajui lolote kuhusu Richmond (mind you this was at the stage Richmond wamekwenda kuomba pesa na Msabaha kakimbilia Ikulu kuomba pesa baada ya Meghji kumtolea nje), je TISS wanafanya kazi gani kulinda usalama wa Taifa letu?

It is not about RO as individual, it is about his responsibilities as London Station Chief and now as DG of TISS that are in question.

Hayo mengine ya ulevi sijui ufuska do not interest me!
 
Ref: http://www.jamboforums.com/showpost....6&postcount=41

na ukarudia kusifia tena hapa

Quote: Field Marshall ES

Mzee wa RO, hata siku moja siwezi kuja kwenye forum kuongelea mambo ya chooni huoni hata aibu kuandika maneno low kiasi hicho kwenye chombo hiki cha kimataifa? Wewe siku nyingi ninakuona una shida ya kuongelea Malecela sasa you got it lete, Sasa hivi the man is doing a great job na sina noma naye, na nimeshakutana naye mara kibao, taifa ni taifa sina mchezo na mtu!

Ref: http://www.jamboforums.com/showpost....6&postcount=60

1. "Sasa hivi the man is doing a great job" eti maana yake ni kumjua na kumfagilia? Hapana maaana yangu ilikuwa wananchi wengi wa kwenye idara waliokuwa wakimpinga, sasa wameanza kumkubali, na mimi sina noma kwa sababu nilikuwa simjui, lakini sasa nimeanza kumjua, the matter of fact "Finally nimekutana naye na hata kusalimiana naye", sasa hiii inanifanya niwe muongo mkuu?

Mkuu nina wasi wasi kuwa kuna mtu ameiba Code yako, maana kwa kawaida huwa una kichwa sana, as opposed na this nonesense!


Eti leo tena unadai humjui na unataka ajiuzulu. Are you the same ES au ni watu tofauti tofauti mnatumia ID moja?

Mkuu no way!, mimi ni yule yule Original SAM(BCS), Mzee ES, Komandoo ES, Field Marshall Super ES, wala sio wa fake ni yule yule, wananchi wengi tulimpigia kura rais Kikwete, unafikiri ni kwa nini tulimpigia kura? Kuna mpaka waliosema kuwa ni nabii kutoka mbinguni, unafikiri ni kwa nini walisema vile then? Kwa hiyo una maana malalamiko ya sasa against rais yanatoka kwa ambao hawakumpigia kura? Kwa hiyo kwa hizi standard zako za siasa ina maana wananchi wote waliompiga kura rais na CCM, wanaolalamika sasa ni waongo?

Lets, say kwamba nilimsifia kuwa anaweza kazi miaka miwili iliyopita, sasa leo sina haki ya kubadilika na kumuona hafai? Hivi ninahitaji hata kurudia sababu ya kumuona mkurugenzi wetu wa sasa wa usalama hafai na inatakiwa ajiuzulu? Mbona niliposema Lowassa, ajuizulu hukuwa na tatizo? Mbona nilipokuwa ninasema Chenge ajiuzulu hukuwa na tatizo? Kwa nini kwenye huyu mkurugenzi wa usalama una tatizo?

Nawaonea huruma wanaoendelea kukubali ‘data' zako. Labda leo uwasaidie hawa unaowadanganya hapa as to what did RO do to impress you to the extent of kumfagilia as quoted above.
Piga madongo panapostahili, bila kuleta uongo. Utaheshimika that way!!!

Hivi kweli wewe unaweza kuongelea habari za uongo na ukweli, je uliyoyafanya kwenye uchaguzi wa wa-Tanzania, unafikiri hatujui? Ya kuwadanganya wa-Tanzania kuwa unataka kuwa mwenyekiti wao, kumbe unazuga tu ni kibaraka wa balozi ili uharibu kura apite mtu wa balozi! Sasa wewe kweli una-qualify kuongelea ukweli na uongo na unafiki wa wengine? Wewe unajua ni kwa nini watu huko hawataki chama cha wa-Tanzania? Unajua chanzo chake ni nini? Hujui kwamba wengi wao walikatishwa tamaa na wewe na matendo yako wakati wa uchaguzi?

Untaka dataz za namna gani tena mkuu? Hapo ndugu zako wamelala macho kumsubiri rais nikawaambia kuwa haji, kuna waliobisha, je alikuja? Nikaawambia badala yake anaenda US kuna waliobisha, je hakwenda?

Heshima? wewe unayo mkuu? mimi tena niongelee heshima yangu, hivi kweli ninahitaji kwenda hiyo avenue ya heshima na mimi? Halafu kama kawaida ya hii forum kuna mpaka waliokushangilia are you kidding me? hizi skeleton utagombea uongozi wapi tena? Tanzania? CCM?

Sababu ya kumkataa mwanzoni mkurugenzi wa usalama nimezisema, kwamba ilikuwa ni kutokubalika kwake huko ndani, na nilipokubali nimesema wazi kuwa ni kwa sababu ya kukubalika huko ndani, kwamba nilikuwa simjui nimesema wazi na naneo "Finally nimekutana naye", sasa uongo wangu hapa uko wapi?

Mkuu again, sina any personal problem na mkurugenzi wa usalama, lakini nina tatizo na utendaji wake wa kazi kwa taifa, na ninaungana na muanzisha hii mada kwamba sasa ni wakati muafaka ajiuzulu, kwa kushindwa kumfahamisha rais mapema, ili asichague viongozi mafisadi, na pia kwa kushindwa kufuatilia hoja za Dr. Slaaa, kuhusiana na viongozi mafisadi, Chenge akiwa mmojawapo.

Otherwise, ninakutakia marudio mema hapa JF, na jaribu kuepuka personal attacks, maana sasa ninakujua sana kuliko then, lets stick to the ishu, hiyo sina tatizo kulumbana na wewe, ila ninasikitika sana kwamba psot yako ya kwanza umaeamua kunishambulia personal zaidi kuliko ishu, kwangu huu ni mjadala muhimu sana kwa taifa langu, na ningependa wananchi wengi wauone ili waamue pumba ziko wapi na mchele ulipo, na mimi binafsi kama nilivyoahidi ninasubiri uishe nianze kukusanya points za kuzipeleka mbele zaidi kwa ili zifanyiwe kazi.

Ahsante sana mkuu, na karibu tena!
 
Ooh yah!

1. Kwanza heshima kwa wakuu wangu Mwafrika Wa Kike, Mkulu Wangu Mwanakijiji, na mkulu wangu Ogah, kwa kunisimamia nikiwa sipo wakuu sina cha kuwalipa, bali kuzifikisha hoja nzito kwenye hii topic zinapotakiwa, na kama nilivyowaambia jana kwenye simu kuwa kuna mkulu ambaye nitakuwa naye karibuni, kwa hiyo nitam-printia hoja zote zinatakiwa kufanyiwa kazi kwenye hii topic, hasa za mabadiliko ya baadhi ya vipengere kama vya uajiri. Halafu unajua mijadala kama hii ndio inatufundisha namna ya kuheshimu baadhi ya members hapa, ambao tunalumbana kila wakati lakini ikiisha tunaingia ishu zingine, kwenye hili lazima niwape heshima watu kama Invisible, MMJ, MWK, Kishoka, Ogah, Nyani, GT, na wengineo, tunalumbana tunasonga mbele, sio kujaribu kubadili mjadala na maneno ya personal, sio uungwana jamani!

2. Brazameni, heshima yako mkulu mimi nilifkiri tutakutana kwenye harusi ya Invisible, Julai, si nimekuambia nitawaleta wazee wa mujini yaani wazee wa ngwasuma! vipi wewe?

3. Off course, nilikuwa kazini bro si unajua tena gurudumu la maisha na familia, si nilikuambia kuwa nina mke na watoto bro, responsibility sio kwamba ninaidai tu kwa viongozi, bali na mimi ninazo mkuu, ingawa pia nilikuwa bussy sana na mkulu Kusaga, kwenye kukamilisha ziara ya senti hamsini.

4. Mkulu wangu Nyangumi,

sina lolote la kuomba msamaha, kwa sababu kwanza sina kosa la kunifanya nifanye hivyo, halafu niwe mkweli kwamba sio tabia yangu, I was never raised to be a poor sorry state being, toka nizaliwe, ninajua things to be black and white, the ishu hapa ni mkurugenzi wa usalama, sio mimi ES, sasa nashangaa na wewe kichwa unaweza kunaswa na huu mtego tena na watu ambao wanajaribu through co-ordination kuuharibu huu mjadala,

Nilipodai Chenge, ajiuzulu mbona sikuwa muongo? Nimekuwa muongo baada ya kumgusa ndugu yao, na wewe mtu kichwa unadiriki kuupanda huo mkenge? Hebu angalia vizuri hayo mashambulizi hivi huoni yote yanatokea London, alikokuwa akiishi mkurugenzi wa sasa wa usalama? Hivi una uhakika gani kuwa wanaorusha mawe hawakuletwa na huyo mkuu huko? Mpaka tuseme yote?

Siwezi kuomba msamaha bila kosa, mtoa mada ni Mwanakijiji, mimi ni mchangiaji kama wengine ssa kwa nini wamenirukia mimi na sio wengine? Unafikiri ni kwa nini? Mimi kumjua au kutomjua huyo mkurugenzi inaongeza nini as far as hii ishu is concerned? Yaani kweli Nyangumi, unataka niombe radhi kwa ajili ya ujinga? Mmimi sio fisadi bro ni mafisadi ndio wanaotakiwa kuomba radhi sio mimi ninayewapiga mawe, huu mjadala hauwezi kuzimwa wala kuharibiwa, labda wengine lakini haiwezi kuwa kutoka kwangu,

Nilipodai Chenge, ajiuzulu sikuwa muongo? Lakini nimedai Mkurugenzi wa usalama, nimekuwa muongo? Na wewe kichwa unaupanda mkenge? Halafu CCM wakishinda kura tunasema wananchi ni wajinga!

5. Mkulu Gembe, Mwanakijiji sio John Mashaka, kama ndicho kinachokusumbua, Mashaka anatoka kijijini kwangu Kinyerezi/Segerea, sasa kwako na kwa wengine wote tuwekane sawa sasa, sio yeye naona wengi mmemshupalia sana, Mashaka ni kijana mdogo sana anyesafiri all the time hana hata muda wa kuingia kwenye mtandao, kwanza he was in abig shock kusikia kuwa ametolewa kwenye mtandao.

Haya wazee turudini kwenye ishu, ishu sio ES, ingawa mimi nimesema ya kutosha, ninasubiri hii topic iiishe tuendelee na kazi zingine za muhimu za the message ya hii ishu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom