Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Na kitendo cha waziri Chenge, kujiuzulu inadhirisha wazi uzito wa hoja yangu kuwa rais angejua mapema, asingemchagua kuwa waziri, lakini kwa sababu hakupewa ripoti mapema na mkurugenzi wa usalama ambaye kisheria ndiye mwenye mamlamka hayo, sasa kwangu it does not matter kwamba mkurugenzi ni nani, lakini ninaungana na mtoa hii hoja kuwa ni lazima ajiuzulu kwa hilo, je hoja yako on kichwa cha hii topic ni ipi? zaidi ya kunishambulia mimi binafsi badala ya hoja?
Mkuu FMES,
Hii hoja yako ya kuwa JK hakuyajua haya sikubaliani nayo kabisa, unless kama utakuwa na proof.
Kama ilivyokuwa kwa mbadhirifu mashuhuri Lowassa ambaye anafahamika kabisa kuwa sio safi lakini bado JK alimpa madaraka, tena makubwa, nafikiri JK pia aliyafahamu ya Chenge lakini hakujali na aliamua tu kumpa ulaji zaidi. Ni vema JK tukamjumlisha na hawa wateule wake na sio kumwacha yeye pembeni kama vile ni mtakatifu. He is not.