Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu!

Status
Not open for further replies.
Dada yangu Mwafrika wa Kike,

SOmetimes najiuliza kama nilizaliwa kwenye nchi yenye laana au vipi! Miye nasubiri Uduo ukamilike nachukua Uraia Rwanda na Congo, kule wanaelekea wameanza kupata akili!
 
Icadon,

Hawa jamaa wanahitaji reform za hali ya juu. Wao wanafikiri kujua Kung-Fu na Judo ndio ujanja.

Si ajabu wengi wao hata kutumia Computer na internet hawajui!

Zama za kufukuzana na watu wanaobeba AK-47 zishaisha siku hizi wa kuwaogopa ni wale wenye flash disks na laptop.....

Mhandisi, tatizo sio kuja hapa tatizo ni wanakuja hapa kwa nia gani...na wanautilize vipi open source.
 
Icadon, sheria ya TISS inasema wapi kuhusu kuwa na wafanyakazi wa TISS kwenye balozi zetu?

Hapa chini ni moja ya departments za MOSSAD....na inazungumzia hiyo issue ya kuwa na mtu ubalozini.....slowly naona ni kweli tuliiga mfumo wao.

Collections Department is the largest, with responsibility for espionage operations, with offices abroad under both diplomatic and unofficial cover. The department consists of a number of desks which are responsible for specific geographical regions, directing case officers based at "stations" around the world, and the agents they control.
 
sisi wa kwetu I have no Idea. Kwa mlioko nyumbani hakikisha u get a copy of "Kulikoni" na wale wa online... it'll be later tomorrow kwenye klhnews.com editorial
 
Mhandisi,

Hawako hapa kujifunza na kujirekebisha! Wako hapa kutafuta nani kasema nini kuhusu Serikali, anakaa wapi na kamsema yupi wa Serikali!

Wamekaa mkao wa wambea kazi kuchukua habari na kusema ohh "vijana wana matusi" nope!

Kwanza ujinga wao na urahisi wao kutabirikia mtaounoa jinsi CCM inavyofanya kazi. Walipokwenda Butiama, unasikia wanasema Tutachapa maadniko ya Nyerere! Hii ilikuwa baada ya watu kukata ishu kuhusu Fikra na legacy ya Nyerere.

Kwenye mkutano wa Rais wa mwisho kwa Taifa, katujubu kihakika JF kuhusu Comorro ili aonekane analofanya ni la maana.

Mbona hawajajibu haya ya Ufisadi? Mbona hawajesma lolote kuhusu maafa yanayotuzingira?

Labda uniambie wale vijana wadogo wakiwasilisha nondo kwa wakubwa na zikifika kwa RO, zinakwama! Then it is justifiable for us to say RO has to go!

Bahati mbaya ni kuwa, juhudi zao za kujua nani ni nani wanazifanya kizamani hadi inachekesha. Mimi nawasoma tu postings zao hapa na kisha najiuliza, hivi huyu naye analipwa kwa kazi gani hasaaa?

Kufuatilia wana JF ni ujinga na uzembe, wengine wenu mko very active kwenye JF na wengine hata wamechangia hii thread as if hatuwajui. Grrrrrrrrrrrr
 
Sikutaka kuanzisha thread lakini tangu wiki iliyopita nimekuwa nikiomba hizi threads ziunganishwe ili tuwe na mtiririko mzuri wa habari

Nimeona bora niwarahishie kazi



RASHID OTHMAN ndiye Boss wa Usalama

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=169&highlight=TISS
Usalama wa Taifa wapo likizo?... Je, Waziri wa Intellijensia ni nani?

The Spies who loved me...AG, TISS, TAKUKURU, POLISI



http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=10207&highlight=TISS

Taifa lilipotekwa Nyara, Usalama wa Taifa walikuwa wapi?

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=11575&highlight=TISS


Rashid Othman: Umeshindwa Kuhakiki Usalama wa Taifa, Jiuzulu !

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12174&highlight=TISS


GEORGE KAHAMA na ANDY YOUNG wamegombana?
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8264&highlight=TISS

Mashushushu kazini kuua waandishi?

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12160&highlight=TISS


Usalama wa Taifa (TISS) kumejaa wezi na mafisadi

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8997&highlight=TISS

Usalama wa Taifa

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9246&highlight=TISS

VETTING na BACKGROUND CHECKS serikalini
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=5519&highlight=vetting







Moderators wao au hawapo humu? ninashindwa kufuatilia vizuri hii thread wakati kumbe ziko zingine zinazohusiana

hebu fuateni ujumbe jama
 
Mada hii haina kichwa wala miguu, naweza kusema udaku tu kama kawaida ya JF.

Hakuna nchi yeyote duniani ambapo waziri amefanya blunder halafu mkuu wa usalama anaambiwa ajiuzulu labda iwe idara inahusika moja kwa moja na usalama wa Taifa. nchi mbali mbali wanajiuzulu mawaziri na watendaji wengine sijawahi kusikia kujiuzulu kwao kuko sambamba na mkuu wa usalama.

Kichwa cha hii thread hakioani na habari yenyewe, tumeona humu kuwa RO ana miaka miwili au kasoro kidogo tu kwenye cheo chake na haya mambo yamefanyika 1999.

Sawa na mtoto kuja kupewa kesi ambayo hata kabla ya kuzaliwa kwake ndio hiyo hujuma ilifanyika.

wapo wanaosema kuwa alienda London wakati wa issue ya Rada, lakini hilo si jibu kwani yeye hakuwa mkurugenzi mkuu wala mkurugenzi wa Idara yeyote wakati huo. ni sawa kabisa na kumlaumu mkuu wa wilaya ya Ilala na kumwambia kuwa ajiuzulu kwa vile EPA imefanyika katika himaya ya wilaya yake au mkuu wa wilaya husika ya Kiwira ajiuzulu kwa kuwa Mkapa kachukuwa machimbo ya makaa ya mawe wilayani kwake,Mkuu wa wilaya kuna watu wangapi juu yake?hakuna uhusiano wowote.

Wengine baada ya kushindwa hoja wamekuja na majibu kuwa aliwapeleka kina TID ulaya, huu ni uvivu wa kufikiri mtu yeyote anaweza kumpeleka Mwanamuziki majuu,Twanga pepeta wanaenda kivyao kila mara.

Kuna wengine wanaleta kazi za usalama na majukumu yao hapa JF kama ni ushahidi wa kumsakama Rashid Othman.

Jamani kila taasisi ina utaratibu wake lazima ufuate taratibu za ngazi za kazini, unatakiwa kuripoti kwa wakubwa wako na huko kuna wasemaje wahusika ambao wanajukumu hilo la kusema hawezi Rashid kuwa msemaji wa mwisho wa Rada wakati yeye alikuwa staff wa kawaida sana si Mkuu wa idara yeyote.

Nashangaa sana kuona watu wanajibizana kwenye udaku usio na dalili ya ukweli kama huu ambao umesimikwa chuki na majungu dhidi ya kijana RO ambaye katika muda wake mfupi tumeona kazi nzuri yake,

Inajulikana wazi Wafrika hawana utaratibu kwa kuheshimu au kupongeza kazi nzuri ya mtu zaidi ya kukosoa kila kitu.

kuna watu hawana kazi hivyo wanaandika kila wanachojisikia na kwa vile JF unaruhusiwa kuweka chochote wanatumia uhuru huo kuwapakazia watu wanaofanya bidii kwenye kazi zao.

Chukua dakika chake kutafakari uchafu wa Chenge umetokea 1999-2002 huyu jamaa hakuwepo katika eneo hilo au hakuwa na madaraka aliyo nayo sasa, vipi umlaumu bila sababu ya msingi?

Inaonesha wazi kuna njama za kuwachafua watu lakini mchafue mtu kwa lile analostahiki si kumlaumu au kumsingizia tu.

Nadiriki kusema Rashid Othman anaonewa au kuna watu wanaumia kuona anaongoza idara hii nyeti, alipoteuliwa tu kuna michango mingi iliandikwa hapa na Michuzi kuwa jamaa hana hata shule ameishia Madrasa ya kiislam tu, mie niliamini kuwa ana elimu ndogo kutokana wachangiaji wa mada yake na sikutaka kuchangia kwa jambo nisilolijua, baadae ikajakujulikana jamaa ana masters tena ya usalama na aliyeondoka (APSON) ni form six,sasa hapo unaona wazi kuwa aliyekuja ni bora zaidi mara mia kielimu kuliko aliyeondoka, lakini watu wakawa wanamtusi kuwa hana elimu ingekuwa kinyume chake hapo pana nafasi ya kusema.

Wakati wa awamu ya Tatu kulikuwa na ujambazi wa hali ya juu kuanzia mabenki na sehemu mbali mbali lakini hakuna waliotoa hoja ya kutathimini idara ya Usalama wa nchi yetu.leo mambo yamewekwa sawa wanakuja watu na hoja za mwaka 1947 na kumtuhumu mtu asiyehusika kwa sababu wanazozijua wao.

Rashid Othman pole sana kwa njama hizi ambazo hazina msingi madhubuti zaidi ya chuki au wanataka kukufanya BANGUSILO kwa jambo ambalo hukusika nalo.
 
Mkjj, kudos kwenye makala ndio nimemaliza kuisoma, by the way if my memory serve me correct RO alisema ataanzisha utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari..tunaendelea kusubiri.
 
Wakuu kama yaliyosemwa yametosha, nitaanza rasmi kukusanya points muhimu kuanzia Jumapili, kutoka hii topic ili kuzifikisha kwa baadhi ya wabunge wetu wa taifa, ili zifanyiwe kazi maana binafsi ninaaamini kwamba huu umekuwa mjadala mzito na wenye hoja nyingi za muhimu kutoka pande zote zinazotetea na zinazoshambulia, yote ilikuwa nia ya kuliletea taifa letu mabadiliko yanayolenga uwajibikaji katika sekta zote muhimu za taifa letu,

Kama vile tulivyowahi kutoa mapendekezo kwa ajili ya foreign(Membe), BOT(Balali), Tanesco(Idrisa), Polisi(Mahita), Chenge, Mkapa, Richimonduli, Lowassa, Msabaha, Karamagi, na wengineo wengi, ninaamini nia ilikuwa ni ile ile nayo ni taifa, sidhani kwamba kuna hata member mmoja hapa aliyetoa mchango wake kwa nia ya ubinasfi.

Binafsi ninawashukuru wote waliochangia hii mada nzito iliyoanzishwa na Mkulu MMJ, ambayo pia imetuhakikishia kuwa uhuru wetu wananchi wa kuuliza maswali muhimu kwa taifa letu kuwa hauna mipaka ndani ya sheria za jamhuri yetu, na Jumapili nitaanza rasmi kuchomoa points.

Ahsanteni
!
 
Mkjj, kudos kwenye makala ndio nimemaliza kuisoma, by the way if my memory serve me correct RO alisema ataanzisha utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari..tunaendelea kusubiri.

Kwa hiyo RO ajiuzulu kwa vile hajakutana na waandishi wa habari?
Kama umefuatlia habari vizuri hao SFO walipata ushirikiano wa serikali kumuhoji Chenge kama RO anahusika asingetoa ushirikiano nao na lazima vijana wake walikuwa bega kwa bega na SFO, hadi sasa sijajua kwanini unalalamika kuhusu Rada na RO.
 
Kwa hiyo RO ajiuzulu kwa vile hajakutana na waandishi wa habari?
Kama umefuatlia habari vizuri hao SFO walipata ushirikiano wa serikali kumuhoji Chenge kama RO anahusika asingetoa ushirikiano nao na lazima vijana wake walikuwa bega kwa bega na SFO, hadi sasa sijajua kwanini unalalamika kuhusu Rada na RO.

Soma mjadala mzima utaelewa, while you at it pitia na sheria ya Usalama wa Taifa ya 70s na TISS Act ya 1996.
 
Wakuu kama yaliyosemwa yametosha, nitaanza rasmi kukusanya points muhimu kuanzia Jumapili, kutoka hii topic ili kuzifikisha kwa baadhi ya wabunge wetu wa taifa, ili zifanyiwe kazi maana binafsi ninaaamini kwamba huu umekuwa mjadala mzito na wenye hoja nyingi za muhimu kutoka pande zote zinazotetea na zinazoshambulia, yote ilikuwa nia ya kuliletea taifa letu mabadiliko yanayolenga uwajibikaji katika sekta zote muhimu za taifa letu,

Kama vile tulivyowahi kutoa mapendekezo kwa ajili ya foreign(Membe), BOT(Balali), Tanesco(Idrisa), Polisi(Mahita), Chenge, Mkapa, Richimonduli, Lowassa, Msabaha, Karamagi, na wengineo wengi, ninaamini nia ilikuwa ni ile ile nayo ni taifa, sidhani kwamba kuna hata member mmoja hapa aliyetoa mchango wake kwa nia ya ubinasfi.

Binafsi ninawashukuru wote waliochangia hii mada nzito iliyoanzishwa na Mkulu MMJ, ambayo pia imetuhakikishia kuwa uhuru wetu wananchi wa kuuliza maswali muhimu kwa taifa letu kuwa hauna mipaka ndani ya sheria za jamhuri yetu, na Jumapili nitaanza rasmi kuchomoa points.

Ahsanteni
!

Bro, unaweza kutoa ka muhtasari wa hizo hoja muhimu unazopeleka huko mbele?
 
Bro, unaweza kutoa ka muhtasari wa hizo hoja muhimu unazopeleka huko mbele?

Mkuu kama una hoja ya kuongeza itoe hapa, next week nitakuwa very busy na wakulu mbali mbali on this topic, kama unataka weka nyongeza!

Nimesema nitaanza Jumapili, kuzichomoa hojas!
 
FMES;

Unajua sikua nataka kweli muhtasari wa kilicho jadiliwa hapa. Wote tumeisoma mada, tumechangia, na bado tunaweza kuisoma. Hasa, nilicho maanisha bila kukitamka ni hiki:

Kulikuwa kuna mawazo yanayopingana sana hapa. Na wewe ulikuwa una hisia kali katika upande fulani wa huu mjadala. Sasa unaposema unapeleka mawazo yetu kwa wakuu najiuliza unaenda kusema nini kuhusu huu mjadala? Utavutia ngozi kwako? Au utasema tumefikiri hivi, na kwa upande mwingine tumefikiria vile. Na huyo mkubwa atakuuliza kwa hiyo mnashauri nini kama kuna pande mbili, au saba?

Kwa hiyo, ukisema unaenda kutuwakilisha wakati wewe una imani kali kuhusu mawazo fulani nina wajibu wa kuuliza unaenda kusema tumesema nini? Tulipomtuma Nyerere kupeleka ujumbe kwa wakubwa mwaka 1956 wote sisi na huyo mesenga letu lilikuwa moja: tunataka Uhuru. Lakini hapa sijui mjumbe wewe utaenda kusema nini huko mbele. Sijui unanielewa bro?
 
ndio maana aondoke afuatane nao huko wanakotumbua fedha za Taifa hili. How can an intelligence agency be unintelligent?

Akili za mafisadi zinafanya kazi kwenye mambo yanayohusiana na ufisadi tu. Kwingine kote ni vihiyo. Mpaka wananchi waanze kupiga kelele kwenye magazeti, TY, Radio na mtandaoni ndio washtuke kwamba nchi inaangamizwa! halafu bila hata aibu wanajiita usalama wa Taifa!!!! labda taifa la mafisadi wanaoiangamiza Tanzania.
 


Waheshimiwa mmezungumza mengi sana lakini binafsi sina mengi zaidi ya kurudia yale yale niliyozungza na Icadon/Rkishoka sometimes back. Nako nilisema hivi:


Nchi kama yetu sisi tuko nyuma sana kwenye departments hizi..


Imagery Intelligence (IMINT)-Huna resource ipo kubwa lakini watu bado wanaendelea kutafuta watu wenye AK47 wakati dunia ya leo mambo yanaenda kwa TXT MSGS na LAPTOP yenye internet connection ..hivi vinatosha kupindua serikali

sehemu zingine ambao sisi tupo sifuri ni:


Signal Intelligence (SIGINT)-

Measurement and Signature Intelligence (MASINT)

Technical Intelligence (TECHINT)


Open Source Intelligence (OSINT)

Sababu ya kukosekana kwa hizi ni kwa sababu wanasiasa hawaoni umuhimu wa hawa jamaa kupewa pesa kwa ajili ya hizo.

baadhi ya jirani zetu wako mbali sana kwenye hizo depts na the same applies to Rwanda nchi ambazo in principle ziko kwenye state of war..both domestic and foreign


Having said that,personally mimi niko zaidi upande wa Policy kuliko operations au systems. Na nadhani kuwa tatizo tulilokuwa nalo ni hatuna Strategy ya maana kutokana na sababu mbali mbali na chache mojawapo ni:



1) Katiba yetu haiweki wazi mambo ya accountability na responsibility



2) Culture iliyojikita pale USALAMA WA TAIFA ya kulindana hata kwenye madhambi/kuajiri watoto wa wakubwa etc




3) Hakuna legislation ambayo iko updated kutokana na nyakati tuliyonayo



4) Hatukuweza kuchukua nafasi tuliyopata baada ya ubalozi wa USA kulipuliwa Dar kwani tungeweza kunufaika zaidi kutokana na msaada ambao Clinton Administration ilikuwa tayari kutupatia
Sidhani kama sisi tuna matatizo ya HUMIT (Humman intelligence) bali tatizo letu ni SIGINT na namna ya maintelligence analysts ambao wanalipwa vizuri na ambao wako free kufanya kazi zao bila kuingiliwa na wanasiasa



USALAMA WA TAIFA UNATIKIWA UPANYIWE REFORM TOP DOWN KWAKU:




a)Improve the integration of foreign and domestic intelligence ambazo kwa kiasi kukibwa ziko shaghara baghala




b)Improve indication and timely warning of impending threats to national security kwa sababu issues kama za BOT,RICHMOND,SERENGETI,IPTL zingeweza kuepukika kama watu wangekuwa responsible from the start




c)Improve analysis of threats both domestic na foreign na zaidi hapa tatizo langu liko kwenye great lakes region ambako silaha zimetapaka kwa kila kundi




d)Improve our ability to use intelligence to counter threats to our national security na hapa ni kuongeza nyezo za kazi kwa hawa jamaa wa UT


e)Na mwisho tunatakiwa kuimprove our ability to set goals and prioritize intelligence requirements, both collection/acquisition and analysis; and Improve the sharing of information in the fullest and most prompt manner. Ma skendo ya siku za karibuni yameonyesha jinsi gani tulivyokuwa nyuma kwenye hii sehemu ya kushare info japo dept ya kukusanya info inaonekana wanaweza kupass the ball kuwa wao kazi wanaifanya vilivyo


Kuhusu idara ya OPERATIONS ambao wao wanajisifu kuwa wako bize kukusanya info na info zipo tele lakini cha ajabu so far wamekuwa kimya kuhusu

1) reliability of source



2) credibility of info


KISIWA CHA PEMBA NA SABOTAGE YA BERNARD MEMBE

Mfano kwa nini UT wako kimya kuwaambia umma wa Tanzania kuhusu safari au movements za maofisa wa Ubalozi wa America kule Pemba?

maana nimeangalia hakuna project yoyote ya kuwafanya maofisa hawa wawe wanafrequent kule au ndio mambo ya Southeast Africa Task Force na kama hatuna info kuhusu role yetu kwenye hili lakini katika kuondoa utatanishi na uvumi wa habari ingekuwa bora UT pamoja na serikali wakaja clean kuhusu mambo haya.


wasi wasi wangu mwingine unaangukia kwa BERNARD MEMBE mabye wengi humu mnaweza kusuma nina beef naye lakini as much as kuwa tunaambiwa publicly kuwa hiyo AFRICOM haipo tena lakini MEMBE amekuwa very instrumental kuwa bypass TISS kwa kumvaa JK direct kuhusu hili. Now the next question je JK kwenye hili ataendelea kumsikiliza MEMBE ambaye alimpa ushauri mbovu kuhusu kupeleka wanajeshi wetu COMOROS kwa pesa za walipa kodi wa Tanznia. Wamarekani wana wanalobby kuweka kambi yao Tanzania na wanaona Pemba ndio perfect place...je hii misele inayopigwa na akina Nicholas Holman (head wa hii task force) manowari ya USS Ashland kwenye ukanda wa pwani yetu...sasa je hili nalo JK amesikiliza ushauri wa R.O au ndio bado anaendelea kumsikiliza MEMBE aka DONALD RUMEFELD?

Zaidi ya hayo mbona membe haytuambii kuhus waTanzania wangapi walioathirika na hii program ya Worldwide Attack Matrix ambayo inawafanya hawa jamaa wa Langley wawe heavily involved Tanzania?

Au ndio maana walikuwa na TISS act ambayo kwa kiasi kikubwa inaonekana kama jamaa walipunguziwa ukali for a reason...ukiangalia kuanzia tangu imesainiwa mpaka leo you will see what I mean.






ZAIDI YA HAYO....kuhusu BOT,RICHMOND na maskendo ya UFISADI


Kuna taarifa kuwa watu wa USALAM WA TAIFA walifanya kazi yao lakini wakubwa wao waliwa overrule. Na hili nakubaliana nalo by 100% kwa sababu politicians wanaingilia sana kazi zao hawa jamaa.Na kutokana na siasa za Tanzania I am sure kuwa hii ni norm na kumlaumu R.O kwa kila kitu hapa nadhani kuwa tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu..inabidi walipa kodi waelewe kuwa hawa jamaa na hasa wa domestic intelligence walitakiwa wawe ni watu ambo wako huru kufanya kazi zao pasipo kuingiliwa na wanasiasa




The bottom line siamini hata siku moja kuwa Usalama wa Taifa wanakosa usingizi kwa sababu yanayosemwa JAMBO FORUMS . after all ukitazama kwa undani Jambo Forums siyo source ya habari bali JF ni vinara wa kuchambua taarifa wanazozipata na in the end ni incompetent politicians ndio ambao wanakosa usingizi. Vile vile tusisahu kuwa its in the best interest kwa USALAMA WA TAIFA kama Jambo forums wakiendelea ku operate kwani inawarahisishia zaidi kazi wale tunaowaita ARMCHAIR officers ambao kazi yao ni kudelegate kwa departments zinginezo


Kuna kipindi REV KISHOKA alizungumzia threats na jinsi gain tunaweza kukabiliana nayo nadhani hiyo ni muhimu lakini usisahau kuwa hiyo nayo inaangukia katika mambo ya Human security hivyo idara hiyo inabidi ijitegemee...na kwa upande wangu mimi ninachukua msimamo wa




Ni kweli wafanya kazi wengi wa Uslama wa Taifa ni watoto wa wakubwa au baba zao walikuwa wako serikalini lakini in my opinion nadhani kuwa ni ma losers tuu I for very simple reason. In 2008 its inot really cool kufanya kazi uslama wa Taifa wakati CITYBANK wanawalipa wafanyakazi wao 20x more. Why waste time kuwa civil servant?





Nadhani Othaman na jamaa zake washaiona hiyo. Sasa hivi strategically dunia imebadilika na what counts now sio GEO=POLITICS bali ni GEO-ECONOMICS na nadhani what we need is more officers who are fluent in MANDARIN and CANTONESE badala ya kunganngania kuwa posted Addis Ababa au New York.

JK angetaka angemrudisha bwana AGOSTINO MAHIGA na angempa nafasi hata ya waziri wa Mambo ya ndani japo Mahiga na Membe picha haziendi lakini jamaa pale NEWYORK ni sawa na multimillion dollar weapon ambayo ni defunct. Of course OTHMAN aendelee kuwa bosi wa USALAM WA TAIFA na MAHIGA akirudishwa awe ana ripoti kwa OTHMAN kwani ndiye bosi mkubwa na independence yake iendelee kama kawaida lakini Personell inabidi ibadilishwe na wengi wao inabidi wapunguzwe. Swali je MAHIGA takubali ku swallow his pride na kurudi nyumbani ? maana nimeambiwa he has big ego lakini personally i'd rather see mtu mwenye big ego kuliko mtu ambaye ni insecure kama MEMBE ambaye maamuzi yake kwenye kila step ni kumuingilia R.O kwenye kasi yake na pili ameweka zaidi mbele ambitions zake za kutaka kuwa rais.





Mimi nina propose jamaa wa TIARA - Tactical Intelligence & Related Activities waongezewe budget halafu jamaa wa Joint Military Intelligence Program(MI) ipunguzwe budget yao kwa sababu wao wanazo resources nyingi za kuwaongezea pesa kasha nian suggest tuwe na National Foreign Intelligence Program(NFIP) ambao wanatakiwa washaestimate impact ya kuwa EAST AFRICAN SUPERSTATE na jinsi gani kazi zao zitakuwa affected na namna gani tutanufaika na kazi yao.




RECOMMENDATIONS ZANGU:
CORE: hawa wanajumisha watu wa system architectures for intelligence systems and applications inabidi waongezewe budget kwani wanajumuisha security organs zote za Tanzania



Idara ya TASKING: Skendo la RICHOMND na BOT zisingetokea kama hawa walikuwa wanafanya kazi zao inavyotakiwa walitakiwa kuwa kiungo baina consumers and producers of intelligence products.Inawezekana kabisa kulikuwa na oversight kubwa idara hii.




Idara ya COLLECTIONS: Idara hii imejaa watu wazima wengi na sikati kuwa mchango wao wa HUMINT ni mzuri lakini in this day and age ni ngumu kwao kudeal na watu amabo hawabebi AK 47 . In short threat iko zaidi kwa watu ambao wanatembea na Laptops au USB stick than anthing else. Sasa hawa walitakiwa waongezewe vifanyia kazi kazi ambavyo vinaendana na serity threats za kileo.



Idara ya PROCESSING Mimi ugomvi wangu mkubwa uko idara hii.Tangu bolu lilipopigwa ubalozi wa USA Dar I am not sure kama kuna heads ziliroll toka idara hii kwani mabomu yalitengenzwa DAR na resources zote zilipatikana Tanzania sasa sielewi hawa jamaa kama wanapewa budget ya kutosha au lakini I suspect hawapewi budhet ya kutosha na sijui kama processing zao ziko uptodate nah ii ninamaanisha both both primary processing and secondary exploitation systems.



Idara ya DISSEMINATION: Kama ipo hii sijui wanafanaya nini lakini I suspect hawa wanashinda kwenye ma bar kunywa bia . Yupio dogo mmoja namjua anadai yuko idara hii lakini mpaka leop sijui watu wa Othama walimpa kazi based on which criteria (lakini hapa si mahala pa kumzungumzia ) kwa msio jua kazi ya idara hii ni kuwa hawa jamaa kazi yao ni kuprovide communications links between collection systems, processors, and users na hawa jamaa kazi zao zaidi ni Comms lakini kama budget iko chini I am sure kuwa wanayo excuse ya kushinda kwenye Makontena wakinywa beer all day


 
GT unasahau kuwa nchi yetu priorities ziko kinyume nyume...I guarantee you ukipropose wanunue UAV watakuona umechanganyikiwa...
 
1.
Unajua sikua nataka kweli muhtasari wa kilicho jadiliwa hapa. Wote tumeisoma mada, tumechangia, na bado tunaweza kuisoma. Hasa, nilicho maanisha bila kukitamka ni hiki:

Hivi kweli unaamini kuwa nilikuwa sijui nia na madhumuni yako? Mbona siku zote huwa ninasema motives zako kwenye ishus, ahsante kwa uhakiki kwamba huwa niko on the right track as far as motives zako kwenye ishus.

2.
Kulikuwa kuna mawazo yanayopingana sana hapa. Na wewe ulikuwa una hisia kali katika upande fulani wa huu mjadala. Sasa unaposema unapeleka mawazo yetu kwa wakuu najiuliza unaenda kusema nini kuhusu huu mjadala? Utavutia ngozi kwako? Au utasema tumefikiri hivi, na kwa upande mwingine tumefikiria vile. Na huyo mkubwa atakuuliza kwa hiyo mnashauri nini kama kuna pande mbili, au saba?

Kwanza ni lazima niiweke wazi kuwa sio lazima nikujibu haya maswali, lakini nitajibu anyways kwa sababu huwa hatukimbii maswali wala hoja, wewe hujanituma na wala sijawahi kutumwa na mtu yoyote hapa, ni uamuzi wangu kuyapeleka mbele, na nimeshafanya sana huko nyuma, umepewa nafasi hapa ya kuweka mawazo yako umefanya, sasa the rest waachie wanaoyaweza kwa sababu you have no control of what is next, wewe ni kuweka mawazo yako tu hapa!

Have a nice day mkuu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom