Mchokozi wa mambo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 201
- 159
Ni Tanzania pekee duniani mfanyabiashara anaweza kupanga bei aitakayo bila kujali chochote
Serikali kupitia waziri wa viwanda na biashara angalieni mfumuko wa bei nchini hasa bidhaa za msingi ni mkubwa mno.
Ukiuliza kila kitu unaambiwa ni sababu ya vita ya Ukraine na Urusi.
Sio kweli wafanyabiashara wengi sasa wanajificha kwenye vita hiyo kuumiza wananchi kwa kupanga bei kubwa na kunufaika juu ya hiyo vita.
Swali dogo tu hivi hapa Tanzania kila kitu tunachotumia kinatoka Urusi na Ukraine?
Bei ya Mafuta ya kula kwa lita ni 7000/= na baadhi ya mikoa ni 10,000/= na mafuta mengi yanazalishwa nchini.
Kwanini bei iko hivi. Wiki kama mbili binafsi nilifanikiwa kuona mfanyabiashara mmoja wa duka jumla unashusha shehena ya mafuta na kuficha nyumbani kwake ndani ya fensi na kupanga madumu kama 300 kuzunguka uwanja wa nyumba yake. Lakini mtaani ukiuliza unaambiwa bidhaa hii ni adimu sana sababu ya vita na ndio maana bei ni kubwa kitu ambacho si kweli.
Kwanini Serikali inafumbia macho wafanyabiashara wenye tamaa kuumiza raia wao?
Bei ya vifaa vya stationery nayo haikamatiki. Fikiria kufikia mwezi Machi mwanzoni ream ya karatasi ilikuwa ilikuwa Tsh 8000/= kwa pc1 na katoni yenye ream iliuzwa kwa Tsh 40000/= Ila kwa sasa ream 1 tu ni Tsh 15000/= mpaka 18000 baadhi ya maeneo huku katoni ikiuzwa kwa Tsh 65000/= .
Mbona Zanzibar vitu bei ni rahisi sana kwanini huku bara tunanyanyasika na huku Rais wetu umekaa kimya? Huna huruma na watu wa bara? Mbona Rais Mwinyi katangaza kushusha kodi kwa bidhaa za msingi kwa kipindi hiki cha mfungo ili bidhaa zishuke kwanini huku bara inashindikana?
Mheshimiwa Rais kauli yako uliyoisema kuwa bidhaa nyingi zitapanda kwa sababu ya vita na zitazidi kupanda sana imechukuliwa kama fimbo na wafanyabiashara kuumiza raia.
Serikali ya awamu ya tano bei ya Sukari ilipanda sana na ikawa sukari ni adimu sana lkn kwa umakini wao walihundua ni janjajanja ya wafanyabiashara walikuwa wameficha sukari ili wapandishe bei kwa kwa kuwa ni adimu.
Lkn tuliona Serikali imejitokeza na kutangaza bei kikomo kwa mikoa yote na huku ikifanya msako kukamata sukari iliyofichwa. Kwanin sasa inashindikana?
Kiukweli Rais bila kuwa mkali nchi hii hautafanikiwa kwa chochote. Watanzania wengi walishaharibika wakipata fursa wanawaza matumbo yao na kujinemeesha wao kwa wao.
Nchi hii kwa sasa ndo tuseme ni ya watu wachache? Hapo nchi jirani ya DRC bei za bidhaa za msingi zilipanda majuzijuzi tu, lakini tumeona Bunge wamemta waziri anayehusika na biashara ajiuzulu ndani ya masaa48.
Tanzania hapa kila kitu ni kusifia hata ujinga. Bunge letu mmekosa mamlaka kisheria kuchukua hatua mbalimbali kurekebisha mambo nchini?