Mwigulu na Ashatu Kijaji wawajibike kwa mfumuko wa bei, vitu vimepanda bei sana na kuyafanya maisha magumu sana

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,641
46,291
Mara nyingi watawala sehemu nyingi duniani hujificha katika kupanda kwa bei ya mafuta kama sababu za mfumuko wa bei nchini mwao lakini kwa sasa mafuta hayajapanda bei duniani kwa muda mrefu ila vitu vimepanda bei sana nchini.

Mwigulu Nchemba na Ashatu Kijaji jitokezeni hadharani mseme sababu za bidhaa na huduma kupanda bei kwa kiwango cha juu sana na kwa kasi kubwa sababu ni nini. Watu wenye vipato vya kawaida na vidogo wanaumia sana.
 
Zalisheni kwa wingi mfumuko wa bei utashuka.

Ukiina factor moja ya mfumuko wa bei wewe haikuhusu ina maana mahitaji yako mengine yanazidi yale ya mafuta.

Kijaji hana kosa hapo, Mwigulu analo la kujibu.

Mimi namshangaa sana Mama Samia hawatumii watu kama Assad kwenye mambo ya uchumi.

Lipumba simuamini sana, ingawa ni mchumi lakini ana kitu hakijanikalia sawa.
 
Kwa nini nauli za mabasi zimepanda bei kwa ongezeko kubwa sana?
 
Zalisheni kwa wingi mfumuko wa bei utashuka.

Ukiina factor moja ya mfumuko wa bei wewe haikuhusu ina maana mahitaji yako mengine yanazidi yale ya mafuta.

Kijaji hana kosa hapo, Mwigulu analo la kujibu.

Mimi namshangaa sana Mama Samia hawatumii watu kama Assad kwenye mambo ya uchumi.

Lipumba simuamini sana, ingawa ni mchumi lakini ana kitu hakijanikalia sawa.
Kwa uchaguzi wako nimepata jibu fulani, Naona umesahau kuongezea Zitto Kabwe, Dr. Ramadhan Dau nk
 
Ramadhan Dau ana kazi zake nzuri tu za kuisaidia Serikali.

Zitto Kabwe mbona tayari ni mkuu wa chama tawala? Au huelewi hilo?

Zitto Kabwe kafanikisha malengo ya chama pinzani siasa kwa muda mfupi sana, mpaka inakuwa ni maajabu. The man is a genius.

Hilo lisikupe shida.
 
Zalisheni kwa wingi mfumuko wa bei utashuka.

Ukiina factor moja ya mfumuko wa bei wewe haikuhusu ina maana mahitaji yako mengine yanazidi yale ya mafuta.

Kijaji hana kosa hapo, Mwigulu analo la kujibu.

Mimi namshangaa sana Mama Samia hawatumii watu kama Assad kwenye mambo ya uchumi.

Lipumba simuamini sana, ingawa ni mchumi lakini ana kitu hakijanikalia sawa.
Assad ni mhasibu siyo mchumi..
 
Mara nyingi watawala sehemu nyingi duniani hujificha katika kupanda kwa bei ya mafuta kama sababu za mfumuko wa bei nchini mwao lakini kwa sasa mafuta hayajapanda bei duniani kwa muda mrefu ila vitu vimepanda bei sana nchini.

Mwigulu Nchemba na Ashatu Kijaji jitokezeni hadharani mseme sababu za bidhaa na huduma kupanda bei kwa kiwango cha juu sana na kwa kasi kubwa sababu ni nini. Watu wenye vipato vya kawaida na vidogo wanaumia sana.
mweshoni mwa mwezi February au katikati ya March 2024, mazao ya mashambani kwa sehemu kubwa nchini yatakua yameanza kukomaa na kutumika majumbani,

hakutakua na mfumuko wa bei tena itakua ni mporomoko wa bei sasa 🐒
 
Mara nyingi watawala sehemu nyingi duniani hujificha katika kupanda kwa bei ya mafuta kama sababu za mfumuko wa bei nchini mwao lakini kwa sasa mafuta hayajapanda bei duniani kwa muda mrefu ila vitu vimepanda bei sana nchini.

Mwigulu Nchemba na Ashatu Kijaji jitokezeni hadharani mseme sababu za bidhaa na huduma kupanda bei kwa kiwango cha juu sana na kwa kasi kubwa sababu ni nini. Watu wenye vipato vya kawaida na vidogo wanaumia sana.
Unaweza shangaa mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda unaendelea kujengwa, halafu watu hao hao kwenye serikali ya Tanzania waliopitisha mradi wa bomba la mafuta hilo wameshindwa kufikiri kujenga bomba la gesi kutoka Dar hadi Dodoma ili kuweka uwezekano wa magari ya mizigo na abiria kutumia gesi na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ambayo ndiyo hasa yanasababisha mfumuko wa bei..
 
Zalisheni kwa wingi mfumuko wa bei utashuka.

Ukiina factor moja ya mfumuko wa bei wewe haikuhusu ina maana mahitaji yako mengine yanazidi yale ya mafuta.

Kijaji hana kosa hapo, Mwigulu analo la kujibu.

Mimi namshangaa sana Mama Samia hawatumii watu kama Assad kwenye mambo ya uchumi.

Lipumba simuamini sana, ingawa ni mchumi lakini ana kitu hakijanikalia sawa.
Assad si Mchumi..
 
Tazama CV yake.
Hajawahi kusoma Uchumi, Under graduate kasoma Bcom..MA Akasoma Accounts..then akaendelea na Accounts .
Assad sio Mchumi, hajawahi kufanya kazi za uchumi wala kufundisha Uchumi.
Kuna utofauti mkubwa kati ya Mchumi na Mhasibu
 
mweshoni mwa mwezi February au katikati ya March 2024, mazao ya mashambani kwa sehemu kubwa nchini yatakua yameanza kukomaa na kutumika majumbani,

hakutakua na mfumuko wa bei tena itakua ni mporomoko wa bei sasa
Kwa nini nauli za vyombo vya usafiri zimepanda bei?
 
Back
Top Bottom