Rais Samia Kuongoza Vikao vya Uongozi wa CCM Ngazi ya Taifa, Jijini Dodoma, Tarehe 9 Julai 2023

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Vikao vya Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu Hassan, vitaketi siku ya tarehe 9, Julai, mwaka 2023, jijini Dodoma.

Vikao hivyo vya kawaida vya Uongozi wa Chama ngazi ya taifa, vitafanyika kwa mujibu wa Katiba ya CM ya Mwaka 1977, Toleo la 2023, vikitanguliwa na Kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, itakayoketi Julai 8, mwaka huu 2023.​

F0cIJ0vXoAQa3Gf.jpeg
 
Hakuna Katiba ya CCM toleo la 2023. Hiyo Katiba toleo la 2023 ni mpya au? Huyu Mwenezi anashindwa kuhariri vitu vidogo kama hivi ndo ataweza kudadavua Mkataba wa Bandari?
 
Kwani msimamo na sera ya nchi ipo kwa Rais kama mtu,Rais kama taasisi,upo kwa CCM kama chama dola au Wizara ya mipango na bunge letu?
Hatujakaa sawa,tutaendelea kutafuta njia kila leo.
 
Hakuna Katiba ya CCM toleo la 2023. Hiyo Katiba toleo la 2023 ni mpya au? Huyu Mwenezi anashindwa kuhariri vitu vidogo kama hivi ndo ataweza kudadavua Mkataba wa Bandari?
Toleo jipya lililoingiza uuzwaji wa rasilimali za taifa kama sera mojawapo ya chama.
 
CCM yetu, nchi yetu, watu wetu, serikali yetu ya CCM, Mungu iliende Daima na Milele Chama hiki, Amen.. 💚💛🙏
 
Back
Top Bottom