Rais Samia Aongoza Kikao Halmashauri ya CCM Taifa, Ikulu DSM Leo Novemba 29, 2023

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 29 Novemba, 2023 Ikulu Jijini Dar es salaam, Awali kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
WhatsApp Image 2023-11-29 at 19.01.15 (1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-29 at 19.01.16.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-29 at 19.01.18.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-29 at 19.01.20.jpeg
 
Kikao kinaendelea au kimekwisha? Na kama kimekwisha nini kimejiri huko?
 
Wapinzani tuna kitu cha kujifunza kwa namna CCM wanavyoendesha mambo yao ,Wananchi wengi hawaipendi CCM lakini mbadala wake ni Changamoto sana .
 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 29 Novemba, 2023 Ikulu Jijini Dar es salaam, Awali kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Hiki ni kikao muhimu, ila hili la CCM kufanyia vikao vya chama chetu kwenye Ikulu yetu, halijakaa vizuri, kwasababu pale CCM Lumumba kuna ukumbi mkubwa tuu wa kutosha kwa vikao vya CC na NEC.

Kwa vile Ikulu ni ya wote, hili la chama kimoja kufanyia vikao vya chama Ikulu, halina karma Njema!. Kama Mama anaweza kuepuka the accumulation of bad karma, it's good and better!.

Enzi za JPM, baada ya kauli hii
View: https://youtu.be/EdA5Zb6liwE?si=FJx-J3jsJpBMbL4y tulilalamikia kuchanganya shughuli za serikali na za chama, tukasauri Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . na kiukweli pamoja na ukali wake wote, JPM alikuwa msikivu sana kwa hoja zenye mashiko, hivyo alianza kubadilika Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana! na tulimpongeza JPM, kutenganisha shughuli za chama na serikali, shughuli za chama zinafanyika chamani, shughuli za serikali zinafanyika serikalini. Pongezi Dkt. Magufuli kutenganisha shughuli za Chama na Serikali, Utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!

Otherwise nawatakia kikao chama.

P
 

Makonda amenuna sana, anamtaka Sabaya kama Katibu mkuu wa chama.
 
Hiki ni kikao muhimu, ila hili la CCM kufanyia vikao Ikulu yetu, wakati pale CCM Lumumba kuna ukumbi mkubwa tuu, halina karma Njema!. Kama Mama anaweza kuepuka the accumulation of bad karma, it's so good.
Tulimpongeza JPM, kutenganisha shughuli za chama na serikali, shughuli za chama zinafanyika chamani, shughuli za serikali zinafanyika serikalini. Pongezi Dkt. Magufuli kutenganisha shughuli za Chama na Serikali, Utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!

Otherwise nawatakia kikao chama.

P
Ikulu wajumbe watakuwa na woga kidogo, hawatotupa viti hata mwenyekiti asipowafurahisha.
 
Hivi CCM pamoja na makumbi yote waliyojilimbikizia karibia kila mkoa lakini bado vikao vya chama wanaemdelea kufanyia kwenye taasisi ya umma...

Halafu bado watakwambia wanapambana na ufisadi na ubadhirifu...

Bado ninasema na nitaendelea kusema, ili Mwafrika aendelee anahitaji akili na namna ya kutumia akili...
 
Wapinzani tuna kitu cha kujifunza kwa namna CCM wanavyoendesha mambo yao ,Wananchi wengi hawaipendi CCM lakini mbadala wake ni Changamoto sana .
Mbadala wa nini wewe unawaza kama nyani? Yaani umekalisha migololi nyumbani ukisubiri mbadala? Mbadala ni wananchi kama wewe kuamka na kudai haki yao. Unadhani kuna watu watakuletea maendeleo wakati wewe umekaa kwenye kochi la uvivu uknywa denge?
 
Back
Top Bottom