Rais Magufuli: Pesa za Uhuru zijenge barabara ya Mwenge-Morocco Dar es Salaam

Yani miaka yake mi3 tuuu naiona Tanzania nyingine kabisaaaa..... Mungu akulinde rais wetu mpendwa JPM
 
Nadhani pesa pia iende katika maji DSM!!!? Kama barabara zinapewa kipaumbele basi ziangaliwe hizi: Morogoro road na Pugu/Nyerere road
 
Lakini unawezaje kuyatoa Magari katika njia NNE na unaya peleka yakarundikane katika njia mbilo hapo sijaelewa
 
Kila siku namshukuru Mungu kwa kutupa Rais Magufuli, sipati picha after 5 years tutakuwa level gani
 
Ni bora ata katiba ije ibadirishwe ili Magufuli aongoze miaka 20 bila kufanyika uchaguzi mkuu tu sasa maana hakuna namna.

Haki ya mungu hata mi nina mawazo kama yako,ofcoz tumempata mkombozi,magufuli anatosheleza sana,miaka kumi ni michache sana aiseee.yaan bora aongoze mpaka kufa kwake.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo hela ingetumika kufanya miundombinu mipya ya maji hapa Dar

Maji tayari inafungu lake,kumbuka juzi ilitangazwa kuwa kulikuwa na mradi wa kusambaza maji lkn ulizuiliwa na Nyumba ya ndugu wa mgombea wa ukawa ila baada ya juzi kuvunjwa Nyumba hio mhandisi kasema mpaka mwezi wa pili mwakan mradi huo mkubwa wa kutosheleza maji kusambazwa dar nzima utakuwa tayar
 
Nchi hii siyo maskini. Fedha hizo sehemu yake ilikuwa ni malipo ya posho na gharama za kukodi magari kwenda uwanja wa uhuru. Hapo watu watalia kwani tayari walishabajeti matumizi hayo hata kabla fedha hawajapata. Imekula kwao.
 
Fanya kazi magufuli mungu yuko na wewe hakuna wa kukufananisha wewe ni kiongozi sio mtawala umethibitisha mie nilijua tz yangu ndio basi kumbe watu wa kutupeleka kwenye nchi ya maziwa na asali wapo mungu akujalie.
 
Ahsante mkuu nimekuelewa vema. Nimeyakumbuka maneno ya Hashim Rungwe kuwa wananchi wanataka wawe na uwezo wa kupata milo 3 kwa siku, wapeleke watoto shule na wapate elimu bora, huduma ya maji safi na salama na afya bora wala hawatayabeba madaraja mgongoni. Kwa mimi naona hii ni wrong decision ameifanya Mh. Rais hizo hela zingesaidia kutatua moja ya hayo juu na angapata kitu cha kuonekana. Barabara ya morocco haina impact kubwa ktk uchumi.

Yeye ameona barabara ya moroko ina impact.ndo mana ameamuru ijengwe.hata angeipeleka siptalini bado mngesema tu ooh oooh angepeleka bodi ya mikopo ya wanafunzi...
 
Hiyo barabara haikua na bajeti yake kabla? Maana tuliambiwa ile ya Tegeta -Mwenge ikikamilika inafuatia Mwenge Morocco, kumbe hukukua na fungu??
 
Ahsante Chama cha mapinduzi demokrasia ndani ya chama ndio imetuletea Jembe hili......

Hapa kazi tu
 
Ni hatua nzuri sana lakini mbona pesa zote zinaelekezwa mkoa wa Dar?
Ina maana sie wa Bukoba hatupaswi kuneemeshwa na hizi pesa za zuio la Magufuli!
Ina maana Dar wao peke yao ndio wanalipa kodi?

Magufuli acha ubaguzi, hizo pesa zilenge kusaidia watanzania wote nchini na sio kwa wakazi wa Dar peke yao.

Mbona kijijini kwako Chato uliweka taa za kuongozea magari wakati hakukuwa na umuhimu kivile maana magari huko ni moja moja.

Usiwe na wivu hata hivyo sherehe hizo hufanyika dar siku zote ni hela zao hizo.
 
Lipumba kuwa gavana Wa benki kuu? Au anapelekwa TRA? Au atakua waziri wa fedha? Kuwa waziri lazima ateuliwe ns rais kisha ahamie ccm
 
Back
Top Bottom