Rais Magufuli: Pesa za Uhuru zijenge barabara ya Mwenge-Morocco Dar es Salaam

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,494
54,906
Rais Magufuli aagiza pesa zilizotengwa kwa ajili ya kusherehekea Sherehe za Uhuru wa Tanganyika, zitumike kwenye upanuzi wa barabara inayo anzia Mwenge hadi Morocco, jijini Dar es Salaam ambayo ina urefu wa Kilometa 4.3
CVD6q02UsAEJKt_.jpg


==================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.

Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja

Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo

Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.
Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.

Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.

30 Novemba,2015

 
Safiiiiiiiiu... ina maana hizo fedha za UHURU DAY, is roughly around tshs. 10 billion nadhani... aiseeeeeeeeee

Kweli Magufuli, unatia moyo..!!
 
nini chanzo cha taarifa yako?

updates.
Aisee ni kweli, nimeona taarifa ya gerson Msigwa, kurugenzi ya habari ikulu. Ni kiasi cha 4 billion
 
Safiiiiiiiiu... ina maana hizo fedha za UHURU DAY, is roughly around tshs. 10 billion nadhani... aiseeeeeeeeee

Kweli Magufuli, unatia moyo..!!

In year 2012 they spent 60b on uhuru day if the source of this data is authentic and am not mistaken while 1km is roughly around 1b so try to imagine 60b how many kms of tarmac road could have been constructed?
 
Back
Top Bottom